Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

Saturday, 21 September 2013

PICHA ZA TUKIO ZIMA LA REDD'S MISS TANZANIA LILIVYOFANYIKA USIKU WA KUAMKIA LEO...!!


Redd's Miss Tanzania 2013,Happiness Watimanywa akipungia mkono mara baada ya kutangazwa mshindi wa Taji hilo kwa mwaka huu.Kushoto ni mshindi wa pili,Latifa Mohamed na kulia  ni mshindi wa tatu,Clara Bayo.

 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa jukwaani usiku huu wakati wa Onyesho la Taifa la Urembo linalofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.



 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakifungua shindano la mwaka huu kwa kuonyesha ufundi wao wa kucheza muziki. Shindano la mwaka huu ambalo limedhaminiwa na kampuni ya vinywaji Tanzania  ya Tanzania Breweries Limited kupitia kinywaji cha Redds limefanyikia katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam. Jumla ya warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali,vyuo nk wameshiriki.


 Warembo walioingia hatua ya kumi na tano bora. 

 Jaji Mkuu wa Shindano la Redd's Miss Tanzania,Dkt. Ramesh Shah akitangaza Warembo walioingia hatua ya tano bora.

Warembo walioingia hatua ya tano bora,toka shoto ni Happiness Watimanya,Elizabert Peter,Clara Bayo,Lucy Tomeka pamoja na Latifa Mohamed.

GHARAMA ZA MATIBABU MUHIMBILI ZAPANDA MARADUFU.....SASA KUMWONA DAKTARI NI SHILINGI 30,000/=


           Gharama za huduma  za kulipia matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili zimepanda maradufu.
Hatua hiyo inayotekelezwa bila kuwashirikisha wadau na watoa huduma ilianza Septemba mosi mwaka huu na kulalamikiwa na wagonjwa na wafanyakazi.

Kwa mujibu wa tangazo la Mkurugenzi wa MNH, lililobandikwa kwenye ubao wa matangazo wa jengo la mateniti la kulipia huduma  IPPM, inaonyesha kuwa gharama zilipanda kuanzia Septemba 2, wakati notisi hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi ilitolewa Septemba 4.

Wagonjwa wanaolipia matibabu  binafsi Muhimbili  waliliambia gazeti hili kuwa  wateja wanaotumia ‘ast truck’  na huduma ya uzazi inayotolewa na  kitengo cha mateniti- IPPM ndizo zilizoongezeka.
 
Kuanzia sasa upasuaji wazazi  unalipiwa Sh. 500,000 badala ya  350,000 za awali. Uzazi  wa kawaida  ni Sh. 250,000 badala ya  Sh. 150,000  zilizokuwa zikitozwa mwanzo.

Walisema kulala kunagharimu  Sh. 20,000  badala ya 15,000 wakati tozo la kumuona daktari kwa mara ya kwanza  ni Sh. 30,000 badala ya Sh. 20,000 za awali.  

Kumuona daktari kwa ajili ya kufuatilia huduma na matibabu zimepanda hadi Sh. 20,000 kutoka Sh. 10,000.

Huduma nyingine kama dawa na uchunguzi wa maabara 
zimepanda japo bei zake hazikutangazwa  kwenye ubao wa matangazo.

Kwa wagonjwa wa kujifungua kawaida ambao  hawalipii gharama  watatozwa gharama ambazo hazikafafanuliwa ingawaje serikali inataka watibiwe bure.

“Mfano mjamzito akipata uchungu ghafla na kufika Muhimbili bila rufaa atatakiwa kalipia gharama” alisema mjamzito jina tunalo.

Msemaji wa MNH Aminieli Aligaesha, alikiri kuongezeka gharama hizo ziliongezeka  na kuongeza kuwa sababu ya ongezeko  hilo ni gharama kubwa za uendeshaji.

Hata hivyo alikataa kutoa maelezo zaidi na kutaka mwandishi wetu kwenda ofisini kwake   kwa maelezo zaidi.

Hospitali ya Muhimbili inatoa huduma kwa utaratibu wa aina mbili kuchangia matibabu kunakofanywa na mgonjwa wa rufani pamoja na serikali.

Njia nyingine ni  wagonjwa kulipia gharama zote  za tiba kama ambavyo wanafanya kwenye hospitali za binafsi.

Hata hivyo gharama za tiba kwa wale wanaochangia matibabu na wale wa rufaa hazijaongezeka.

"NINA WAKE FEKI WENGI SANA HAPA MJINI".....MZEE MAJUTO


             Majuto anasema kuwa ana watoto tisa ingawa hakuwa tayari kuwazungumzia mama wa watoto hao zaidi ya kumwongelea mkewe wa sasa, Aisha Mbwana kwa kuwa wake zake aliozaa nao baadhi ya watoto kwa bahati mbaya walishafariki dunia.
Alisema kuwa yanapokuja masuala ya familia huwa anapenda azungumze mkewe na kwa ridhaa yake. Kwa mujibu wa Majuto anapenda aitwe mke halali kwa kuwa wake feki anao wengi kupitia michezo ya kuigiza na wengine wenye fikira potofu hutumia picha hizo kutengeneza habari za uongo.
Aisha anaizungumziaje familia yake
Kama kawaida ya wanawake wa Tanga ana lafudhi ya huko ambayo huvutia kuzungumza nao, anaanza kwa kunieleza kuwa alianza kuitwa mke halali wa nguli huyo wa sanaa za maigizo mwaka 1997, walipofunga ndoa .
Anasema kuwa alikutana na nguli huyo maeneo ya Buguruni, Dar es Salaam, ambako alikuwa akiishi na dada yake aliyekuwa kaolewa na rafiki yake mzee Majuto, ‘Mwanachia’ (kwa sasa ni marehemu), ambaye walikuwa wakiigiza pamoja.
Anasema hakuwa na hili wala lile hadi alipoamua kuondoka na kurudi kwao maeneo ya Vingunguti, ambako ndiko walikokuwa wanaishi wazazi wake na kupewa taarifa kuwa posa imepelekwa kwa ajili yake.
Nilipoambiwa kuhusu hiyo posa sikufikiria kama atakuwa ni mzee Majuto kwa kuwa alikuwa ni kama shemeji yangu kutokana na kuwa karibu na shemeji yangu,” anasema Aisha ambaye ni mama wa watoto watatu.
Anaendelea kueleza kuwa siku ambayo wanafamilia walikutana na kumuuliza kama anamfahamu mchumba na kutajiwa jina kuwa ni Amri Athumani, aliuliza mara mbili kwa kuwa alikuwa hamfahamu huyo mtu hadi alipoambiwa kuwa ni King Majuto.
“Kwa mila za Wabondei mchumba wa kwanza anakubaliana na wazazi, halafu binti anapewa taarifa na kwa kuwa wazazi ni wakubwa inabidi binti akubali, na ndivyo ilivyokuwa kwangu nikakubali na kuolewa na Majuto,” anasema mama huyo.
Anaingia kwenye uigizaji kufuata nyayo za mumewe
Aisha anafafanuwa kuwa kabla ya kuolewa na Majuto hakuwa mwigizaji lakini baada ya kuolewa, mumewe huyo alimwingiza kwenye uigizaji na filamu ya kwanza kuigiza na mumewe huyo ni ‘Fukara hatabiriki’.
Mkewe huyo anasema kipindi hicho Majuto alikuwa anafanya kazi bila kuwa na kikundi zaidi ya wanafamilia, hivyo na yeye alikuwa mmoja wao akicheza kama mama na Majuto kama baba.

