Wanamuziki 11 mahiri wa BongoFleva wameshirikiana kuimba wimbo kuhamasisha wadau kushirikiana ili 'KUTOKOMEZA ZERO' ambazo sasa zimezoeleka kwenye sekta ya elimu katika ngazi zote, kuanzia shule za msingi mpaka vyuoni.
Wanasema kwamba mwanafunzi akitoka na Zero shuleni hawezi kutimiza ndoto zake. Kwani uongo? Kala Jeremiah, mshindi wa tuzo tatu za mziki wa KILI anamalizia wimbo kwa kuwaasa vijana kwa kusema: PANDA MBEGU BORA, KITABU NDIYO MAISHA YAKO.
Wasanii walioimba wimbo huo ni: Linex, Roma, Linah, MwanaFA, Mwasiti, Stamina, Diamond, Maundo Zoro, Peter Msechu, Keisha na Kala Jeremiah.
SIKILIZA HAPO CHINI:
Showing posts with label ELIMU. Show all posts
Showing posts with label ELIMU. Show all posts
Saturday, 21 September 2013
Friday, 20 September 2013
MWALIMU MKUU ANASWA NA MAGUNIA 6 YA BANGI HUKO MKOANI KAGERA...!!

MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Mukubu, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Silidion Kaiza (43), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na bangi gunia sita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi alisema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 17, mwaka huu, shuleni hapo katika kata na kijiji cha Muganza majira ya saa tano asubuhi.
Alisema kuwa raia wema walitoa taarifa kituo cha polisi Rulenge kwamba kuna mwalimu anajihusisha na biashara ya kuuza dawa za kulevya, jambo walilohofia kuwa huenda akawaathiri wanafunzi wa shule hiyo kwani anazihifadhi shuleni.
Kalangi alifafanua kuwa baada ya polisi kupata taarifa hiyo walifika shuleni hapo na kumhoji mwalimu Kaiza, na alikiri kufanya biashara hiyo kisha akawapeleka katika moja ya darasa ambalo alikuwa akitunza bangi hiyo.
Kamanda alisema kuwa baada ya polisi kukamata bangi hiyo, waliifikisha kituoni na kwamba mwalimu huyo anaendelea kuhojiwa kisha atafikishwa mahakamani wakati wowote ili kujibu tuhuma hizo.
Aliwataka wananchi kuendelea kuwafichua wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya uuzaji wa dawa za kulevya ambavyo vimekuwa tishio kwa taifa.
CCM YATOA MIEZI 6 KWA WAZIRI WA ELIMU KUJIUZULU..!!
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa kujiuzulu kwa kushindwa kulipa madeni ya walimu nchini.Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana pia ametoa muda wa miezi sita kwa Waziri huyo na Naibu wake Philip Mulogo kutekeleza hilo agizo hilo vinginevyo chama kitawatumia wabunge wake kuwatimua kwa nguvu.
Kwa mujibu wa taarifa za madeni zilizokusanywa na Chama cha Walimu Tanzania (CWT), hadi sasa walimu wanadai malimbikizo yao ya Sh bilioni 49 ambayo hajalipwa na Serikali.
Kinana alikuwa akihutubia mikutano ya hadhara jana katika wilaya za Bariadi na Busega.
Alisema CCM haiko tayari kuona walimu wakinyanyaswa wakati wana madai ya msingi.
Hivi sasa imejengeka tabia kwa baadhi ya mawaziri na watendaji wa wizara ya kuwadharau walimu na hata kuwanyanyasa huku wengine wakishusha utu na heshima ya walimu kwa kuwatukana, alisema.
Kinana ambaye yupo katika ziara ya mikoa ya Kanda ya Ziwa alisema kwa mawaziri kushindwa kutatua kero za walimu, imefika wakati wahusika waondoke wenyewe na wasipofanya hivyo chama kitawaagiza wabunge wake wawafukuze kwa nguvu.
“Ninatoa muda wa miezi sita kwa Waziri wa Elimu na wasaidizi wake wakiwamo watendaji kuhakikisha wanalipa madeni ya walimu haraka. Haiwezeni hii ni nchi ya watu wote wakiwamo walimu wadharauliwe na hata kunyanyaswa kwa maneno ya matusi
“Hili hapana CCM haiko tayari kuona walimu kila siku wakipigwa danadana kutokana na uzembe wa watu waliokabidhiwa dhamana za kuongoza sekta ya elimu katika nchi yetu,” alisema.
MTANZANIA ilimtafuta Katibu Mkuu wa CWT, Ezekiah Oluoch ambaye alisema hadi sasa madeni ya walimu yamefikia Sh bilioni 49 ambayo ni malimbikizo ya mishahara na mapunjo.
“Kila mara tunawaambia kuwa ni vema Serikali itafute Sh bilioni 100 katika fungu la dharura ili iweze kulipa madeni ya walimu na iachane nao lakini hawasikii,” alisema Oluoch.
-Mtanzania
Tuesday, 17 September 2013
SEKONDARI YA ILBORU VIPAJI MAALUM YAFUNGWA KWA MUDA USIOJULIKANA KWA HOFU YA KUCHOMWA MOTO...
SHULE ya Sekondari ya Ilboru, jijini Arusha imefungwa kwa muda usiojulikana kuanzia leo baada ya kuwepo hofu ya kuchomwa moto.
Uchunguzi wa madai ya shule hiyo kuchomwa moto, unaendelea kufanywa huku ikielezwa kwamba wanafunzi wanne wanahojiwa na polisi wilayani Arumeru wasaidie kubaini ukweli juu ya madai hayo.
Wanafunzi wengine 10 inadaiwa wamepewa barua za kusimamishwa shule kwa siku kadhaa wakihusishwa na suala hilo.
Tangazo la kufunga shule hiyo lilitolewa ghafla leo asubuhi na Mkuu wa Shule, Julius Shila baada ya kushauriana na bodi yake, huku polisi wa kawaida wakifanya doria kudhibiti vurugu zozote ambazo zingeweza kutokea.
Ingawa Mkuu wa Shule, Shila hakutaka kuzungumzia suala hilo, Kaimu Ofisa Elimu wa Mkoa, Sifael Mollel, alisema uchunguzi wa madai hayo unaendelea katika kipindi hiki ambacho wanafunzi wamepewa likizo.
Alisema kuwepo kwa hofu hiyo na wasiwasi wa kuzuka vurugu ndiko kulikosababisha shule ifungwe kwa muda licha ya kwamba walikuwa hawajamaliza mitihani.
