Showing posts with label Afya. Show all posts
Showing posts with label Afya. Show all posts

Saturday, 21 September 2013

GHARAMA ZA MATIBABU MUHIMBILI ZAPANDA MARADUFU.....SASA KUMWONA DAKTARI NI SHILINGI 30,000/=


           Gharama za huduma  za kulipia matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimepanda maradufu.
Hatua hiyo inayotekelezwa bila kuwashirikisha wadau na watoa huduma ilianza Septemba mosi mwaka huu na kulalamikiwa na wagonjwa na wafanyakazi.

Kwa mujibu wa tangazo la Mkurugenzi wa MNH, lililobandikwa kwenye ubao wa matangazo wa jengo la mateniti la kulipia huduma  IPPM, inaonyesha kuwa gharama zilipanda kuanzia Septemba 2, wakati notisi hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi ilitolewa Septemba 4.

Wagonjwa wanaolipia matibabu  binafsi Muhimbili  waliliambia gazeti hili kuwa  wateja wanaotumia ‘ast truck’  na huduma ya uzazi inayotolewa na  kitengo cha mateniti- IPPM ndizo zilizoongezeka.
 
Kuanzia sasa upasuaji wazazi  unalipiwa Sh. 500,000 badala ya  350,000 za awali. Uzazi  wa kawaida  ni Sh. 250,000 badala ya  Sh. 150,000  zilizokuwa zikitozwa mwanzo.

Walisema kulala kunagharimu  Sh. 20,000  badala ya 15,000 wakati tozo la kumuona daktari kwa mara ya kwanza  ni Sh. 30,000 badala ya Sh. 20,000 za awali.  

Kumuona daktari kwa ajili ya kufuatilia huduma na matibabu zimepanda hadi Sh. 20,000 kutoka Sh. 10,000.

Huduma nyingine kama dawa na uchunguzi wa maabara 
zimepanda japo bei zake hazikutangazwa  kwenye ubao wa matangazo.

Kwa wagonjwa wa kujifungua kawaida ambao  hawalipii gharama  watatozwa gharama ambazo hazikafafanuliwa ingawaje serikali inataka watibiwe bure.

“Mfano mjamzito akipata uchungu ghafla na kufika Muhimbili bila rufaa atatakiwa kalipia gharama” alisema mjamzito jina tunalo.

Msemaji wa MNH Aminieli Aligaesha, alikiri kuongezeka gharama hizo ziliongezeka  na kuongeza kuwa sababu ya ongezeko  hilo ni gharama kubwa za uendeshaji.

Hata hivyo alikataa kutoa maelezo zaidi na kutaka mwandishi wetu kwenda ofisini kwake   kwa maelezo zaidi.

Hospitali ya Muhimbili inatoa huduma kwa utaratibu wa aina mbili kuchangia matibabu kunakofanywa na mgonjwa wa rufani pamoja na serikali.

Njia nyingine ni  wagonjwa kulipia gharama zote  za tiba kama ambavyo wanafanya kwenye hospitali za binafsi.

Hata hivyo gharama za tiba kwa wale wanaochangia matibabu na wale wa rufaa hazijaongezeka.

