Showing posts with label UNYAMA. Show all posts
Showing posts with label UNYAMA. Show all posts

Saturday, 21 September 2013

SHUHUDIA PICHA ZAIDI YA 20 ZA MAUAJI YA KUTISHA YALIYOTOKEA NCHINI KENYA LEO, INASIKITISHA KWA KWELI!






              WATU waliokuwa na silaha wamefyatua risasi mjini Nairobi, Kenya, kwenye eneo la maduka katika mtaa wa Westlands.
Walioshuhudia tukio hilo, wanasema kuwa maguruneti piya yalitumika.
Inaarifiwa watu watano wamekufa.(P.T)

Mwandishi wetu mjini Nairobi anaeleza kuwa washambuliaji inaarifiwa walivaa vilemba kama vya al-Shabaab, lakini haikuthibitishwa kama wapiganaji hao wamehusika.
Polisi waliojihami kwa silaha wamezingira jengo la maduka liitwalo Westgate, katika mtaa wa Westlands, na kuna taarifa ya watu waliojeruhiwa wakitolewa hapo kwa machera.



























Friday, 20 September 2013

STORI YA KUSIKITISHA:MLEMAVU AFICHWA NDANI MIAKA 12 BILA KULIONA JUA

 
       Ni umbali wa kilomita saba kutoka katikati ya Mji wa Dodoma upande wa Mashariki barabara iendayo Morogoro, kipo kijiji maarufu cha Nzuguni.

Katika Mtaa wa maarufu wa Mapinduzi iko familia ambayo wakati mwingine kwa mtu wa kawaida unaweza usiamini simulizi yake lakini ni ukweli mtupu kwamba kuna tatizo katika familia hiyo jambo ambalo linahitaji juhudi za makusudi kuwasaidia.

Waswahili wanasema ‘kama hujui kifo basi kachungulie kaburi’ hivyo basi, hali ya maisha ya familia hii kwa ujumla inahitaji kusaidiwa, wanaishi kwenye katika kibanda kidogo cha tope.

 Ni katika familia ya Lameck Mwitewe Senyagwa na mkewe Anastazia Alfred yupo Stephen Lameck (21), kijana ambaye hajui mwanga wa jua la kijiji hicho ukoje, wala haijulikani ni lini kijana huyo ataishi walau kama binadamu wengine.

Stephen (Leba) ni mtoto wa kwanza katika familia ya  watoto wanne wote wakiwa wa kiume, lakini yeye pekee ndiye ambaye hajawahi kuyafaidi maisha katika kipindi chote cha uhai wake.

Ni mlemavu wa miguu, mgongo na hazungumzi chochote ingawa kwa ishara anaweza kueleza nini anachotaka kutendewa wakati huo.

Kwa namna ilivyo, angeweza hata kuendesha baiskeli ya miguu mitatu, lakini nani wa kumpa baiskeli hiyo ili imsaidie kijana huyo kuona mwanga wa jua, ni tabu na mateso makubwa juu yake.

Nilifika katika kibanda kidogo ambacho familia hiyo ya watu sita (watoto wanne na wazazi wawili wanaishi), inatia huruma lakini ndiyo hali halisi waliyo nayo, na haikuwa mara ya kwanza kuona maisha duni kama hayo isipokuwa mateso yapo kwa Stephen.

Simulizi ya mama mzazi

Katika kibanda hiki, nakutana na mama mzazi wa kijana huyu, mara baada ya kujitambulisha anaonyesha ushirikiano,  isipokuwa anapinga mimi kuingia ndani huku akitaka historia ya kijana wake niipate nikiwa nje. Baada ya dakika kadhaa tunakubaliana kuingia ndani aliko Leba.

Nilitaka kujua historia kamili na yeye alianza kwa kusimulia “Leba ni mwanangu wa kumzaa, ndiye mtoto wangu mkubwa kati ya watoto wanne,” anaanza kusimulia Anastazia Alfred.

Mama huyo anasema kuwa tatizo la kutokutembea kwa Leba halikumuanza hivi karibuni, bali ni tangu alipokuwa tumboni na lilitokana na tatizo alilokuwa nalo mama yake mzazi kabla ya kuzaliwa kwa mtoto.

Chanzo cha ulemavu

Anasema tatizo la mwanaye lilianza katika ugonjwa ambao yeye mzazi aliupata wakati akiwa na mimba ya miezi sita.

“Niliambiwa kuwa ninaumwa kifafa cha uzazi, wakati huo nilikuwa siwezi kufanya jambo lolote na hata macho yangu yalikuwa hayaoni,” anasimulia Anastazia.

Mama huyo anasema  mara baada ya ugonjwa huo kumzidi, alipelekwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma ambako alijifungua mtoto wakati huo akiwa na mimba ya miezi saba.

Anasema baada ya kujifungua, mtoto alikuwa ni dhaifu kiasi kwamba wengi walikata tamaa kuwa asingeliweza kupona. Hata hivyo kwa mapenzi ya Mungu akapona.

Atoroka na kumwacha mtoto

Kwa maneno yake anasema kuwa alitoroka hospitalini na kwenda kwa ndugu zake katika Mtaa wa Makole ambako aliwaeleza kuwa asingekuwa tayari kuendelea kuishi na mtoto ambaye watu walishamwambia kuwa ni mkosi kuishi naye.

Hata hivyo, alikumbana na changamoto nyingine kutoka kwa watu ambao walimtaka arudi tena kwa ajili ya kumchukua mtoto  na kwamba wasingekuwa tayari kumpokea mahali popote kama angerudi bila ya Leba.


“Nilikuwa nimechanganyikiwa na wakati mwingine utoto ulikuwa bado unanisumbua na kwa kuwa sikuwa na mama wakati huo ambaye angeweza kunifunda zaidi hivyo nikaona njia njema ya kunisaidia ni kumtelekeza mtoto,” anasimulia.

Hata hivyo, anampongeza marehemu baba yake kuwa alikuwa ni msaada mkubwa kufanya mtoto huyo aendelee kuishi kwani aliposikia mambo hayo, alimwita kijijini kwao Kwamtoro Wilaya ya Chemba (zamani Kondoa) ambapo alimketisha chini na kumwonya juu ya tendo hilo.

Anasema baba yake huyo alimtaka kuishi na mtoto bila ya kumtenga, na akampa mifano hai ya watu wenye ulemavu ambao wanaishi hadi wakati huo.

Mateso ya mtoto

Mbali na kukubaliana na kuishi na mtoto huyo, hali ya Leba kwa sasa inatisha, hana msaada wowote. Hawezi kutoka nje, amekuwa akifichwa ndani kwa zaidi ya miaka 12 sasa.

Chakula ni tabu, mazingira anayoishi hayaendani na hali yake na haijulikani ni lini atapata nafasi ya kuona mwanga.

Ni zaidi ya miaka 12 sasa kijana huyo anaishi ndani ya nyumba na watu wengi hawamjui licha ya kuwa mama yake anajulikana kwa jina la Mama Leba, mwenye jina majirani hawamjui.

