Showing posts with label bongo za kitaa. Show all posts
Showing posts with label bongo za kitaa. Show all posts

Saturday, 21 September 2013

PICHA ZA TUKIO ZIMA LA REDD'S MISS TANZANIA LILIVYOFANYIKA USIKU WA KUAMKIA LEO...!!


Redd's Miss Tanzania 2013,Happiness Watimanywa akipungia mkono mara baada ya kutangazwa mshindi wa Taji hilo kwa mwaka huu.Kushoto ni mshindi wa pili,Latifa Mohamed na kulia  ni mshindi wa tatu,Clara Bayo.

 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa jukwaani usiku huu wakati wa Onyesho la Taifa la Urembo linalofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.



 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakifungua shindano la mwaka huu kwa kuonyesha ufundi wao wa kucheza muziki. Shindano la mwaka huu ambalo limedhaminiwa na kampuni ya vinywaji Tanzania  ya Tanzania Breweries Limited kupitia kinywaji cha Redds limefanyikia katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam. Jumla ya warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali,vyuo nk wameshiriki.


 Warembo walioingia hatua ya kumi na tano bora. 

 Jaji Mkuu wa Shindano la Redd's Miss Tanzania,Dkt. Ramesh Shah akitangaza Warembo walioingia hatua ya tano bora.

Warembo walioingia hatua ya tano bora,toka shoto ni Happiness Watimanya,Elizabert Peter,Clara Bayo,Lucy Tomeka pamoja na Latifa Mohamed.

"NINA WAKE FEKI WENGI SANA HAPA MJINI".....MZEE MAJUTO


             Majuto anasema kuwa ana watoto tisa ingawa hakuwa tayari kuwazungumzia mama wa watoto hao zaidi ya kumwongelea mkewe wa sasa, Aisha Mbwana kwa kuwa wake zake aliozaa nao baadhi ya watoto kwa bahati mbaya walishafariki dunia.
Alisema kuwa yanapokuja masuala ya familia huwa anapenda azungumze mkewe na kwa ridhaa yake. Kwa mujibu wa Majuto anapenda aitwe mke halali kwa kuwa wake feki anao wengi kupitia michezo ya kuigiza na wengine wenye fikira potofu hutumia picha hizo kutengeneza habari za uongo.
Aisha anaizungumziaje familia yake
Kama kawaida ya wanawake wa Tanga ana lafudhi ya huko ambayo huvutia kuzungumza nao, anaanza kwa kunieleza kuwa alianza kuitwa mke halali wa nguli huyo wa sanaa za maigizo mwaka 1997, walipofunga ndoa .
Anasema kuwa alikutana na nguli huyo maeneo ya Buguruni, Dar es Salaam, ambako alikuwa akiishi na dada yake aliyekuwa kaolewa na rafiki yake mzee Majuto, ‘Mwanachia’ (kwa sasa ni marehemu), ambaye walikuwa wakiigiza pamoja.
Anasema hakuwa na hili wala lile hadi alipoamua kuondoka na kurudi kwao maeneo ya Vingunguti, ambako ndiko walikokuwa wanaishi wazazi wake na kupewa taarifa kuwa posa imepelekwa kwa ajili yake.
Nilipoambiwa kuhusu hiyo posa sikufikiria kama atakuwa ni mzee Majuto kwa kuwa alikuwa ni kama shemeji yangu kutokana na kuwa karibu na shemeji yangu,” anasema Aisha ambaye ni mama wa watoto watatu.
Anaendelea kueleza kuwa siku ambayo wanafamilia walikutana na kumuuliza kama anamfahamu mchumba na kutajiwa jina kuwa ni Amri Athumani, aliuliza mara mbili kwa kuwa alikuwa hamfahamu huyo mtu hadi alipoambiwa kuwa ni King Majuto.
“Kwa mila za Wabondei mchumba wa kwanza anakubaliana na wazazi, halafu binti anapewa taarifa na kwa kuwa wazazi ni wakubwa inabidi binti akubali, na ndivyo ilivyokuwa kwangu nikakubali na kuolewa na Majuto,” anasema mama huyo.
Anaingia kwenye uigizaji kufuata nyayo za mumewe
Aisha anafafanuwa kuwa kabla ya kuolewa na Majuto hakuwa mwigizaji lakini baada ya kuolewa, mumewe huyo alimwingiza kwenye uigizaji na filamu ya kwanza kuigiza na mumewe huyo ni ‘Fukara hatabiriki’.
Mkewe huyo anasema kipindi hicho Majuto alikuwa anafanya kazi bila kuwa na kikundi zaidi ya wanafamilia, hivyo na yeye alikuwa mmoja wao akicheza kama mama na Majuto kama baba.

KIBAKA AUMBUKA...!!! BAADA YA KUIBA SIMU WIKI MOJA BAADAE SIMU YAITA TUMBONI.



Kijana mmoja mkazi wa kitongoji cha DDC Mji mdogo wa Mbalizi wilaya ya Mbeya, Mkoani Mbeya Bwana GOODSON MWASYOGE amejikuta yupo katika wakati mgumu baada ya kuiba simu ya mfanyabiashara wa eneo hilo. Baada ya wiki moja kuiba hiyo simu imekuwa ikilia tumboni na kuchukua kama dakika kumi na tumbo lake kuvimba.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa Bwana ASIFIWE MWAKALONGE amethibitisha kwa tukio hilo akiwa sambamba na mjumbe Bwana MOHAMMED SAID.




Wakati huo huo Kaka wa muhanga wa tukio hili Bwana DANIEL MWASYOGE akiwa na Mama mzazi Bi CHRISTINA MWAKALONGE amemtaka aliyeibiwa simu kumsamehe kijana wao kwa kosa alilolifanya naye amekiri kutenda tukio hilo na anaomba msamaha kuwa abilisi alimpitia tuu hakuwa na tabia ya wizi na baadhi ra wananchi wa mtaa huo wanashangaa.

Kijana GOODSON ni mmoja wa wafanyakazi wa Machinjioni maarufu kama Butchery Mbalizi.



