Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts
Showing posts with label KIMATAIFA. Show all posts

Saturday, 21 September 2013

AL SHABAAB WAJITAPA NA KUDAI WAMEUA WAKENYA 100 JANA,TWITTER WAFUNGA ACCOUNT YAO..RAIS KENYATA WANENA



              Zaidi ya watu 39 wameuawa na wengine 150 kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kuliteka jengo lenye maduka la Westgate, jijini Nairobi, Kenya.

Tukio hilo lilitokea jana mchana ambapo watu waliokuwa wakizungumza lugha ya kigeni, inayodhaniwa kati ya Kiarabu au Kisomali, kuvamia jengo la ghorofa na kushambulia watu kwa risasi.


“Hawakuwa wakizungumza Kiswahili. Walikuwa wakizungumza kwa lugha kama vile Kiarabu au Kisomali, lakini sina hakika sifahamu lugha hizo,” alisema mmoja wa mashuhuda aliyefanikiwa kutoka ndani ya jengo hilo na kujitambulisha kwa jina moja la Jay.


Shuhuda mwingine aliyejitambulisha ni mfanyakazi wa Ubalozi wa Uholanzi jijini Nairobi, Rob Vandijk, alisema tukio hilo lilitokea wakati akipata chakula cha mchana ndani ya jengo hilo.


Alisema watu hao waliingia ndani ya jengo la maduka hayo 
na kuanza kushambulia watu kwa risasi.


Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu, Abbas Guled alisema: “Ninachoweza kusema tuna takriban maiti 20. Majeruhi ni wengi.”


Katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja baadaye, Rais Uhuru Kenyatta alithibitisha kuwa zaidi ya watu 39 walikufa katika shambulizi hilo la kinyama, na wengine 150 kujeruhiwa.


"Vyombo vya usalama vinafanya kila jitihada kuthibiti eneo hili na kuwakamata waliohusika," asema Mr Kenyatta, akiongeza kuwa naye pia amepoteza wanafamilia katika tukio hilo. 
 
Polisi Waingia

Taarifa zingine zilisema kuwa polisi waliwasili eneo la tukio dakika 30 baada ya watu hao kuvamia jengo hilo.


Kamanda wa Polisi wa Kenya, Inspekta Jenerali David Kimaiyo alisema kwamba polisi walifika katika jengo hilo baada ya kupata taarifa, ambapo nao walianza kujibizana kwa risasi na magaidi hao waliokuwa hapo ndani.


Alisema watu hao wanaosadikiwa ni magaidi walikuwa wakijaribu kuiba pesa katika jengo hilo, kabla ya polisi hawajatokea na kuanza kurushiana risasi.

Helikopta za polisi zilionekana zikilizunguka jengo hilo kwa juu kuhakikisha hakuna mhalifu yeyote ambaye anaweza kutoroka.


Mashuhuda walisema kwamba walikuwa wakipata chakula cha mchana jirani na jengo hilo, ghafla wakashuhudia milio wa risasi kutoka katika eneo hilo.

Polisi walifanikiwa kuingia katika jengo hilo baada ya kukaa kwa muda mrefu kuangalia namna ya kuingia kwa sababu hawakujua watu hao walikuwa wamejificha eneo gani.

Baada ya polisi kuingia katika jengo hilo watu waliokuwa ndani walipata fursa ya kutolewa, huku polisi wengine wakiendelea kuwatafuta wahalifu hao.

Al-Shabab Yanena
Wakati shambulizi likiendelea jana jioni, wanamgambo wa kikundi cha Kiislamu cha Al-Shabab walivyambia vyombo vya habari kupitia Twitter kuwa wamehusika na tukio hilo.

“Tulishaionya serikali ya Kenya kuwa dhahama itaikumba kama isipoondoa vikosi vyake kutoka Somalia,” Al-Shabab waliandika kupitia akaunti yao ya Twitter inayoitwa @HSM_Press.


Wanamgambo hao waliongeza kuwa wamefanikiwa kuua watu wengi  ( 100 ) kuliko idadi inayotajwa na serikali ya Kenya, huku wakibeza jitihada za uokoaji.