Hiyo itatokana na kushindwa kupata msaada wowote walau wa baiskeli au hata njia nyingine, zaidi ya kutegemea mama yake mzazi ambaye anasema kuwa kijana huyo amekuwa mzito hawezi kumbeba.

Hali ya familia

Maisha ya familia ya Lameck ni magumu, hawana nyumba, wanaishi katika kibanda kidogo ambacho wamepewa na mlo wao ni shida, humlazimu baba wa familia kutafuta kwa bidii huku watoto wote watatu wakimtegema kwa masomo mmoja akiwa kidato cha nne, mwingine amemaliza darasa la saba na wa mwisho  darasa la pili.

Hata hivyo, upendo wa kuwa pamoja bado umeendelea kuwafanya wasitupane wala kuwa na migogoro.

Nini wanahitaji


Anastazia anasema kama watapata nafasi ya kusaidiwa baiskeli kwa ajili ya Leba akaweza kutoka nje, naye angepata nafasi ya kupumua na kutafuta biashara yoyote ya kumsaidia mumewe kwani kwa sasa hawezi kutoka umbali wa mita 100 na kumwacha mtoto.

Anasema katika umri wa miaka mitatu wa kijana huyo, walikutana na mtaalamu kutoka Asia ambaye alisaidiana na wataalamu wa hospitali ya mkoa kumfanyia mazoezi kijana huyo, kiasi cha kumwezesha kwa sasa akipewa baiskeli anaweza kuendesha japo kwa shida.

Kwa sasa ni kama wamepoteza matumaini lakini wanaamini kwa misaada kutoka kwa wasamaria wema labda hali ya maisha yao inaweza kubadilika na kuwa nzuri zaidi ya ilivyo sasa.

-Mwananchi

Wednesday, 18 September 2013

SAMAHANI KWA HIZI PICHA: MTU MMOJA APOTEZA MAISHA BAADA YA KUSHAMBULIWA NA SIMBA HUKO MKOANI LINDI...

Mwanakijiji mmoja (45) mkoani LINDI wilayani NACHINGWEA katika kijiji cha LIONJA ameuwawa kinyama na simba wakati akielekea shambani alfajiri kwenda kuangali korosho, wakati akielekea shambani ndipo aliposhambuliwa na simba hao wawili.
Kabla ya tukio hilo simba hao walikuwa wakishambulia mbwa katika kijiji hicho, Tukio hilo lilitokea siku chache zilizopita.
MUNGU ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi..AMEN








Wanakijiji wakitaharuki baada ya kuona mwili wa marehemu....

Tuesday, 17 September 2013

INASIKITISHA SANA...!!! MWANAMKE ABAKWA NA KISHA KUFUKIWA ARDHINI AKIWA HAI...

TAZAMA VIDEO YA MWAMKE ALIYEFANYIWA UKATILI WA HALI YA JUU:MWANAUMWE ASIYEKUWA NA HURUMA AMBAKA NA KISHA KUFUKIA CHINI YA ARDHI TENA AKIWA MZIMA NA MTUPU KAMA ALIVYOZALIWA:TAFADHALI KAMA UNA ROHO NYEPESI TUNAKUOMBA USITAZAME VIDEO HII:Tazama video yenyewe hapo chini.....

Saturday, 14 September 2013

MTOTO WA MIAKA 7 ACHOMWA MOTO MIKONO NA MAMA YAKE MZAZI KISA ADAI ALIIBA MAYAI YA KUKU MKOANI MBEYA

 
Mtoto EMILLY GEORGE[7] Mkazi wa kijiji cha RUANDA wilaya ya Mbeya akilia kwa uchungu maumivu ya vidonda baada ya kuchomwa moto na mama yake mzazi kisa akidaiwa kuiba mayai ya kuku jamani ukatili gani huu?
 
Mama mzazi wa mtoto aliyechomwa moto  ELESIA MWASILE[41]  akipelekwa kituoni na wanausalama
 

 



Hapa wanausalama na mama mzazi wa mtoto huyo wakielekea kumwona mtoto huyo katika hospitali ya Rufaa Mbeya

 

Baada ya kukamatwa mama huyo katili alkabidhiwa kwa Dawati la Polisi Jinsia na watoto chini ya Kiongozi wa Wilaya D\SSGT PUDENSIANA BAITU akimjulia hali mtoto Emilly
Wimbi la ukatili dhidi ya watoto bado limezidi kuchukua sura mpya baada ya mtoto EMILLY GEORGE[7] Mkazi wa kijiji cha RUANDA wilaya ya Mbeya kuunguzwa vibaya mikono yote miwili na mama yake mzazi ELESIA MWASILE[41] kwa maji ya moto kisha kufungiwa ndani kwa siku saba bila matibabu yoyote.

Akiongea huku akitetemeka kwa hofu ELESIA amesema kuwa chanzo cha cha kumchoma mtoto huyo ni kutokana na malalamiko ya majirani wakimtuhumu mtoto huyo kujihusisha na vitendo vya wizi vikiwemo wizi wa pesa na mayai ya kuku.

Tukio la mwisho lililopelekea mtoto huyo hadi kuchomwa ni pale ilipodaiwa na mama huyo kuwa mtoto aliiba mayai akidai amechoshwa na tabia za malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa jirani zake.

Baada ya kuunguzwa kikatili mtoto huyo alifungiwa ndani kwa siku saba  bila matibabu yoyote hali iliyowafanya majirani kuuliza aliko mtoto kutokana na mtoto huyo kutoonekana mitaani hali iliyopelekea kutolewa taarifa ofisi ya kijiji ili kubaini aliko mtoto.

Uongozi wa kijiji baada ya kupata taarifa kwa majirani walifanya upekuzi na kumkuta mtoto amefungiwa ndani huku akiwa na majeraha makubwa katika mikono yote miwili ndipo taarifa ilitolewa kituo cha Polisi MBALIZI ambapo mama huyo alikamatwa.

Baada ya kukamatwa mama huyo katili alkabidhiwa kwa Dawati la Polisi Jinsia na watoto chini ya Kiongozi wa Wilaya D\SSGT PUDENSIANA BAITU na Mwenyekiti MARY GUMBO ambaye muda wote alikuwa akiangua kilio kutokana na kitendo alichofanyiwa mtoto na mama yake mzazi.

Hivi sasa mwanamke huyo anahojiwa na Polisi kituo kikuu cha kati na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo na mtoto amelazwa katika Hospitali ya Rufaa wadi namba tano akiendelea kupatiwa matibabu.

Vitendo vya unyanyasaji vimendelea kukemewa Mkoani Mbeya na Asasi mbalimbali hasa kwa watoto vikiwemo vya ubakwaji,ulawiti,kazi za ndani na baadhi ya watoto wamepata ulemavu wa kudumu ikiwemo kupoteza viungo.

