Showing posts with label Mbele. Show all posts
Showing posts with label Mbele. Show all posts

Saturday, 21 September 2013

P SQUARE NDO HABARI YA MJINI AFRIKA KWASASA

           KUNA jambo moja ambalo mashabiki wa timu ya soka ya Arsenal wa Bongo wanajivunia kwa sasa. Unajua hao mashabiki wamefanya nini? Wamegeuza kibwagizo cha wimbo maarufu wa ‘Personally’ unaotamba kwa sasa wakaupa jina la ‘Arsenally’.
Wimbo huo ni wa wakali wa muziki wa Afrika kwa sasa ambao ni Peter na Paul Okoye wa Nigeria. Kimuziki wakali hao wanajulikana kwa jina la P-Square.
Kwa sasa wamevunja rekodi ya kuwa wasanii ambao nyimbo zao hazijawahi kuachwa kupigwa kwenye majumba ya starehe tangu mwaka 2003 mpaka dakika hii unaposoma ukurasa huu.
Mwaka huo ndipo walipozindua albamu yao ya kwanza ‘Last Night’ ambayo ilitengenezwa na Timbuk Music Label.
Wasikilizaji wazuri wa muziki, watakumbuka kwamba tangu kutolewa kwa ngoma yao ya kwanza, kila mwaka wakali hao wanadondosha nyingine na mpaka sasa hawajawahi kupotea kwenye ramani.
Unaposoma makala haya, wimbo wao bora wa ‘Alingo’ unatesa na huku ‘Personally’ ukiendelea kupasua anga vilevile.
P-Square wametoka mbali mpaka kufikia hapo walipo sasa, kati ya mambo yaliyowawezesha kufikia mafanikio walionayo ni pamoja na kuwa na moyo wa kupenda kujifunza kutoka kwa wasanii wenzao waliowatangulia.
Walianza kuonyesha vipaji vyao tangu walipokuwa katika elimu ya sekondari nchini kwao Nigeria.
Waliwahi kujiunga na chama cha muziki na maigizo baada ya kupata mafunzo. Wakati huo waliimba na kucheza nyimbo za wasanii wa nje ya nchi yao kama vile Micheal Jackson, Bobby Brown na MC Hammer.
Mwaka 1997 waliunda kikundi kilichojulikana kwa jina la MMMPP, ikiwa ni majina yao na wenzao, M Clef a.k.a Itemoh, Micheal, Melvin, Peter na Paul. Kutokana na kumkubali sana Micheal Jackson, walianza kucheza Break Dance.
Mwaka 1999, P-Square walirudi katika shule ya muziki ili kujiendeleza katika mafunzo ya upigaji gitaa, kinanda, ngoma, filimbi na kadhalika. Mpaka sasa wao ndiyo wanamuziki nguli wanaomudu kupiga ala mbalimbali.
Baada ya hapo walijiendeleza na masomo katika Chuo Kikuu cha Abuja wakisomea masomo ya Utawala wa Biashara.
Ni hapo ndipo walipoanza rasmi kutumia jina la Double P&P, Da Pees na baadaye wakatulia na jina hili la P-Square chini ya udhamini wa Bayo Odusami ‘Howie T’ ambaye pia ni promota na CEO wa Adrot Nigeria Limited.
P-Square ya sasa ina albamu nne; ‘Last Night’, ‘Danger’, ‘Get Squared’ na ‘Game Over’.
Kwenye Get Squared ndiyo kuna ngoma kama Story, Bizzy Body, Get Squared, Say Your Love na Temptation. Kwenye Danger kuna nyimbo zilizowika pia kama vile I Love You, Possibility, Danger, No Easy na Gimme Dat.
Kwenye Game Over ndio walimaliza mchezo kiukweli. Humo kuna nyimbo kali kama vile No One Like You, Do Me waliyomshirikisha Waje, Ifunanya na Roll It.
Wamechukua tuzo zaidi ya 20 mpaka sasa huku wakiwa wasanii wanaomiliki studio yao wenyewe. Kwa jinsi walivyojitosheleza, kama unataka kuwachukua kwa ajili ya onesho unapaswa kutokuwa na chini ya Dola 300,000.
Kipya na kizuri ambacho kimeongezwa kwenye kundi la vijana hawa pacha ni jinsi maonesho yao yanavyokuwa, kuanzia mwezi Julai mwaka huu wamegoma kabisa kufanya muziki wa ‘Playback’.
P-Square wa sasa wanafanya onesho kwa saa tatu huku wakiwa na wanamuziki wenzao 11 na onesho lao halipungui saa tatu.
Ukizungumzia kipato, wanamuziki hawa tangu mwaka hu uanze, wamekuwa na onesho kubwa kila mwezi ambapo kwa wiki 52 za mwaka wanakisiwa wataingiza maelfu ya dola.
Pia wana ndege binafsi waliyonunua, jumba la kifahari walilolipa jina la Squareville, studio yao ya Square Records pamoja na mkataba mnono walionao na kampuni ya simu ya Globacom ya nchini Nigeria