“Uongozi umeamua wanafunzi warudishwe nyumbani kutokana na hofu ya kuchomwa moto shule, wanafunzi walikuwa wakifanya mitihani kabla ya kuanza likizo fupi lakini uwepo tishio hilo na kuzuka kwa vurugu, ilionekana ni vema ikafungwa,” amesema.
Alisema kwa kawaida likizo fupi ni ya siku 10 lakini kwa tukio hili wanafunzi hao wamepewa maelekezo ya kwenda kuonana na wakuu wa wilaya zao kwa udahili kabla ya kurejea tena shuleni.
Akizungumzia vitisho vya moto, alisema wanafunzi hao waliwasilisha barua ofisini kwake wakitoa madai kuwa baadhi ya walimu walikuwa wanataka kuchoma moto shule hiyo.
Alisema polisi walienda kufanya uchunguzi Ijumaa ambapo walinusa harufu ya petroli iliyokuwa imemwagwa jirani na bweni.
Hata hivyo Kaimu Ofisa Elimu huyo hakutawataja wanafunzi ambao wanahojiwa na polisi wala wanafunzi 10 ambao wamesimamishwa kwa siku 21.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Liberatus Sabas, alikiri polisi kuwepo shuleni hapo wakati tangazo la kufungwa shule likitolewa akasema hiyo ilikuwa ni kwa sababu ya kuimarisha usalama.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, wanafunzi wote watatakiwa kurejea shuleni hapo baada ya kudahiliwa na wakuu wa wilaya zao.
MWALIMU ANASWA AKIWAFANYIA WANAFUNZI MTIHANI WA DARASA LA SABA HUKO IRINGA...!!

Jeshi la polisi mkoani Iringa linamshikilia mwalimu wa shule ya msingi Makungu wilaya ya Mufindi Bw Edwin Ambukile kwa tuhuma za kuwasaidia majibu wanafunzi wa darasa la saba katika mtihani wa Taifa wa kuhitimu elimu ya msingi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Bw Ramadhan Mungi (pichani) amesema kuwa tukio hilo limetokea Septemba 15 mwaka huu.
Alisema kuwa mwalimu huyo ambae ni mwalimu wa masomo ya Sayansi katika shule hiyo pia alikuwa ni mwalimu wa masomo ya ziada ( katika shule hiyo na sababu ya kuwasaidia wanafunzi majibu ni kutaka kupata umaarufu kwa wanafunzi watano aliokuwa akiwafundisha masomo ya ziada aliopata kuwaahidi kuwa watafaulu mtihani huo.
Alisema kuwa mwalimu huyo tarehe 11 septemba alipokea mitihani kutoka kwa msimamizi na baada ya hapo akafungua bahasha ya masomo ya Sayansi na kuanza kufanya mwenyewe na majibu kuyatuma kwa Sms kwa mke wake .
Hata hivyo siku ya mtihani mmoja kati ya wanafunzi waliopata majibu hayo alipoingia katika chumba cha mtihani alionekana akitetemeka kupita kiasi na hivyo msimamizi wa mitihani alipompekua alimkuta na majibu hayo na kueleza jinsi alivyosaidiwa na mwalimu huyo .
Kamanda wa polisi alisema siku ya mtihani mwalimu Ambukile alipangiwa kusimamia shule ya msingi Igomaa na sasa amekamatwa na atafikishwa mahakamani wakati wowote kuanzia sasa.
MAMA SALMA KIKWETE ATOA WOSIA MZITO KWA WANAFUNZI WA KIKE...

MKE wa Rais Mama Salma Kikwete amewataka wanafunzi wa kike kujiepusha na 'mafataki' wanaotaka kuwarubuni kwa vitu mbalimbali ili kujikinga na hatari ya kupata ujauzito na ugonjwa wa Ukimwi na kusababisha kutofikia malengo katika maisha yao.
Pia amewataka wanafunzi wa kiume kuachana na tabia ya kuvaa suruali milegezo na uvutaji wa sigara ambao utawasababishia kupata ugonjwa wa saratani ya koo na mapafu.
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema hayo hivi karibuni wakati akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Msimbu iliyopo Kata ya Msimbu Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani.
“Kama wazazi wenu hawawasimamii kufuatilia mienendo yenu mjisimamie nyinyi wenyewe kwa kukanyana na kutoa taarifa kwa walimu wenu pale ambapo mtaona mwenzenu ana tabia ambazo ni kinyume na maadili ya mwanafunzi kwa kufanya hivyo mtaepukana na tatizo la mimba za utotoni’, alisema Mama Kikwete.
Kuhusu madai ya wanafunzi hao kuwa wazazi wao wanakabiliwa na tatizo la umasikini jambo ambalo linawafanya waweze kuingia katika vishawishi mbalimbali Mama Kikwete alisema umasikini isiwe ni kigezo cha mtu kufanya mambo yasiyofaa ili aweze kupata fedha wakati ni hatari katika maisha yake.
“Ni muhimu wazazi wakatafuta mbinu mbadala ya kuweza kukabiliana na hali hii ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwani mtu akifanya kazi kwa bidii ni lazima atafanikiwa na kuweza kupambana na hali ya umasikini kwani atalima mazao na kuuza, atafanya biashara ndogondogo na kuweza kujipatia kipato”, alisema Mama Kikwete.
Aidha Mama Kikwete pia aliwataka wanafunzi hao kuitumia teknolojia vizuri katika kujiletea maendeleo ikiwa ni pamoja na kujitafutia nyaraka za kusoma kwa ajili ya masomo yao.
Akisoma taarifa ya shule hiyo, Mwalimu Mkuu Renatus Rweyemamu alisema tangu shule hiyo ilipoanzishwa mwaka 2007 hadi sasa idadi ya wasichana waliopata ujauzito ni 34 na wahusika wameshafikishwa kwenye vyombo vya dola na hivi sasa suala hilo linasimamiwa na watendaji wa vijiji husika.
Alitaja changamoto zinazoikabili shule hiyo kuwa ni wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata shule jambo ambalo linasababisha kuingia darasani wakiwa wamechoka.
Alisema pia wasichana wanakutana na vishawishi vingi wakiwa njiani kutokana na hosteli moja haitoshi kwa kuwa ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 48 pia haina vitanda wala magodoro ya kulalia.
Mwalimu Rweyemamu alisema, “Changamoto nyingine ni wazazi kutofuatilia kwa ukaribu mienendo ya watoto wao pia kutokutoa ushirikiano wakati wa kuwafuatilia wahusika waliowapatia ujauzito watoto wao”.