TAHADHALI
 PICHA NI MBAYA SANA NDIO MAANA HATUJAZIWEKA ILA KWA MAAMUZI YAKO MWENYEWE UNAWEZA  ANGALIA KWA KUBOFYA HAPO CHINI
                                                       <<picha ya kwanza>> 
                                                                  <<picha ya pili>>

Thursday, 12 September 2013

RIPOTI YA KUSIKITISHA TANZANIA JUU YA UBAKAJI NA ULAWITI KWA WATOTO WADOGO

 
                         NI sahihi kusema kuwa mwaka 2013 ni wa ubakaji, ulawiti na udhalilishaji wa watoto chini ya miaka 18 kufuatia matukio ya aina hiyo kushamiri katika jamii ambapo ripoti inatisha.
Tangu Januari hadi Septemba, mwaka huu, vyombo vya habari nchini vimekuwa vikiripoti matukio hayo hadi inatisha huku vitendo hivyo vikizidi kushika kasi.
Kuna madai kwamba, wengi wanaofanya unyama huo wanaelekezwa na waganga wa kienyeji ili kujipatia utajiri, ingawa ripoti nyingi hazioneshi kama kuna ukwasi ndani yake, bali ni tabia na kushindwa kujizuia.
Watoto wengi waliokumbwa na mikasa hiyo wanakuwa na uhusiano wa karibu na watuhumiwa, kama baba mzazi, baba wa kufikia, mjomba au mtu mwingine wa jirani sana.
Mfano, mtoto wa kike mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu (jina linahifadhiwa), amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru, akiwa hoi baada ya mwanaume aliyejulikana kwa jina moja la John, mkazi wa jijini humo ambaye ni baba wa kufikia, kudaiwa kumbaka.
 John alidaiwa kutenda tukio hilo mwishoni mwa Agosti, mwaka huu nyumbani kwake, majira ya saa 7:00 mchana, kufuatia mama wa mtoto huyo, Christina Ruendi kutishia kuondoka zake kutokana ya kuchoshwa na manyanyaso ya mtuhumiwa huyo na chanzo kikiwa ni mtoto huyo.
Mtuhumiwa huyo alitaka mtoto huyo apelekwe kwa baba yake mzazi.
Siku ya tukio, mwanamke huyo hakuwepo nyumbani, aliporudi alimkuta mtoto wake amelala hajitambui huku sehemu ya kitanda ikiwa imetapakaa damu.
 Mama huyo alipiga kelele ambapo majirani na viongozi wa serikali wa eneo hilo, walifika na kukuta unyama alioutenda mtuhumiwa huyo bila kujali umri wa mtoto huyo na akawa ameshatoroka.
 Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linamtafuta mtuhumiwa huyo huku mtoto huyo akiwa bado kwenye wodi ya watoto hospitalini hapo.
Jijini Dar es Salaam, waandishi wetu wanaripoti kuwa mtoto mmoja wa kiume mwenye miaka 6 (jina tunalo), amedai kulawitiwa na mwanaume mmoja aliyemtaja kwa jina moja la Hamis ambaye ni mmiliki wa kibanda cha kuangalia video, Gongo la Mboto, Dar.
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo hayo baada ya majirani kutilia shaka mwenendo wa mtoto huyo na mtuhumiwa.
Ilidaiwa kuwa baada ya kufuatilia mwenendo wao, ndipo mama aliposhtuka na kumhoji mtoto wake ambapo alikiri kuingiliwa na mwanaume huyo.
Akizungumza  kwa masikitiko, mama mkubwa wa mtoto huyo alisema alibaini kasoro kwa mwanaye huyo kwa kuwa mara nyingi alikuwa akitokwa na haja kubwa bila kujizuia, jambo ambalo lilimshtua.
“Nilimhoji akasema alikuwa akimpeleka vichakani na kumbaka halafu akipiga kelele alikuwa akimtolea kisu na kumtishia,” alisema mama mkubwa huyo.
Wazazi wa mtoto huyo waliripoti ukatili huo kwenye Kituo cha Polisi cha Gongo la Mboto, Dar na kupewa PF3 kwa ajili ya matibabu Hospitali ya Amana kisha wakafungua kesi yenye kumbukumbu namba GBT/RB/3018/2013 KULAWITI, mtuhumiwa anasakwa baada ya kuingia mitini.
Ukiachia mbali watoto kulawitiwa, vitendo vya kuwadhalilisha vimepamba moto nchini ambapo hivi karibuni, kikongwe wa miaka inayokadiriwa kufika sabini aitwaye Babu anakabiliwa na shitaka la kuwafungia ndani kwake wanafunzi kumi wa kike wa Shule ya Msingi Mtoni Kijichi, Temeke, Dar na kuwashika nyeti zao.
Tukio hilo lilibainika Agosti 28, mwaka huu baada ya mwanafunzi mmoja (jina tunalo) kupewa barua awapelekee wazazi wake baada ya kutoonekana shule kwa takriban miezi mitatu kumbe alikuwa anaishia nyumbani kwa kikongwe huyo.
Kwa mujibu wa maelezo aliyoyatoa Kituo cha Polisi Mbagala Kizuiani, mzee huyo alikiri kuwafungia ndani wanafunzi hao kwa muda waliohitajika kuwepo shuleni kwa miezi mitatu na kudai kuwa alikuwa akiwafundisha ‘twisheni’. Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi hao na kufunguliwa kesi yenye kumbukumbu namba MBL/RB 8738/13 UNYANYASAJI.
Jitihada za Amani kumpata Waziri wa Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba, zilishindikana baada ya juzi simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa.
Amani lilizungumza na mchungaji mmoja wa kanisa la kiroho nchini ambaye hakupenda jina lake liandikwe  ambapo alisema wazazi wanapaswa kumwomba sana Mungu ili watoto wao wasikumbwe na ushetani ulioenea sasa Tanzania akisema hali itazidi kuwa mbaya zaidi mwishoni mwa mwaka huu.

Wednesday, 11 September 2013

PICHA NA STORY YA KIJANA ALIYEAMUA KUMCHINJA MPENZI WAKE KAMA KUKU

            Tukio hilo lililoibua simanzi kubwa kutokana na marehemu kuhitimu Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Nyihogo, Kahama mwaka jana, lilijiri saa 12:45 Februari 6, mwaka huu.

Kitendo hicho kilifanyika katika banda la mbuzi lililopo nyumbani kwa kijana huyo ambaye baada ya kutekeleza mauaji na yeye alifanya jaribio la kutaka kujitoa roho kwa kisu.



Jessica Elialinga baada ya kuchinjwa.

Akisimulia juu ya tukio hilo, rafiki wa karibu wa Musa ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa ajili ya usalama, alisema wiki moja kabla ya tukio hilo, mtuhumiwa huyo alikuwa akiwatangazia jamaa zake kwamba ana dhamira ya kumuua binti huyo kufuatia kubaini kuwa anamsaliti kimapenzi.