Hili jambo ni FAIDA kwani ni fundisho kwa vijana ambao hupendelea tabia ya kusogeza mali katika jamii na kusababisha Janga la Umasikini kuendelea kuchukua nafasi.

Na HASARA yake M wenye mali yake atachukuliwa/kutafsiriwa ndivyosivyo ndani ya jamii endelea kufuatilia matandao huu ambapo utakuletea taarifa zaidi kwa njia ya picha.

VIDEO!! JIHADHARI NA WIZI WA AINA HII KAMA WEWE NI MGENI ARUSHA....TAZAMA KIBAKA HUYU ALIVYOKAMATWA STENDI YA MABASI ARUSHA

           Kijana huyu alichezea kipigo juzi katika stend ya mabasi ya mikoani jijini Arusha baada ya kuiba begi la msafili mmoja baada ya kuiba kibaka huyu alivaa nguo zote katika mwili ili asishitukiwe Lakini walikuwepo waliomuona .
Ndipo walimtaja kijana huyu baada ya kupokea kipigo kitakatifu ndipo alieza kuwa yeye ndiye alieiba begi hilo na alipoulizwa nguo zipo wapi aliwaambia kuwa amevaa mwilini ndipo hapo alipoamuliwa kuvua nguo hizo kwakuwa nilikuwa na safari na basi ndio lilikuwa linaondoka niliacha kijana huyu akiwa katika hatua za kupelekwa polisi





           TAZAMA VIDEO HAPA     

  

FLORA LYIMO AWASHUKIA BLOGGERS NA WALE WOTE WANAO SEMA KAPOST PICHA ZA UCHI, SOMA HAPA ALICHOKISEMA


               "Ndugu zangu Watanzania na Nyota zangu' Poleni sana kwa yale mnayoyasoma kwenye Baadhi ya Mamburulaz'' Blogs na Facebook bila kusahau Vipage Group vyao'' Sasa napenda kuwaambieni kwamba Poleni sana kwa Mnavyoandikiweni ''Yani Picha za Uchi '' Mimi kama Mimi Sioni Uchi wa Hizo Picha'' Nakama Ninavyo elewa ''HAMJAWAHI KUONA PICHA ZANGU ZA UCHI AU NISEME HAMJUI NINI MAANA YA UCHI'' FULL STOP'' 
Pili'' HII NI AHADI NA MNAJUA AHADI NI DENI'' NAWAAHIDINI KILA PALE NITAKAPO PATA  NAFASI '' NITAWAPIGIENI PICHA KAMA HIZI NA ZAIDI 'NA SIYO ZA UCHI NINAOUFAHAMU MIMI AU UNAOFAHAMIKA NA WASOMI NA WAELEWA PIA'' SASA WALE WASIO WAELEWA NA WASOMI ''WATAPATA CHA KUWASUKUTUA MIDOMO YAO NA MENO YAO YALOOZA 'KWA HIZO PICHA NITAKAZO POST KILA NITAKAPO JINAFASI TENA NAJIFYETUA MWENYEWE'' CHEZEA MPIGA PICHA WA UKWELI TENA SASA NINA CAMERA 4''NNE'' YANI FULL KUWASNAPIENI''
NI HAYO KUTOKA KWA MSEMA KWELI WENU NA 
YOUR TOP IN TOWN ''FLORA LYIMO FASHION POLICE'' 
HAVE NICE WEEKEND MY DEARS'' AND THANKS KWA WINGI WENU WA KUMIMINIKA KWENYE HII BLOG LEO''YANI NIMESTUKAJE KUONA WINGI WENU ? KUMBE MWASEMA HAMNIPENDI NA HUKU MWANIPENDA HIVI'' RUWA MANGI 'AIKENYI NDAO 'MORE PHOTOS LIKE HIZI EVERY DAY NIKIWEZA''
DONT FORGET TO FOLLOW THIS BLOG''
Hii nimewapa Vidonge vyao Mburulas huko Facebook''
Flora Lyimo YATA WASHINDA.......KUMBE NYIE WOTE WAJINGA MAMBURALAZ HIVI.....? HIVI MNAJUA NINI MAANA YA UCHI ?? SASA KWA TAARIFA YENU ..NITAJIPIGA PICHA KILA SIKU ZA HIVI '' NA NITA POST KWA YOUR TOP IN TOWN ...FLORA LYIMO FASHION POLICE BLOG....ILI MPATE KUSUKUTUA MIDOMO YENU MICHAFU NA MENO KAMA YA MMNYWA UGOROO..HAHHAHAHAAAA...NYIE MLIE TUU''MCHEKE KWANI MNA MWANYA" Says Flora Lyimo
                <<INGIA HAPA KUSOMA ALICHOKIANDIKA KWENYE BLOG YAKE>> 
                                       <<PICHA ZENYEWE ALIZOPIGA HIZI HAPA>>


MTUHUMIWA AJISAIDIA HAJA KUBWA MAHAKAMANI..MATUKIO KATIKA PICHA

               KIOJA cha mwaka kilitokea Jumatano wiki hii katika Mahakama ya Jiji ya Sokoine Drive jijini Dar es Salaam, baada ya mkazi mmoja wa Buguruni, Hassan Omary kujisaidia haja kubwa kizimbani wakati akisomewa shtaka lake la uzururaji.
Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi alikuwa akimsomea shtaka hilo, mbele ya Hakimu Mfawidhi, William Mutaki na alipotakiwa kukiri au kukanusha kosa lake, mtuhumiwa huyo alibaki kimya akiwa amemtumbulia macho hakimu.
Katika hali isiyotarajiwa, mtuhumiwa huyo alionekana akijikamua kama anayejisaidia na ghafla, harufu kali ya kinyesi ikatanda mahakamani hapo.
Hakimu alitahayari kufuatia tukio hilo, kwani aliziba pua yake kwa kutumia koti lake na kuuliza chanzo cha mtuhumiwa kufanya kitendo hicho kortini, lakini katika hali iliyoashiria kama ni kiburi, kijana huyo hakujibu chochote zaidi ya kutazama chini, licha ya swali hilo kurudiwa zaidi ya mara tatu.
Kutokana na kosa hilo ambalo liliharibu na kusimamisha karibu shughuli zote za mahakama kwa muda, Hakimu Mutaki alimhukumu kijana huyo kwenda jela kwa muda wa miezi sita ili kuwa fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo.
Kana kwamba haitoshi, askari waliokuwepo mahakamani hapo walilazimika kumchapa bakora kijana huyo ili kumlazimisha kupiga deki baada ya eneo hilo kuchafuka vibaya kwa kinyesi kilichochanganyika na mkojo.