Friday, 20 September 2013

WANAUME NAO KUMEZA VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO

            Ni dhahiri kwamba wanaume watashtuka, lakini huenda nao wakashiriki uzazi wa mpango bila upasuaji
Vidonge vya uzazi wa mpango vimezoeleka kutumiwa  zaidi na wanawake pekee, kiasi kwamba ni jambo la ajabu kusikia kuwa wanaume nao wanaweza kuvimeza.
Hata hivyo, watafiti mbalimbali wamefanikiwa kutengeneza vidonge vya uzazi  ambavyo vinazifanya mbegu za kiume  katika mfuko wa uzazi wa mwanamume zisiwe na nguvu ya kuweza kutungisha mimba. Utafiti wa dawa hiyo ambao umewaumiza kichwa wanasayansi kwa miaka mingi umewezesha kupatikana kwa vidonge hivyo ambavyo havina vichocheo kama vile wanavyotumia wanawake ambavyo huingia katika mfuko wa mbegu za uzazi na kisha kuzidhoofisha.
Matokeo ya utafiti huo  ambayo yalichapishwa Agosti mwaka huu yanaonyesha kuwa vidonge hivyo vya uzazi kwa wanaume vitazuia kutunga mimba bila ya kuathiri uwezo wa mwanamume kushiriki tendo la ndoa kama kawaida.
Dk James Brander wa Taasisi ya Dana-Farberanasema utengenezaji wa  vidonge vya uzazi wa mpango kwa wanaume  umekuwa na changamoto kubwa kutokana na  upatikanaji wa dawa ambazo zinaweza kuzuia  mfumo wa utengenezwaji wa  seli za mbegu za kiume.
Dawa hizo ziitwazo JQI zilizotengenezwa katika maabara ya Bradner zinafanya kazi kwa kulenga protini maalumu zilizoko katika korodani  ambazo ni muhimu katika uzazi.
Vidonge hivyo vilichanganywa na vichocheo vya ‘Desogetrel’ ambazo huzuia uzalishwaji wa mbegu za kiume.
Profesa Malise Kaisi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Shirikishi Muhimbili (Muhas) ambaye ni Mtanzania wa kwanza kuzalisha watoto kwa njia ya upandikizaji (IVF) anasema ana wasiwasi mkubwa kuhusu dawa hizo kutumiwa kwa wanaume.
“Dawa za uzazi wa mpango ni rahisi kutumiwa na  wanawake kwa sababu wanawake wana mfumo mwepesi kwa dawa kufanya kazi na kuzuia utungishwaji wa mimba,” anasema.
Hata hivyo, Profesa Kaisi anahisi  kwa wanaume itakuwa hatari kwao kutumia dawa hizo kwani kunaweza kusababisha hata kuua kabisa uzalishwaji wa mbegu.
“Wanaume wana maumbile tofauti na mwanamke. Korodani za mwanaume ni kama kiwanda kinachofanya kazi usiku na mchana. Kwa siku moja mwanamume anazalisha mbegu milioni 10,” anafafanua Prof.  Kaisi.
Katika kuzifanyia utafiti, panya dume alipewa dawa hizo, kisha akawekwa pamoja na mwenza wake ambapo  licha ya kujamiiana hata baada ya miezi kadhaa  panya jike hakupata mimba
 Utafiti huo ulibaini kuwa pamoja na kuzuia uzalishwaji wa mbegu, vilevile dawa hizo zilionekana kuwa hazina madhara yeyote kwa kuwa hazina mchanganyiko wa vichocheo vya aina yoyote.
“Hazikuwa na madhara ya vichochezi (hormone). Mwanamume atakayezitumia hatabadilika tabia au mwili kupata mabadiliko yeyote yale” anasema Dk Martin Matzuk, mtafiti mwingine wa dawa hizo.
Dk Matzuk anasema hakuna kinga yeyote nyepesi ya uzazi wa mpango kwa wanaume iliyowahi kugunduliwa tangu kugunduliwa kwa mipira ya kiume miongo kadhaa iliyopita.
Inaelezwa kuwa utafiti huo  ni mkubwa na utakaoleta mapinduzi katika uzazi wa mpango baada ya vidonge vya uzazi kwa wanawake kuonekana na upungufu kadhaa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Cyriel Massawe wa Chuo  Kikuu cha Sayansi ya Tiba Shirikishi Muhimbili , anasema iwapo kweli dawa za uzazi wa mpango zitagunduliwa basizitasaidia wanandoa kujadili namna bora zaidi ya kupanga uzazi.
“Wenza wanapokuwa na uchaguzi wa kutosha wa namna ya kupanga uzazi inawasaidia wote wawili. Kwa mfano kama mama ana matatizo kadhaa, basi baba atachukua jukumu la kutumia vidonge ili kupanga uzazi,” anasema Dk Massawe.
Anasema kwa sasa wanaume wana njia moja tu ya kupanga uzazi ambayo ni mipira ya kiume hivyo basi iwapo njia nyingine zaidi zimepatikana basi itasaidia.
Dk Massawe anasema vidonge vya uzazi wa mpango kwa wanaume  bado vina changamoto kwa sababu ya mfumo wa uzazi wa mwanamume.
“Zile dawa zinatakiwa zikazuie uzalishwaji wa mbegu kwa wanaume kwa hiyo ili kuingilia mfumo wa uzalishwaji na  pindi mwanamume atakapoacha kutumia awe kama kawaida…ni changamoto” anasema.
Hata hivyo, Dk Massawe anasisitiza kuhusu ushirikiano wa wenza katika kupanga uzazi na kusema kuwa, ni suala linalohitaji watu wawili kujadiliana ili kujua ni njia ipi na salama ya uzazi wa mpango.
 Anaongeza kuwa wenza wanapopanga uzazi itawasaidia kuimarisha afya zao, za watoto na hata kupunguza mzigo wa majukumu ambayo hayakutarajiwa.
Utafiti mwingine unaofanana na huu ulifanywa mwaka 2010 ambapo wanasayansi waliwauliza wanawake na wanaume iwapo wanaume wanaweza kutumia dawa za uzazi wa mpango  pindi zitakaposhauriwa na 
 Katika utafiti huo ulioongozwa na Dk JudithEberhardt wa Chuo Kikuu cha Masuala ya Jamii,wanaume, 140 na wanawake 240 waliulizwa kuhusu matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango kwa wanaume.
 Hata hivyo matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa ingawa wanaume wote walisema watafurahi kutumia vidonge hivyo lakini wanawake walipata hofu iwapo wenza wao watakubali kutumia vidonge hivyo au kuvitumia inavyotakiwa ili kuimarisha uzazi wa mpango.
 Katika utafiti huo, wanaume walio kwenye mahusiano ya kudumu walitoa maoni ya kuvikubali vidonge hivyo huku wale walio katika mahusiano ya muda mfupi waliikosoa njia hiyo ya uzazi wa mpango.
Mei 2009, wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Manchester, Uingereza walitumia wanawake na wanaume kuzifanyia utafiti njia za uzazi wa mpango kwa wanaume kujua iwapo zinafanya kazi ipasavyo na zina manufaa.
 Watafiti hao waliwaambia wenza walioshiriki katika utafiti huo kuwa wanaume pekee watumie njia za uzazi wa mpango huku wanawake wakiambiwa kutotumia njia yeyote ili kupima iwapo njia za uzazi wa mpango zinafanya kazi kwa ubora au la.
Hata hivyo, wanaume kadhaa  nchini walioulizwa  iwapo watakubali kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango ikiwemo vidonge na wanaume wanane kati ya kumi, walikataa kutumia njia yeyote ile.
 Mmoja wao,     Edwin Mnzeru anasema, yeye na mke wake hawawezi kutumia njia ya uzazi wa mpango  ya vidonge, mipira ya kiume, wala ya kitanzi   kwa sababu  zina madhara kiafya na ni kinyume na dini.
chanzo:mwananchi

DAKTARI FEKI AKAMATWA HOSPITALI YA MUHIMBILI



              DAKTARI anayedaiwa kuwa bandia amekamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, akiwa na vitambulisho bandia vya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) akisomea Shahada ya Pili.
 
‘Daktari’ huyo ambaye amekuwa akitafutwa na uongozi wa chuo kwa zaidi ya mwaka alikamatwa jana asubuhi akiwa hospitalini hapo karibu na jengo kilimo kitengo cha meno.
Katika kitambulisho chake cha kupigia kura anatambulishwa kwa jina la Dismas John Macha aliyezaliwa mwaka 1979 Kilimanjaro na anaishi maeneo ya Upanga Magharibi, Dar es Salaam.
 