 
Muuaji Musa Petro.
 “Unajua Musa anafanya kazi ya kuchuna ngozi za wanyama machinjio ya Wilaya ya Kahama, alitutangazia dhamira yake hiyo, lakini tulichukulia kauli yake kama mzaha.

“Alisema anataka kufanya hivyo kwa sababu amekuwa akitumia gharama kubwa kwa mpenzi wake huyo tangu walipoanza uhusiano, msichana akiwa kidato cha pili, lakini anatoka kimapenzi na mwanaume mwingine,” alisema rafiki huyo.

 Hata hivyo, inadaiwa baada ya mtafaruku wa usaliti, wawili hao walipatana na kuendelea na mapenzi, lakini baada ya mwanafunzi huyo kuhitimu kidato cha nne alibadilika ambapo mwanaume alisikia kuwa tayari ana mwanaume mwingine kutoka jijini Mwanza ambaye walikubaliana kufunga pingu za maisha baada ya kumaliza masomo.
Jessica Elialinga enzi za uhai wake.
 Inadaiwa siku chache kabla ya mauaji hayo, rafiki mmoja wa karibu wa mtuhumiwa alikutana na marehemu njiani na kumsimamisha kwa lengo la kumweleza kauli zenye kutishia maisha yake anazozitoa mpenzi wake, lakini binti huyo hakusimama kumsikiliza.

 Baada ya Musa kudaiwa kufaulu kumchinja mpenzi wake huyo na yeye kujikata koromeo na kuanguka akiwa ameishiwa nguvu, kijana mchunga mbuzi ambaye wengi katika eneo hilo humchukulia kama kaka yake Jessica, ndiye aliyekuwa wa kwanza kumshuhudia Musa akiwa katika hali hiyo.

 
 Alipomhoji kulikoni, hakupata jibu zaidi ya kushuhudia jitihada za mtuhumiwa huyo kufungua mlango wa chumbani mwake zikishindikana.

Kijana huyo alitoa taarifa kwa watu ambao walifika na kumchukua Musa na kumkimbiza hospitali ya wilaya kuokoa uhai wake.

Watu waliobaki nyumbani walifuatilia michirizi ya damu hadi kwenye zizi la mbuzi ambako walimkuta Jessica ameshafariki dunia baada ya kuchinjwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Everest Mangala alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani Kahama katika Hospitali ya wilaya hiyo anakoendelea kupatiwa matibabu.

MWANDISHI WA GAZETI LA MWANANCHI AKATWA KATWA MAPANGA MKOANI SINGIDA....

     Mwandishi wa habari wa gazeti la The Citizen na mwananchi mkoani Singida, Awila Silla amenusurika kuuawa na mtu anayedhaniwa kuwa Jambazi baada ya kukatwa katwa  mapanga kichwani na kusababisha kuzirai. Tukio hilo limetokea juzi saa mbili usiku jirani na mahakama ya mwanzo ya Utemini mjini Singida.   

Awila ambaye amelazwa wodi 2   katika hospitali ya mkoa amedai kuwa  baada ya kukutana na kijana huyo aliamuriwa kutoa fedha na baada ya kudai hana, jibu hilo lilisababisha kijana huyo kuanza kumkata Mapanga na alipoangauka na kuzirai alinyang’anywa  simu yake ya  kiganjani.
 Hata hivyo Awila amedai kuwa bado hajatoa taarifa ya tukio hilo polisi.

Tuesday, 10 September 2013

AKATWA MKONO NA MUMEWE KWA UPANGA NA KUSABABISHIWA ULEMAVU WA MAISHA, KISA WIVU...

Mchali akionyesha mkono aliokatwa.Picha na Rehema matowo 

  • Baada ya kuwa katika mapenzi na mwanaume huyo kwa zaidi ya miaka 17, wakipendana na kuitana majina yote mazuri unayoyajua yakiwamo kuambiwa ‘mpenzi wangu nakupenda, nikinywa maji nakuona kwenye glasi’…leo mapenzi yamegeuka shubiri.
Kuna mikasa mbalimbali huwatokea watu katika suala zima la mapenzi, kiasi cha kusababisha baadhi yao kutopenda tena kuingia kwenye jambo hilo wakiliona kama ni kitu kisichofaa, ingawa ukweli unaweza kuwa sio huo.
“Sitaki tena wanaume, ni watu wabaya, wameniumiza moyo wangu mno,” anasema Hawa Francis, mkazi wa Ubungo, Dar es Salaam. Sababu kubwa ni kero ambazo amewahi kuzipata katika suala zima la uhusiano. Vivyo hivyo wapo wanaume hawataki kuoa, kwa maelezo kuwa kuna wanawake wamewahi kuwatesa.
Kama wewe ni kati ya watu ambao umekata tamaa na suala la uhusiano, fahamu kuwa si wewe pekee.Kuna kundi kubwa la watu wameshatendewa kiasi cha kufanya wasiwe na raha tena.

Mkasa wa mwanamke kukatwa mkono

Ilikuwa Agosti 7, mwaka huu, saa mbili usiku. Ilikuwa ni siku iliyobadili historia ya maisha yake. Baada ya kuwa katika mapenzi na mwanaume huyo kwa zaidi ya miaka 17, wakipendana na kuitana majina yote mazuri unayoyajua yakiwamo kuambiwa ‘mpenzi wangu nakupenda, nikinywa maji nakuona kwenye glasi’…leo mapenzi yamegeuka shubiri.
Mwanamke huyo, Mchali Kihiyo (35), mama wa watoto sita, aliyepoteza viungo vyake kutokana na ukatili wa kijinsia uliofanywa na mwanaume ambaye wamekuwa na uhusiano nae (jina limehifadhiwa).
“Uhusiano wetu ulikuwa mzuri, hata hivyo kwa sasa naona mambo yamekuwa magumu kwangu, leo hii mimi sina mkono wa kushoto na nimeondolewa sehemu ya viungo vyangu vya upande mmoja,”anasema Mchali,akibubujikwa machozi kutokana na ulemavu alioupata.
Chanzo cha ulemavu
Anasema maisha yao ya uhusiano yalikuwa ya furaha kwa kipindi chote lakini yamegeuka shubiri baada ya mwanamume wake huyo kuonyesha dalili ya kutompenda kama awali, hali ambayo anaitafsiri kama labda alikuwa na mwanamke mwingine.
Mchali, anasema mikasa na mateso ilianza miaka mitatu iliyopita baada ya kuhisi kwamba mwanamume wake huyo amezaa na mwanamke mwingine. Ubaya zaidi ulimtokea baada ya mtoto wa huyo mwanamke mwingine, kutumbukia kwenye kisima cha maji na kisha kupoteza maisha.
 “Kifo cha mtoto huyo, ndicho kilichozaa tatizo hili la ukatili dhidi yangu na kunisababishia ulemavu, kwa kuwa huyo mwanaume wangu na huyo mwanamke aliyezaa nae, walidai kwamba mimi ndiyo nilimtupia majini marehemu mtoto wao ili afe,”anasema mama huyo.