Aliitaja mikakati waliyojiwekea kuwa ni kufanya mikutano na wazazi ili kuwapa ushauri jinsi gani wanaweza kufuatilia mienendo ya watoto wao na kutafuta wafadhili watakaowasaidia kujenga hosteli ikiwa ni pamoja na kununua vitanda, magodoro na kuweka umeme jua.
“Pamoja na majukumu mengi yanayokukabili ombi letu kubwa kwako kwa sasa ni tunaomba kama itawezekana utununulie vitanda na magodoro kwa hosteli yetu”, alisema Rweyemamu.
Shule ya Sekondari ya Msimbu ni shule ya kata ambayo ina jumla ya wanafunzi 463 wasichana wakiwa ni 250 na wavulana 213 ambao wanatoka katika vijiji sita vilivyopo katika Kata ya Msimbu.
MWALIMU ATIWA MBARONI KWA KOSA LA KUWABAKA WANAFUZI WAKE WAWILI NDANI YA SIKU MOJA...!!!

MWALIMU wa Shule ya Sekondari Mwembeni mkoani Mara, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, akikabiliwa na mashitaka mawili ya kuwabaka wanafunzi kwa nyakati tofauti.
Andrew Shadrack (26) ambaye aliwahi kufundisha masomo ya Kingereza na dini katika Shule ya Sekondari ya Montfort wilayani Mbarali mkoani Mbeya alifikishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kamago Minja.
Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Luchagula Mazoya alidai mwalimu huyo alitenda makosa hayo Septemba 13 mwaka huu usiku.
Katika shitaka la kwanza, Mazoya alidai saa 3:30 usiku wa tarehe hiyo, Mwalimu Shadrack alimbaka kwa nguvu mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Montfort mwenye umri wa miaka 17, aliyekuwa akijisomea baada ya kumwita na kumpeleka gizani.
Alidai katika shitaka lingine, siku hiyo Septemba 13 saa 4:00 ikiwa ni nusu saa kupita baada ya tukio la kwanza, Mwalimu Shadrack alimbaka mwanafunzi mwingine wa kidato cha nne shuleni hapo aliye na umri wa miaka 18, aliyemwita kutoka katika bweni alimokuwa amelala.
Alidai mbinu iliyotumiwa na mshitakiwa kwa wanafunzi hao wote, licha ya kutumia nguvu, alikuwa akiwaahidi mambo mbalimbali, ikiwemo kuwasaidia kimasomo, akiwaeleza kuwa anataraji kurudi shuleni hapo na kushika wadhifa wa ukuu wa shule.
Kutokana na kile kilichodaiwa ni uzito wa mashitaka husika, upande wa walalamikaji uliiomba Mahakama, kutoruhusu dhamana kwa mshitakiwa.
Hakimu Minja alikubaliana na maombi hayo na kufunga dhamana, hivyo mwalimu huyo ataendelea kukaa rumande hadi Septemba 18 mwaka huu.
Friday, 13 September 2013
MFUNGWA AHITIMU DARASA LA SABA DAR.

Serikali imempa fursa ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka huu, mfungwa wa Gereza la Watoto lililopo jijini Dar es Salaam baada ya kumruhusu kufanya mitihani ya taifa ya darasa la saba kwenye Shule ya Msingi Ukonga.
Afisa Elimu wa Mkoa wa Pwani, Yusufu Kipengele, jana alisema kuwa amefanikiwa kuhitimu darasa la saba jana baada ya kuungana na wanafunzi wengine nchini kufanya mitihani hiyo akiwa chini ya ulinzi wa askari magereza na wa polisi kuanzia juzi.
Alisema wakati anahukumiwa kwenda jela, alikuwa ni mwanafunzi wa shule moja ya msingi iliyopo wilayani Kibaha.
Alisema alisajiliwa kufanya mitihani yake katika shule hiyo na kwamba kutokana na umbali, aliombewa kuifanyika katika Shule ya Msingi Ukonga ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Alisema wakati akihukumiwa kwenda jela, namba yake ya kufanya mtihani ilipelekwa Mei mwaka huu kwenye shule aliyokuwa akisoma.
“Mwezi Mei huwezi kufanya mabadiliko ya vituo ila kutoa taarifa baraza la mitihani kama kuna tatizo kama hilo na kama kuna haja ya kulitatua kwa vyote inavyoona inafaa,” alisema.
Alisema baada ya baraza kupelekewa taarifa kuhusiana na mtahiniwa huyo liliagiza mkoa wa Pwani umtafutie shule iliyopo jirani na gereza hilo ili afanye mitihani hiyo.
Kipengele alisema kuwa baada ya kupata shule hiyo, mitihani yake ilifungwa kwenye bahasha ya peke yake na kupelekwa Kibaha kisha kupelekwa Shule ya Msingi Ukonga ambako aliruhusiwa kuifanya.
Alisema baada ya kufanya mitihani hiyo, ilipelekwa Kibaha kwenye shule alikokuwa akisoma na kuunganishwa na ya wenzake na kupelekwa kusahihishwa.
Alisema kwa siku mbili mfululizo mfungwa huyo alikuwa akitokea kwenye gereza hilo kuanzia Septemba 11 hadi Septemba 12, mwaka huu na kupelekwa na askari hao kwenye kituo chake cha kufanyia mtihani na kurudishwa gerezani.
Alisema alihukumiwa kwenda jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wilayani Kibaha mapema mwaka huu.
Akizungumzia kuhusu hatima yake ya kuendelea na masomo ya sekondari endapo atafaulu mitihani hiyo, alisema atalazimika kusubiri amalize kifungo.
Vilevile alisema kuwa wanafunzi 19 wenye ulemavu wa uoni hafifu nao ni miongoni mwa waliofanya mitihani hiyo mkoani Pwani.
Kipengele alisema kuwa hakuna taarifa zozote za kuwapo kwa vitendo vya udanganyifu vilivyoripotiwa kutokea.
CHANZO: NIPASHE
Wednesday, 11 September 2013
WALIMU KUGOMA BAADA YA MWEZI MMOJA WASIPOLIPWA MALIMBIKIZO YAO YALIYOFIKIA BILIONI 33....
CHAMA cha Walimu Tanzania (CWT), kimetoa mwezi mmoja kwa serikali kulipa malimbikizo yao ya madeni ya walimu yanayofikia bilioni 33.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, rais wa chama hicho, Greisoni Mukoba, alisema wamechoka kupewa ahadi hewa na serikali ndio maana wamefikia hatua hiyo.