Thursday, 19 September 2013

WANASAYANSI WADAI MWISHO WA DUNIA UTAFIKA BAADA YA MIAKA BILIONI 3.5 AMBAPO JUA LITAKUWA KALI SANAA



             Mwisho wa dunia kwa mujibu wa wanasayansi bado sana. Maisha duniani yataendelea kuwepo kwa miaka bilioni 3.5 mingine.

Baada ya hapo wanasayansi wanaamini jua litakuwa kali kiasi ambacho hakuna kiumbe kitakachoweza kuishi. Tangu iwepo, sayari ya dunia imekuwa kwenye umbali sahihi kutoka kwenye jua kiasi cha kuifanya iwe  na maisha.

Wanasema tatizo ni kwamba nyota zimeendelea kuchemka kadri muda unavyoenda na zikiendelea kutoa joto zaidi, maji ya dunia yataendelea kukauka na kupote kabisa. 

Utabiri huo umetoka kwa wataalam wa chuo kikuu cha East Anglia ambapo mtafiti mmoja wapo, Andrew Rushby amesema baada ya miaka hiyo dunia itakuwe na joto kali kiasi ambapo hata bahari zitageuka kuwa mvuke.
 
Alisema binadamu watakuwa viumbe wa kwanza kupotea.

Source: Daily Mail via Bongo5

HUYU NDIYE MWANAMITINDO KIKONGWE KULIKO WOTE DUNIANI.TAZAMA PICHA SABA ZA HUYU KIKONGWE MWANAMITINDO.



 
            Imezoeleka zaidi Dunia ya mitindo huwa ni ya vijana lakini hii tofauti kwa Kikongwe Jean Woods mwenye umri wa miaka 75 ndiye anayeelezwa kuwa ni mwanamitindo mzee kuliko wote duniani.

WASANII WA KIKE WATAMBIANA KUONYE UZURI WA MAZIWA YAO...!!















                              Anita Joseph VS Cossy Orjiakor nani mkali hapo??

JAY Z NA BEYONCE WATISHA,CHEKI PICHA ZA MJENGO WAO NI HATARIIIII





                                                                     Aerial view of the mansion








A view of the backyard/pool






A view of the master bathroom






Master bedroom





Personal Bowling Alley, wow wish I had this!





Dining room




Living room



“5-TV room”


Elegant Kitchen


Living space



Family Room
Executive Office



A view of the skatepark/rock climbing wall that Jay Z and Beyonce totally need


HII NDO PICHA ILIYOMFANYA AMBER ROSE AACHANE NA KANYE WEST

 
               SIRI  mojawapo  ya  penzi  la  dhati  ni  heshima.Tendo  la  ndoa pekee  halitoshi  kumfanya  mtu  ajione  anapendwa  na  kuthaminiwa....

Katika  hali  ya  kawaida, utajisikiaje  mpenzi  wako  akikupiga DOLE   la  makalioni  mbele  wa  watu  kiasi  hiki?. Ni  ishara  ya  kupendwa  au  kudharauriwa...



Kwa  Amber  Rose, hii  ilikuwa  ni  dharau  tosha  aliyowahi  kutendewa  na  Kanye west   kiasi  cha  kumfanya  achukue  maamuzi  magumu.

KALI YA MWAKA...!!! MWANAMKE ARUDISHIWA POCHI YAKE ILIYOIBWA ZAIDI YA MIAKA 20 ILIYOPITA..

                    jeri Cox Chastain akikagua baadhi ya vitu vilivyokuwamo ndani ya pochi hiyo.
  

Vitu visivyouzika ambavyo mwanamke mmoja alipoteza kwa zaidi ya kipindi cha miaka 20 hatimaye vimerejeshwa kwake.