Vitisho kabla ya ulemavu

Mchali, anasema mara baada ya msiba wa mtoto kumalizika, mwanamume wake huyo alihamia kwa mke mdogo lakini akawa anarejea nyumbani na kumtukana huku akitishia kufanya lolote analofikiri linafaa.
Anasema baada ya mateso na vitisho kuzidi aliamua kuondoka kwa mumewe huyo toka mwezi Aprili mwaka huu na kuamua kurudi kwa wazazi wake huku akiwaacha watoto wake kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi.
Anasema alilazimika kuwaacha watoto kutokana na agizo la mumewe, aliyekataa asiwachukue, hivyo akaanza maisha mengine ya upweke bila watoto huku akiendesha maisha yake kwa biashara ya kuuza samaki.
Anasema mwanzoni mwa mwezi huu, aliugua malaria na kukaa nyumbani bila kwenda kwenye biashara zake. Agosti saba mwaka huu, alipata nafuu na kuamua  kwenda kumsalimia kaka yake, anayeishi mbali kidogo na nyumbani kwao na ndipo yakamkuta yaliyomkuta.
Anaeleza kuwa alikaa kwa kaka yake hadi muda wa futari wakafuturu na kushangaa simu yake ikiita, kuangalia ni namba ya mpenzi wake huyo. Alipoipokea, aliulizwa aliko, yeye alimweleza yuko kwa kaka yake na kumtaka amfuate mnadani akale nyama kitendo ambacho anasema alipingana nacho.
Anasema baadaye aliamua  kurudi nyumbani na kusindikizwa na wifi yake hadi karibu na nyumba yao ikiwa ni saa mbili usiku.Walipoagana, ghafla akashangaa kusikia sauti ya mumewe ikimuita, alipogeuka alimwona, kisha akamuuliza  alikotoka na kumwambia alikuwa kwa kaka yake.

Kipigo na ulemavu 

Anasema mara baada ya kumjibu mwanamume huyo alianza kumpiga na hatimaye alianguka chini na mumewe akatoa panga na kuanza kumkatakata sehemu mbalimbali za mwili wake.
Hakika hujafa hujaumbika. Mchali amecharangwa kwa mapanga kuanzia chini ya goti mguu wa kushoto hadi kwenye makalio, amekatwa sehemu zaidi ya saba mwilini.
Ni kama alitaka kumkata shingo
Anasema kwa namna anavyoona ni kama alidhamiria kumuua akisema kuwa mara nyingi akiwa na huo upanga alikuwa analenga kumtenganisha shingo. Alichofanya mama huyo ni kuweka mikono shingoni kuzuia panga, kitendo kilichosababisha  mkono wake wa kushoto kukatwa kabisa.

Hawezi kukaa

Mwandishi wa makala haya baadaye alimwomba mwanamke huyo angalau akae chini, kwani muda mwingi wa mahojiano alikuwa amelala, ndipo alipojibiwa kwamba hawezi kukaa kwa vile kuna nyama kubwa kwenye makalio ambayo imeshindikana kushonwa.
Mama huyo anasema wakati mumewe akimcharanga mapanga, mama yake mzazi aliendelea kupiga ngolo (yowe) kuomba msaada, kaka yake alikwenda lakini akashindwa kutoa msaada kwa kuwa shemeji yake huyo alikuwa akimkimbiza na panga.
Anasema kelele za mama yake zilisaidia kuokoa maisha yake, kwa kuwa majirani walijitokeza, hivyo mwanamume huyo akaanza kuwakimbiza akitaka kuwadhuru kitendo ambacho mama huyo aliona ndiyo nafasi pekee kukimbilia ndani.

Matibabu

Mchali, anasema baadaye ndugu zake, walitafuta usafiri na kufanikiwa kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ambako alilazwa kwa siku nne na kurejea nyumbani kutokana na ushauri wa daktari anayemhudumia.
Kwa mujibu wa mama huyo, daktari anayemtibu alimtaka Mchali akubali kutibiwa majeraha akiwa nyumbani ili kuepuka maambukizi ya magonjwa nyemelezi pamoja na kuepuka gharama za matibabu.
“Sina uwezo wa kukabiliana na gharama za matibabu kwa kuwa siwezi kutembea, nalazimika kukodi gari na kwa wiki naoshwa mara tatu. Nisaidieni ndugu zangu, ndoa yangu imenifikisha hapa,” anasema.

Mchali na hali ya ukatili mkoani Manyara

Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa anasema mtuhumiwa bado hajakamatwa kwa vile hajulikani aliko, huku akiahidi kuendelea kulifanyia kazi suala hilo.
Akielezea zaidi ukatili mkoani Manyara, anasema upo, japo ni mdogo ikilinganishwa na mikoa mingine. Anaamini kuwa bado changamoto ni kubwa  kwa wanawake ambao wengi wao wamekuwa wakinyanyasika.

Sababu kubwa za kunyanyasika kwa wanawake ni mfumodume. Akasisitiza kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo linaendelea kuelimisha jamii madhara ya ukatili na kusema jitihada hizo zinapaswa kuigwa na wananchi na asasi nyingine kuhakikisha ukatili wa kijinsia unatokomezwa.

Msimamo wa wanaharakati

Mkurugenzi wa asasi ya kiraia ya Kwieco, inayojihusisha na utoaji wa msaada wa kisheria na haki za binadamu mkoani Kilimanjaro,Wakili Elizabeth Minde, anasema hali ni mbaya hasa kwa wanandoa wa kike, kwani wengi ndani ya ndoa hawana nguvu.

Taifa lilipofikia

Hali ya ukatili dhidi ya wanawake nchini bado ni kubwa kutokana na takwimu zinazoonyesha asilimia 39 ya wanawake wenye umri kati ya mika 15 hadi 49 wanafanyiwa vitendo vya ukatili.

Waziri anena

Naibu waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto, Ummy Mwalimu alikiri ukatili dhidi ya  wanawake kuongezeka na kusema vitendo kama kupigwa na kubakwa ni matukio yanayoongoza zaidi na yanafanywa na wanaume, huku akisisitiza kuendelea kuangalia namna ya kufanya ili wanawake nchini waendelee kufurahia maisha.