‘Tumetoa mwezi huu wa tisa uwe wa mwisho kuililia serikali, baada ya hapo tutaamua hatua gani tufanye, maana tumekutana na makatibu wakuu wa wizara zinazowahudumia walimu lakini bado tunaishia kupewa ahadi hewa,” alisema Mukoba.
Mukoba aliongeza kuwa Agosti 14, mwaka huu, walikutana na makatibu wakuu wanaowahudumia walimu pamoja na Katibu Mkuu ofisi ya Rais Menejimenti ya Umma, wakatakiwa kuwasilisha madai yao yote.
“Tulikutana na makatibu, katika kikao hicho, tuliwafahamisha kuwa walimu wanaidai serikali zaidi ya sh bilioni 33 na mwisho wa kikao hicho tulikubaliana CWT iwakilishe madai hayo ndani ya wiki mbili,” aliongeza Mukoba.
Mukoba alisema wiki mbili zilipofika, walienda kuonana tena na Katibu Mkuu, ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na kuwasilisha vitabu vyenye madai mbalimbali ya walimu.
“Madai hayo tuliyaambatanisha kwenye barua Na CWT/004/UTMS/VOL.11/94 na madai hayo sasa yamefikia sh bilioni sita,” alisema Mukoba.
Mukoba aliishangaa serikali kuanzisha Mpango wa Matokeo Makubwa sasa “Big Result Now”, huko walimu ambao ndio watekelezaji wakubwa wa mpango huo, wana maisha magumu kutokana na mishahara kuwa midogo na kuzidi kwa malikimbizo ya madeni yao.
“Walimu ambao ndiyo watelekezaji wakuu wa mpango huu japo hawaelewi au hawajapewa semina elekezi, lakini ndio watekelezaji wakubwa.
Naishangaa serikali kuwadharau walimu na nakuhakikishia mpango huo hautafanikiwa kama walimu hawapati haki zao,” alisema Mukoba.
Mukoba aliionya serikali ikamilishe madai ya walimu ili wafanye kazi kwa moyo tofauti na sasa ambapo wengi wamekata tamaa.
‘‘Walimu wa nchi hii wamekata tamaa. Mioyo yao imekufa ganzi kwa sababu serikali imekataa kuwalipa malimbizo yao.
Kwa nini serikali imeamua kuwatendea jeuri walimu kiasi hiki?” alihoji Mukoba.
Tuesday, 10 September 2013
SERIKALI YAKUSUDIA KUANZISHA MTIHANI WA TAIFA WA DARASA LA PILI
Mtihani mpya wa Taifa utaanzishwa kwa wanafunzi wa darasa la pili nchi nzima, ili kuchuja watakaoshindwa kusoma, kuandika na kuhesabu.
Akifafanua uamuzi wa kuanzishwa mtihani wa Taifa wa darasa la pili, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema mtihani huo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa matokeo makubwa sasa katika sekta ya elimu.
Malengo ya mtihani huo kwa mujibu wa Mulugo ni kuondoa uwezekano wa kuwa na wanafunzi katika madarasa ya juu, wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu na ili kufikia malengo hayo, watakaoshindwa

mtihani huo, watarudia mpaka wajue kusoma na kuandika.
Aprili mwaka jana, Mulugo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), alikaririwa akikiri kuwa katika mtihani wa Taifa wa kumaliza elimu ya msingi wa mwaka juzi, kulikuwa na wanafunzi wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu, waliochaguliwa kujiunga na sekondari.
Kutokana na udanganyifu katika mitihani ya Taifa, Mulugo alikaririwa akiagiza wanafunzi walioingia kidato cha kwanza wapimwe uwezo wao wa kusoma na kuandika na kuhesabu.
Alikaririwa akisema kwa mujibu wa tathmini, mkoa wa Kilimanjaro uliongoza kwa kuwa na wanafunzi wengi wasiojua kusoma, kuandika na kuhesabu.
"Mkoa wa Kilimanjaro una wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika wapatao 660, Tanga 490 na Dar es Salaam 208," alikaririwa Mulugo bila kutaja matokeo ya mikoa mengine.
“Hili ndilo janga la kitaifa sasa. Si hayo mengine ambayo watu wanasema ni majanga ya kitaifa. Lazima tujiulize kwa nini watoto wanamaliza darasa la saba wakiwa hawajui kusoma na kuandika na wanafaulu?” Alihoji na kuongeza: “Je, siku hizi hakuna tena somo la kusoma na kuandika? Kwa nini mtoto amalize shule bila kuwa na maarifa ya KKK (Kusoma, Kuandika na Kuhesabu)? Jambo la kusikitisha kuna mpaka baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tatu, ambao hawajui kusoma wala kuandika. Tulipofikia si pazuri hata kidogo, lazima tuwe makini jamani. Tuheshimu Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), tupate ufumbuzi wa mambo haya, Taifa hili ni letu sote, lazima tuhakikishe linasimama imara,” alikaririwa Mulugo.

- HabariLeo
Sunday, 8 September 2013
MAELFU YA WATAHINIWA KUKOSA MTIHANI KIDATO CHA NNE 2013
Dk. Joyce Ndalichako
Watahiniwa 3,000 wa kujitegemea wako hatarini kutofanya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka huu kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) kutokuwa na taarifa zao za kulipia karo za mtihani huo pamoja na zile za usajili.
Tayari Necta imetuma barua kwa watahiniwa hao kuwaeleza kuwa hawatafanya mtihani mwaka huu.
Licha ya maelezo hayo ya Necta, taarifa zinaonyesha kuwa watahiniwa hao walishalipa ada za mtihani huo kupitia njia mbalimbali za kielektroniki zilizoainishwa na baraza hilo, ikiwamo benki na kampuni za simu za mkononi.
Watahiniwa walipaswa kulipa Sh35,000 ikiwa ni ada za mtihani huo kupitia wakala mbalimbali walioteuliwa na Necta.
Gazeti hili lilifanikiwa kuona barua ya Necta kwenda kwa mmoja wa wanafunzi waliojisajili kufanya mtihani huo kwa mwaka 2013 ikimweleza kuwa, hataweza tena kufanya mtihani huo kwa kuwa hakulipa karo ya mtihani huo.
Barua hiyo ilieleza kuwa, kumbukumbu za Necta zinaonyesha kuwa wanafunzi hao wamejiandikisha kufanya mtihani, lakini hawajawasilisha fomu za usajili wala kulipa karo za mtihani huo.