Pochi ya rangi ya bluu bahari iliyoibwa Desemba, 1990 kutoka kwa Jeri Cox Chastain, mama aliyekuwa akifanya kazi mbili wakati huo, imerejeshwa katika himaya yake.
Msamaria mwema aliiona pochi hiyo katika paa la vigae vya jengo moja huko Spartanburg, South Carolina, majengo kadhaa kutoka sehemu ambako Chastain alikuwa akifanya kazi wakati huo, na kumpa kumbukumbu ya miaka kadhaa iliyopita katika mchakato huo.
Chastain anakumbukia siku hiyo, 'siku ya malipo,' kwa uwazi. Alikuwa akifanya kazi Hospitali ya Doctor's Memorial, ambayo ilifungwa mnamo mwaka 1994.
Pochi hiyo ilikuwa imeibwa wakati alipotoka ofisini kwake, kabati la chuma, kwenda kununua vitafunwa.
Wakati huo aliamini kuna mtu katika jengo la ofisi yake amemuibia fedha hizo na kisha kuitupa pochi hiyo.
"Nilihisi tu ilikuwa imetupwa kwenye pipa la taka mahali fulani."
Badala yake, Chastain alipigiwa simu kutoka polisi mapema wiki hii ikimweleza kwamba pochi hiyo aliyodhani imetoweka kabisa, imepatikana.
Shastain alikwenda kituo hicho cha polisi siku iliyofuata kuitambua pochi hiyo, ambayo ilikuwa katika 'hali safi.'
Ingawa pesa hizo zilizokuwamo, hakika, zilikwenda Shastain alifurahi kupita kiasi kuona mlolongo wa picha na kitabu cha kumbukumbu.
Picha mojawapo kwa namna ya kushangaza ilikuwa muhimu kabisa kwa Chastain.
Ilikuwa ni picha ya kijana wake, sasa ana miaka 28, alipokuwa na miaka mitano akiwa kavalia nguo ambazo wakati fulani zilikuwa zikimilikiwa na baba yake.
Pia katika pochi hiyo kulikuwa na kadi za manunuzi na hata kadi za huduma ya matibabu kwa ajili yake na mwanae, pia cheti cha kuzaliwa cha mwanae huyo.
"Kuna mtu anawezekana kuwa alichukua [vyote hivi] na kufanya maisha mapya kwa [wao wenyewe]."
Kwa sasa Chastain ana furaha kufanya safari hii ya kumbukumbu, lakini anataka kumshukuru mtu aliyerejesha pochi yake.
Hii hakika si mara ya kwanza mtu mwaminifu kurejesha pochi iliyopotea kipindi kirefu sana.


Kutoka kwenye jengo hilo hilo, miaka michache iliyopita alirejesha pochi iliyopotea tangu mwaka 1996.

MWANAFUNZI AMCHINJA MWALIMU WAKE DARASANI, KISA SIMU YA MKONONI.

Mwanafunzi wa China amemchinja mwalimu wake katika kulipiza kisasi baada ya simu yake ya mkononi kutaifishwa.

Mwanafunzi huyo, aliyetajwa kwa jila la Lei katika taarifa za habari za mjini humo, alibambwa na mwalimu wake, Sun Wakang akiwa anachezea simu wakati wa somo la Kemia katika shule moja mjini Fuzhou, mashariki mwa jimbo la Jiangxi nchini China.


Siku iliyofuata Lei alikwenda kwenye darasa analofundisha Sun ambako mwalimu huyo alikuwa ameketi akisahihisha mitihani, na kumchinja kutokea kwa nyuma.

Mwalimu huyo mwenye miaka 32 ambaye ni baba wa watoto watatu alifariki papo hapo huku mwanafunzi huyo akitokomea kusikojulikana.

Jana Lei alipiga namba ya simu ya dharura na kukiri kuhusika na uhalifu huo kabla ya kujisalimisha mwenyewe polisi mjini Shanghai.

Sun alifanya kazi kama mwalimu wa Kemia katika Shule ya Kati ya Linchuan No. 2 kwa miaka mitano kabla ya mauaji yake ya kutisha, ofisa wa shule Xiong Hainshuo alieleza.

Alikuwa amechukua simu ya mwanafunzi huyo baada ya kijana huyo kuwa akiitumia wakati wa somo, lakini ilirejeshwa mwishoni mwa siku hiyo.

Licha ya hilo, Lei alimshambulia Sun wakati akiandaa masomo ndani ya darasa lake, siku nne tu baada ya Siku ya Walimu wa China, siku ya kitaifa ambapo wanafunzi huwaenzi walimu wao.

Maofisa wanasema mwalimu mwenzake alisikia Sun akilia kwa uchungu na kuita huduma za dharura, lakini mwalimu huyo alikuwa amefariki dunia kabla ya gari la wagonjwa kuwasili.

Nchini China, 'shule ya kati' huchukua miaka 7-9 na 10-12 na ni hatua ya mwisho kabla ya elimu ya juu.