MAELFU YA WANANCHI WAJITOKEZA KATIKA MKUTANO WA CHADEMA,NCCR, CUF HUKO JANGWANI JIJINI DAR.


     Maelfu  wakazi wa jiji la Dar es salaam  wengi wao wakiwa ni  wafuasi wa vyama vya Chadema ,Cuf na NCCR Mageuzi  wemefurika katika  viwanja vya jangwani kuwasilikza  viongozi wakuu wa vyama hivyo ambapo kwa pamoja viongozi hao  wanapinga  hatua  ya serikali  kuingiza baadhi ya vipengele  katika mswada wa  sheria  ya marekebisho  ya  sheria  ya mabadiliko ya katiba .

Viongozi  hao  wanadai  kuwa  vipengele hivyo vitapelekea kupatikana kwa katiba  ya upande mmoja  na kuongeza kuwa kama mswada huo hautafanyiwa marekebisho, basi  wao  hawatashiriki katika bunge la katiba.
  
Katika viwanja hivyo  ulinzi uliimarishwa kutoka katika vikundi mbalimbali  vinavyomilikiwa na vyama hivyo  huku shamra shamra za huko na kule zikiwa hazikosekani ili mradi kunogesha mkutano.
 

Mwenyekiti wa taifa wa Chadema  na ambaye  ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Mh Freeman Mbowe amewataka watanzania kuacha uoga na wasimame imara kudai katiba bora.
 

Naye mwenyekiti wa Cuf Mh Profesa Ibrahim Lipumba  amesema Tanzani inahitaji katiba ambayo italinda na kusimamia rasilimali za taifa  kuweza kutimia kwa usawa na kuzingatia mahitaji ya watanzania wenyewe.
 
Kwa upande wake mwenyekiti wa NCCR Mageuzi  na mbuge wa kuteuliwa amesema hakuna haja ya kutumia  mabavu  na badala yake ameitaka serikali itumie busara zaidi ili kuweza kufikia  mwafaka wa jambo hili.

WATU WATATU WA FAMILIA MOJA WAUAWA KWA KUNYONGWA NA KUCHINJWA HUKO BUHONGWA JIJINI MWANZA...

                Akiongea  na  ITV, mkuu wa  upelelezi  wa  makosa  ya  jinai  RCO Joseph  Konyo  amesema  kuwa  baba  wa  familia  hiyo  aliyejulikana  kwa  jina  la  Jonas  Lulinga  anaekadiriwa  kuwa  na  umri  wa  miaka  44  ameuawa  kwa  kuchinjwa  na  kisu  huku  mkewe  na  mtoto  wao  mchanga  wakiuawa  kwa  kunyongwa  na  waya  wa  umeme...
Tukio  hilo  linadaiwa  kutekelezwa  majira  ya  saa  nane  usiku  na  mtu  mmoja  ambaye  walimkaribisha  na  kuishi  nae  kwa  siku  nne....
Binti  mmoja  aliyesalimika  anasimulia  tukio  hilo  kwa  kina  katika  video  iliyopachikwa  hapo  chini. 
 

MWANAFUNZI AUWAWA KWA KUCHOMWA KISU MBAVUNI HUKO MUSOMA..

                  MWANAFUNZI mmoja wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Mukendo  Masejo Mashanshu (19) amefariki dunia  akitibiwa katika hospitali ya Mkoa wa Mara,baada ya kuchomwa kisu na kujeruhiwa vibaya sehemu ya ubavuni na kijana mwenzake ambaye akuweza kufahamika mpaka sasa.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Mara  Ferdinand Mtui alisema mnamo septemba  17mwaka huu majira ya saa 11 jioni katika maeneo ya Rwamlimi mjini hapa marehemu alichomwa kisu na kijana mwenzake  na kujeruhiwa vibaya sehemu ya ubavuni upande wa kulia hali iliyompelekea kuvuja damu nyingi na kupelekea kupoteza maisha akiwa kwenye matibabu.

Alisema baada ya kujeruhiwa alifikishwa kituo cha polisi na kupewa PF.3. lakini ilipotimu majira ya saa mbili usiku alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Mara.

Kamanda  Mtui alisema chanzo cha tukio hilo bado alijafahamika na hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo,na kusisitiza kuwa jeshi la polisi linaendelea kumsaka  mtu aliyehusika na tukio hilo na mara atakapopatikana atafikishwa katika vyombo vya sheria kwa ajili ya hatua zaidi

Mtui alitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa  za siri kwa jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo ili kuweza kufanikisha kukamatwa wale wote waliohusika na kuwatakawanafunzi pale wanapoona viashilia vya kutisha uhai kujiepusha kwa kukaa mbali na kutoa taarifa jeshi la polisi kama kuna mtu ama watu wanaotishia uhai.