Friday, 20 September 2013

BINTI WA MIAKA 16 AOLEWA,AELEZEA RAHA YA NDOA

                      BINTI wa miaka 16, Husna amefungukia ndoa yake na mwanaume anayetajwa kwa jina la Juma na kudai anafurahia ndoa yake..
Akizungumza na waandishi wetu, Mbande nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, Husna alisema aliolewa na mwanaume huyo Julai mwaka huu, mkoani Lindi na mwezi uliopita walihamia Dar.
Alipohojiwa kwa nini alikubali kuolewa akiwa na umri mdogo, alisema kwamba alikosa kazi ya kufanya.
Binti huyo aliwashangaza waandishi na polisi pale alipodai kwamba yeye si mtoto mdogo kwani ana mdogo wake mwenye umri wa miaka 15 ambaye ameolewa na amezaa mtoto hivyo yeye asikodolewe macho.
“Mbona mdogo wangu ana miaka 15 ameolewa. Mimi siyo mtoto mdogo ninaijua raha ya ndoa yangu,” alisema Husna.
Waandishi wetu walipotaka kujua kama huwa anapatwa na maumivu anapokutana na mumewe,  alisema anajisikia kawaida kwani alianza mapenzi tangu akiwa shuleni.
Kama vile haitoshi, binti huyo alisema kuwa huwa anawashangaa hata polisi ambao wanajaribu kulifuatilia suala hilo.
Hata hivyo, Husna alisema kuwa angependa kuendelezwa kimasomo kama akipatikana mfadhili na kuachana na mumewe huyo.
“Nipo tayari kuachana na mume wangu na kwenda kusoma kwa kuwa umasikini ndiyo uliochangia kuolewa mapema,” alisema.
Awali waandishi wetu walipewa taarifa za kuwepo mwanaume aliyeoa mtoto mdogo na majirani wa wanandoa hao na kuwataka kulivalia njuga suala hilo.
”Tunashangaa mwanaume amemuoa binti mdogo sana yaani sawa na mwanaye kabisa. Muda mwingi binti anachezea michanga na watoto wengine. Sijui kamtoa wapi?” alisema mmoja wa majirani hao.
Baada ya kufanyia uchunguzi jambo hilo. Waandishi wetu walibaini nyumba wanayoishi wanandoa hao, ndipo Septemba 14 mwaka huu, waandishi wetu walivamia nyumba hiyo wakiwa na askari ili kumtia nguvuni mwanaume huyo ambaye kwa mujibu wa majirani aliambiwa na watu wake wa karibu na kutoroka eneo hilo.
Akizungumza na waandishi wetu kuhusiana na tukio hilo, Mwakilishi wa Mtandao wa Wanawake Kanda ya Kipolisi Temeke, Eva Michael alisema kuwa wazazi wengi wenye mabinti wadogo hawajui sheria zinazowahusu kama ilivyo kwa Husna ambaye anaona kuolewa katika umri wake ni jambo sahihi kwake.
“Kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya mwaka 2009 hairuhusiwi mwanamke kuolewa chini ya miaka 18, kwani huo ni kama ubakaji. Watu bado wanaitambua sheria ya mwaka 1971 inayoruhusu mwanamke kuolewa kuanzia umri wa miaka 14, sheria ambayo imeshabadilishwa, kwa hiyo mume wa Husna anachukuliwa kama mbakaji,” alisema mwanaharakati huyo.
Akibainisha jinsi ya kushughulikia suala la Husna, Bi. Eva alisema kuwa atashirikiana na watu wa Ustawi wa Jamii watakaomjenga kisaikolojia na kumpa hifadhi ya muda kabla ya kuwapata wafadhili watakaojitolea kumsaidia.
Mume wa Husna bado anatafutwa na polisi na amefunguliwa kesi katika Kituo cha Polisi Mbagala Kizuiani yenye  namba, MBL/RB/9435/13 KUBAKA.