Safari ya ndoa

Kwa mujibu wa Mwanasaikolojia, Modesta Kimonga anayefanya shughuli zake za ushauri Mkoani Mbeya, ndoa inaweza kufananishwa na safari ndefu yenye matukio yasiyotazamiwa, mengine yenye kupendeza na mengine yenye kuumiza.
Anasema mafanikio katika ndoa hayapimwi kwa panda shuka za safari bali yanapimwa kwa jinsi wenza wanavyoshughulikia hali hizo  Ndio kusema ni suala la msingi kwa walio kwenye ndoa kujifunza namna ya kupambana na changamoto zinapotokea, siyo kutesana au kukimbiana.
Ushauri zaidi
Mshauri maarufu wa ndoa nchini Uingereza, Hussain Zahid anasema katika makala ya kitabu chake cha ‘My marriage’ yaani ndoa yangu kuwa msingi wa kuwa na ndoa nzuri ni kupata muda wa kuzungumza baina ya wanandoa wenyewe ili kuondoa tofauti zao.
“Kila mtu ajione analo deni la kumpenda na kumfanyia mema mwenza wake. Kila mtu ajifunze kauli nzuri na matendo mazuri kwa mwenzi wake…kwamba kabla ya kufanya lolote, tafakari, ungefurahi kufanyiwa hilo unalotaka kulifanya,” anaonya.

Staili mpya ya maisha kwa baadhi ya  wanawake

Tafiti zinaonyesha kwamba kutokana na uwepo kwa mikwaruzo mingi katika mapenzi, kuna wanawake hawataki tena kuolewa.  Kama lengo ni kupata mtoto au watoto, huwa tayari kuzaa na yeyote hata kama ni mume wa mtu, kisha jukumu la kulea kwa asilimia kubwa hufanya wao au kwa kushirikiana na hao waliozaa nao.

Hata hivyo wataalamu mbalimbali wa masuala ya ndoa, wanashauri watu kuacha tabia hiyo ya kuzaa tu, badala yake wapende kuzaa wakiwa kwenye ndoa kwa sababu mtoto ambaye hana mzazi mmoja, huathiriwa sana na matatizo ya kisaikolojia.

Mfano wa utafiti 

Kulingana na utafiti  uliotolewa hivi karibuni na Ofisi ya Taifa ya Takwimu Marekani, uko uwezekano mkubwa wa watoto wenye kulelewa na mzazi mmoja kuwa na tabia mbaya zaidi ya watoto wenye wazazi wote.

“Kama ni suala la kuiga tabia na matendo mabaya, watoto ambao wana mzazi mmoja wanaharibika mara tano zaidi ya watoto ambao wana wazazi wote wawili,” inasema sehemu ya utafiti huo.
Utafiti unaongeza kuwa hata wanapofika kwenye umri wa ujana, vijana ambao wana mzazi mmoja, wanaharibika zaidi ya wale ambao wana wazazi wote; Wana uwezekano wa kuharibika mara tatu zaidi ya vijana ambao wanaishi na wazazi wote wawili.

Si wote huharibika

Hata hivyo utafiti unasisitiza kuwa si watoto wote wenye mzazi mmoja huwa na tabia mbaya, bali kinachosemwa ni kwamba kwa asilimia kubwa watoto wa aina hiyo huharibika zaidi ya wale ambao wanalelewa na wazazi wote wawili. Wanaoathirika zaidi ni wale ambao wazazi wao wametalakiana, hasa kwa sababu mara nyingi hata nguvu za kulea watoto hupungua kutokana na wazazi au mzazi husika kuwa na msongo wa mawazo.

Matendo mabaya kama vile ya mzazi mmoja kuteswa na mwingine au mtoto kuona mama au baba yake akimshtaki mwenzi wake, huchangia kwa kiasi kikubwa kuendelea kumuathiri mtoto kitabia.Tabia kama za kupigana au mateso mengine kabla ya wanandoa kuachana, huchangia kuharibu maisha ya mtoto kwa kuona labda kupigana ndio njia nzuri ya kupambana na mtu anayekukwaza au mwingine kutishwa na uhusiano kwamba unaweza kusababisha mateso.

Sababu ya migogoro na tiba yake

Mtafiti maarufu wa masuala ya ndoa kutoka Urusi, Korotayev, A, katika chapisho lake alilolipa jina “Division of Labor by Gender’ yaani mgawanyiko wa majukumu katika jinsia, anasema msingi wa kuwa na uhusiano mbaya katika ndoa nyingi ni kutokuwa na fursa ya kukaa pamoja na kukubali kuondoa kasoro.

“Hakuna mtu ambaye yuko safi kwa asilimia 100. Umekaa tumboni mwa mama yako na kuna wakati mnagombana, iwe mtu ambaye mmekutana tu mitaani?”anahoji Korotayev, huku akiwasisitiza watu walio kwenye ndoa  kubuni mbinu za kupendana na kufanya mikakati mingine ya maisha badala ya kuendekeza ugomvi, kufikiria kuachana au kutafuta wapenzi wengine.

Monday, 9 September 2013

MTOTO WA MIAKA MIWILI AUAWA KIKATILI NA MJOMBA WAKE AMBAYE NI TEJA JIJINI DAR.

Kijana Said Hassan anadaiwa kumuua kikatili mtoto wa dada yake, Fatihia ‘Fety’ Said (2) na kuibua simanzi nzito.

Tukio hilo la kinyama lilitokea hivi karibuni maeneo ya Keko-Tolori jijini Dar ambapo ilidaiwa kuwa jamaa huyo ni teja.

Akizungumza kwa uchungu, mama wa Fatihia alisema kuwa siku ya tukio (Jumatano iliyopita) aliamka asubuhi salama na mtoto wake ambapo ilipofika muda wa saa 2:00 asubuhi alimpa mwanaye chai akawa anakunywa huku anatembea, wakati huo yeye alikuwa akifanya kazi zake za usafi wa ndani.

“Nilipomaliza usafi na kazi zangu nikaanza kumtafuta mtoto, sikumuona, niliingiwa na hofu hivyo nikawa namsaka kila kona ya nyumba lakini sikumuona.

“Nilikwenda nyumba ya jirani ambapo ndiko huwa anakwenda mara nyingi kucheza lakini pia sikumkuta, baada ya kujiridhisha kuwa hayupo nilienda kutoa matangazo msikitini kuwa mtoto amepotea,” alisema Mwamvita Hassan, mama wa mtoto huyo.

Alisema kuwa baada ya jitihada zote hizo bila mwanaye kupatikana aliondoka na wenzake na kwenda Mbagala, Dar akihisi labda kuna mtu amemchukua mtoto wake kwani huko kuna nyumba yao nyingine lakini nako hawakumkuta.

Kwa mujibu wa bibi wa mama Fatihia, walipomuuliza mtoto wa jirani alisema kuwa amemsikia mtoto akilia chumbani kwa mjomba’ke Said waende wakaangalie huenda alikuwa huko.

“Kweli tulivyoangalia tulimkuta mtoto amewekewa nguo chini ya kitanda, juu yake kawekewa magodoro, tayari alishaaga dunia, hatukujua kama alimnyonga au alimfanya nini kwani bado uchunguzi unafanyika kwa sababu mtoto alikutwa na mapovu mdomoni,” alisema bibi huyo.

Mjomba wa mtuhumiwa, Shaban Juma alisema kuwa mtuhumiwa hakuwa na akili nzuri kwani mara nyingi amekuwa akimpeleka Hospitali ya Wilaya ya Temeke, Dar na akawa anapewa dawa ingawa yeye hakutambua ni dawa gani.