MTUHUMIWA AJISAIDIA HAJA KUBWA MAHAKAMANI..MATUKIO KATIKA PICHA

               KIOJA cha mwaka kilitokea Jumatano wiki hii katika Mahakama ya Jiji ya Sokoine Drive jijini Dar es Salaam, baada ya mkazi mmoja wa Buguruni, Hassan Omary kujisaidia haja kubwa kizimbani wakati akisomewa shtaka lake la uzururaji.
Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi alikuwa akimsomea shtaka hilo, mbele ya Hakimu Mfawidhi, William Mutaki na alipotakiwa kukiri au kukanusha kosa lake, mtuhumiwa huyo alibaki kimya akiwa amemtumbulia macho hakimu.
Katika hali isiyotarajiwa, mtuhumiwa huyo alionekana akijikamua kama anayejisaidia na ghafla, harufu kali ya kinyesi ikatanda mahakamani hapo.
Hakimu alitahayari kufuatia tukio hilo, kwani aliziba pua yake kwa kutumia koti lake na kuuliza chanzo cha mtuhumiwa kufanya kitendo hicho kortini, lakini katika hali iliyoashiria kama ni kiburi, kijana huyo hakujibu chochote zaidi ya kutazama chini, licha ya swali hilo kurudiwa zaidi ya mara tatu.
Kutokana na kosa hilo ambalo liliharibu na kusimamisha karibu shughuli zote za mahakama kwa muda, Hakimu Mutaki alimhukumu kijana huyo kwenda jela kwa muda wa miezi sita ili kuwa fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo.
Kana kwamba haitoshi, askari waliokuwepo mahakamani hapo walilazimika kumchapa bakora kijana huyo ili kumlazimisha kupiga deki baada ya eneo hilo kuchafuka vibaya kwa kinyesi kilichochanganyika na mkojo.

Friday, 20 September 2013

RAIS KIKWETE AWATOA HOFU WAWEKEZAJI WA MAREKANI KUHUSU TISHIO LA CHINA NCHINI


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Hakuna tishio la China – Rais Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa maslahi ya makampuni ya Marekani yanayotaka kuwekeza katika Tanzania hayataathiriwa na kuwepo kwa China katika uchumi wa Tanzania kwa sababu China siyo moja ya wawekezaji wakuu katika uchumi wa Tanzania kwa sasa.

Rais Kikwete amesema kuwa miongoni mwa wawekezaji wakuu wa uchumi wa Tanzania, China inashikilia nafasi ya 10 huku Uingereza ikiwa inaongoza katika kuwekeza katika Tanzania.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa China ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa misaada ya maendeleo kwa Tanzania lakini siyo katika makampuni ya nchi hiyo kuwekeza katika uchumi wa Tanzania na hivyo nchi hiyo haiwezi kuwa tishio kwa
 uwekezaji wa makampuni ya Marekani.

Rais Kikwete ametoa ufafanuzi huo mchana wa Jumatano, Septemba 18, 2013, wakati alipokutana katika mkutano wa kikazi na Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Mahusiano ya Nje na Bajeti ya Miradi ya Maendeleo ya Bunge la Marekani mjini Washington, D.C., pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati yake.

Katika mkutano huo, Rais Kikwete aliulizwa jinsi gani fedha ya Jamhuri ya Watu wa China katika uchumi wa Tanzania inavyoathiri uwekezaji wa makampuni ya Marekani.

“Napenda kuwahakikisheni kuwa hakuna athari yoyote. China inashikilia nafasi ya 10 katika uwekezaji katika nchi yetu na hivyo siyo miongoni mwa nchi zinazoongoza katika uwekezaji. Nchi ya kwanza kabisa ni Uingereza ikifuatiwa na Kenya, India na Afrika Kusini. Hizi ndizo nchi kubwa nne.”
 
Ameongeza Rais Kikwete: “China iko zaidi katika kutoa misaada ya maendeleo ambako kwa kweli huko ni miongoni mwa nchi zinazoongoza siyo kwenye uwekezaji. Walitujengea TAZARA, wamejenga Uwanja wa Taifa, sasa wanajenga Bomba la Mafuta kutoka Mtwara hadi Dar Es Salaam, watajenga Bandari ya Bagamoyo…yote hii ni kwenye misaada ya maendeleo.”

“Ni msaada wa maendeleo wa China kwa nchi yetu kama tunavyopokea misaada ya nchi nyingine na kama China inavyotoa misaada kwa nchi nyingine. Hivyo, kwa kweli hakuna tishio lolote kwa uwekezaji wa Marekani kutoka kwa Wachina katika Tanzania, sijui nchi nyingine. Kwa Marekani nadhani mtu wa kumwogopa katika uwekezaji katika Tanzania ni Uingereza.”

Wakati huo huo, Rais Kikwete ametoa rambirambi kwa Serikali na Bunge la Marekani kufuatia mauaji ya watu 12 yaliyofanywa na kijana mmoja mwenye umri wa miaka 34 kwenye Kambi Moja ya Jeshi la Maji la Marekani mjini Washington, D.C.,mwanzoni mwa wiki hii.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kwa niaba ya nchi yangu, Serikali na mimi binafsi kutoa salamu zangu za rambirambi kufuatia tukio hili la kusikitisha sana ambako watu wasiokuwa na hatia wamepoteza maisha yao.”