-GPL

WANAUME NAO KUMEZA VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO

            Ni dhahiri kwamba wanaume watashtuka, lakini huenda nao wakashiriki uzazi wa mpango bila upasuaji
Vidonge vya uzazi wa mpango vimezoeleka kutumiwa  zaidi na wanawake pekee, kiasi kwamba ni jambo la ajabu kusikia kuwa wanaume nao wanaweza kuvimeza.
Hata hivyo, watafiti mbalimbali wamefanikiwa kutengeneza vidonge vya uzazi  ambavyo vinazifanya mbegu za kiume  katika mfuko wa uzazi wa mwanamume zisiwe na nguvu ya kuweza kutungisha mimba. Utafiti wa dawa hiyo ambao umewaumiza kichwa wanasayansi kwa miaka mingi umewezesha kupatikana kwa vidonge hivyo ambavyo havina vichocheo kama vile wanavyotumia wanawake ambavyo huingia katika mfuko wa mbegu za uzazi na kisha kuzidhoofisha.
Matokeo ya utafiti huo  ambayo yalichapishwa Agosti mwaka huu yanaonyesha kuwa vidonge hivyo vya uzazi kwa wanaume vitazuia kutunga mimba bila ya kuathiri uwezo wa mwanamume kushiriki tendo la ndoa kama kawaida.
Dk James Brander wa Taasisi ya Dana-Farberanasema utengenezaji wa  vidonge vya uzazi wa mpango kwa wanaume  umekuwa na changamoto kubwa kutokana na  upatikanaji wa dawa ambazo zinaweza kuzuia  mfumo wa utengenezwaji wa  seli za mbegu za kiume.
Dawa hizo ziitwazo JQI zilizotengenezwa katika maabara ya Bradner zinafanya kazi kwa kulenga protini maalumu zilizoko katika korodani  ambazo ni muhimu katika uzazi.
Vidonge hivyo vilichanganywa na vichocheo vya ‘Desogetrel’ ambazo huzuia uzalishwaji wa mbegu za kiume.
Profesa Malise Kaisi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba Shirikishi Muhimbili (Muhas) ambaye ni Mtanzania wa kwanza kuzalisha watoto kwa njia ya upandikizaji (IVF) anasema ana wasiwasi mkubwa kuhusu dawa hizo kutumiwa kwa wanaume.
“Dawa za uzazi wa mpango ni rahisi kutumiwa na  wanawake kwa sababu wanawake wana mfumo mwepesi kwa dawa kufanya kazi na kuzuia utungishwaji wa mimba,” anasema.
Hata hivyo, Profesa Kaisi anahisi  kwa wanaume itakuwa hatari kwao kutumia dawa hizo kwani kunaweza kusababisha hata kuua kabisa uzalishwaji wa mbegu.
“Wanaume wana maumbile tofauti na mwanamke. Korodani za mwanaume ni kama kiwanda kinachofanya kazi usiku na mchana. Kwa siku moja mwanamume anazalisha mbegu milioni 10,” anafafanua Prof.  Kaisi.
Katika kuzifanyia utafiti, panya dume alipewa dawa hizo, kisha akawekwa pamoja na mwenza wake ambapo  licha ya kujamiiana hata baada ya miezi kadhaa  panya jike hakupata mimba
 Utafiti huo ulibaini kuwa pamoja na kuzuia uzalishwaji wa mbegu, vilevile dawa hizo zilionekana kuwa hazina madhara yeyote kwa kuwa hazina mchanganyiko wa vichocheo vya aina yoyote.
“Hazikuwa na madhara ya vichochezi (hormone). Mwanamume atakayezitumia hatabadilika tabia au mwili kupata mabadiliko yeyote yale” anasema Dk Martin Matzuk, mtafiti mwingine wa dawa hizo.
Dk Matzuk anasema hakuna kinga yeyote nyepesi ya uzazi wa mpango kwa wanaume iliyowahi kugunduliwa tangu kugunduliwa kwa mipira ya kiume miongo kadhaa iliyopita.
Inaelezwa kuwa utafiti huo  ni mkubwa na utakaoleta mapinduzi katika uzazi wa mpango baada ya vidonge vya uzazi kwa wanawake kuonekana na upungufu kadhaa.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake, Cyriel Massawe wa Chuo  Kikuu cha Sayansi ya Tiba Shirikishi Muhimbili , anasema iwapo kweli dawa za uzazi wa mpango zitagunduliwa basizitasaidia wanandoa kujadili namna bora zaidi ya kupanga uzazi.
“Wenza wanapokuwa na uchaguzi wa kutosha wa namna ya kupanga uzazi inawasaidia wote wawili. Kwa mfano kama mama ana matatizo kadhaa, basi baba atachukua jukumu la kutumia vidonge ili kupanga uzazi,” anasema Dk Massawe.
Anasema kwa sasa wanaume wana njia moja tu ya kupanga uzazi ambayo ni mipira ya kiume hivyo basi iwapo njia nyingine zaidi zimepatikana basi itasaidia.
Dk Massawe anasema vidonge vya uzazi wa mpango kwa wanaume  bado vina changamoto kwa sababu ya mfumo wa uzazi wa mwanamume.
“Zile dawa zinatakiwa zikazuie uzalishwaji wa mbegu kwa wanaume kwa hiyo ili kuingilia mfumo wa uzalishwaji na  pindi mwanamume atakapoacha kutumia awe kama kawaida…ni changamoto” anasema.
Hata hivyo, Dk Massawe anasisitiza kuhusu ushirikiano wa wenza katika kupanga uzazi na kusema kuwa, ni suala linalohitaji watu wawili kujadiliana ili kujua ni njia ipi na salama ya uzazi wa mpango.
 Anaongeza kuwa wenza wanapopanga uzazi itawasaidia kuimarisha afya zao, za watoto na hata kupunguza mzigo wa majukumu ambayo hayakutarajiwa.
Utafiti mwingine unaofanana na huu ulifanywa mwaka 2010 ambapo wanasayansi waliwauliza wanawake na wanaume iwapo wanaume wanaweza kutumia dawa za uzazi wa mpango  pindi zitakaposhauriwa na 
 Katika utafiti huo ulioongozwa na Dk JudithEberhardt wa Chuo Kikuu cha Masuala ya Jamii,wanaume, 140 na wanawake 240 waliulizwa kuhusu matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango kwa wanaume.
 Hata hivyo matokeo ya utafiti yalionyesha kuwa ingawa wanaume wote walisema watafurahi kutumia vidonge hivyo lakini wanawake walipata hofu iwapo wenza wao watakubali kutumia vidonge hivyo au kuvitumia inavyotakiwa ili kuimarisha uzazi wa mpango.
 Katika utafiti huo, wanaume walio kwenye mahusiano ya kudumu walitoa maoni ya kuvikubali vidonge hivyo huku wale walio katika mahusiano ya muda mfupi waliikosoa njia hiyo ya uzazi wa mpango.
Mei 2009, wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Manchester, Uingereza walitumia wanawake na wanaume kuzifanyia utafiti njia za uzazi wa mpango kwa wanaume kujua iwapo zinafanya kazi ipasavyo na zina manufaa.
 Watafiti hao waliwaambia wenza walioshiriki katika utafiti huo kuwa wanaume pekee watumie njia za uzazi wa mpango huku wanawake wakiambiwa kutotumia njia yeyote ili kupima iwapo njia za uzazi wa mpango zinafanya kazi kwa ubora au la.
Hata hivyo, wanaume kadhaa  nchini walioulizwa  iwapo watakubali kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango ikiwemo vidonge na wanaume wanane kati ya kumi, walikataa kutumia njia yeyote ile.
 Mmoja wao,     Edwin Mnzeru anasema, yeye na mke wake hawawezi kutumia njia ya uzazi wa mpango  ya vidonge, mipira ya kiume, wala ya kitanzi   kwa sababu  zina madhara kiafya na ni kinyume na dini.
chanzo:mwananchi

SERENGETI FIESTA 2013 NDANI YA MUSOMA USIKU WA LEO IMEBAMBA MBAYA




 Msanii mwingine anaefanya vyema hivi sasa katika anga ya muziki wa Bongofleva,Rich Mavoko akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu,mbele ya wakazi wa mji wa musoma waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Karume mkoani Mara.