Kutokana na malalamiko kutoka kwa waathirika wa tukio na vyombo mbalimbali vya usalama, FastCompany inaripoti kuwa Twitter ililazimika kuifunga akaunti hiyo  usiku  wa  kuamkia  leo.

HIZI  NI  TWEET  ZAO  KATIKA  ACCOUNT  YAO  NYINGINE  MAANA  WANAZO  KAMA  3  ivi:

 

SHUHUDIA PICHA ZAIDI YA 20 ZA MAUAJI YA KUTISHA YALIYOTOKEA NCHINI KENYA LEO, INASIKITISHA KWA KWELI!






              WATU waliokuwa na silaha wamefyatua risasi mjini Nairobi, Kenya, kwenye eneo la maduka katika mtaa wa Westlands.
Walioshuhudia tukio hilo, wanasema kuwa maguruneti piya yalitumika.
Inaarifiwa watu watano wamekufa.(P.T)

Mwandishi wetu mjini Nairobi anaeleza kuwa washambuliaji inaarifiwa walivaa vilemba kama vya al-Shabaab, lakini haikuthibitishwa kama wapiganaji hao wamehusika.
Polisi waliojihami kwa silaha wamezingira jengo la maduka liitwalo Westgate, katika mtaa wa Westlands, na kuna taarifa ya watu waliojeruhiwa wakitolewa hapo kwa machera.



























Thursday, 19 September 2013

WAUAWA WAKIJARIBU KUMTETEA MWANAMKE ALIYEKUWA AKISUMBULIWA...


Baadhi ya waandamanaji kwenye ghasia hizo zilizokatisha uhai wa watu 19.
Vurugu zilizoambatana na ghasia zimeua watu 19 kaskazini mwa India baada ya makundi ya Wahindu na Waislamu kushambuliana kwa bunduki na visu kutuliza makelele ya matusi mtaani.

Ghasia hizo zilianza kwa mauaji ya wanakijiji watatu ambao walijitokea kumlinda msichana mmoja aliyekuwa akisumbuliwa huko Kawal, Jimbo la Uttar Pradesh wiki iliyopita.
Hasira ilifoka katika eneo tangu tukio hilo, lakini vurugu zinabadilika na kuwa za kutisha Jumapili pale mwandishi mmoja, mpigapicha mmoja wa polisi na wanakijiji kadhaa walipokufa kutokana na vurugu hizo.
Zaidi ya watu ishiri wamekufa kutokana na majeraha yao yaliyotokana na mapigano ya Jumamosi katika wilaya ya Muzaffarnagar, baada ya vurugu kusambaa kwenye vijiji kadhaa vya jirani.
Serikali imeingilia kati kwa kupeleka mamia ya askari kuzima vurugu hizo na kufanya msako wa silaha katika eneo hilo, wakati hali ya hatari ikiwa imeweka huko Uttar Ptadesh, eneo la makazi ya watu milioni 200.
"Amri ya kutotembea usiku imewekwa kwenye maeneo matatu yaliyoathiriwa zaidi na ghasia hizo ya Muzaffarnagar," alisema mkuu wa mambo ya ndani ya jimbo hilo, R.M. Srivastava.
Ghasia zililipuka Jumamosi mchana baada ya maelfu ya wakulima wa Kihindu kufanya mkutano kwenye kijiji cha Kawal kudai haki katika mauaji ya Agosti 27 ya wanaume watatu ambao waliongea pale mwanamke mmoja alipokuwa akisumbuliwa kwa maneno.
Waziri mdogo wa afya jimboni humo, Mohammad Azam Khan, alisema wahudhuriaji hao walikuwa wakihutubia kutaka Waislamu wauwawe kujibu mapigo ya vifo vya wanakijiji hao watatu.
Wakulima hao walishambuliwa wakati wakirejea nyumbani baada ya mkutano huo, ofisa wa juu wa polisi Arun Kumar alisema, akiongeza kwamba washambuliaji hao wanaonesha kuwa walipanga shambulio lao kutokana na kuwa na silaha za 'bunduki kubwa na vitu vyenye ncha kali.'
Milio ya bunduki iliripotiwa kutoka sehemu mbalimbali za kijiji hicho. Ndani ya masaa kadhaa mapigano yakaibuka kwenye vijiji vya jirani, alisema Kumar.
Mtangazaji wa kituo cha habari cha IBN 7, Rajesh Verma alipigwa risasi kifuani wakati akiripoti maandamano ya jumuiya mjini Abupura, na kufariki katika eneo hilo la tukio.
Uttar Pradesh lilikuwa kitovu cha mapigano mabaya zaidi ya jumuiya nchini India Desemba mwaka 1992, baada ya kundi la Hindu kuharibu kabisa msikiti wa Babri uliojengwa karne ya 16 mjini Ayodhya.
Serikali imeonya kwamba India inashuhudia ongezeko la ghasia za jumuiya, huku matukio 451 yakiwa tayari yameripotiwa mwaka huu, kulinganisha na 410 kwa mwaka mzima wa 2012.
Kwa mwezi Agosti pekee ghasia za jumuiya zimeua watu wawili na kujeruhi 22 katika kijiji kimoja huko jimbo la Bihar, mashariki mwa Uttar Pradesh, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya India.