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

20 Septemba, 2013

WANAUME NAO KUMEZA VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO

            Ni dhahiri kwamba wanaume watashtuka, lakini huenda nao wakashiriki uzazi wa mpango bila upasuaji
Vidonge vya uzazi wa mpango vimezoeleka kutumiwa  zaidi na wanawake pekee, kiasi kwamba ni jambo la ajabu kusikia kuwa wanaume nao wanaweza kuvimeza.
Hata hivyo, watafiti mbalimbali wamefanikiwa kutengeneza vidonge vya uzazi  ambavyo vinazifanya mbegu za kiume  katika mfuko wa uzazi wa mwanamume zisiwe na nguvu ya kuweza kutungisha mimba. Utafiti wa dawa hiyo ambao umewaumiza kichwa wanasayansi kwa miaka mingi umewezesha kupatikana kwa vidonge hivyo ambavyo havina vichocheo kama vile wanavyotumia wanawake ambavyo huingia katika mfuko wa mbegu za uzazi na kisha kuzidhoofisha.
Matokeo ya utafiti huo  ambayo yalichapishwa Agosti mwaka huu yanaonyesha kuwa vidonge hivyo vya uzazi kwa wanaume vitazuia kutunga mimba bila ya kuathiri uwezo wa mwanamume kushiriki tendo la ndoa kama kawaida.
Dk James Brander wa Taasisi ya Dana-Farberanasema utengenezaji wa  vidonge vya uzazi wa mpango kwa wanaume  umekuwa na changamoto kubwa kutokana na  upatikanaji wa dawa ambazo zinaweza kuzuia  mfumo wa utengenezwaji wa  seli za mbegu za kiume.
Dawa hizo ziitwazo JQI zilizotengenezwa katika maabara ya Bradner zinafanya kazi kwa kulenga protini maalumu zilizoko katika korodani  ambazo ni muhimu katika uzazi.
Vidonge hivyo vilichanganywa na vichocheo vya ‘Desogetrel’ ambazo huzuia uzalishwaji wa mbegu za kiume.
Profesa Malise Kaisi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Shirikishi Muhimbili (Muhas) ambaye ni Mtanzania wa kwanza kuzalisha watoto kwa njia ya upandikizaji (IVF) anasema ana wasiwasi mkubwa kuhusu dawa hizo kutumiwa kwa wanaume.
“Dawa za uzazi wa mpango ni rahisi kutumiwa na  wanawake kwa sababu wanawake wana mfumo mwepesi kwa dawa kufanya kazi na kuzuia utungishwaji wa mimba,” anasema.
Hata hivyo, Profesa Kaisi anahisi  kwa wanaume itakuwa hatari kwao kutumia dawa hizo kwani kunaweza kusababisha hata kuua kabisa uzalishwaji wa mbegu.
“Wanaume wana maumbile tofauti na mwanamke. Korodani za mwanaume ni kama kiwanda kinachofanya kazi usiku na mchana. Kwa siku moja mwanamume anazalisha mbegu milioni 10,” anafafanua Prof.  Kaisi.
Katika kuzifanyia utafiti, panya dume alipewa dawa hizo, kisha akawekwa pamoja na mwenza wake ambapo  licha ya kujamiiana hata baada ya miezi kadhaa  panya jike hakupata mimba
 Utafiti huo ulibaini kuwa pamoja na kuzuia uzalishwaji wa mbegu, vilevile dawa hizo zilionekana kuwa hazina madhara yeyote kwa kuwa hazina mchanganyiko wa vichocheo vya aina yoyote.
“Hazikuwa na madhara ya vichochezi (hormone). Mwanamume atakayezitumia hatabadilika tabia au mwili kupata mabadiliko yeyote yale” anasema Dk Martin Matzuk, mtafiti mwingine wa dawa hizo.
Dk Matzuk anasema hakuna kinga yeyote nyepesi ya uzazi wa mpango kwa wanaume iliyowahi kugunduliwa tangu kugunduliwa kwa mipira ya kiume miongo kadhaa iliyopita.
Inaelezwa kuwa utafiti huo  ni mkubwa na utakaoleta mapinduzi katika uzazi wa mpango baada ya vidonge vya uzazi kwa wanawake kuonekana na upungufu kadhaa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Cyriel Massawe wa Chuo  Kikuu cha Sayansi ya Tiba Shirikishi Muhimbili , anasema iwapo kweli dawa za uzazi wa mpango zitagunduliwa basizitasaidia wanandoa kujadili namna bora zaidi ya kupanga uzazi.
“Wenza wanapokuwa na uchaguzi wa kutosha wa namna ya kupanga uzazi inawasaidia wote wawili. Kwa mfano kama mama ana matatizo kadhaa, basi baba atachukua jukumu la kutumia vidonge ili kupanga uzazi,” anasema Dk Massawe.
Anasema kwa sasa wanaume wana njia moja tu ya kupanga uzazi ambayo ni mipira ya kiume hivyo basi iwapo njia nyingine zaidi zimepatikana basi itasaidia.
Dk Massawe anasema vidonge vya uzazi wa mpango kwa wanaume  bado vina changamoto kwa sababu ya mfumo wa uzazi wa mwanamume.
“Zile dawa zinatakiwa zikazuie uzalishwaji wa mbegu kwa wanaume kwa hiyo ili kuingilia mfumo wa uzalishwaji na  pindi mwanamume atakapoacha kutumia awe kama kawaida…ni changamoto” anasema.
Hata hivyo, Dk Massawe anasisitiza kuhusu ushirikiano wa wenza katika kupanga uzazi na kusema kuwa, ni suala linalohitaji watu wawili kujadiliana ili kujua ni njia ipi na salama ya uzazi wa mpango.
 Anaongeza kuwa wenza wanapopanga uzazi itawasaidia kuimarisha afya zao, za watoto na hata kupunguza mzigo wa majukumu ambayo hayakutarajiwa.
Utafiti mwingine unaofanana na huu ulifanywa mwaka 2010 ambapo wanasayansi waliwauliza wanawake na wanaume iwapo wanaume wanaweza kutumia dawa za uzazi wa mpango  pindi zitakaposhauriwa na 
 Katika utafiti huo ulioongozwa na Dk JudithEberhardt wa Chuo Kikuu cha Masuala ya Jamii,wanaume, 140 na wanawake 240 waliulizwa kuhusu matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango kwa wanaume.
 Hata hivyo matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa ingawa wanaume wote walisema watafurahi kutumia vidonge hivyo lakini wanawake walipata hofu iwapo wenza wao watakubali kutumia vidonge hivyo au kuvitumia inavyotakiwa ili kuimarisha uzazi wa mpango.
 Katika utafiti huo, wanaume walio kwenye mahusiano ya kudumu walitoa maoni ya kuvikubali vidonge hivyo huku wale walio katika mahusiano ya muda mfupi waliikosoa njia hiyo ya uzazi wa mpango.
Mei 2009, wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Manchester, Uingereza walitumia wanawake na wanaume kuzifanyia utafiti njia za uzazi wa mpango kwa wanaume kujua iwapo zinafanya kazi ipasavyo na zina manufaa.
 Watafiti hao waliwaambia wenza walioshiriki katika utafiti huo kuwa wanaume pekee watumie njia za uzazi wa mpango huku wanawake wakiambiwa kutotumia njia yeyote ili kupima iwapo njia za uzazi wa mpango zinafanya kazi kwa ubora au la.
Hata hivyo, wanaume kadhaa  nchini walioulizwa  iwapo watakubali kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango ikiwemo vidonge na wanaume wanane kati ya kumi, walikataa kutumia njia yeyote ile.
 Mmoja wao,     Edwin Mnzeru anasema, yeye na mke wake hawawezi kutumia njia ya uzazi wa mpango  ya vidonge, mipira ya kiume, wala ya kitanzi   kwa sababu  zina madhara kiafya na ni kinyume na dini.
chanzo:mwananchi

DAKTARI FEKI AKAMATWA HOSPITALI YA MUHIMBILI



              DAKTARI anayedaiwa kuwa bandia amekamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, akiwa na vitambulisho bandia vya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) akisomea Shahada ya Pili.
 