Gazeti hili, lilimshuhudia mtuhumiwa huyo akiwa katika kituo cha usalama cha Muhas na kupekuliwa na askari Polisi wa Muhimbili, Anthony Mwamatepela na kukutwa akiwa na vifaa vya udaktari .
 
Baadhi ya vifaa alivyokutwa navyo ni pamoja na koti jeupe la udaktari na stetoskopu ambacho ni kifaa cha kusikilizia mapafu yanavyofanya kazi na mapigo ya moyo.
 
Pia alikuwa na begi jeusi lenye aina mbalimbali za dawa, vitambulisho na karatasi nyingi, lakini alipoulizwa alidai kuwa hizo ni dawa zake.
 
Macha alikutwa pia na vitambulisho vitatu tofauti, kimoja kikimtambulisha kuwa mwanafunzi wa Muhas wa Shahada ya Pili ya Udaktari (Masters of Medicine ) yenye jina la Macha Dismas kikionesha kusajiliwa kwa namba 60520/2011 na kumaliza muda wake Septemba 30 mwakani. Kitambulisho kingine kilimtambulisha kwa jina la Macha Rogers anayesoma Shahada hiyo hiyo ikionesha kuwa anamaliza masomo yake mwakani.
 
Alikutwa pia na kitambulisho kinachomwonesha kuwa mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza na kadi ya anuani yenye jina la Amos Nnko ambaye ni Ofisa Rasilimaliwatu wa Chuo hicho.
 
Akizungumzia alivyomkamata askari wa chuo hicho, Fulgence Semfukwe alisema walimkamata baada ya kupata taarifa za yeye kuwa maeneo hayo na kupanga mbinu za kumkamata.
 
Alisema saa 4.45 asubuhi jana alimkuta kwenye jengo la meno na kumwomba kwa nafasi yake ya udaktari amsaidie tatizo lake na hivyo waongee pembeni, naye bila wasiwasi akakubali. Alimwuliza anatibu magonjwa gani naye kumjibu anatibu maradhi ya aina nyingi na kumwomba kitambulisho na yeye kumpa cha kwake.
 
Baada ya hapo alishituka na kudai kuwa ni daktari wa Mwananyamala na amekuja hapo kwa ajili ya kuona wagonjwa wake wa dharura ndipo alipokamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi.
 
Alisema amekuwa akiwachenga kwa muda mrefu kutokana na kuwa kila walipopewa taarifa yuko wodi au sehemu Fulani hawakumkuta kwani walipishana naye baada ya kuvua koti na kuweka kwenye begi lake jeusi.
 
Akizungumza na gazeti hili, Macha limweleza mwandishi wa habari hizi kuwa yeye ni mwanafunzi ambaye anaelewa masuala yote ya matibabu, lakini alifeli chuoni hapo mwaka jana.
 
Alidai kuwa dawa alizokutwa nazo ni zake kwani ana matatizo katika njia ya mkojo na kifua huku akiamua kufanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.
 
“Uwezo wa kutibu ninao na nimesoma katika chuo hiki, lakini mwaka jana nilifeli ndiyo maana nikaamua kuwa hivi,” alisema.
 
Ofisa Uhusiano wa Muhas, Hellen Mtui alisema kutokana na kukamatwa na nyaraka akijitambulisha kuwa mwanafunzi wa ‘Masters of Medicine’, ambaye anaweza kutibu watu hawana uhakika na idadi ya watu ambao ameshatapeli hospitalini hapo.
 
Kuhusu kusoma Muhimbili, Mtui alikana akisema baada ya kupekua nyaraka za chuo hawakubaini jina la mwanafunzi wa aina hiyo na katika vyeti vyake bandia vinaonesha kusainiwa na Mkuu wa Chuo aliyekuwapo kabla chuo hakijapanda hadhi na kuwa chuo kikuu.
 
Mtui alisema baada ya kumkamata na kumpiga picha akiwa na mavazi ya udaktari, kumpekua na kumhoji walimpeleka katika kituo cha Polisi cha Selander Bridge kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.

-Habari leo

Wednesday, 18 September 2013

UTAFITI:SIMU ZA KUPAPASA(SMART PHONE)ZINA UCHAFU MWINGI KULIKO CHOO


Simu  ya  kupapasa.
 Watafiti wamebaini kuwa baadhi ya vifaa vya kisasa vya mawasiliano vinavyotumika kwa kupapasa kama tablet komputa na smart-phones huwa na vijidudu vingi vya uchafu kuliko hata choo.



Bakteria hao huachwa na watumiaji wavifaa hivyo kwa kupapasa vioo vya vifaa kama Apple iPads na Samsung Galaxy tablets kutokana na kutumia bila ya kuosha mikono.
Choo


Moja ya tablet iliyofanyiwa vipimo na taasisi ya kulinda mtumiaji ya Which? ilikutwa na baktaria aina ya staphylococcus aureus ambao hutoa sumu ambayo hupelekea mtu kutapika.
USHAURI:
Kuwa  na  smart phones  ni  sawa  na  kutembea  na  choo  mkononi (  kwa  mujibu  wa  utafiti  huu) ...Tuwe  waangalifu ili  simu  hizi  zisiguswe  na  watoto  wetu.

Tuesday, 17 September 2013

TAMBUA UMUHIMU WA ASALI KATIKA AFYA YAKO


ASALI inafahamika kwa muda mrefu
kama chakula muhimu ambacho pia
kinasaidia sana katika kupambana na
magonjwa mbalimbali na matatizo
yatokanayo na uzee.
Kwa mujibu wa tafiti mpya za
wataalamu wa madawa lishe na vifaa
tiba, imedhihirika kwamba, uwezo wa
asali kutibu unaweza kuongezeka
maradufu kama itachanganywa na
mdalasini.