 Madansa wa msanii wa muziki wa kizazi kipya,Shilole wakitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya Uwanja wa Karume,ndani ya mji wa Musoma mkoani Mara

 Anajiita tajiri wa Mahaba Cassim Mganga kutoka Manzabay akiwaimbisha jukwaani wakazi wa mji wa Musoma

 Mashabiki wakijinafasi kwa raha zao.

 Kundi la Wanaume TMK likiongozwa na Chege na Temba wakilishambulia jukwaa la serengeti fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.

 Mkali mwingine wa muziki wa Reggae kutoka kanda ya Ziwa,Jita Man akiwakumusha mashabiki wa muziki wake enzi hizo,mbele ya wakazi wa mji wa Musoma usiku huu

Anaitwa Godzilla kutoka maskani ya Sala sala,akishusha mistari yake live mbele ya mashabiki wake waliojitokeza kwenye tamasha la serengeti fiesta

Makamuzi yakiendelea jukwaani

 Sehemu ya umati wa watu.

 Msanii wa muziki wa bongofleva ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga hizo,Neylee akiimba jukwaani wakati wa tamasha la serengeti fiesta 2013  ndani ya uwanja wa Karume,Musoma mkoani Mara.

 Kundi la Wanaume TMK Halisi likiongoza na msanii nguli Juna Nature wakilishambulia vyema jukwaa  kwa staili yao mapanga shaa shaa,huku mayowe yakipigwa kutoka mashabiki.

Kila shabiki alikuwa na mzuka wake.

 Mashabiki wa tamasha la serengeti fiesta wakifuatilia yanayojiri ndani ya uwanja wa Karume

 Sehemu ya umati wa watu ndani ya uwanja wa Karume

 Mwanadada Shilole akionesha umahiri wake wa kunengua jukwaani mbele ya maelfu ya watazamaji waliojitokeza  kwenye tamasha la Serengeti fiesta 2013.

 Anaitwa Linah Sanga,kutoka nyumba ya vipaji THT akiimba jukwaani


 Watu kibao,kila mmoja akijaichai kivyake huku jukwaa likiwaka moto vilivyo kwa miondoko ya bandika bandua ya wasanii wanaotumbuiza. 

 Wakali wengine wanaokuja kwa kasi katika anga bongofleva-hip hop,Stamina na Youngkiller wakilishambulia jukwaa kwa kushusha mistari mikavu live.

 Shangwe kila kona za mashabiki zimetawala uwanjani hapa.

DAKTARI FEKI AKAMATWA HOSPITALI YA MUHIMBILI



              DAKTARI anayedaiwa kuwa bandia amekamatwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, akiwa na vitambulisho bandia vya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Muhimbili cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS) akisomea Shahada ya Pili.
 
‘Daktari’ huyo ambaye amekuwa akitafutwa na uongozi wa chuo kwa zaidi ya mwaka alikamatwa jana asubuhi akiwa hospitalini hapo karibu na jengo kilimo kitengo cha meno.
Katika kitambulisho chake cha kupigia kura anatambulishwa kwa jina la Dismas John Macha aliyezaliwa mwaka 1979 Kilimanjaro na anaishi maeneo ya Upanga Magharibi, Dar es Salaam.
 
Gazeti hili, lilimshuhudia mtuhumiwa huyo akiwa katika kituo cha usalama cha Muhas na kupekuliwa na askari Polisi wa Muhimbili, Anthony Mwamatepela na kukutwa akiwa na vifaa vya udaktari .
 
Baadhi ya vifaa alivyokutwa navyo ni pamoja na koti jeupe la udaktari na stetoskopu ambacho ni kifaa cha kusikilizia mapafu yanavyofanya kazi na mapigo ya moyo.
 
Pia alikuwa na begi jeusi lenye aina mbalimbali za dawa, vitambulisho na karatasi nyingi, lakini alipoulizwa alidai kuwa hizo ni dawa zake.
 
Macha alikutwa pia na vitambulisho vitatu tofauti, kimoja kikimtambulisha kuwa mwanafunzi wa Muhas wa Shahada ya Pili ya Udaktari (Masters of Medicine ) yenye jina la Macha Dismas kikionesha kusajiliwa kwa namba 60520/2011 na kumaliza muda wake Septemba 30 mwakani. Kitambulisho kingine kilimtambulisha kwa jina la Macha Rogers anayesoma Shahada hiyo hiyo ikionesha kuwa anamaliza masomo yake mwakani.
 
Alikutwa pia na kitambulisho kinachomwonesha kuwa mwanafunzi wa Shahada ya Kwanza na kadi ya anuani yenye jina la Amos Nnko ambaye ni Ofisa Rasilimaliwatu wa Chuo hicho.
 
Akizungumzia alivyomkamata askari wa chuo hicho, Fulgence Semfukwe alisema walimkamata baada ya kupata taarifa za yeye kuwa maeneo hayo na kupanga mbinu za kumkamata.
 
Alisema saa 4.45 asubuhi jana alimkuta kwenye jengo la meno na kumwomba kwa nafasi yake ya udaktari amsaidie tatizo lake na hivyo waongee pembeni, naye bila wasiwasi akakubali. Alimwuliza anatibu magonjwa gani naye kumjibu anatibu maradhi ya aina nyingi na kumwomba kitambulisho na yeye kumpa cha kwake.
 