Mjomba huyo alipoulizwa kama mtuhumiwa alikuwa akitumia madawa ya kulevya, alikubali na kusema kuwa kuna mtu alimthibitishia kuwa amekuwa akimuona ‘akijidunga’.

Habari za uchunguzi zilibainisha kuwa mtuhumiwa huyo amewahi kufanya matukio mbalimbali kama kujaribu kuchoma nyumba yao, kukojolea maji ya kunywa na kutishia kufanya kitu cha ajabu ambacho watu hawatakisahau.

Baba wa mtoto aliyejitambulisha kwa jina moja la Said alisema kuwa alisikitishwa na tukio lililompata mtoto wake lakini huyo shemeji yake alikuwa akimtishia kila siku.


“Nimeumia sana lakini naacha sheria ichukue mkondo wake kwa sababu ameshakamatwa,” alisema.

Sunday, 8 September 2013

UNYAMA WA KUSIKITISHA....!!! MKE AZALIA CHOONI NA KUUA KICHANGA.

KWELI dunia inakwenda ukingoni, mwanamke mmoja anayedaiwa kuwa ni mke wa mtu, amefanya kitendo cha kinyama baada ya kujifungua msalani na kukiua kichanga chake.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni maeneo ya Mazizini, Ukonga Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam baada ya mwanamke huyo ambaye jina lake halikupatikana kukitumbukiza kichanga hicho chooni.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, mwanamke huyo ni mkazi wa Ukonga Moshi Bar alidaiwa kunywa dawa kwa ajili ya kuutoa ujauzito aliokuwa nao wa miezi minane  na baada ya kuona hali imebadilika alitoka nyumbani kwake Moshi Bar na kukimbilia Ukonga Mazizini kwa ajili ya kutaka msaada kwa mama yake mdogo.
Baada ya kufika kwa mama yake mdogo aliomba maji kwa ajili ya kwenda chooni, hata hivyo alizunguka nyuma ya choo kwa ajili ya kujipa msaada wa siri lakini hali ilivyokuwa mbaya zaidi, aliamua kuingia ndani ya choo hicho na kujifungua kichanga hicho na kukidumbukiza ndani  ya shimo la choo.
 
 Mashuhuda wa tukio hilo walisema kuwa walimuona  mwanamke huyo akibebwa kwenda ndani kwa mama yake mdogo ili aweze kupatiwa msaada zaidi lakini hali ilizidi kuwa mbaya kwa kuanza kuvimba mwili  kutokana na kutokwa na damu nyingi.
Waandishi wetu walifanikiwa  kuzungumza na mama mdogo wa mwanamke huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la mama Athony alikiri binti huyo kukumbwa na mkasa huo wakati yeye akiwa kwenye shughuli zake.
“Kweli nafahamu, alikuwa ni mjamzito na alifika nyumbani kwangu saa tano asubuhi, alichokifanya hapa si kitu cha bahati mbaya ni makusudi,” alisema mama huyo.
Mama Antony alisema kuwa  wakati anarudi  nyumbani aliukuta umati wa watu na alipoingia ndani ndipo alipopewa habari za tukio hilo.
Alipotakiwa kutaja jina la binti huyo,  mama huyo alianza kuangua kilio  na kuwafanya waandishi wetu washindwe kuendelea na mahojiano naye.
Mwakilishi wa mjumbe na shina namba 34 Ukonga Mazizini, Bi Mtende alisema kuwa tukio hilo limewashangaza kutokana na mwanamke  huyo kwenda kutupa kichanga chooni kwa makusudi.
Bi Mtende alisema kwanza mwanamke huyo siyo mkazi wa maeneo hayo, hivyo hakuna aliyeweza kumjua kwa jina.
Kikosi cha zimamoto na uokoaji kilifika katika eneo hilo majira ya saa saba mchana kwa ajili ya kutimiza wajibu wao
Kikosi hicho kikiwa kimesheheni zana za uokoaji kilikuta  kichanga hicho kikielea chooni na kwa kutumia mbinu zao za uokoaji na walifanikiwa kukitoa kichanga hicho kikiwa kikiwa maiti.     
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, ACP Marietha Minangi alikiri kutokea kwa tukio hilo ambalo yeye aliliita ni la kikatili  na mwanamke huyo amepelekwa katika Hospitali ya Amana kwa matibabu na mwili wa kichanga hicho kimepelekwa  Hospitali ya Taifa ya  Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
Waandishi wetu walifika katika Hospitali ya Amana kwa ajili ya kupata mahojiano na mama huyo Jumanne iliyopita, hata hivyo

VIDEO: BINTI WA MIAKA 5 ABAKWA NA KUUAWA NA MJOMBA WAKE.

 

Saturday, 7 September 2013

UNYAMA...!!! MWANAMKE AMWAGIWA TINDIKALI USONI NA KUHARIBIKA VIBAYA, KISA NI WIVU WA MAPENZI.

Blessing baada ya kuharibiwa sura
Cyrill Okusan kijana wa miaka 22 ametajwa kama muhusika wa unyama huu,Tayari ameshafunguliwa mashtaka kwa kosa hili.

Nadhani ni wivu tu wa kimapenzi na roho mbaya ndiyo iliyosababissha yote haya,jamaa akaona wacha nimuharibu reception tuone baada ya mimi kama kuna mtu atakubinyia hata kijicho..mbaya sana! Kina dada kuweni makini na 
 
ma-boyfriend wa kukutana nao mitaani bila hata kujua background na tabia ya mtu.

Thursday, 5 September 2013

MWIZI AKATWA KIGANJA CHA MKONO NA KISHA KUACHWA AONDOKE ZAKE

kiganja cha mwizi kilichokatwa na kisha mwiszi kuachiwa aende zake

Kijana mmoja ambae hakujuilkana jina lake mpaka anaondoka maeneo ya Buzuruga mjini mwanza aliambulia kukatwa mkono wake baada ya kukamatwa akiwa ameiba simu ya mama mmoja aliekuwa amepanda nae daladala. katika hali ya kustaajabisha mwizi huyo baada ya kukamatwa watu walisema inabidi apewe adhabu itayomfanya asirudie tena kuiba, ndipo walipoamua kumkwata mkono na kumuacha aende zake...
-USWAZI