‘Daktari’ huyo ambaye amekuwa akitafutwa na uongozi wa chuo kwa zaidi ya mwaka alikamatwa jana asubuhi akiwa hospitalini hapo karibu na jengo kilimo kitengo cha meno.
Katika kitambulisho chake cha kupigia kura anatambulishwa kwa jina la Dismas John Macha aliyezaliwa mwaka 1979 Kilimanjaro na anaishi maeneo ya Upanga Magharibi, Dar es Salaam.
 
Gazeti hili, lilimshuhudia mtuhumiwa huyo akiwa katika kituo cha usalama cha Muhas na kupekuliwa na askari Polisi wa Muhimbili, Anthony Mwamatepela na kukutwa akiwa na vifaa vya udaktari .
 
Baadhi ya vifaa alivyokutwa navyo ni pamoja na koti jeupe la udaktari na stetoskopu ambacho ni kifaa cha kusikilizia mapafu yanavyofanya kazi na mapigo ya moyo.
 
Pia alikuwa na begi jeusi lenye aina mbalimbali za dawa, vitambulisho na karatasi nyingi, lakini alipoulizwa alidai kuwa hizo ni dawa zake.
 
Macha alikutwa pia na vitambulisho vitatu tofauti, kimoja kikimtambulisha kuwa mwanafunzi wa Muhas wa Shahada ya Pili ya Udaktari (Masters of Medicine ) yenye jina la Macha Dismas kikionesha kusajiliwa kwa namba 60520/2011 na kumaliza muda wake Septemba 30 mwakani. Kitambulisho kingine kilimtambulisha kwa jina la Macha Rogers anayesoma Shahada hiyo hiyo ikionesha kuwa anamaliza masomo yake mwakani.
 
Alikutwa pia na kitambulisho kinachomwonesha kuwa mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza na kadi ya anuani yenye jina la Amos Nnko ambaye ni Ofisa Rasilimaliwatu wa Chuo hicho.
 
Akizungumzia alivyomkamata askari wa chuo hicho, Fulgence Semfukwe alisema walimkamata baada ya kupata taarifa za yeye kuwa maeneo hayo na kupanga mbinu za kumkamata.
 
Alisema saa 4.45 asubuhi jana alimkuta kwenye jengo la meno na kumwomba kwa nafasi yake ya udaktari amsaidie tatizo lake na hivyo waongee pembeni, naye bila wasiwasi akakubali. Alimwuliza anatibu magonjwa gani naye kumjibu anatibu maradhi ya aina nyingi na kumwomba kitambulisho na yeye kumpa cha kwake.
 
Baada ya hapo alishituka na kudai kuwa ni daktari wa Mwananyamala na amekuja hapo kwa ajili ya kuona wagonjwa wake wa dharura ndipo alipokamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi.
 
Alisema amekuwa akiwachenga kwa muda mrefu kutokana na kuwa kila walipopewa taarifa yuko wodi au sehemu Fulani hawakumkuta kwani walipishana naye baada ya kuvua koti na kuweka kwenye begi lake jeusi.
 
Akizungumza na gazeti hili, Macha limweleza mwandishi wa habari hizi kuwa yeye ni mwanafunzi ambaye anaelewa masuala yote ya matibabu, lakini alifeli chuoni hapo mwaka jana.
 
Alidai kuwa dawa alizokutwa nazo ni zake kwani ana matatizo katika njia ya mkojo na kifua huku akiamua kufanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.
 
“Uwezo wa kutibu ninao na nimesoma katika chuo hiki, lakini mwaka jana nilifeli ndiyo maana nikaamua kuwa hivi,” alisema.
 
Ofisa Uhusiano wa Muhas, Hellen Mtui alisema kutokana na kukamatwa na nyaraka akijitambulisha kuwa mwanafunzi wa ‘Masters of Medicine’, ambaye anaweza kutibu watu hawana uhakika na idadi ya watu ambao ameshatapeli hospitalini hapo.
 
Kuhusu kusoma Muhimbili, Mtui alikana akisema baada ya kupekua nyaraka za chuo hawakubaini jina la mwanafunzi wa aina hiyo na katika vyeti vyake bandia vinaonesha kusainiwa na Mkuu wa Chuo aliyekuwapo kabla chuo hakijapanda hadhi na kuwa chuo kikuu.
 
Mtui alisema baada ya kumkamata na kumpiga picha akiwa na mavazi ya udaktari, kumpekua na kumhoji walimpeleka katika kituo cha Polisi cha Selander Bridge kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.

-Habari leo

ANGALIA PICHA YA HAKIMU AKIWA AMELOA DAMU BAADA YA KUCHOMWA KISU MAHAKAMI--SHINYANGA

Hakimu wa mahakama ya mwanzo mkoani Shinyanga achomwa kisu na mlalamikaji baadaya ya kutoa hukumu kwa mtuhumiwa,hakimu huyo alitoa hukumu kwa mtuhumiwa wa wizi wa baiskeli yenye thamani ya 150000 aina ya neria,hukumu hiyo alitoa ikiwa mtuhumiwa hayupo mahakamani mala tu baada ya kutoa hukumu hiyo mlalamikaji aliwashukuru mahakama kwa uamuzi huo kisha akatoka nje baadaye akaingia ofisini kwa hakimu kwa kigezo cha kwamba alisahau kumpatia risti alyonunulia baiskeli baada ya muda kidogo alipoingia alianza kumshambilia hakimu kwa kumchoma kisu sehemu mbalimbali za, mwili wake na baadaya akakamatwa na jeshi la polisi na kisha hakimu kukimbizwa hospitari ya mkoa wa Shinyanga.
Hakimu wa mahakama ya mwanzo mkoani Shinyanga achomwa kisu na mlalamikaji baadaya ya kutoa hukumu kwa mtuhumiwa,hakimu huyo alitoa hukumu kwa mtuhumiwa wa wizi wa baiskeli yenye thamani ya 150000 aina ya neria.CHANZO : MATUKIO NA MICHAPO BLOG

MWALIMU MKUU ANASWA NA MAGUNIA 6 YA BANGI HUKO MKOANI KAGERA...!!


               MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Mukubu, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Silidion Kaiza (43), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na bangi gunia sita.
  
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi alisema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 17, mwaka huu, shuleni hapo katika kata na kijiji cha Muganza majira ya saa tano asubuhi.

  
Alisema kuwa raia wema walitoa taarifa kituo cha polisi Rulenge kwamba kuna mwalimu anajihusisha na biashara ya kuuza dawa za kulevya, jambo walilohofia kuwa huenda akawaathiri wanafunzi wa shule hiyo kwani anazihifadhi shuleni.
  