Baada ya hapo alishituka na kudai kuwa ni daktari wa Mwananyamala na amekuja hapo kwa ajili ya kuona wagonjwa wake wa dharura ndipo alipokamatwa na kupelekwa kituo cha Polisi.
 
Alisema amekuwa akiwachenga kwa muda mrefu kutokana na kuwa kila walipopewa taarifa yuko wodi au sehemu Fulani hawakumkuta kwani walipishana naye baada ya kuvua koti na kuweka kwenye begi lake jeusi.
 
Akizungumza na gazeti hili, Macha limweleza mwandishi wa habari hizi kuwa yeye ni mwanafunzi ambaye anaelewa masuala yote ya matibabu, lakini alifeli chuoni hapo mwaka jana.
 
Alidai kuwa dawa alizokutwa nazo ni zake kwani ana matatizo katika njia ya mkojo na kifua huku akiamua kufanya hivyo kutokana na ugumu wa maisha.
 
“Uwezo wa kutibu ninao na nimesoma katika chuo hiki, lakini mwaka jana nilifeli ndiyo maana nikaamua kuwa hivi,” alisema.
 
Ofisa Uhusiano wa Muhas, Hellen Mtui alisema kutokana na kukamatwa na nyaraka akijitambulisha kuwa mwanafunzi wa ‘Masters of Medicine’, ambaye anaweza kutibu watu hawana uhakika na idadi ya watu ambao ameshatapeli hospitalini hapo.
 
Kuhusu kusoma Muhimbili, Mtui alikana akisema baada ya kupekua nyaraka za chuo hawakubaini jina la mwanafunzi wa aina hiyo na katika vyeti vyake bandia vinaonesha kusainiwa na Mkuu wa Chuo aliyekuwapo kabla chuo hakijapanda hadhi na kuwa chuo kikuu.
 
Mtui alisema baada ya kumkamata na kumpiga picha akiwa na mavazi ya udaktari, kumpekua na kumhoji walimpeleka katika kituo cha Polisi cha Selander Bridge kwa mahojiano na uchunguzi zaidi.

-Habari leo

MWALIMU MKUU ANASWA NA MAGUNIA 6 YA BANGI HUKO MKOANI KAGERA...!!


               MWALIMU Mkuu wa Shule ya Msingi Mukubu, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Silidion Kaiza (43), anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na bangi gunia sita.
  
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi alisema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 17, mwaka huu, shuleni hapo katika kata na kijiji cha Muganza majira ya saa tano asubuhi.

  
Alisema kuwa raia wema walitoa taarifa kituo cha polisi Rulenge kwamba kuna mwalimu anajihusisha na biashara ya kuuza dawa za kulevya, jambo walilohofia kuwa huenda akawaathiri wanafunzi wa shule hiyo kwani anazihifadhi shuleni.
  
Kalangi alifafanua kuwa baada ya polisi kupata taarifa hiyo walifika shuleni hapo na kumhoji mwalimu Kaiza, na alikiri kufanya biashara hiyo kisha akawapeleka katika moja ya darasa ambalo alikuwa akitunza bangi hiyo.
  
Kamanda alisema kuwa baada ya polisi kukamata bangi hiyo, waliifikisha kituoni na kwamba mwalimu huyo anaendelea kuhojiwa kisha atafikishwa mahakamani wakati wowote ili kujibu tuhuma hizo.
  
Aliwataka wananchi kuendelea kuwafichua wahalifu wanaojihusisha na vitendo vya uuzaji wa dawa za kulevya ambavyo vimekuwa tishio kwa taifa.

STORI YA KUSIKITISHA:MLEMAVU AFICHWA NDANI MIAKA 12 BILA KULIONA JUA

 
       Ni umbali wa kilomita saba kutoka katikati ya Mji wa Dodoma upande wa Mashariki barabara iendayo Morogoro, kipo kijiji maarufu cha Nzuguni.

Katika Mtaa wa maarufu wa Mapinduzi iko familia ambayo wakati mwingine kwa mtu wa kawaida unaweza usiamini simulizi yake lakini ni ukweli mtupu kwamba kuna tatizo katika familia hiyo jambo ambalo linahitaji juhudi za makusudi kuwasaidia.

Waswahili wanasema ‘kama hujui kifo basi kachungulie kaburi’ hivyo basi, hali ya maisha ya familia hii kwa ujumla inahitaji kusaidiwa, wanaishi kwenye katika kibanda kidogo cha tope.

 Ni katika familia ya Lameck Mwitewe Senyagwa na mkewe Anastazia Alfred yupo Stephen Lameck (21), kijana ambaye hajui mwanga wa jua la kijiji hicho ukoje, wala haijulikani ni lini kijana huyo ataishi walau kama binadamu wengine.

Stephen (Leba) ni mtoto wa kwanza katika familia ya  watoto wanne wote wakiwa wa kiume, lakini yeye pekee ndiye ambaye hajawahi kuyafaidi maisha katika kipindi chote cha uhai wake.

Ni mlemavu wa miguu, mgongo na hazungumzi chochote ingawa kwa ishara anaweza kueleza nini anachotaka kutendewa wakati huo.

Kwa namna ilivyo, angeweza hata kuendesha baiskeli ya miguu mitatu, lakini nani wa kumpa baiskeli hiyo ili imsaidie kijana huyo kuona mwanga wa jua, ni tabu na mateso makubwa juu yake.

Nilifika katika kibanda kidogo ambacho familia hiyo ya watu sita (watoto wanne na wazazi wawili wanaishi), inatia huruma lakini ndiyo hali halisi waliyo nayo, na haikuwa mara ya kwanza kuona maisha duni kama hayo isipokuwa mateso yapo kwa Stephen.

Simulizi ya mama mzazi

Katika kibanda hiki, nakutana na mama mzazi wa kijana huyu, mara baada ya kujitambulisha anaonyesha ushirikiano,  isipokuwa anapinga mimi kuingia ndani huku akitaka historia ya kijana wake niipate nikiwa nje. Baada ya dakika kadhaa tunakubaliana kuingia ndani aliko Leba.