DAKTARI ANASWA AKIMTOA MIMBA MWANAMKE NDANI YA MJENGO WA CCM

             AMA kweli hii bombastiki! Daktari Afrika Kweka amenaswa katika Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’ akiwa katika jaribio la kumtoa mimba mwanamke aliyejulikana kwa jina moja la Stella.
Tukio hilo lilitokea juzikati kwenye chumba kilichopo katika jengo la Chama cha Mapinduzi (CCM), Tawi la Makurumla, Magomeni-Kagera, Dar.
Awali, raia wema wa eneo hilo walituma malalamiko yao kwa OFM wakidai kwamba, Dokta Kweka amekuwa akifanya ‘mauaji’ hayo ya vichanga waziwazi, hali inayowakera kupita maelezo.
“Jamani ninyi si ndiyo Oparesheni Fichua Maovu? Kwa taarifa yenu hapa Magomeni-Kagera kwenye jengo la CCM, Tawi la Makurumla, kuna daktari anaitwa Kweka anatoa sana mimba, hasa wake za watu, njooni mumnase.”
 Baada ya kupata taarifa hiyo, OFM ilipanga mtego ambapo mmoja wa waandishi wetu wa kike alikwenda kwa Dokta Kweka na kujifanya mwanafunzi wa chuo lakini ana mimba anataka kuichoropoa.
Mwandishi huyo aliingia na paparazi wa kiume aliyejifanya ni mpenzi wake aliyempa mimba hiyo. Ndani ya eneo la tukio walipokelewa kwa bashasha na daktari huyo ambaye alihitaji shilingi 60,000 kama gharama za kutoa mimba japo baadaye alikubali kushusha bei hadi shilingi 45,000.
Baadaye daktari huyo alimchukua mwandishi wetu bila kujua kama hakuwa na mimba wala kitambi na kumpeleka chumba cha kuchomea sindano ambapo almanusura mpango mzima uharibike kwa kuwa mwandishi wetu hakupaswa kuruhusu daktari huyo amchome sindano ambayo ilisadikika kuwa ni ya ganzi.
Hata hivyo, wakati paparazi wetu akijishauri kuhusu sindano hiyo, ndipo Stella alifika kwenye zahanati hiyo na kuingia ndani kwa dhumuni la kutoa mimba.
Alipofika aliingia moja kwa moja chumbani kwa daktari huyo na kuchoma sindano ya ganzi bila woga kisha akaingia chumba cha kuchoropolea.
OFM ilipata uhakika kuwa, mwanamke huyo ameingia chumba cha kutolea mimba, ndipo ‘wapenzi’ hao (mapaparazi wetu) waliwasiliana na wapiga picha wetu waliokuwa chobingo na polisi ambao walitia timu na kuwanasa.
Daktari huyo na mteja wake walipelekwa kituo cha polisi na kufunguliwa jalada la kesi namba MMP/RB/567/2013 kosa likiwa kujaribu kutoa mimba huku ikibainika kuwa zahanati hiyo ni batili kwa kuwa aliisajili kama maabara.
Naye Katibu Mwenezi wa CCM wa tawi hilo, Hashim Kimambe alizungumzia tukio hilo juzi na kukiri kuwa taarifa za kunaswa kwa daktari Kweka anazo.
Alisema: “Hata hivyo, sisi tulikuwa mbioni kumfukuza kwa sababu alipoomba kupanga hapa alisema anaweka duka la dawa (famasi), baadaye tukashangaa anaziba watu wanaingia ndani.
“Mbaya zaidi huyu jamaa amekuwa akitumia risiti za CCM katika mambo yake, lazima aondoke kwa kweli, tunamwandikia barua.”

-GPL

WATOTO WANNE WA SHULE YA MSINGI WAMBAKA MWENZAO WA DARASA LA PILI MPAKA KUPOTEZA FAHAMU..!!




MATUKIO ya uvunjifu wa maadili kwenye shule mbalimbali hapa nchini yameendelea kushamiri baada ya wanafunzi wanne wa Shule ya Msingi Lulanzi wilayani Kibaha mkoani Pwani kutuhumiwa kumbaka mwanafunzi wa darasa la pili na kumsababishia maumivu yaliyopelekea kulazwa Hospitali ya Tumbi kwa matibabu.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana babu wa mtoto huyo, Jacob Mrope alisema tukio hilo lilitokea Septemba 2 saa 6 mchana ambapo mjukuu wake ambaye ni yatima alikuwa akitoka shuleni huku akiwa na wenzake wawili wakike, walikimbizwa na watuhumiwa hao ambapo yeye alishindwa kukimbia kutokana na kuumia mguu na kujikuta akibakwa.


Mrope alisema kuwa wanafunzi wenzake aliokuwa nao walisema kuwa baada ya watuhumiwa hao kumkamata walimziba mdomo kisha wakaanza kumuingilia kwa zamu ambapo mwanafunzi huyo hakuweza kupata msaada wowote hadi watuhumiwa hao kutimiza haja zao.


"Wenzake waliokuwa nao walitoa taarifa nyumbani kwa mlezi wake ambaye ni dada yake ambapo alikwenda na kumkuta akitokwa na damu nyingi na alipomuuliza alisema kuwa wenzake wamembaka ndipo alimchukua na kumpeleka shuleni kutoa taarifa," alisema Mrope.


Kwa upande wake dada yake Lwiza alisema kuwa yeye alipata taarifa kupitia kwa wanafunzi hao ambao alikuwa nao wakati wanatoka shule na kukimbizwa na watuhumiwa hao, ambapo walisema kuwa ilibidi warudi na kumkuta mwenzao akitokwa damu, wamkokota mwenzao hadi nyumba iliyojirani na kumjulisha.


"Alikuwa kwenye hali mbaya kwani alikuwa akitokwa na damu nyingi na nilipomuuliza alisema kuwa amebakwa na mtuhumiwa ambaye alimtambua na kumtaja jina mwenye umri wa miaka 10 akiwa na wenzake watatu," alisema Lwiza.


Lwiza alisema kuwa baada ya kuona hali ile walimpeleka shule na uongozi wa shule ukamwelekeza kufuata taratibu za kisheria ambapo walikwenda Serikali ya mtaa kisha kwenda polisi na baadaye Hospitali ya Tumbi kwa matibabu zaidi ambapo hadi juzi mwanafunzi huyo alikuwa bado kalazwa na hali yake inasemekana kuwa ni mbaya.


Naye Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Lulanzi, Anna Bilali alisema kuwa wao kama uongozi wa shule hawawezi kusema lolote kwani suala hilo liko kwenye vyombo vya sheria pamoja na kitabibu na watakuwa tayari kusema mara taarifa zitakapokamilika.


"Ni kweli tukio hili limetokea lakini bado haijathibitishwa kama ni kweli au la na pia lilitokea nje ya shule na muda wa shule kwa wanafunzi wa madarasa ya chini walisharuhusiwa kurudi nyumbani mara baada ya masomo kwisha," alisema Bilali.


Akizungumzia tukio hilo mjumbe wa mtaa wa Lulanzi, Rasul Shaban alisema kuwa walipata taarifa hiyo na kushangazwa na kitendo hicho ambapo tukio hilo ni la mara ya kwanza kutokea katika shule hiyo ambayo iko kwenye mtaa huo na pia walitoa barua za kuwadhamini wanafunzi wanaotuhumiwa kufanya tukio hilo.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Ulrich Matei alisema kuwa hadi sasa wanawashikilia wanafunzi wanne wenye umri kati ya miaka 10 na 13 kuhusiana na tukio hilo.