Aidha, uchunguzi wa kila wiki
unaofanywa na jarida la World News
kuhusu tiba unasema, wataalamu wa
madawa yatokanayo na mimea,
imeonekana kwamba kuna dazani
nyingi za umuhimu wa asali na
mdalasini katika kujenga afya bora.

Asali ikishachanganywa na mdalasini
pamoja na mafuta ya vuguvugu ya
mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa
cha kuotesha nywele kinachotumika
katika dawa ya Dork.

Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa
kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa
dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa
madawa tiba, Dk Alexander Andreyed na
Eric Vogelmann, madhara yaletwayo na
vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza
kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa
matumizi ya mara kwa mara ya chai
iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko
wa asali na mdalasini.

Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema
kwenye jarida mashuhuri
linalozungumzia masuala ya tiba la
nchini Denmark la Julai 1994. Uchunguzi
mwingine pia umeonesha kwamba
matumizi ya kila siku ya asali
yanapunguza viwango vya lehemu
mwilini.

Asali inatajwa pia kuwa dawa ya jino,
inaponya pia ngozi iliyoharibika, ni
dawa asilia ya shinikizo la juu la damu ni
kiungo muhimu katika utengenezaji wa
asilimia kubwa ya madawa mmimiko na
asilimia kubwa ya vipodozi na mafuta ya
kupaka.


Ugonjwa wa mafua ambao huwakera
na kuwanyima watu wengi raha
imegundulika na wataalamu kwamba
hupungua na kupotea kabisa ikiwa
watatumia kijiko kimoja cha chai cha
asali vuguvugu iliyochanganywa na robo
kijiko cha chai cha mdalasini. Mtafiti
mmoja wa Hispania imethibitisha
kwamba, aina ya dawa moja asilia
iliyofanikiwa kuharibu vimelea viletavyo
mafua ilitengenezwa kwa kiwango
kikubwa na asali.

Mchanganyiko huo pia ni mahususi
katika kusaidia kupunguza na kuondoa
chafya na kuvimba kwa koo. Asali
inaaminika pia huamsha hamu ya tendo
la ndoa. Wale ambao mambo katika
eneo hilo si mazuri wanashauriwa
angalau kunywa vijiko viwili vya mezani
kila siku kabla ya muda wa kulala usiku.
Kuna wakati asali ilipigwa marufuku
kwa makasisi katika baadhi ya dini za
Mashariki mwa dunia ili isiwe sababu ya
kuwaongezea mihemko.

Asali inaaminika kuwa dawa ifaayo
katika kuondoa mchafuko wa tumbo
pamoja na kichefuchefu. Ukiwa katika
kadhia hiyo, unashauriwa kuongeza
kiasi kidogo cha mdalasini na asali
kwenye chai ama maji, itapunguza hali
hiyo na maumivu yaletwayo na vidonda
vya tumbo.

Utamaduni wa kula asali pamoja na
mdalasini, huweza kuondoa mchafuko
wa tumbo na utumbo uletwao na gesi
kwa mujibu wa uchunguzi mahsusi
uliofanywa huko India na Japani kwa
miaka mingi. Unaweza kukinga kupata
ugonjwa wa moyo na kuzuia
mkusanyiko wa mtandao wa mafuta
kwenye mishipa ya damu kwa kula asali
na mdalasini mara kwa mara wakati wa
kifungua kinywa.

Kula mkate uliopakwa asali kijiko kimoja
cha mezani kila siku nyuzi nyuzi zake ni
muhimu pia kiafya. Tiba hii, iliweza
kupunguza kuganda kwa mishipa ya
damu kwa asilimia 74 ya wagonjwa
waliofanyiwa utafiti. Shinikizo la damu,
pamoja na matatizo yaambatanayo na
maumivu ya kifua na kizunguzungu
yalitoweka kutoka kwa wagonjwa
wengi wiki chache tu baada ya watafiti
wa Kiitaliano kuwapa dozi za mara kwa
mara za asali iliyochanganywa na
mdalasini.

Kinga ya mwili, itaongezeka mara tatu
zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara
asali na mdalasini kwa pamoja,
wataalamu wanasema. Utafiti wa kitiba
unaonesha kwamba, asali ina hazina
kubwa ya virutubisho na madini pamoja
na michanganyiko mingine iondoayo
magonjwa pamoja na kinga, itolewayo
na chembechembe nyeupe za damu,
husaidia kuzuia magonjwa pamoja na
kuharibu vimelea virusi na bakteria.
Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa
mdalasini kabla ya mlo, huondoa
kiungulia pia. Inasemekana kuwa,
unaweza kuishi hadi miaka 100
ukifurahia maisha ya afya bora na
madhubuti kwa kunywa kila siku
kikombe baridi cha chai iliyowekwa
mdalasini na asali.

Kutengeneza kinywaji
hiki kitamu, weka vijiko vinne vikubwa
vya mdalasini katika vikombe vitatu vya
maji na koroga kwa dakika 10, kunywa
robo kikombe kutwa mara tatu au nne,
watafiti wanasema.

Asali ni tiba rafiki na asilia kwa watu
wenye shida ya chunusi. Ili kutibu tatizo
hilo watafiti wanasema changanya vijiko
vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja
cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi.
Uwezo wa asali wa kuua bakteria
utaufanya uso wako kuwa kawaida
katika muda wa wiki mbili pekee.
Asali, wanasema inairudisha ngozi
iliyoharibiwa na wadudu waharibifu
kama dondola, washawasha na hata
ngozi iliyopata madhara kutokana na
kuungua moto. Pakaa asali na mdalasini
moja kwa moja kwenye sehemu
zilizoathirika na rudia wakati mwasho
unapokuathiri. Rudia tena hadi uvimbe
unapotoweka.