Kalangi alifafanua kuwa baada ya polisi kupata taarifa hiyo walifika shuleni hapo na kumhoji mwalimu Kaiza, na alikiri kufanya biashara hiyo kisha akawapeleka katika moja ya darasa ambalo alikuwa akitunza bangi hiyo.
  
Kamanda alisema kuwa baada ya polisi kukamata bangi hiyo, waliifikisha kituoni na kwamba mwalimu huyo anaendelea kuhojiwa kisha atafikishwa mahakamani wakati wowote ili kujibu tuhuma hizo.
  
Aliwataka wananchi kuendelea kuwafichua wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya uuzaji wa dawa za kulevya ambavyo vimekuwa tishio kwa taifa.

WAPINZANI WAMTAHADHARISHA KIKWETE....WADAI AKIENDEKEZA KEJELI DAMU ITAMWAGIKA..!!

 
              SIKU moja, baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema anashangazwa na uongo wa baadhi ya wanasiasa kumtuhumu juu ya mambo mbalimbali kuhusu mchakato wa Katiba Mpya, viongozi wa vyama vitatu vya upinzani wameibuka na kusema madai hayo hayana msingi wowote.

Viongozi hao ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) na James Mbatia (NCCR-Mageuzi).

Wakizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana muda mfupi baada ya kumalizika kikao kati yao na viongozi wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, walisema endapo Rais Kikwete atasaini muswada huo kwa kutegemea nguvu ya dola, ataingiza nchi kwenye machafuko.

Kwa upande wake Mbowe, alisema kama Rais atachukuliwa mzaha na kuamua kusaini muswada huo bila kufikiria maslahi mapana ya taifa, nchi itaingia kwenye machafuko na kamwe nguvu ya dola haiwezi kushinda nguvu ya umma.

“Tunarudia kumshauri na kumsihi Rais Kikwete, Katiba ni haki ya Watanzania wote inahitaji busara, ushirikiano, uvumilivu, staa, kuangalia maslahi, kuaminiana na vitu vingine kama hivyo.

Kama atapuuza na kuanza kukejeli malalamiko yanayotolewa na makundi mbalimbali na kuamua kusaini, hakika taifa litaingia kwenye machafuko, hawezi kupuuza Shura ya Maimamu yenye Waislamu wengi na makundi mengine.

“Kamwe hatuwezi kupiga magoti kwa kuomba Katiba Mpya, hii si zawadi kwa wanasiasa na hatupiganii kupatikana kwa Katiba nzuri kwa maslahi yetu wenyewe, bali kwa Watanzania wote, ndio maana nasema hatuwezi kuomba, tunataka Katiba Mpya iliyoshirikishwa makundi yote.

“Katika suala hili, kuna uwezekano wa kutokea shari au heri,
lakini kwa upande wetu hatupo kabisa kwenye shari bali tunataka pawepo na heri kwa kufungua milango, ili kila kundi lisikilizwe na lipate uwakilishi sehemu pale panapowezekana,” alisema.

Kwa upande wake, Profesa Lipumba alisema Rais Kikwete ameanza kuonyesha mwenendo ambao si mzuri kwa maslahi ya taifa.

“Kwanza naomba niseme, Rais Kikwete kawadanganya Watanzania huko Califonia nchini Marekani kupitia jumuiya yao, kule amekwenda kupumzika, asitumie nafasi hiyo kuficha ukweli.

“Tunasema yeye anadanganya, kuliko baadhi ya wanasiasa hao anaowasema, tunataka atambue Katiba ni ya Watanzania wote na sio ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),” alisema.

Naye, James Mbatia wa NCCR Mageuzi, alisema kama Rais Kikwete anadai ametumia mapendekezo ya wadau kuteua wajumbe, anapaswa kumweka wazi anayewakilisha kundi la walemavu.

Alisema Shirikisho la Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA), lilipendekeza majina matatu ili achaguliwe mmojawapo, lakini wote walitupwa nje na kulifanya kundi hilo kujiona halina umuhimu ndani ya jamii.

“Kama kweli anajua ameongozwa na mapendekezo hayo, asimame atueleze kila kundi limewakilishwa na nani, yapo mambo mengi tunayolalamikia tunataka haki itendeke kwa kila Mtanzania,” alisema.

Kwa upande wake, Amiri Mkuu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Mussa Yusuph Kundecha, alisema wameungana na upinzani kudai Katiba iliyokidhi matakwa ya Watanzania.

“Tumejadiliana na kuafikiana kuungana, ili Katiba ipatikane yenye mawazo ya makundi yote, kwa bahati nzuri malalamiko yetu Waislamu yamekuwa na uwiano sawa na malalamiko ya wapinzani.

Sasa kama wote tumekutana na wazo au shida moja, lazima tuamue tufanye nini ili tupate jibu, sasa tunataka muswada urudi bungeni ujadiliwe upya ili kuondoa upungufu uliopo na vipengele vilivyochomekwa kinyemela.

Juzi Rais Kikwete akiwa Marekani alisema anasikitishwa na baadhi ya wanasiasa kueneza uongo kwa kudai hakufuata mapendekezo ya wadau katika kuteua wajumbe, jambo ambalo analipinga.


-Mtanzania

TAHADHARI TOKA JWTZ KUHUSU UVUMI WA"AJIRA ZA WATAALAMU JESHINI"



          Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kuwataarifu Wananchi wote kuwa taarifa zilizoenea kwa njia ya ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu za mkononi (sms) na mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba JWTZ limeanza kuajiri wataalamu Jeshini (Professionals) siyo kweli na halina utaratibu wa kutangaza ajira kupitia mitandao ya kijamii au kupitia simu za mikononi.

Kwa kawaida, utaratibu wa kujiunga na Jeshi hutangazwa kwenye Vyombo vya Habari pale ambapo Jeshi linahitaji kuandikisha askari wapya. 


 JWTZ huelekeza utaratibu wa kuzingatia katika kuwasilisha maombi husika kwa taarifa hii, wananchi wote wanatahadharishwa kuhusu ujumbe huo unaoelekea kusababisha usumbufu kwa wananchi na JWTZ.  