TAZAMA VIDEO JINSI WACHAWI WALIVYONASWA WAKIWANGA TENA WAKIWA WATUPU KAMA WALIVYOZALIWA:










HUYU NDIYE MWANAMAMA WAKIKENYA AMBAYE NI HATARI SANA KWA BIASHARA YA KUUZA MADAWA YA KULEVYA AYEKAMATWA TANZANIA....OBAMA AMTANGANZA KUWA NI ADUI YAKE

 
MWANAMKE raia wa Kenya, Naima Mohamed Nyakiniywa ambaye pia anatumia pasiport ya kusafiria ya Tanzania ikiwa na jina la Mwanaidi Ramadhani Mfundo maarufu kama Mama Leila, ni adui mkubwa wa Rais wa Marekani, Barack Hussein Obama kutokana na madai kwamba amebobea kwenye biashara ya madawa ya kulevya.
Obama, ambaye pia baba yake mzazi alikuwa Mkenya, mwaka 2011 alimtaja Naima katika orodha ya watu saba yeye akiwa wa 6 kuwa ni hatari kwa biashara hiyo haramu ya ‘unga’ ambapo pia aliamuru mali zake na wenzake hao zilizoko Marekani kutaifishwa, pia wasiruhusiwe kukanyaga ardhi ya taifa hilo kubwa duniani.
Septemba 16 na 17, mwaka huu, Mama Leila (na wenzake nane) alifikishwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa mashitaka ya kukutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin, Juni Mosi, 2011 Mbezi Beach jijini Dar.
Rekodi zinaonesha kuwa mwanamke huyo alizaliwa Septemba 2, 1962, Majengo, Nairobi, Kenya. Ingawa ni maarufu maeneo mengi ya mji huo mkuu wa nchi jirani, Pumwani, Majengo, Kariokor, Kaloleni, Biafra na Bahati, lakini katika hali ya usiri mkubwa, mwanamke huyo hafahamiki kwa majina ya Mama Leila, Naima au Nyakiniywa, isipokuwa anafahamika kama Kanyanya.
Kanyanya anayedaiwa kuwa mama wa watoto watano, katika eneo analoishi la Mbezi Beach jijini Dar es Salaam anajulikana ni Mtanzania kutoka kabila la Wadigo na majirani wanasema ni mtu mwema, mwenye moyo wa kusaidia walio na shida, akiwa pia ni mfanyabiashara wa magari, saluni na ‘internet cafes’.
Nchini Kenya, inadaiwa Kanyanya alikuwa mtu mwema katika eneo la Majengo huku majirani wakisema hakukuwa na njaa katika eneo lolote ambalo Naima alikuwepo na kila mtu alipata alichokihitaji.
Kutajwa kwake na Rais Obama kunadaiwa kuwashtua wakazi wengi wa Nairobi ambako kama ilivyo Mombasa na Dar es Salaam, anamiliki mali mbalimbali, yakiwemo majumba ya kifahari.
Hata hivyo, mwaka 2009, Polisi wa Kenya walidaiwa kuwakamata vijana watatu wakiwa na madawa ya kulevya na wote walimtaja Naima kama ndiye mwenye mzigo lakini ilikuwa vigumu kwao kumuunganisha kutokana na kukosa ushahidi.
Chanzo  chetu kimethibitisha kwamba wakati mmoja Naima aliwahi kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya na kushikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kilimani jijini Nairobi lakini shinikizo kutoka ‘juu’ lilisababisha mwanamama huyo kuachiwa bila kufunguliwa mashitaka.
Inadaiwa kuwa hata alipokamatwa Dar es Salaam kwa tuhuma za kuhusika na biashara hiyo, kulikuwa na idadi ya simu za kutosha kutoka ofisi ‘kubwa’ jijini Nairobi zilizotaka aachiwe lakini polisi wa Bongo ‘walikomaa’ naye ili kumfahamu zaidi.
Naima anamiliki zaidi ya hati sita za kusafiria zenye majina na sura tofauti ili kufanikisha safari zake za mara kwa mara nje ya nchi na mojawapo ni ya Tanzania ambayo haifahamiki ilipatikana kutoka ofisi gani ya uhamiaji hapa nchini.
Katika orodha ya Rais Obama ya watu hao kutakiwa kufilisiwa mali zao na kutokanyaga Marekani, pia yupo mbunge wa zamani wa Jimbo la Kilome, John Harun Mwau kutoka chama cha siasa cha Party of Independent Candidates of Kenya (PICK).
Wengine katika orodha hiyo ni Manuel Torres Felix wa Mexico, Gonzalo Inzunza Inzunza (Mexico) Haji Lal Jan Ishaqzai (Afghanistan), Kamchybek Asanbekovich Kolbayev (Kyrgyzstan) na Javier Antonio Calle Serna wa Colombia.