Utafiti uliofanywa karibuni nchini
Australia na Japan, umeonesha kuwa,
asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya
mgonjwa kwa mtu anayetumia madawa
ya kutibu saratani. Katika utafiti
uliofanywa kwa wagonjwa waliokuwa
wanaugua kwa kiwango kikubwa
saratani ya mifupa na tumbo, wale
waliokuwa wakitumia kila siku dozi za
asali na mdalasini, walionesha kupata
nafuu maradufu kuliko wale waliokuwa
wakitumia madawa ya saratani pekee.
“Tuliwapa kijiko cha mdalasini na asali
kutwa mara tatu kwa mwezi,” anasema
Dk Hiroki Owatta. Upo ushahidi mpya
kwamba, sukari asilia zilizopo kwenye
asali, zina uwezo wa kuongeza nishati
mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi
zinaweza kuwasaidia wazee na
wengine wanaosumbuliwa na uchovu.

Wataalamu wanapendekeza
kuchanganya nusu kijiko cha asali katika
nusu bilauri ya maji kisha nyunyizia
mdalasini na kunywa masaa mawili
baada ya kuamka asubuhi. “Kunywa
tena saa 9:00 alasiri wakati nishati
(nguvu) inapoanza kushuka,” anashauri
Dk Milton Abbozza ambaye kazi zake
kuhusu asali na mdalasini kama
kichocheo cha nishati mwilini
zinatambulika kimataifa.

Asali inao uwezo mkubwa wa
kupunguza na kuponya miguu
iliyopasuka kwenye kisigino. Chua asali
na mdalasini vuguvugu katika miguu au
nyayo zilizoathirika baada ya siku ndefu
na kazi au baada ya mazoezi marefu.
Rudia kila siku asubuhi halafu, osha
nyayo zako kwenye maji baridi na vaa
viatu.

Baadhi ya watu Marekani ya Kusini,
wanasukutua maji ya vuguvugu
yaliyowekwa asali na mdalasini kila
asubuhi ili kufanya harufu mdomoni
kuwa nzuri na safi kiasilia. Katika Asia ya
Kusini Mashariki, watu hutumia kijiko
cha mdalasini na asali ili kuondoa harufu
mbaya mdomoni (halitosis).

Wataalamu wanaamini kwamba, uwezo
wa kuua bakteria uliopo kwenye asali
ndiyo unaopigana na harufu mbaya
itokayo mdomoni. Dozi za kila siku za
asali na mdalasini, hufanya hali ya
usikivu murua kwa wanafunzi wawapo
darasani au viongozi mkutanoni kama
ilivyogunduliwa na Wagiriki wa zamani.
Hiyo ndiyo asali. Ni chakula na dawa.

Lakini inayozungumzwa hapa ni asali
mbichi ambayo inapatikana kwa wingi
Tanzania, lakini tatizo ni kubwa ipo pia
feki inayouzwa kama mbichi!

Sunday, 15 September 2013

HATARI:SAMAKI HATARI WAINGIZWA NCHINI KINYEMELA.

                    Dar es Salaam. Afya za Watanzania ziko shakani kutokana na kuwapo kwa biashara ya kuingiza samaki kutoka nje ya nchi, wanaodaiwa kuharibika na kuuzwa katika la Soko la Feri jijini Dar es Salaam.

Samaki hao kutoka Yemen, Dubai, China na Japan, wanaoingizwa nchini wakiwa wameganda kwenye barafu, wengi huharibika muda mfupi baada ya barafu kuyeyuka au baada ya kununuliwa.

Uchunguzi wa gazeti hili umegundua kuwa samaki hao huletwa nchini kutafutiwa soko baada ya kukaa kwenye majokofu kwa muda mrefu huko wanakotoka, kiasi cha kuelekea kuharibika.

Ili wasiharibike, samaki hao aina ya Marckerel hukaangwa hadi wakauke. Uchunguzi zaidi umebaini kuwa wanunuzi wake wakuu ni wafanyabiashara wa chakula wakiwamo wamiliki wa migahawa na Mama Lishe wanaofanya shughuli zao katika miji ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Dodoma.

Samaki hao wanauzwa kwa bei ya chini ambayo ni Sh38,000 kwa boksi lenye uzito wa kilo 15, ikilinganishwa na wanaovuliwa hapa nchini ambao bei yake ni Sh60,000, kwa uzito huohuo.

Inaelezwa kuwa samaki hao baadhi yake ni wale ambao wamekwisha muda wake wa kutumika katika nchi hizo, hivyo kuingizwa nchini kutafutiwa soko.

Gazeti hili lilifika katika soko hilo kwa siku mbili na kushuhudia samaki hao wakiuzwa kwa wingi, huku wauzaji wakihimizwa wateja wao kuwahi kuwakaanga au kuwaweka kwenye jokofu.

Gazeti hili pia lilinunua boksi moja la samaki hao lenye uzito wa kilo 15 kwa Sh38,000, lakini lilipodai kupewa stakabadhi wauzaji walisema: “Hatuna stakabadhi ya kukupa ndugu yangu,” alisema muuzaji.

Baada ya kuwasafirisha kutoka Soko la Feri hadi ofisi za gazeti hili zilizopo Tabata Reli, Barabara ya Mandela kwa muda wa saa moja, tayari walikuwa wameharibika.

Baadhi ya samaki hao walianza kuoza huku wengine wakiwa wamelegea tofauti na samaki wa kawaida. Baada ya saa nne kupita, samaki hao waliharibika na kuanza kutoa harufu mbaya.

Dk Raymond Mwenekano wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, anayataja madhara ya ulaji wa samaki wa aina hiyo kuwa ni kupata magonjwa kama vile kansa ya utumbo, mwili kuwasha, kubabuka na vidonda mwilini.