Nilitaka kujua historia kamili na yeye alianza kwa kusimulia “Leba ni mwanangu wa kumzaa, ndiye mtoto wangu mkubwa kati ya watoto wanne,” anaanza kusimulia Anastazia Alfred.

Mama huyo anasema kuwa tatizo la kutokutembea kwa Leba halikumuanza hivi karibuni, bali ni tangu alipokuwa tumboni na lilitokana na tatizo alilokuwa nalo mama yake mzazi kabla ya kuzaliwa kwa mtoto.

Chanzo cha ulemavu

Anasema tatizo la mwanaye lilianza katika ugonjwa ambao yeye mzazi aliupata wakati akiwa na mimba ya miezi sita.

“Niliambiwa kuwa ninaumwa kifafa cha uzazi, wakati huo nilikuwa siwezi kufanya jambo lolote na hata macho yangu yalikuwa hayaoni,” anasimulia Anastazia.

Mama huyo anasema  mara baada ya ugonjwa huo kumzidi, alipelekwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma ambako alijifungua mtoto wakati huo akiwa na mimba ya miezi saba.

Anasema baada ya kujifungua, mtoto alikuwa ni dhaifu kiasi kwamba wengi walikata tamaa kuwa asingeliweza kupona. Hata hivyo kwa mapenzi ya Mungu akapona.

Atoroka na kumwacha mtoto

Kwa maneno yake anasema kuwa alitoroka hospitalini na kwenda kwa ndugu zake katika Mtaa wa Makole ambako aliwaeleza kuwa asingekuwa tayari kuendelea kuishi na mtoto ambaye watu walishamwambia kuwa ni mkosi kuishi naye.

Hata hivyo, alikumbana na changamoto nyingine kutoka kwa watu ambao walimtaka arudi tena kwa ajili ya kumchukua mtoto  na kwamba wasingekuwa tayari kumpokea mahali popote kama angerudi bila ya Leba.


“Nilikuwa nimechanganyikiwa na wakati mwingine utoto ulikuwa bado unanisumbua na kwa kuwa sikuwa na mama wakati huo ambaye angeweza kunifunda zaidi hivyo nikaona njia njema ya kunisaidia ni kumtelekeza mtoto,” anasimulia.

Hata hivyo, anampongeza marehemu baba yake kuwa alikuwa ni msaada mkubwa kufanya mtoto huyo aendelee kuishi kwani aliposikia mambo hayo, alimwita kijijini kwao Kwamtoro Wilaya ya Chemba (zamani Kondoa) ambapo alimketisha chini na kumwonya juu ya tendo hilo.

Anasema baba yake huyo alimtaka kuishi na mtoto bila ya kumtenga, na akampa mifano hai ya watu wenye ulemavu ambao wanaishi hadi wakati huo.

Mateso ya mtoto

Mbali na kukubaliana na kuishi na mtoto huyo, hali ya Leba kwa sasa inatisha, hana msaada wowote. Hawezi kutoka nje, amekuwa akifichwa ndani kwa zaidi ya miaka 12 sasa.

Chakula ni tabu, mazingira anayoishi hayaendani na hali yake na haijulikani ni lini atapata nafasi ya kuona mwanga.

Ni zaidi ya miaka 12 sasa kijana huyo anaishi ndani ya nyumba na watu wengi hawamjui licha ya kuwa mama yake anajulikana kwa jina la Mama Leba, mwenye jina majirani hawamjui.

Hiyo itatokana na kushindwa kupata msaada wowote walau wa baiskeli au hata njia nyingine, zaidi ya kutegemea mama yake mzazi ambaye anasema kuwa kijana huyo amekuwa mzito hawezi kumbeba.

Hali ya familia

Maisha ya familia ya Lameck ni magumu, hawana nyumba, wanaishi katika kibanda kidogo ambacho wamepewa na mlo wao ni shida, humlazimu baba wa familia kutafuta kwa bidii huku watoto wote watatu wakimtegema kwa masomo mmoja akiwa kidato cha nne, mwingine amemaliza darasa la saba na wa mwisho  darasa la pili.

Hata hivyo, upendo wa kuwa pamoja bado umeendelea kuwafanya wasitupane wala kuwa na migogoro.

Nini wanahitaji


Anastazia anasema kama watapata nafasi ya kusaidiwa baiskeli kwa ajili ya Leba akaweza kutoka nje, naye angepata nafasi ya kupumua na kutafuta biashara yoyote ya kumsaidia mumewe kwani kwa sasa hawezi kutoka umbali wa mita 100 na kumwacha mtoto.

Anasema katika umri wa miaka mitatu wa kijana huyo, walikutana na mtaalamu kutoka Asia ambaye alisaidiana na wataalamu wa hospitali ya mkoa kumfanyia mazoezi kijana huyo, kiasi cha kumwezesha kwa sasa akipewa baiskeli anaweza kuendesha japo kwa shida.

Kwa sasa ni kama wamepoteza matumaini lakini wanaamini kwa misaada kutoka kwa wasamaria wema labda hali ya maisha yao inaweza kubadilika na kuwa nzuri zaidi ya ilivyo sasa.

-Mwananchi

TAZAMA PICHA NYINGINE 200 PAMOJA NA VIDEO ZA UTAMU ZA MANAIKI SANGA:HII NDIO FUNGA KAZI:

             Katika hali ya kushtua msanii chipukizi Manaiki Sanga “The Don” aliyejipatia umaarufu mkubwa nchini na duniani baada ya picha zake za utupu akiwa na wanawake zaidi ya 400 wakiwemo wazungu akifanya nao ngono nzembe na baadae kusambaa kwenye mitandao yote duniani na kuonwa na mamilioni ya watu hasa wale wanaopata habari kupitia mitandao ya kijamii, sasa ameamua kutengenezea filamu halisi ya matukio hayo akiwa na wanawake walewale aliofanya nao ngono.
                                                   <<BOFYA HAPA KUONA PICHA NA VIDEO HIZO>>

RECORD:HUYU NDIYE MZEE ALIYEVUNJA REKODI YA KUWA NA WATOTO 130 KUTOKA UGANDA.....CHEKI VIDEO YAKE

 

WAKE WENZA WASHIKANA UCHAWI HUKO KIMARA...!!