Wednesday, 18 September 2013

PICHA: MAMBA AZUA BALAA BAADA YA KUINGIA CHINI YA KITANDA HOTELINI.....

Katika hali isiyo ya kawaida mamba mkubwa mwenye futi 8 amezua tafrani baada ya kuingia chini ya kitanda cha Mkurugenzi wa hoteli moja ya kitalii iitwayo Humani iliyopo pembezoni mwa mto Turgwe huko nchini Zimbabwe na kukaa zaidi ya masaa 8. 

Mr Whittall, ambaye ni mkurugenzi wa hoteli hiyo alisema kuwa mamba huyo aliingia kwa siri chumbani kwake na kukaa chini ya kitanda chake usiku na kugundulika asubuhi ya siku iliyofuata.


Alisema kuwa mamba huyo alitoka nyuma ya pori lililopo karibu na hoteli hiyo ambapo hata yeye alipoamka hakumuona na alining’iniza miguu yake huku mamba huyo akiwa chini ya kitanda ambapo alitoka kwenda kupata kifungua kinywa kwenye mgahawa wa hoteli hiyo.



Inaelezwa kuwa mamba huyo aligundulika na mfanyakazi aliyekuwa akifanya usafi katika chumba hicho na kupiga mayowe yaliyomshtua Mr Whittall ambapo alitoka mbia kwenda kushuhudia kulikoni na kumkuta mamba huyo akiwa chini ya kitanda chake kumbe alilala naye kwenye chumba hicho usiku mzima.



Mamba ni wataalam wa kujificha na ndiyo maana hunusirika kuuwawa na wanyama wengine hususani binadamu hata wakiwa nje ya maji,alisema Mr Whittall.



Na huweza kutulia sehemu moja kwa muda mrefu bila kugundulika na myama yoyote hivyo kumtambua inakuwa ni vigumu hiyo ni kutokana na maumbile yao yalivyo na hukimbilia ndani ya vichaka au kuingia kwenye nyumba kama hotelini hapo kufuata joto hasa katika kipindi cha mvua na baridi kali na alipenda kukaa chini ya kitanda hicho kwasababu kulikuwa na joto.