“Madhara yake ni makubwa, ndiyo maana siku zote tunasisitiza kula vyakula visivyokaa sana kwani vingine vimehifadhiwa kwa dawa na wanaofanya hivi ni wafanyabiashara kwa faida yao,” alisema Dk Mwenekano.

Friday, 13 September 2013

MAREKANI YADAI KUGUNDUA CHANJO INAYO ANGAMIZA VIRUSI VYA UKIMWI


Chanjo ya Ukimwi, siyo iliyogunduliwa na marekani  

Katika majaribio ya chanjo hiyo, wanasayansi hao wameelezea kuwa imeonyesha mafanikio kwa kuangamiza kabisa virusi wanaofanana na VVU kwa nyani.Wanasayansi nchini Marekani wamegundua chanjo ambayo wanaamini itaweza kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa binadamu Katika majaribio ya chanjo hiyo, wanasayansi hao wameelezea kuwa imeonyesha mafanikio kwa kuangamiza kabisa virusi wanaofanana na VVU kwa nyani.
Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limechapisha kwenye tovuti yake kuwa baada ya kubaini hilo sasa wamekusudia kufanya majaribio ya chanjo hiyo kwa binadamu.
Likinukuu taarifa iliyochapishwa kwenye jarida la kisayansi linaloitwa; Nature, lilimnukuu Mwanasayansi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Oregon, nchini Marekani akisema walijiridhisha kuwa chanjo hiyo iliangamiza virusi vyote kwenye mwili wa nyani.
Virusi hao jamii yake inafanana sana na VVU wanajulikana kama Simian Immunodeficiency Virus (SIV) ikiwa na maana ni virusi vinavyosababisha upungufu wa kinga ya kujikinga na maradhi kwa nyani.
Taarifa za kisayansi zinaonyesha kwamba SIV ni virusi ambao wamekuwa wakienea kwa njia ya kujamiiana miongoni mwa vizazi vya nyani na vilibadilika baada ya kuambukizwa kwa binadamu vikawa vimezaa VVU.
Wanasayansi hao wanasema kati ya nyani 16 waliopewa chanjo hiyo, waliyoipa jina la Cytomegalovirus (CMV),tisa walipona kabisa maradhi ya SIV.
Mtaalamu wa Taasisi ya Chanjo na Jeni katika Chuo Kikuu cha Oregoni, ambaye alihusika kwenye utafiti huo, Profesa Louis Picker aliielezea chanjo hiyo kuwa ni ya kutia moyo ukilinganisha na nyingine ambazo zimewahi kufanyika.
“Katika chanjo nyingi ambazo ziliwahi kuonyesha mafanikio ya kuangamiza virusi ni kwamba kuna baadhi ya seli virusi walibakia,” alisema Profesa Picker, akifafanua:
“Lakini kwa chanjo hii tulichunguza sehemu nyingi nyeti katika mwili wa nyani tukagundua kwamba hakuna kirusi aliyebakia.”
Alisema chanjo yao wameiamini kutokana na uwezo wake wa kupenya maeneo mbalimbali ya mwili kiasi kwamba siyo rahisi kirusi kubakia.
Wanasayansi hao walisema kwa kawaida nyani ambaye ameambukizwa SIV hufa ndani ya kipindi cha miaka miwili.-MWANANCHI

TAMBUA UHUSIANO WA KORODANI ZA MWANAUME NA MAJUKUMU KAMA MZAZI

             Wanasayansi wanasema kuwa kuna uhusiano kati ya ukubwa au udogo wa Korodani (Testicles) za baba na uwezo wa baba kutekeleza majukumu yake kama mzazi wa watoto wao.
Watafiti katika chuo kikuu cha Emory nchini Marekani, wanasema kuwa wanaume walio na Korodani ndogo huenda wakayachukualia majukumu yao kwa uzito na hata kujihusisha na kumbadilisha mtoto nepi, kumlisha na hata kumuogesha mtoto.

Pia uligundua kuwa utofauti katika picha ya ubongo wa baba wakitizama picha za waoto wao, ilihusishwa na ukubwa au udogo wa Korodani.
Lakini mambo mengine ya kitamaduni yanaweza kuchangia kwenye uhusiano kati ya Korodani na majukumu ya baba kwa mwanawe.
Uasherati na ukubwa wa korodani zinajulikamna kuwa na uhusiano mkubwa kwa wanyama , wale walio Korodani kubwa hujamiiana na wanyama wengi kinyume na walio na Korodonani ndogo.
Watafiti walikuwa wanachunguza nadharia kuhusu ikiwa wanaume hutumia muda zaidi katika kuwa na mahusiano ya kimapenzi au kulea watoto wao. Wazo lao likiwa kwamba wanaume walio na Korodani kubwa hutumia muda wao katika kuzaa watoto wengi kuliko katika kuwalea watoto hao.
Utafiti huo ulichunguza uhusiano kati ya ukubwa wa Korodani na mfumo wa uzazi katika wananume 70 waliokuwa na watoto walio kati ya umri wa mwaka mmoja na miwili.
Watafiti waliwapiga wanaume hao picha ya ubongo wakiwa wanatizama picha za wanao.
Utafiti wao ulionyesha kuwa wanaume wenye Korodani ndogo walionekana kuwa makini katika malezi kuliko wale wenye kubwa.
Wale waliokuwa na Korodani ndogo walionekana kuwa na wazazi wazuri wanaojihusisha na kubadilisha mtoto nepi na kumuogesha, yaani alijihusisha vyema katika majukumu ya mzazi.
Mmoja wa watafiti alisema kuwa uchunguzi wao unaonyesha kwamba kuna baadhi ya wanaume ambao ni wazazi wazuri tu na ambao wanajihusisha na majukumu ya ulezi kuliko wengine.
Watafiti hao waliona kuwa ukubwa au udogo wa Korodani unaweza kuathiri tabia za mtu, lakini haijulikani kama hatua ya kumpata mtoto hubadili mawazo na mienendo ya baba.