Taarifa hiyo haijatolewa na JWTZ hivyo wananchi wajihadhari na yeyote atakayejitokeza kuwarubuni na hatimaye kutapeliwa kwa namna yoyote.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi
Dar es salaam,
Tanzania

Thursday, 19 September 2013

MAANDAMANO YA WAPINZANI YAPIGWA MARUFUKU

            Jeshi la Polisi Jijini Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya umoja wa vyama vya CUF, NCCR na CHADEMA siku ya Jumamosi yaliyokuwa yamepangwa  kuanzia Tazara hadi Jangwani na Mwenge hadi Jangwani na sehemu mbalimbali ...

Taarifa  iliyotolewa  na kamanda Kova  kupitia  ITV   imeeleza  kuwa  Polisi wamechunguza na kugundua kwamba  maandamano  hayo  yataleta usumbufu kwa watu wengine na kwamba kwa kuwa lengo ni kufika Jangwani basi Viongozi wa vyama hivyo wawaambie wafuasi wao waende Jangwani bila Maandamano.

Source: ITV

SITTA AWATETEA WAHAMAJI HARAMU.



Ataka operesheni ifanywe kibinaadamu

• Ahoji kama Watanzania nao watafukuzwa itakuaje

Na Fatuma Kitima,DSM

WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, ametoa wito kwa mamlaka zinazohusika katika operesheni ya kuwasaka wahamiaji haramu kutumia ubinadamu zaidi katika utelezaji wa zoezi hilo.

Hayo yalisemwa jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Sitta alikiri kuna mapungufu katika zoezi hilo na kusema amri ya rais inatakiwa kutekelezwa lakini kwa kuzingatia haki za binaadamu.

Alisisitiza kuwa ubinadamu utumike kwa kuwa baadhi ya wahamiaji hao, wana familia na wamewekeza nchini kwa muda mrefu.

“Baadhi yao wana familia, mali zao sasa endapo atachukuliwa tu ataenda wapi,” alihoji.

Alisema suala hilo linahitaji kufikiriwa kwa kina na kuhoji jee itakuwa vizuri kama Watanzania wanaoishi mipakani mwa nchi jirani nao watafukuzwa.

Kuhusu Tanzania kutoshirikishwa katika mikutano ya wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Sitta alisema nchi hizo zina haki ya kufanya mikutano na kushirikiana katika baadhi ya mambo kwa mujibu wa mkataba iwapo nchi moja itakuwa haijawa tayari kushiriki lakini akasema wanachoomba ni ushirikishwaji.

Alisema kwa sasa Tanzania haijakubaliana na nchi nyengine wanachama wa Afrika Mashariki kuwa ifikapo Oktoba 15 rasimu ya shirikisho iwe tayari jambo ambalo haliwezekani kwa haraka kwakuwa bado kuna mambo matatu hayajatelezeka katika makubaliano.

Aliyataja mambo hayo ni makubaliano ya ushuru wa pamoja, soko la pamoja na mfumo wa sarafu moja.

APATA MATESO MAKALI BAADA SANGOMA KUNG'OA VYUMA ALIVYOWEKEWA HOSPITALI NA KUSABABISHA MGUU KUOZA...!!


          HAYA ni mateso 100%! Dereva mmoja wa boda boda mkazi wa Kimara King’ongo jijini Dar es Salamaa anayejulikana kwa jina la Joseph Nyunza, yupo katika mateso makali yaliyosababishwa na Sangoma aliyeng’oa vyuma alivyowekewa hospitalini na kusababisha mguu wake kuoza.
Akizungumza na gazeti hili akiwa hoi kitandani nyumbani kwa shangazi yake, Joseph alisema awali alikuwa dereva wa pikipiki lakini Julai mwaka huu, alipata ajali maeneo ya Kimara Suka jijini Dar es Salaam baada ya kugongwa na gari lililohama njia na kumvunja mguu wake wa kulia.
Baada ya kupata ajali hiyo, alikimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alipokelewa na kupelekwa katika kitengo cha mifupa (Moi) ambako baada ya kufanyiwa vipimo, iligundulika kuwa mfupa mkubwa wa mguu wake ulivunjika, hivyo kuwekewa vyuma ‘antena’ ili uweze kuunga. Aliruhusiwa kurudi nyumbani huku akitakiwa kurejea tena hospitalini kwa ajili ya upasuaji.
Baada ya kurejea nyumbani na kukaa wiki kadhaa huku akitembelea magongo, alikosa fedha za kurudi hospitalini kwa ajili ya upasuaji ndipo alipojitokeza mganga wa jadi aliyemtaja kwa jina la Mama Sura aliyeahidi kumponya kidonda hicho.
Mganga huyo alimpaka dawa zake kwa siku kadhaa lakini hakuona nafuu yoyote. Kuona hivyo, Sangoma huyo alishauri kuondolewa kwa vyuma hivyo vya kitaalamu vingeuwezesha mguu huo kuunga vizuri.
“Kweli, siku iliyofuata mganga wangu alikuja na mtu mwingine, akanitoa vyuma bila ganzi, niliumia sana lakini nilivumilia kwa sababu alinihakikishia ningepona.
 “Kadiri siku zinavyozidi kwenda ndiyo mguu unazidi kutoa wadudu wa chooni, jamani ninaomba mnisaidie Watanzania wenzangu, ninateseka sana mimi,” alisema Joseph.
Alisema baada ya kutolewa vyuma hivyo, aliendelea kupakwa dawa hizo za kienyeji kiasi kwamba hadi sasa mguu umeoza na unatoa funza huku kijana huyo akiwa hawezi hata kunyanyuka kitandani.

MGANGA ANASEMAJE?
Baada ya mapaparazi wetu kuzungumza na Joseph walimtafuta mganga huyo ambaye pia anaishi maeneo ya King’ong’o, hakuwepo nyumbani lakini alipatikana kwa njia ya simu.
“Mimi sijamkuta na hali hiyo aliyonayo sasa, naamini anaendelea vizuri na atapona kwa sababu nimeshawatibu watu wengi sana wa aina hiyo, mbona sasa hivi ana nafuu, muulizeni mwenyewe atawaambia,” alisema

MWENYEKITI ANENA
Naye Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King’ong’o, Demetrius Mapesi amekiri kupokea taarifa hizo kwa masikitiko na kuanzisha harambee ya kumsaidia kupitia namba 0654 880707.

HAKIMU ACHOMWA KISU MAHAKAMANI WAKATI AKITOA HUKUMU HUKO SHINYANGA

 
            Hakimu wa mahakama ya Mwanzo mjini Shinyanga Mheshimwa Nyanguoa Masaba amejeruhiwa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali akiwa Mahakani akitoa  hukumu.