Mkurugenzi huyo alilazimika kuwaita wafanyakazi wengine ambao walisaidiana kumuondoa mamba huyo kutoka kwenye chini ya kitanda na kumtupa kwenye bwawa la hoteli hiyo.





URUSI NA UFARANSA WAZIDI KUMUUMIZA RAIS OBAMA.....WADAI SYRIA HAISTAHILI KUVAMIWA NA MAREKANI



               Urusi na Ufaransa zimeeleza wazi wazi tofauti zao kuhusu ripoti ya wataalamu wa silaha wa Umoja wa Mataifa, ambayo ilithibitisha kwamba silaha za kemikali zilitumiwa nchini Syria.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Sergei Lavrov ambaye alikutana na mwenzake wa Ufaransa Laurent Fabius mjini Moscow jana, alitupilia mbali madai kwamba serikali ya Syria ndio iliyotumia silaha hizo katika mashambulizi ya Agosti 21 karibu na Damascus.

Ingawa ripoti hiyo haikusema upande gani ulitumia silaha hizo, Laurent Fabius alisema hakuna shaka lolote kwamba serikali ya rais Bashar al-Assad ndio iliyofanya mashambulizi hayo, ambayo Marekani inasema yaliuwa watu zaidi ya 1400.

Lavrov alisema hakuna ushahidi wowote kuthibitisha madai hayo, na alikariri msimamo wa nchi yake kwamba silaha hizo zilitumiwa na waasi ili kuzivuta nchi za magharibi ziingilie kati kijeshi.

HUYU NDIO MSANII WA NYIMBO ZA INJILI ALIYEJITANGAZA KUWA YEYE NI SHOGA..!!!

Mwimbaji wa nyimbo za Injili Jijini Nairobi,Kenya,George Barasa maarufu kama Joji Baro amejiatangaza kuwa yeye ni shoga.Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 22 akizungumza na mtandao mmoja wa nchini humo alisema kuwa alizaliwa Jijini Nairobi na baadaye kuhamia Bungoma miaka michache baadaye. 

 Aidha ameongeza kuwa pamoja ya kuwa ni shoga pia ameathirika na ugonjwa hatari wa Ukimwi pia ni mwanaharakati wa kutetea Haki za Mashoga na Wasagaji na wana zaidi ya wanachama 2,800,Ambao wote ni mashoga na wasagaji ambapo vijana idadi yao 15 na watu wazima ni 68.
Alisema kuwa aliamua kuhamia Mjini EMBAKASI BAADA YA FAMILIA yake kumtenga alipojuliakana anajihusisha na vitendo hivyo.

Alipokuwa anasoma shule ya Mtakatifu Paulo Miluki High School ndipo alipoanza kujifunza vitendo hivyo vya ushoga na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na kiongozi mmoja wa kanisa Katoliki.

Machi 11, 2012 , Madaktari walimpima na kugundulika kuwa ni mwathirika wa VVU / UKIMWI na kwamba amedai kuwa kwenye muziki wa INJILI amekuwa akipata upinzani mkubwa kutoka kwa wanamuziki mwenzake wa muziki huo.
Anasema amechoka kuhukumiwa na kuonewa huku akinyanyapaliwa na watu wengine baada ya kugundulika kuwa nafanya vitendo hivyo.

‘Mimi ni binadamu,Kama binadamu yeyote naumia sana ninavyonyanyapaliwa,’alisema Barasa.

Anasema kwenye masuala ya urembo hayuko nyuma ana mawigi 15 na zaidi ya pea za viatu virefu ‘High hills’30.
‘Napenda sana urembo na pia naandika kitabu cha maisha yangu kiitwacho "Dream Boy"ambacho kitaeleza historia nzima ya maisha yangu na jina la albanu yangua ya injili inaitwa "Bora Siku"alisema Barasa.

‘Namtumikia Mungu na natumaini Mungu anakubali utumishi wangu,’alimalizia Barasa.