chanzo:bbcswahili

Thursday, 12 September 2013

HUYU NDIYE SAMAKI ANAWEZA KURUDISHA NGUVU ZA KIUME NDANI YA MUDA WA DAKIKA 10 TU

             Endapo utafanikiwa kumla samaki huyu mwenye gamba gumu anayekwenda kwa jina la Oyster basi utakuwa na asilimia 99 ya kuongeza nguvu za kiume ndani ya dakika 10
.Samaki huyu atakurudishia uwezo wako wa zamani kabla mambo hayajaanza kukuharibikia, tena dawa hii ni salama kwa kuwa ni kama chakula tu.Mtaalamu wa mapishi kutoka Culinary Chamber kwa moyo mkunjufu ameamua kushare nasi habari hii njema. Huna nguvu za kutosha kufanya tendo la ndoa? Unakosa kabisa hamu ya kufanya tendo la ndoa? Perfomance imeshuka? "Basi tatizo lako ni 'low T' au low testosterone," na ni tatizo kubwa kwa wanaume wengi.Testosterone ni hormone inayozalishwa katika vifuko vya mbegu za uzazi wa mwanaume, inasaidia sana sana katika kuhamasisha uwezo na msukumo wa tendo la ndoa. Inasaidia sana pia kumaintain strong bones, muscle mass and strength,

Testosterone inaanza kujitengeneza na kuongezeka katika mwili wa mwaume wakati wa adolescence na unapopevuka, na hupoteza ubora au kushuka kiwango hasa pale unapofikia umri wa miaka 30 kwa kiwango cha asilimia 1 kila mwaka.  Kukosa ubora au kushuka kwa kiwango kunasababishwa na stressau mzongo wa mawazo ya maisha, mlo usio kamili, obesity na sababu nyingine. Inaposhuka ndio balaa inapoanza nawe kukosa hamu au kupungukiwa nguvu za tendo la ndoa mfano uume kutosimama imara na kukosa hamu pengine hata kufanya tendo chini ya kiwango kabisa na kusababisha kutomridhisha mwezi wako.Protein, magnesium na madini ya zinc  kwa wingi sana kuliko chakula chochote duniani, ambayo zinc hiyo inasaidia sana kuongeza testosterone, kukuimarisha na kukuza misuli katika mwili, ukakamavu wa hisia za kimwili na kuzalisha manii ya kutosha (sperm). Chakula kingine chenye zinc nyingi kinachoweza kukusaidia ni maini ya kuku na mbegu za maboga.
Juu, ni hatua za kumwandaa samaki huyo
Unaonahiyo nyama baada ya kumfunua samaki huyo
Mtaalamu amechombeza kuwa ukiona kinyaa wakati wa kumla, basi weka chumvi na limao kisha umle taratibu, lakini pia unaweza kumwagia balsamic vinegar au siki kuongeza ladha.Dozi: vipande viwili au vitatu vinatosha kabisa kwa dozi moja na inashauriwa kula mara moja kila baada ya wiki moja. Kama kumla akiwa mbichi inakupa tabu basi nunua wale wa kwenye makopo au wa kuchemsha lakini chonde chonde usile wale wa BBQ au wa kukaanga. Baada ya kazi muulize wife atakupa majibu!!!
Chanzo:hood infotainment

Wednesday, 11 September 2013

HATARIII!!! VYOO VYA KUKAA VINA STAREHE KUBWA LAKINI NI ‘MAJANGA’ KWA WATUMIAJI


            Waswahili husema, ‘nyumba ni choo’, wakiwa na maana kuwa nyumba haiwezi kuwa kamili bila kuwa na huduma hiyo ya choo.

Hata hivyo, pamoja na umuhimu wa choo, lakini si kila nyumba iliyo na choo au hata zile ambazo zina huduma hiyo, basi vyoo ni vibovu, havina hadhi. Zipo aina mbalimbali za vyoo kwa matumizi ya binadamu katika maisha yake ya kawaida.

 
Vyoo vina matumizi mengi ingawa  bado  watu wengi  hasa katika nchi maskini na zinazoendelea ikiwamo Tanzania wanatumia choo cha kuchuchumaa wakati wa kujisaidia, lakini mijini na katika nchi zilizoendelea, wao hutumia vyoo vya kukaa.

Nyumba nyingi mijini na ofisi mbalimbali zinazojengwa hivi sasa, huwekewa vyoo vya kukaa. Hata zile za zamani zinakarabatiwa na kubadilishwa kwa kuwekewa hivi ambavyo vinaonekana vya ‘kisasa’.
Mgunduzi wa vyoo vya aina hii, Thomas Crapper anasema kwa mtazamo wake aliona kukaa wakati wa kujisaidia ni utambulisho wa ustaarabu na maendeleo.

Hata hivyo, madaktari wanapingana naye wakisema kujisaidia katika vyoo vya kukaa kuna madhara kiafya kwa kuwa mkao huo unaweza kuleta matokeo mbalimbali ndani ya mwili.

Utafiti uliofanywa na mtandao wa ‘naturesplatform’ umegundua kuwa matumizi ya choo cha kukaa huweza kusababisha matatizo mbalimbali ikiwemo kansa ya utumbo mkubwa.

Mtaalamu wetu wa afya wa gazeti la MWANANCHI, Samwel Shita anasema, madhara ya vyoo vya kukaa ni makubwa kwani wakati mwingine yanaweza kuwa chanzo cha saratani ya  utumbo mkubwa kutokana na haja kubwa kubaki kwa muda mrefu katika utumbo huo.

Shita anasema mtu anapojisaidia haja kubwa katika choo cha kuchuchumaa, kinasaidia haja yote kutoka kwa sababu ya msukumo unaosababishwa na mkao huo.