Tukio hilo limetokea leo katika mahakama ya mwanzo mjini Shinyanga.

Hakimu huyo alijeruhiwa na mlalamikaji katika kesi ya wizi wa Baiskeli wakati akitoa hukumu.

Tukio hilo limesababisha mahakama hiyo kusimama kumnusuru hakimu huyo na kumkimbiza katika hosptali ya Mkoa kwa matibabu.

Mtuhumiwa wa tukio hilo Emmanule Zenge naye alijeruhiwa kwa kipigo na kupelekwa katika hosptali ya Mkoa.

Jeshi la polisi mkoani shinyanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.


Star Tv

UGOMVI WA MIAKA 20 ILIYOPITA KATI YA KANISA LA EAGT NA TAG WAIBUKA UPYA BAADA YA ASKOFU KULOLA KUFARIKI



           Kanisa la Evangelistic Assemblies of God (EAGT) linatarajia kuuanza mwezi ujao kwa machungu mapya kabisa huku yale ya kuaga dunia kwa aliyekua Askofu wake mkuu Askofu Moses Kulola yakiwa  hayajapoa.....

 Kanisa hilo linatakiwa kusimama mahakamani mwezi ujao Oktoba 1 kujitetea ili waumini wake wasiondolewe kwenye kanisa la Bugando ambako askofu Kulola amezikwa. 
 
Chanzo kimojawapo cha habari kimeeleza kwamba, licha ya kanisa la Tanzania Assemblies of God TAG kugonga mwamba lilipojaribu kuzuia mahakamani askofu Kulola asizikwe hapo , bado shauri la TAG kutaka EAGT waondolewe lingalipo na litakuwepo mahakamani kama kawaida.. 

Shauri la  kesi  hiyo  lenye nambari 121/2013 lilifunguliwa mwaka huu  kabla ya  kifo  cha Askofu Kulola .Kwa  mujibu  wa  maelezo ya Askofu Mkuu wa TAG Dkt. Barnabas Mtokambali , kesi hiyo ni ya kudai kanisa la Bugando  na ni mwanzo wa tu katika kudai mengine mengi. 


Hili  ni  kaburi la Askofu Dr.Moses Kulola  lililojengwa katika kanisa la EAGT Bugando. Pichani  ni Rais Jakaya Kikwete alipoongoza maelfu ya wakazi wa Mwanza na mikoa mbambali katika mazishi ya Askofu Dr.Moses Kulola

EAGT inatetewa na wakili Deocles Rutahidurwa wa Rwelu Attorney,Mwanza

Kwa mujibu wa nyaraka za TAG makanisa mengine yaliyoko kwenye orodha inayotakiwa EAGT wayaachie ni pamoja na yale yaliyopo Tabora, Dar es Salaam,Mbeya,Arusha ,Shinyanga,Tanga,Mwanza,Morogoro,Pwani,Singida,

Kilimanjaro, na maeneo mengine nchini.

Kwa Dar es Salaam makanisa yanayotakiwa na TAG ni pamoja na kanisa la Temeke ambako mwili wa wa marehemu Kulola uliagwa kwa mara ya kwanza kabla ya kusafirishwa kwenda Mwanza.
 


 Katibu mkuu wa Kanisa la EAGT Mch.Brown Mwakipesile

Akielezea namna ambavyo kanisa la EAGT wamejiaandaa na changamoto hiyo, katibu mkuu wa Kanisa la EAGT Mch.Brown Mwakipesile amesema kwamba:


''Kwetu sisi tatizo hilo ni dogo,ni kubwa kwenu ninyi waandishi,,kwani hiyo ni kesi ya kwanza wao kufungua dhidi yetu mbona bado tunaendelea kuabudu kwenye makanisa hayo,,hujiulizi??? ''

"Ikiwa Yesu alipelekwa mahakani sisi ni kina nani hata tuogope kushitakiwa,,sisi kama EAGT tupo tayari kwa chochote ambacho Mungu ataruhusu kitupate''

Upya wa kesi hiyo hiyo iliyofunguliwa na TAG baada ya kupita miaka 21 tangu makanisa hayo yagawanyike kutoka Assemblies of God (AG) na kuwa Tanzania Assemblies of God na Evangelistic Assemblies of God ni ishara kwamba kwa  sasa TAG ina mtazamo mpya na kusudio thabiti la kuyadai makanisa hayo chini ya Askofu mkuu wa TAG Barnabas Mtokambali tofauti na maaskofu waliotangulia.




Askofu Mkuu wa TAG Barnabas Mtokambali

Mapema mwezi huu wa September , Askofu Mkuu wa TAG Barnabas Mtokambali ilieleza alitoa  kauli  ifuatayo  akielezea  msimamo  wa  kanisa  lake.



"Mila za kiafrika mtu akizikwa pale pale panakuwa kwake. Sasa tukasema kama tukikaa kimya hili likatokea baadae huko mbele tutasema nini ,.. tutajibu nini kwa sababu kanisa sio langu kanisa ni la general Council ..

"Mimi nawajibika kama mwenyekiti wa bodi ya wadhamini kwa wachungaji wote. Halafu sisi tutaondoka watakuja watoto hapa na wanataka kuchukua kanisa lao  ambapo tayari  kuna kaburi pale.Tusipokuwa makini watu wakachinjana hapo baadae.
 

"Lakini nawaambieni ukweli hakuna mtu aliyefurahia kama mimi kwa mzee kulola kuzikwa Bugando .Mimi nimefurahi sana   na naomba muandike hivyo ndugu waandishi, nimefurahi sana Mzee kulola kuzikwa Tanzania Assemblies of God Bugando. (TAG ).

"Mzee kwa Heshima zote ameanza kazi Tanzania Assemblies of God mwaka 1968 , mzee akaombwa na EAGT uongozi. Kwa busara yao kubwa na nzuri wameona alipoanzia ndio apumzishwe, amerudishwa nyumbani amerudishwa nyumbani baba yetu . 


"Mimi kama TAG na kama mwenyekiti wa bodi ya wadhamini lengo letu ilikua ni kuweka records  sawasawa kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo kuzuia maafa makubwa yanayoweza kutokea baadae.

"Lakini haikua  nia yangu kuzuia Mzee Kulola kuzikwa pale . Hata kesho tutakaporudishiwa lile jengo   na  kupewa umiliki  kwa asilimia 100, mtu akitaka kuja kumuondoa  mzee Kulola nyumbani mimi nitaweka stop order usimuondo." 


 -Baraka  Samson wa mjap blog.