“Hivyo kwa barua hii, unafahamishwa kuwa umeondolewa kuwa mtahiniwa mwaka 2013,” ilisema sehemu ya barua hiyo zilizosambazwa kwa watahiniwa hao.
Kutokana na kuwepo hali hiyo, baadhi ya watahiniwa kutoka maeneo mbalimbali nchini, wameanza kufuatilia Necta kujua hatima yao wakiwa na vielelezo vya malipo yao.
Ofisa Habari wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), John Nchimbi alithibitisha kuwa baraza hilo liliandika barua kwenda kwa watahiniwa takriban 3,000 waliokuwa wamejiandikisha kama watahiniwa binafsi na kuwaeleza kuwa hawatafanya mtihani huo kwa mwaka huu.
Alifafanua kuwa, baadhi yao walifika Necta wakiwa na stakabadhi zilizothibitisha kuwa wamelipa karo hiyo na hivyo kurudishwa kwenye kundi la watakaofanya mtihani huo mwaka huu.
“Necta hatupokei fedha moja kwa moja, tuna mawakala, kilichotokea ni kuwa baadhi ya watu walilipa karo za mitihani, lakini kwenye mfumo wetu tulikuwa hatuoni kama walilipa,” alisema na kuongeza:
“Kwa hiyo watu wote walioandikiwa hizo barua ni wale ambao kwenye mfumo wetu hawaonekani kama wamelipa, lakini wengi wa hawa walikuja na risiti zikionyesha kuwa walikuwa wamelipa na wakarudishwa kwenye mfumo,” alisema.
Alipoulizwa ni wanafunzi wangapi ambao tayari walikuwa wamelalamika na kurejeshwa kwenye orodha ya watakaofanya mtihani huo mwaka huu, Nchimbi alisema mpaka wiki ijayo watakuwa na idadi ya waliothibitisha kuwa wamelipa fedha hizo.
“Mfumo wetu sisi uko sawa, hauna tatizo lolote. Na siwezi kusema ni wapi tatizo lilitokea, lakini ninachojua ni kuwa suala hilo kwa sasa linashughulikiwa,” alisema.
Alieleza kwamba, wiki ijayo wataweza kujua ni watahiniwa wangapi bado wana matatizo, kwani utaratibu wa kupanga namba za watahiniwa utakuwa umekamilika.
Alisema pia kuwa, idadi hiyo inaweza kuonekana kubwa kutokana na baadhi ya walioomba kurudia mtihani huo kuahirisha kufanya hivyo, baada ya matokeo ya mtihani wa taifa yaliyotangazwa mara ya pili kuwawezesha kuendelea na kidato cha tano ama mfumo mwingine wa elimu ya juu.
Alisema kwamba, kwa wale ambao wamepata barua na walishalipa karo hiyo, wanatakiwa kupeleka stakabadhi zao za malipo hayo Necta ili warudishwe kwenye kundi la watahiniwa watakaofanya mtihani huo mwaka huu.
Kwa mwaka 2012 watahiniwa wa kujitegemea waliosajiliwa kufanya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne walikuwa 68,804 ambapo wasichana walikuwa 34,605 sawa na asilimia 50.30, huku wavulana wakiwa 34,199 sawa na asilimia 49.70.
Kati ya watahiniwa hao, waliofanya mtihani walikuwa 61,001 wakiwamo wasichana 30,918 na wavulana 30,083. Watahiniwa 7,803 sawa na asilimia 11.34 hawakufanya mtihani huo.
Hata hivyo, kutokana na matokeo ya mwaka jana kuwa mabaya zaidi yakilinganishwa na yale ya mwaka juzi, ilitarajiwa kuona idadi kubwa zaidi ya watahiniwa wakijiandikisha kufanya mtihani huo mwaka huu kama watahiniwa wa kujitegemea. Jumla ya watahiniwa wote waliosajiliwa kufanya mtihani huo mwaka jana walikuwa ni 480,029, wakiwamo wasichana 217,587 na wavulana 262,442 na waliofanya mtihani huo walikuwa ni 458,139 sawa na asilimia 95.44.
Mfumo wa udahili kwa kutumia mtandao wa kompyuta ulikwaza pia baadhi ya wanafunzi walioomba kujiunga na vyuo vikuu mbalimbali chini ya Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU).
Hivi karibuni Necta ilikumbwa pia na utata katika matokeo ya mtihani wa taifa wa kidato cha nne yaliyokuwa kwenye mtandao, hali iliyolazimisha Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Joyce Ndalichako na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kulitolea ufafanuzi.
-MwananchiWednesday, 28 August 2013
DR NDALICHAKO:SIASA ZISIPEWE NAFASI KATIKA MITIHANI YETU
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), Dk Joyce Ndalichako amesema siasa hazipaswi kupewa nafasi katika mchakato wa usimamizi wa mitihani na kwamba athari za mwenendo wa aina hiyo ni kubwa kwa taifa.
Dk Ndalichako alisema akiwa kiongozi wa Necta hapendi ifike mahali ambako kila mtu atatakiwa afaulu hata kama hana sifa kwani madhara yake yatakuja kuonekana kwenye rasilimali watu siku zijazo.
Akizungumza katika mahojiano maalumu Arusha hivi karibuni alisema: “Tukiruhusu mitihani iingiliwe na wanasiasa tutakuwa tunajimaliza wenyewe, kama ni wanasiasa wafanye kazi ya kushauri halafu waache wanataaluma husika wafanye kazi yao.
“Wanaohusika na kutunga sheria watekeleze jukumu lao siyo kuingilia moja kwa moja suala la mitihani. Sisemi kuwa tuachwe tu tufanye kazi kama tunavyotaka, ikibidi kuwe na chombo cha wanataaluma kutukagua, kwa sababu hii ni taaluma siyo kitu cha kila mtu kuingilia.
“Madhara ya kuingilia mitihani matokeo yake yataweza kuja kuonekana baada ya miaka hata 10 ijayo, ili kukwepa hali hiyo, kila mtu afanye kazi yake kama itaonekana watendaji hawana sifa waondolewe wawekwe wengine wenye sifa.”
Dk Ndalichako ambaye hivi karibuni alichaguliwa kuongoza Mabaraza ya Mitihani Afrika (AEAA) alisema: “Mtu akipewa alama asizostahili na akawa mwalimu atawafundisha nini watoto? Hawa ndiyo utakuta wana sababu zisizokwisha, kila siku utamsikia akisema watoto wa siku hizi hawaelewi kabisa.”
