Friday, 16 August 2013

FOOLISH AGE’ YA LULU KUZINDULIWA AGOSTI 30

STAA  katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’,  anatarajia kuzindua filamu yake aliyoipa jina la Foolish Age Agosti 30, mwaka huu.



 Akiteta  na mtandao huu  hivi karibuni Lulu alisema  filamu hiyo ndiyo itakuwa ya kwanza  kuitoa tangu apate dhamana kutoka ‘lupango’ kuhusiana na kesi ya mauaji ya Kanumba.  Kwa mujibu wake, ndani ya filamu hiyo kuna vitu kavicheza ambavyo yeye mwenyewe alikuwa akivifanya enzi ya umri wake mdogo.
“Ni filamu yangu ya kwanza ambayo naamini mashabiki wangu wataipenda na licha ya wao kuipenda pia naamini watakaoiona watajifunza mengi sana,” alisema.
Uzinduzi wa filamu hiyo utafanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, ukisindikizwa na Machozi Band inayoongozwa na Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’.

No comments:

Post a Comment