 
WANAWAKE wawili walioolewa katika familia moja ‘wake wenza’, mama Hashimu na mama Fadhila, wakazi wa Kimara King’ong’o jijini Dar, hivi karibuni walifikishwa serikali za mtaa kwa kosa la kutukanana matusi ya nguoni pamoja na kushikana uchawi.
Inadaiwa kuwa wanawake hao ‘walimwagiana’ matusi hayo usiku wa manane na kusababisha watu wengine kukosa usingizi na kukusanyika kuwasikiliza.
Mara baada ya kufikishwa serikali ya mtaa, wake wenza hao walitakiwa kueleza ugomvi wao na kila mmoja kuanza kushusha tuhuma kwa mwenzake.
Mapaparazi wetu waliwashuhudia wakati wake wenza hao walipokuwa wakijieleza mbele ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King’ong’o, Demetrius Mapesi na Mtendaji wake Amina Rashid.
Mama Hashimu alianza kuelezea kisa kizima na kufuatiwa na mama Fadhila ambaye wakati akijieleza alipandisha mori kiasi cha kumfanya atake kumrukia mwenzake.
Unajua nasikia hasira sana kwa sababu mama Fadhila ameniita mchawi huko mtaani unadhani mimi nitaelewekaje? Ukweli kauli hiyo inaniuma sana,” alisema mama Hashim na kuangua kilio.
Hata hivyo, baada ya kila mmoja kueleza ya moyoni, mwenyekiti wa serikali za mtaa pamoja na mtendaji wake, waliwaamuru wake wenza hao kupeana mkono na kuombana msamaha. 

“Sasa hapa hakuna kesi, kwani wote mna makosa, hebu niambieni mnawafundisha nini watoto wetu kwa matusi
mliyotukanana hadharani?” alihoji mwenyekiti na kuwataka wayamalize mambo hayo.
Aidha, mwenyekiti huyo aliahidi kuwafuatilia ili kuona kama watakuwa wamebadili tabia zao.
Kama vile haitoshi aliwaahidi kama watarudia atawahamisha mtaa pamoja na waume zao kwani mtaani kwao hawahitaji watu wanaotukanana ovyo na kuzushiana mambo ya kichawi.
Baada ya tamko la mwenyekiti, mtendaji wake aliwaamuru wake wenza hao kuandika matusi waliyotukanana kisha akawapiga faini ya shilingi 20,000 kila mmoja.
“Kutokana na matusi yenu nalazimika kuwapiga faini ya shilingi elfu ishirini kila mmoja, ingawaje kwa mujibu wa sheria ya Tanzania mtu akikutwa na hatia ya kutukana anatakiwa kutozwa faini ya shilingi elfu hamsini au kufungwa jela miezi sita,” alisema mtendaji huyo.
Kila mmoja alilipa nusu ya faini na kuahidi kumalizia huku wakisema kuwa hawatarudia kufanya kosa hilo tena

HAWA NDIO WEZI WA MTANDAO WALIOKAMATWA KATIKA OFISI ZA TIGO BUGURUNI...!!

                            Huyu ndiye mhusika mkuu aliyechonga mchongo wote na kumshawishi mwanamke kutumia kitambulisho chake kufanyiwa wizi huo wa kimtandao.Mrembo akijitetea kuwa hahusiki kabisa katika wizi huu na pia kujitetea kuwa kaacha mtoto mdogo nyumbani.
Hapa akitoa maelezo kuwa yeye si mwizi  na hawafahamu kabisa wahusika wenzake na yeye ni mfanyabiashara wa vipodozi.

Mrembo huyu ni mmoja wa watuhumiwa wa kesi hii ya wizi wa mtandao baada ya kutumia kitambulisho chake na  kutaka kuja kurudisha line ambayo siyo yake kwa kuahidiwa kupewa pesa kidogo kama ujira wake na katika maelezo yake akasema hawatambui wahusika wenzake kwani amekutana nao tu Sinza na wakampa dili hilo na kuamua kuchukua bajaji ambayo iliwaleta mpaka ofisi za Tigo zilizopo Rozana, Buguruni.

Watuhumiwa wenzake wakificha sura zao huku wakitoa maelezo kwa wafanyakazi wa Tigo na walinzi waliowatia chini ya ulinzi baada ya kuweka mtego mzuri wa kuyanasa matapeli hayo ya kimtandao.Kitambulisho alichotaka kutumia mwanamke kuswap line ambayo sio yake lakini aliweka jina la mhusika wa line na namba alizokuwa anapiga mara nyingi ndipo mfanyakazi mmoja wa Tigo kwa jina Octavian Rweyendera alifanikiwa kubaini udanganyifu huo na kuamuru awekwe chini ya ulinzi  mara moja.Aliyesimama hapo yeye alibiwa kiasi cha miioni moja kwa njia ya Sim Banking ya NMB baada ya line kuharibika ghafla kumbe mmoja wa watuhumiwa ali-renew na kuiba pesa zake.
Hapa mtuhumiwa mmoja akiwa kajilaza chini kwa kugoma kutoa maelezo kwa walinzi.Hapa huyu binti akilia kwa uchungu na kuomba asamehewe.Wakiwa ndani ya gari la polisi kuelekea kituo cha polisi Buguruni.Umati wa watu uliofurika kushuhudia tukio hilo la aina yake.
Mmoja ya wafanyakazi mahiri wa Tigo, Octavian Rweyendera ambaye alifanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao akitoa maelezo kwa baadhi ya wa polisi jinsi watuhumiwa walivyotaka kufanya wizi huo wa mtandao.
Askari polisi wakisikiliza kwa makini jinsi watuhumiwa hao walivyokamatwa.