Shule ya Kati ya Linchuan No.2 ni moja ya shule bora katika Jimbo la Jiangxi na ina moja ya wastani wa juu wa kupokea wanafunzi katika eneo hilo.

RECORD:TAZAMA PICHA 8 ZA WANAWAKE WANAONGOZA KUWA NA MAZIWA MAKUBWA DUNIANI

 












Wednesday, 18 September 2013

UTAFITI:SIMU ZA KUPAPASA(SMART PHONE)ZINA UCHAFU MWINGI KULIKO CHOO


Simu  ya  kupapasa.
 Watafiti wamebaini kuwa baadhi ya vifaa vya kisasa vya mawasiliano vinavyotumika kwa kupapasa kama tablet komputa na smart-phones huwa na vijidudu vingi vya uchafu kuliko hata choo.



Bakteria hao huachwa na watumiaji wavifaa hivyo kwa kupapasa vioo vya vifaa kama Apple iPads na Samsung Galaxy tablets kutokana na kutumia bila ya kuosha mikono.
Choo


Moja ya tablet iliyofanyiwa vipimo na taasisi ya kulinda mtumiaji ya Which? ilikutwa na baktaria aina ya staphylococcus aureus ambao hutoa sumu ambayo hupelekea mtu kutapika.
USHAURI:
Kuwa  na  smart phones  ni  sawa  na  kutembea  na  choo  mkononi (  kwa  mujibu  wa  utafiti  huu) ...Tuwe  waangalifu ili  simu  hizi  zisiguswe  na  watoto  wetu.

HURUMA...!!! MWALIMU AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME NDANI YA DARASA...


              Diane Krish-Veeramany na wenzake watatu mara baada ya kujifungua salama mtoto wa kiume darasani. 

Mwalimu wa shule ya msingi alilazimika kujifungulia ndani ya darasa pale mtoto wake alipotokeza kabla ya wakati, huku wenzake wakifanya kazi kama wakunga.
Diane Krish-Veeramany aliingia leba katika wiki 39 - siku moja kabla ya siku aliyopanga kuanza likizo ya uzazi - na dakika chache kabla ya kengele ya shule kulia Alhamisi iliyopita.
Baada ya dakika zipatazo ishirini za ufupisho, alijifungua mtoto wa kiume, Jonah, akiwa ameketi kwenye kiti cha compyuta huku akizungukwa na wasaidizi wake ambao walimzalisha mtoto huyo.
Bi Krish-Veeramany, mwenye miaka 30, ambaye pia ana mtoto wa kiume mwenye umri wa miezi 18, Noah, aliyezaa na mumewe Vijaye, miaka 31, alisema kujifungua huko kilikuwa kitu ambacho hakupanga.
Alisema: "Kila mtu mwenye mtoto anafahamu unajaribu na kupanga mambo haya kichwani kwako lakini kila kitu kilitokea haraka mno, sikuweza kufikiria.
"Ilikuwa kikamilifu, yuko salama kabisa, niko salama kabisa, na ninashukuru sababu vinginevyo ningeweza kujifungulia kwenye kiti cha nyuma cha gari."
Bi Krish-Veeramany, mwalimu wa watoto, alisema aliwasili kazini katika Shule ya Msingi Manford, huko Hainault, kaskazini mashariki mwa London, mapema kuhudhuria Klabu ya Chai Alhamisi iliyopita.
Muda mfupi baada ya kula kipande cha mkate wa kuchoma alianza kupata msisimko wa hisia na kujihisi tumbo kukaza, lakini aliendelea kuchukulia kama kawaida.
Alisema: "Ilipotimu takribani Saa 2:20 asubuhi nikamtumia meseji mume wangu kusema sijisikii vizuri. Kisha baada ya mkutano wa wafanyakazi nikaongea na mkuu na kusema ninajihisi namna ya ajabu kidogo na siwezi kukaa shuleni.
"Mkuu aliniuliza kama nilikuwa nataka gari la wagonjwa lakini nilikataa na kusema hakukuwa na jambo kubwa. Nilikuwa natembea kuelekea upande mwingine wa shule nikiwa na msaidizi wangu ndipo nikahisi kitu fulani.
"Wanafunzi walikuwa wakijiandaa kuingia madarasani na nikasema nisingependa watoto wanione nikiwa hivi sababu sipendi kuwatia hofu hivyo tulikwenda kwenye darasa ambalo lilikuwa halitumiki."
Alisema alikaa kwenye dawati la kompyuta juu ya kiti cha kompyuta huku msisimko wake wa hisia ukiongezeka.
Sasa akiwa ameungana na wasaidizi watatu, akaendelea kukataa gari la wagonjwa, na alikusudia kumsubiria mumewe awasili hivyo kuweza kumpeleka hospitalini.
Alisema: "Nilikuwa mkaidi siwezi kujifungua mtoto kwenye sakafu ya darasa.
"Lakini dakika ishirini baada ya msisimko wa hisia kuanza na ndani ya dakika 40 za kumweleza mkuu nikajihisi rundo kiasi la furaha likiwasili."
Wenzake Sam Mustafa, Dita Gojnovci na Chris Sword walimzalisha mtoto huyo huku wakipokea maelekezo kutoka kwa daktari kwa njia ya simu.
Wakati madaktari wakiwasili mtoto huyo tayari alikuwa katika mikono ya mama yake.
Ilikuwa tu hadi baada ya kujifungua ndipo mataulo yalipokusanywa kutoka kila kona ya shule hiyo na Jonah akafunikwa kama sweta.
Zawadi za kwanza za Jonah zilikuwa nepi na mavazi zilizopatikana kutoka kwenye duka moja ya jirani.
Mwalimu Mkuu Tina Jacobs alisema: "Tulipiga simu kuita gari la wagonjwa lakini kabla ya kufika hapa akawa ameshajifungua ndani ya darasa tupu kwa msaada wa wasaidizi watatu wa darasa. Ilifanyika haraka mno.
"Wasaidizi hao watatu wa darasa walikuwa wenye akili sana na nimetunuku vyeti na medali katika mkusanyiko wa Ijumaa."