WADAU WA IPHONE 5S WAWEKA KAMBI NJE YA DUKA LA APPLE SIKU 4 KABLA HAZIJAANZA KUUZWA

                 ‘Die Hard customers’ wa simu za iPhone wameamua kupanga foleni nje ya duka la simu hizo jijini London, Uingereza na kuamua kuweka kambi ya muda kwa kufunga matenti na kuhamishia makazi yao hapo huku wakisubiri siku rasmi ya kuanzwa kuuzwa kwa toleo jipya la iPhone5S linalosubiriwa kwa hamu kote ulimwenguni ambayo ni Ijumaa hii (September 20).
iphone 5SIphone 5S zitakazokuwa zikipatikana katika rangi tatu
Mmoja wa wateja hao ambaye hii ni siku pili kushinda na kulala hapo akisubiri kujipatia simu yake mara zitakapoanza kuuzwa, amesema mpaka sasa ameshakataa ofa ya £200 (515,000 Tsh) kwaajili ya kuuza nafasi yake kwenye foleni hiyo na kuwa na matarajio ofa inaweza kuja kufikia £1000(2,575,000)baadaye.
iphone fan-2
iPhone fan-3
Vijana hao wawili ambao wameweka kambi jana usiku nje ya duka la Apple wamedai kuwa siku zote wao huwa miongoni mwa wateja wa kwanza kuzipata simu mpya za iPhone kila zinapotoka, hivyo wameamua kuweka kambi nje ya duka ili wahakikishe wawe wateja wa kwanza kuzinunua siku ya Ijumaa.
-BONGO5

Tuesday, 17 September 2013

MAHARAMIA 1O WANAWAKE HATARI KWA MADAWA YA KULEVYA DUNIANI

             IPO  dhana kwamba wanawake ni daraja hatari sana. Machoni huonekana laini lakini wanaweza kutenda mambo ambayo ni vigumu kwa mtu wa jinsia ya kiume. Biashara ya madawa ya kulevya inahitaji watu hatari, katili, wenye roho isiyotishika.

 

Mireya Moreno Carreon.

Nancy Botwin katika ‘siriz’ yake ya Weeds kwenye TV, anajaribu kuonesha jinsi mwanamke anaweza kuwa hatari katika biashara ya bangi na madawa ya kulevya kwa jumla, hata hivyo katika uhalisia, hajawafikia hata chembe wanawake hawa hatari ambao wameitikisa dunia.Hawa ni maharamia 10 wauza unga, wametengeneza fedha nyingi na kila mmoja ameshahusika kwa namna moja au nyingine na mauji. Kwa muuza madawa ya kulevya, kitendo cha kutoa roho ya mtu kipo jirani yake sana.


 

1. GRISELDA BLANCO
Inawezekana huyu ndiye akawa muuza unga mwanamke katili, mwenye uwezo mkubwa kuliko wote kuwahi kutokea katika historia ya dunia. Ameshahusika na mauaji ya watu zaidi ya 200. Ni raia wa Colombia, akiwa na miaka 11, tayari alishahusika na tukio la utekaji wa mtoto. 

 

Baadaye alihamia Marekani, kwenye Jimbo la Florida ambako alitengeneza mtandao wa madawa ya kulevya ambao ulimpa utajiri mkubwa.

2.  SANDRA AVILA BELTRAN
Ni raia wa Mexico, alizaliwa mwaka 1960. Aliwahi kupewa jina la Mungu wa Kike wa Madawa ya Kulevya. Vyombo vya habari nchini mwake vikamwita Malkia wa Pacific. Serikali za Marekani na Mexico zinamtaja kuwa kiungo wa magenge ya unga ya Sinaloa Cartel la Mexico na Norte del Valle Cartel la Colombia. 

 

Anadaiwa kujipatia mabilioni ya dola kwa usafirishaji wa unga kati ya Colombia, Mexico na Marekani. Kwa sasa yupo gerezani nchini Mexico kwa kosa la utakatishaji wa fedha haramu.

3. ANGIE SANCLEMENTE VALENCIA
Ni raia wa Colombia, aliwahi kushika taji la urembo la taifa katika nchi hiyo lakini alinyang’anywa baada ya kubaini ameshaolewa. Mume wake alikuwa mmoja wa vinara wa unga na walipoachana, alitumia njia zilezile kujipatia utajiri haramu. 

