Tuesday, 27 August 2013

BIASHARA YA NGONO YARUHUSIWA RASMI KUFANYIKA KWENYE MAGARI BARABARANI

Jiji limehalalisha na kufungua vyumba 9 ambavyo vitatumiwa na machangudoana wateja wao kihalali na kwa usalama zaidi
Drive-in ya ngono imefunguliwa rasmi, Zurich katika mkakati wa kuwalinda makahaba ili kuhamisha biashara ya umalaya nje ya mji wa Swiss.
Vibanda(pichani kulia) tisa vya ngono vilivyojificha ndani ya uzio mkubwa vimeandaliwa kwaajili ya wauza miili ‘malaya’ na wateja wao kuanzia leo na kuendelea.
Kuna saini ndogo inayoonesha muda wa kazi, mwamvuli mwekundu kutambulisha eneo hilo kama eneo la shughuli hiyo ambalo zamani lilikuwa ni eneo la viwanda magharibi mwa jiji hilo. 

Pamoja na hayo kuna sharia maalumu zimewekwa(kushoto pichani). Mteja lazima awe na umri usiopungua miaka 18, mtu mmoja tu kwenye gari, na kondom lazma itupwe kwenye vyombo maalumu baada ya kutumika.

Kuna eneo ambalo mteja anaweza kuchagua mwanamke anayemfaa, pamoja na makubaliano ya bei kabla ya kuelekea kwenye kibanda, ambacho ni cha mbao kinacho fanana na eneo la kuegesha gari.

Kila kiboksi kina alamu ili kuwalinda Malaya hao.

Michael Herzig, mkurugenzi katika huduma ya jamii ya wafanyakazi wa ngono jijini alisema “Umalaya ni biashara” 

“Hatuwezi kuzuia, hivyo tunataka kudhibiti ili kuwasaidia wafanyakazi wa ngono na jamii, sababu bila kufanya hivyo uhalifu unaongezeka na wahuni wanazidi kuwa wengi”
Ursula Kocher, Mkurugenzi wa Flora Dora, mtandao unaounga mkono Malaya, alisema kuwa machangu doa mara nyingi huchukuliwa na kupelekwa porini au nje ya mji na kujikuta katika mazingira hatari.

Alisema “ hapa wanabakia humuhumu ndani na kuhudumia wateja wao haraka” 

Eneo hilo la drive-in ya ngono limehalalishwa na wakazi wa Zurich katika sharia ya mwezi machi, 2012baada ya kupigiwa kura kwa asilimia 52.6 kukubaliana nalo.

Eneo hilo pia lina makubaliano mazuri tu yanayohusisha vyama vyote vya siasa nchini humo, likiwa na wanachama wengi wa chama cha Swiss People's Party (SVP) wanaopinga mpango huo.

"haitofanikiwa, labda kwasababu wateja hawatokuja au eneo hilo halitotumiwa na machangudoa” alisema Sven Oliver Dogwiler, mwanasiasa wa eneo hilo ambae ni mwanachama wa SVP


No comments:

Post a Comment