Dk Ndalichako pia alipinga mawazo kwamba Necta inapaswa kushirikiana na wadau wa elimu katika kila kitu. Alisema ni hatari... “Tusifike mahali tuambiwe tuwaulize watoto tuwaletee maswali gani kwenye mtihani.”
Kauli ya Dk Ndalichako imekuja wakati taifa likiendelea kuugulia maumivu yaliyotokana na matokeo mabaya ya mitihani ya kidato cha nne ya 2012 ambayo karibu nusu ya wanafunzi walifeli. Matokeo hayo yaliifanya Serikali kuunda tume iliyoogozwa na Katibu Mkuu wa sasa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome ambayo ilipendekeza matokeo hayo yafutwe na yapangwe upya, hatua ambayo wengi waliita ni ya kisiasa.
Mahojiano kati ya Dk Ndalichako
Swali: Hii ni mara ya tano kwa Necta kuwa mwenyeji wa mkutano wa AEAA, na pia mmekuwa mkihudhuria mikutano kama hii inapofanyika nje ya nchi, ni nini hasa mmeona kuwa ni changamoto kwa mitihani inayotungwa katika ngazi ya shule?
Jibu: Hii mitihani inayotungwa shuleni ni changamoto sana, lakini ukiangalia utagundua kuwa tatizo lipo kwenye mitalaa ambayo walimu wanafundishiwa. Huko suala la ufundishaji limetiliwa mkazo sana lakini lile la kuwapima watoto halijapewa kipaumbele kabisa.
Wanachofundishwa huko ni kama orientation (utangulizi) tu, walimu wanatakiwa wajue mbinu gani zitumike kutunga mitihani.
Sisi kwenye ngazi ya taifa tunapotunga maswali tunazingatia mengi, kuanzia idadi ya watahiniwa na mambo kama hayo. Mwalimu darasani angetakiwa kutunga mtihani kwa kuangalia watoto wake na ajue ni mbinu gani za kutumia.
Tumekuwa tukifanya mafunzo kwa baadhi ya walimu kuhusu namna bora ya kutunga mitihani, ili waweze kufanya tathmini ya kile walichowafundisha watoto. Hata hivyo kwa kuwa sisi tupo wachache na mitihani yetu ni mingi tunashindwa kuwafikia wote. Tuna mpango wa kutoa mafunzo hayo kwa wakufunzi 200 wa walimu.
Swali: Vipi kuhusu ubora wa mitihani inayotungwa na Necta, mnadhani inakidhi viwango?
Jibu: Ubora wa mitihani inayotungwa na Baraza upo juu sana, hata usahihishaji wake ni wa hali ya juu. Mfumo wa kuwa kila mwalimu anasahihisha swali lake ni wa kipekee na sisi tulikuwa kati ya nchi za kwanza kuutumia.
Kuna nchi mtu anapewa burungutu la mitihani ya watoto anakwenda nayo nyumbani kusahihisha akishamaliza analeta majibu kisha watoto wanatangaziwa. Sisi mfumo wetu ni bora sana na sijui kwa nini watu wanakuwa na mtazamo hasi na Necta. Sifa kubwa ya baraza lolote lile la mitihani ni kutoa majibu yanayofanana na hali halisi ya elimu ilivyo.
Tunachotaka siku zote kuona ni mtu anapewa kile anachostahili. Watu wengine wanasema mitihani inayotungwa na kupewa watoto wote siyo sawa kwa sababu kuna baadhi ya shule walikuwa hawana walimu au vitabu, sasa swali la kujiuliza nani alitakiwa kutoa hivyo vitabu?
Kwa vipi utunge mtihani mmoja useme ni kwa ajili ya shule ambayo haina vitabu na walimu! Ni watoto gani ambao tumewaandaa kwa sababu ya kwenda kwenye hizo shule?
Naona ni bora kabisa shule isiwepo kama hakuna walimu na vitabu kwa sababu hii ndiyo roho ya elimu. Kukiwa na walimu na vitabu watoto wanaweza kukaa hata chini ya mti na wakafundishwa na kupata maarifa.
Necta tunatunga maswali kwa kuzingatia vitu vingi na kutokana na suala la uwazi, kila swali linalotungwa kuna sehemu tunaonyesha mada ambayo swali hilo lilipotolewa kwa mujibu wa silabasi pia kuorodhesha baadhi ya vitabu vyenye mada hiyo, mpaka ukurasa tunaonyesha. Hata Tume ya Waziri Mkuu walipokuja tuliwaonyesha vitu vyote hivyo.
Swali: Katika mkutano huu, baadhi ya mambo yaliyozungumziwa ni pamoja na athari za siasa kuingizwa kwenye mitihani, kwa upande wa Tanzania unazungumziaje hali hiyo?
Jibu: Tukiruhusu mitihani iingiliwe na wanasiasa tutakuwa tunajimaliza wenyewe, kama ni wanasiasa wafanye kazi ya kushauri halafu wawaache wanataaluma husika wafanye kazi yao, wanaohusika na kutunga sheria watekeleze jukumu lao siyo kuingilia moja kwa moja suala la mitihani.
Sisemi kuwa tuachwe tu tufanye kazi kama tunavyotaka, ikibidi kuwe na chombo cha wanataaluma kiwe kinatukagua, kwa sababu hii ni taaluma siyo kitu cha kila mtu kuingilia.
Madhara ya kuingilia mitihani matokeo yake yataweza kuja kuonekana baada ya miaka hata 10 ijayo, ili kukwepa hali hiyo kila mtu afanye kazi yake kama itaonekana watendaji hawana sifa waondolewe wawekwe wengine wenye sifa.
Tukitaka kila mtu afaulu hata kama hana sifa madhara yake yatakuja kuonekana kwenye suala la rasilimali watu, mtu akipewa alama asizostahili na akawa mwalimu atawafundisha nini watoto? Hawa ndiyo utakuta wana sababu zisizokwisha, kila siku utamsikia akisema watoto wa siku hizi hawaelewi kabisa.
Pia hili suala la kusema kila kitu tushirikishe wadau ni la kuangalia. Tusifike mahali tuambiwe tuwaulize watoto tuwaletee maswali gani kwenye mtihani.
Tuesday, 27 August 2013
WANAFUNZI WAFELI WOTE MTIHANI WA FORM SIX NA KUSHINDWA KUJIUNGA CHUO KIKUU HUKO LIBERIA
Inakuaje pale wanafunzi wa form six ambao wanatarajiwa kujiunga na chuo kikuu wanafeli wote nchi nzima na kushindwa kujiunga na chuo kikuu?.Kwa mara ya kwanza katika historia ya Liberia, wanafunzi wote wamefeli mtihani wao wa mwisho wa sekondari na hivyo kumaanisha kuwa hakuna hata mmoja ambaye atafuzu kuingia chuo kikuu.