“Unapokaa unakuwa umekaa katika choo mwili unakuwa umelegea, hivyo inabidi utumie nguvu kubwa kujikamua kutoa haja, tofauti na unapochuchumaa,” anasema Shita na kuongeza:
“Matatizo huanza hapo, unapojisaidia ukiwa umekaa na kulazimisha kujikamua unaweza kusababisha vimishipa vidogo katika utumbo mpana sehemu ya haja kubwa ya ndani na ya nje kuvimba na maumivu makali husababishwa na ugonjwa unaojulikana kama ‘hemorrhoid,” anasema.

Anasema ‘hemorrhoid’ ni ugonjwa ambao pia huitwa bawasiri. Mgonjwa hupata uvimbe katika njia ya haja kubwa na hivyo kupata maumivu wakati wa kujisaidia na haja yake mara nyingine huambatana na damu.

Aidha, anasema vyoo hivi pia vinaweza kuwa chanzo cha magonjwa yanayotokana na shambukizi katika utumbo  mpana, kitaalamu ‘Inflammatory Bowel Disease’.

“Kila binadamu anapaswa kujisaidia na kuhakikisha haja yote imetoka na kwisha kabisa, inapobakia inaweza kusababisha maambukizi katika utumbo mpana kwa kuwa ule ni uchafu wenye mchanganyiko wa vitu vingi,” anasema Shita.

“Haja kubwa inapokuwa tayari imeshajitengeneza inapaswa kutoka yote, kama itabaki kipindi kirefu inaweza pia kuleta uambukizi katika utumbo mkubwa na hata katika kidole tumbo,” anasema Shita.

“Uchafu huu si tu unaweza kusababisha maambukizi, lakini pia unaweza kuwa chanzo cha saratani ya utumbo mkubwa. Wote tunajua kuwa mkusanyiko wa sumu mbalimbali mwilini unakuweka katika hatari ya kupata saratani, hivyo tatizo hili lisipotafutiwa ufumbuzi mapema linaweza kufikia huku,” anasema Shita.

Daktari  Berko Sikirov kutoka Misri ambaye alifanyia utafiti matumizi ya vyoo vya kukaa anasema kuwa iwapo mtu ana  tatizo la vivimbe vya ‘hemorrhoid’ linaweza kumalizika iwapo ataacha kutumia vyoo vya kukaa.

Hata hivyo, anasisitiza kuwa tatizo hili linaweza kwisha kama litakuwa katika hatua za awali. Kwa wenye tatizo lililokomaa watalazimika kufuata matibabu kulingana na ukubwa wake.

Dk Sikirov anaongeza kuwa mbali na kupata vivimbe, pia mgonjwa anaweza kupata tatizo la kutokupata choo kwa muda mrefu.

Anabainisha kuwa kitendo cha haja kutoka kidogo na nyingine kubakia husababisha kuganda katika ukuta wa utumbo na zoezi hilo huendelea mpaka kuwa tatizo sugu.

“Haja kubwa huganda katika kuta za utumbo, hali hii huifanya haja izunguke kwa muda mrefu na ndiyo tatizo hili huanzia hapa,” anasema na kuongeza:
“Unapojisaidia ukiwa umekaa, ile njia ya haja kubwa huwa kama imejifunga, inabidi utumie nguvu nyingi sasa ukiwa na tatizo hili la kukosa haja kubwa huifanya itoke kwa uchache zaidi,” anasema Dk Sikirov.

Aidha, anasema kupata haja kubwa mara kwa mara ni muhimu kwa kuwa usipoitoa maana yake inazungusha sumu katika damu jambo ambalo ni hatari kwa afya.

Anaongeza kuwa kutopata haja kubwa ni kichocheo chenye uwezo mkubwa wa kusababisha saratani ya utumbo mkubwa na uambukizi katika kidole tumbo.

Tafsiri ya kitabibu inasema hali ya kukosa haja kubwa ni pale mtu anaposhindwa kuipata angalau mara tatu kwa wiki. Hata hivyo, ili ujue afya yako ni njema unapaswa kuwa unapata haja kubwa angalau mara moja kila siku.
Daktari Denis Burkitt aliwahi kuandika kitabu cha maelekezo ya chakula ili kuepuka ugonjwa wa saratani. Katika kitabu hicho alieleza namna ambavyo watu wanaweza kujikinga na saratani za aina mbalimbali.

Akizungumzia saratani ya utumbo mpana pamoja na kuelezea vyakula na aina ya maisha, pia aliwaasa watu kutumia choo cha kukaa ili kujiepusha na tatizo hilo.

Anaeleza kuwa kwa Marekani pekee, watu zaidi ya 150,000 hufa kila mwaka kutokana na ugonjwa wa saratani ya utumbo mkubwa.

Mtaalamu wa Ngozi katika Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya na Tiba Muhimbili (MUHAS), Profesa Kisali Pallangyo anasema matumizi ya vyoo hivyo yanaweza kuwa chanzo cha maambukizi ya magonjwa ya ngozi. Profesa Pallangyo anasema ni rahisi kuambukizwa magonjwa ya ngono na ngozi kwa urahisi pale unapotumia vyoo vya kukaa tofauti na vile vya kuchuchumaa.

Aidha, anayataja  magonjwa yanayoweza kuwambukizwa kwa kutumia vyoo vya kukaa kuwa ni kaswende, harara, mba, kisonono, upele na mengine.

“Mtu mwenye magonjwa ya ngozi au ya ngono, anaweza kuyaacha katika ‘sink’ anapolikalia, hivyo ni rahisi kwa mtu mwingine ‘kuyachukua’ mara atakapokaa wakati wa kujisaidia,” anasema Prof Pallangyo.

Anasema vyoo hivi ni hatari kwa afya hasa pale vinapotumika katika jumuiya na kuongeza kuwa ni bora kutumia vile vya kukaa ili kujikinga na magonjwa.


Source: MWANANCHI