VIDEO:JE...!! UNAMJUA MTU ALIYEVUNJA RECORD YA DUNIA KWA KUVUNJA NAZI KWA KIDOLE

       Huyu ndiye Mzee aliyewekwa katika kumbukumbu za GUINNESS WORLD RECORDS kwa kitendo cha kuvunja nazi kwa kidole kimoja haya ni maajabu na ni kweli.



 
Tazama video yenyewe hapo chini....  


WADAU WA IPHONE 5S WAWEKA KAMBI NJE YA DUKA LA APPLE SIKU 4 KABLA HAZIJAANZA KUUZWA

                 ‘Die Hard customers’ wa simu za iPhone wameamua kupanga foleni nje ya duka la simu hizo jijini London, Uingereza na kuamua kuweka kambi ya muda kwa kufunga matenti na kuhamishia makazi yao hapo huku wakisubiri siku rasmi ya kuanzwa kuuzwa kwa toleo jipya la iPhone5S linalosubiriwa kwa hamu kote ulimwenguni ambayo ni Ijumaa hii (September 20).
iphone 5SIphone 5S zitakazokuwa zikipatikana katika rangi tatu
Mmoja wa wateja hao ambaye hii ni siku pili kushinda na kulala hapo akisubiri kujipatia simu yake mara zitakapoanza kuuzwa, amesema mpaka sasa ameshakataa ofa ya £200 (515,000 Tsh) kwaajili ya kuuza nafasi yake kwenye foleni hiyo na kuwa na matarajio ofa inaweza kuja kufikia £1000(2,575,000)baadaye.
iphone fan-2
iPhone fan-3
Vijana hao wawili ambao wameweka kambi jana usiku nje ya duka la Apple wamedai kuwa siku zote wao huwa miongoni mwa wateja wa kwanza kuzipata simu mpya za iPhone kila zinapotoka, hivyo wameamua kuweka kambi nje ya duka ili wahakikishe wawe wateja wa kwanza kuzinunua siku ya Ijumaa.
-BONGO5

PICHA:HATIMAYE MSHINDI WA BBA'DILLISH' AKUTANA NA BABA YAKE MKENYA ALIYEHUDHURIA BIRTHDAYA YAKE NAMIBIA JUZI

             Wiki iliyopita mshindi wa mwaka huu wa Big Brother Africa ‘The Chase’ Dillish Mathews kutoka Namibia alimfahamu baba yake mzazi ambaye ni raia wa Kenya baada ya mama yake kuthibitisha kuwa ndiye baba yake.
Dillish n dad
Dillish akiwa na baba yake Abdi Guyo
Baada ya Standard Media ya Kenya kufanya kazi ya kuwaunganisha baba Dillish aitwaye Abdi Guyo na mama yake Selma kwa njia ya mtandao baada ya kupotezana kwa miaka 23, Selma alimkaribisha ahudhurie birthday ya binti yake nchini Namibia ambayo ilikuwa jana (September 16).
dillish2
dillish n dad 2
“The dance with my dad was priceless”
Kupitia akaunti yake ya facebook Dillish ameshare picha za birthday yake akiwa na dad wake mkenya.