Chuo kikuu cha Liberia kwa mwaka 2013/2014 hakitakuwa na mwanafunzi hata mmoja kwa ajili ya kozi yoyote ile kutokana na wanafunzi hao kufeli. Waziri wa elimu wa Liberia anasema wanafunzi wameshindwa kufaulu mtihani huo kutokana na lugha walioitumia ya kiingereza. Wanafunzi hao hawakuwa na uelewa mzuri wa lugha ya kiingereza ambayo ilitumiwa kuwatahini.
Hata hivyo wanafunzi wengi hawana imani na matokeo hayo na waziri wa elimu anajaribu kuongea na chuo kikuu cha Liberia kuona jinsi watakavyofanya.
Monday, 19 August 2013
WIZARA YA ELIMU YAMUUMBUA MBATIA
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imemuumbua Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, kuwa mitihani ya majaribio ya darasa la saba aliyosema ina makosa ya kisarufi na ilikuwa migumu, ilikuwa feki. Mitihani iliyotajwa na Mbatia kuwa ina makosa ni ya masomo ya Hisabati, Kiingereza na Kiswahili na ilifanywa Julai 8-9, 2013 katika wilaya 40 za Tanzania.
Taarifa hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi wa Elimu ya Msingi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Zuberi Samataba, alipokuwa akizungumza na MTANZANIA.
“Siyo kweli hata kidogo, mitihani aliyokuwanayo Mbatia ni feki na haikufanywa na wanafunzi wa darasa la saba kama alivyosema.
“Sisi hatujui Mbatia aliipata wapi hiyo mitihani, halafu wizara haitungi mitihani bali mitihani inatungwa na NECTA, mitihani ile ilitungwa ikiwa ni programu maalumu ya kupima uelewa wa wanafunzi wa darasa la saba na sio moko kama alivyosema.
“Pili ni kwamba, Mbatia alipoiona ile mitihani angefanya jambo la busara kuwasiliana na sisi kwa ajili ya kujiridhisha kabla ya kuzungumza na vyombo vya habari, kwa sababu tungemueleza ukweli, kwamba mitihani aliyokuwa nayo ni feki na haijafanywa na wanafunzi wa darasa la saba,” alisema Samataba.
Alisema kwamba, hata Kamishina wa Elimu wa wizara hiyo, Profesa Ellustela Bhalalusesa, amelitolea ufafanuzi suala hilo kwamba mitihani iliyotajwa na Mbatia ilikuwa feki.
“Kamishina kalizungumzia hilo na mimi narudia kulizungumzia, kwamba mitihani hiyo ilikuwa feki, sasa wewe mtafute Mbatia umuulize mitihani hiyo aliipata wapi maana iko tofauti kabisa na ile tuliyowapa wanafunzi wa darasa la saba kuifanya,” alisema.
Majibu hayo, yamekuja ikiwa ni siku chache tangu wizara hiyo izindue Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), katika sekta ya elimu na kujiwekea mikakati tisa ya kuitekeleza.
Mbatia alipotafutwa ili aweze kutoa ufafanuzi juu ya mitihani hiyo, hakupatikana.
Akizungumza na vyombo vya habari Dar es Salaam hivi karibuni, Mbatia alisema ameibua madudu mapya ya elimu katika mitihani ya Hisabati, Kiswahili na Kiingereza.
Aliyataja madudu hayo katika mitihani hiyo kuwa, katika Somo la Kiswahili na Kiingereza, kulikuwa na makosa ya kisarufi wakati katika Hisabati kulikuwa na maswali yasiyokuwa na majibu.
Alisema aliupeleka mtihani wa Hisabati uliofanywa na wanafunzi hao katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kumkabidhi profesa mmoja (hakutaka kumtaja jina), ambapo aliufanya na kukuta kuna maswali mengine hayakuwa na majibu kwa sababu yalikosewa.
Aidha, alisema katika mtihani wa Kiingereza na Kiswahili uliokuwa na makosa makubwa ya kisarufi, aliupeleka katika Jumuiya ya Wanataaluma wa Chuo Kikuu hicho, ambapo wasomi hao walisikitishwa na makosa yaliyokuwa katika mitihani hiyo.
Kutokana na madudu hayo, alipendekeza Serikali iunde Tume ya Kudumu ya Elimu itakayokuwa na hadidu za rejea 12, mojawapo ikiwa ni kushughulikia ubora wa elimu na kudhibiti mambo yote yanayosababisha kutetereka kwa ubora huo.

Sunday, 18 August 2013
MWALIMU WA MIAKA 30 AMUWEKA KINYUMBA MWANAFUNZI WAKE WA MIAKA 14
MWANAFUNZI wa darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Sokoine, Manispaa ya Dodoma (jina linahifadhiwa), anadaiwa kuwekwa kinyumba na mwalimu wake David Macha (30).
Mwanafunzi huyo wa miaka 14 ni kati ya watoto wanaofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Compassion International Tanzania kituo cha Tz 807 FPCT kilichoko Chamwino.
Hata hivyo, katika hali ya kushangaza Jeshi la Polisi mkoani hapa, limelalamikiwa na wazazi wa mtoto huyo kwa kitendo cha kumlinda mtuhumiwa licha ya kupewa taarifa za uhalifu huo kwa zaidi ya miezi mitano sasa, limeshindwa kumchukulia hatua.
Uchunguzi wa Tanzania Daima ambao umethibitishwa na wazazi wa mwanafunzi huyo, umebaini kuwa mwalimu Macha amekuwa akifanya mapenzi na mwanafunzi huyo kwa zaidi ya miezi mitano sasa.
Wazazi wa mwanafunzi huyo wanathibitisha kuwa kwa zaidi ya miezi mitano, mtoto wao alikuwa na tabia ya kutoroka nyumbani nyakati za usiku na kulala nje, jambo ambalo lilianza kuwatia mashaka na kuanza kufuatilia nyendo zake.
Walidai kuwa wakati mwingine alikuwa akirudi nyumbani asubuhi kwa ajili ya kujiandaa kwenda shule na anapoulizwa alikolala, alisema alikuwa katika mkesha.
Akisimulia mkasa huo, mjomba wa mwanafunzi huyo, Silas Mjengi, alisema binti yao anaishi na mama yake pekee katika eneo la Area ‘A’ mjini hapa baada ya mzazi huyo kutengana na mumewe.
Mjengi alisema kuwa baada ya kumbana binti yao, alikiri kufanya mapenzi na mwalimu huyo nyumbani kwake.
“Kwa muda mrefu nilipokea malalamiko toka kwa dada yangu juu ya vitendo vya mjomba wangu kuwa amekuwa akitoroka na kulala nje, ndipo nilipoamua kulifuatilia kwa umakini ikiwemo kumbana ambapo alikiri kuwa alikuwa anaishi na mwalimu kama mke na mume na hata kwenye simu yake alimwandika kwa jina la ‘my husband’,” alisema.
Kwa upande wake, mama mzazi wa mwanafunzi huyo, Esther Mjengi, alisema kuwa baada ya kuona tabia ya mwanaye imebadilika alianza kumfuatilia ndipo marafiki zake walipomueleza ukweli kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwalimu wake.
Alisema baada ya kufuatilia aliweza kumbamba akiwa nyumbani kwa mwalimu huyo kama mke wake na hata alipomfuata ili kuhojiana naye, aligoma kutoka ndani na ghafla alilazimika kuvua nguo na kumwachia blauzi ambayo alikuwa amevaa na kukimbia akiwa kifua wazi.
“Niliumizwa sana na mwanagu kujikita katika mapenzi na mwalimu, ukizingatia mwanagu bado ni mdogo na mwalimu ana miaka 30; wanangu naangaika nao sana kutokana na baba yao kutokuwa karibu nao, mbaya zaidi ni watoto ambao wanasoma kwa ufadhili wa Compassion Tanzania.
“Lakini baada ya kumbana alikiri kufanya ngono na mwalimu kwa zaidi ya miezi mitano sasa. Nilikwenda kushtaki kituo cha polisi cha kati Dodoma katika kitengo cha dawati la jinsia. Huweziamini! Sikutapa ushirikiano wowote; sijui nini kilifanyika kwani nilianza kubezwa badala ya kushughulikiwa na mtuhumiwa aliachiwa huru bila hata kuhojiwa,” alisema.
Tanzania Daima lilifanikiwa kuzungumza na mwanafunzi huyo, ambaye alikiri kuwa na uhusiano na mwalimu na kwamba alifikia uamuzi huo baada ya mwalimu huyo kumhudumia kwa vitu mbalimbali, ikiwemo kumpatia fedha.
“Aliahidi kunisaidia kwa kila kitu, kwani licha ya kunipa fedha kwa ajili ya matumizi ya nyumbani na shuleni, lakini pia alikuwa akininunulia nguo zangu za ndani, pamoja na simu ya mkononi aina ya Tecno,” alisimulia bila woga.
Ofisa Elimu Manispaa ya Dodoma, Winfrida Bario, alikiri kupokea taarifa za tukio hilo, akisema kuwa alikaa nao wote mzazi na mwalimu, ambapo mwalimu na mwanafunzi walikiri makosa yao ya kuwekana kinyumba.
“Nilichoagiza kwa polisi ni kuhakikisha hatua zinachukuliwa dhidi ya mwalimu huyo kwani moja kwa moja amevunja kanuni na taratibu za kazi na hata kama ingekuwa vipi mwalimu huyo tayari ameishamharibu kisaikolojia mwanagunzi huyo.
“Mwanafunzi huyo yuko darasa la saba unafikiri anaweza kuwa na akili nzuri tena maana ameishamharibia kila kitu. Mbali na hili, kwa mwalimu wa miaka 30 kutembea na mwanafunzi wa miaka 14 ni kosa la ubakaji,” alisema ofisa elimu huyo.
Aliongeza kuwa kitendo hicho ni cha aibu kwani mtumishi wa umma hapaswi kukiuka maadili ya utumishi wake.
Naye mwalimu ambaye alibambwa kwa kosa hilo la kumweka mwanafunzi kinyumba alijitetea kuwa alifanya hivyo kutokana na tamaa za mwili lakini si tabia yake.

“Ni kweli nilikuwa naishi na mwanafunzi huyo lakini mimi si tabia yangu bali shetani alinipitia, nimewaomba radhi wazazi wa mtoto wanisamehe sitarudia tena na nasubiri kama watanisamehe ila sikutarajia kabisa,” alijitetea.
Upande wa jeshi la polisi umeonekana kuwa na kigugumizi kwani hakuna ufafanuzi wowote wa kina uliotolewa licha ya mzazi wa mtoto kuonyesha vielelezo vyote vya polisi na daktari kuhusiana na mtoto wake kutendewa vitendo vya ngono na mwalimu huyo.
Kamanda wa polisi mkoa Dodoma, David Misime, hakupatikana kulizungumzia tukio hilo lakini ofisa habari wa jeshi hilo, Kung’alo Lupy, alisema suala hilo linaendelea kufanyiwa uchunguzi.

Saturday, 17 August 2013
DR JOYCE NDALICHAKO ATEULIWA KUWA RAIS WA UMOJA WA MABARAZA YA MITIHANI AFRIKA
Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania ( Necta), Dk Joyce Ndalichako, ameteuliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabaraza ya Mitihani Afrika (AEAA), nafasi ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na Serara Moahi wa Botswana.
Akizungumza baada ya kutangazwa kuteuliwa kwake, Dk Ndalichako alisema atatumia fursa hiyo kuendeleza ajenda mbalimbali zitakazosaidia kuinua elimu Bara la Afrika.
“Hii ni heshima ya pekee kwa Baraza la Mitihani Tanzania, kipindi cha mwaka mmoja nikiwa Rais wa AEAA nitaendeleza yaliyoanzishwa na mtangulizi wangu, pia kutekeleza ajenda mbalimbali zitakazoleta manufaa kwa nchi yetu,” alisema Dk Ndalichako. Pia, alisema atajitahidi kuwa mbunifu na kupanua ushirikiano na nchi nyingine.
, kuhakikisha anawajengea uwezo zaidi wafanyakazi wa mabaraza ya mitihani kwa nchi wanachama.
“Kwa mfano kwetu naona changamoto kubwa ni suala la standardisation (kusanifisha alama za mitihani), nitajitahidi kuhakikisha watu wetu wanajengewa uwezo kwenye nyanja hii,” alisema.
Alitumia fursa hiyo kushauri nchi za Afrika kuhakikisha zinatilia mkazo zaidi kuongeza walimu wa kutosha, walio bora na vifaa vya kujifunzia. Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Selestine Gesimba, alisema kupata cheo hicho ni heshima kwa nchi.
Subscribe to:
Posts (Atom)