 

Alikuwa na genge kubwa la wasafirishaji wa cocaine na kila mtu alimlipa dola 5,000 kwa safari moja. Alisafirisha zaidi Argentina, Uingereza na Mexico. Ana umri wa miaka 35, yupo gerezani Argentina tangu Oktoba 27, 2010.

4. KATH PETTINGILL
Alizaliwa mwaka 1935. Jina lake la utani ni Bibi Kizee Shetani (Granny Evil). Ni mwenyeji wa Jiji la Melbourne, Australia. Alianza kama kahaba kabla ya kugeukia madawa ya kulevya. 

 

Alipoteza jicho moja baada ya kupigwa risasi katika moja ya matukio ya uharamia, akimtetea binti yake, Vicky, aliyekuwa anadaiwa dola 300 na maharamia wenzake. Nguvu ya mtandao wa unga aliyoitengeneza, ni hatari na imehusika na mauaji mengi nchini Australia.

5. ENEDINA ARELLANO FELIX
Katika genge ambalo lilikuwa linaongozwa na kaka zake, Ramon na Eduardo, mwanzoni yeye alishika nafasi ya umeneja wa fedha. Baada ya Ramon kuuawa na Eduardo kukamatwa, alishika uongozi. 

 

Maofisa usalama wa Mexico waliwahi kukiri kwamba Enedina ndiye alikuwa dira ya kaka zake. Ana umri wa miaka 

 

 Amebadili mfumo na sasa anaendesha kazi zake kisayansi,
hakuna fujo za magenge ya wahuni kiasi kwamba inakuwa ngumu kumtia hatiani.

6.  BLANCA CAZARES SALAZAR
Ni raia wa Mexico, alianza kujihusisha na utakatishaji wa fedha haramu, aliponogewa akajikita kwenye unga. Ana umri wa miaka 37.

 

 Biashara yake ameitanua na yupo makini sana. Anaongoza mtandao mkubwa wenye makundi 42. Ni ngumu kumkamata kwa sababu hahusiki moja kwa moja. Marekani imempiga marufuku kuingia nchini humo.

 

7. MARIA JIMENEZ
Ana umri wa miaka 27. Alikuwa kiongozi wa genge lililokufa la La Tosca. Baada ya kufanya biashara kwa muda mrefu, alikamatwa mwaka jana nchini kwake Mexico kwa tuhuma za usafirishaji wa unga na mauaji. Baadaye alikiri kuua watu 20 na mpaka sasa yupo jela.

8.  EDITH LOPEZ LOPEZ
Anajulikana kama Malkia wa Kusini. Amekuwa kinara wa madawa ya kulevya tangu alipoolewa na haramia wa unga, Raul Nunez Morales, maarufu kama 

 

The Cowboy. Tangu mwaka 2000, Edith amebaki kuwa mmoja kati ya wanawake tisho kwa biashara hiyo haramu duniani.

 

9. THELMA WRIGHT
Alishirikiana na marehemu mumewe, Jackie Wright katika biashara ya unga kati ya miaka ya 1980 na 1990. Mwaka 1986, mumewe aliuawa, kwa hiyo akashika usukani kwa kulisuka genge lao la Black Mafia ambalo lilifanya matukio mengi. 

 

Hata hivyo, kwa kuhofia maisha ya mtoto wake, Jackiem,  kuharibika, aliachana na kazi hiyo na kufanya shughuli nyingine halali. Ni mara chache sana kutokea.

10. MIREYA MORENO CARREON
Ndiye mwanamke pekee kushika nafasi ya juu kwenye Genge la Zetas. Ndani ya kipindi kifupi alifanya matukio mengi ya utakatishaji wa fedha haramu na usafirishaji wa unga. 

 

Akiwa nchini kwake, Mexico, mwaka 2010, maofisa usalama wa siri walimkamata akiwa akiwa na gari lenye cocaine na bangi na mpaka leo yupo korokoroni.

Sunday, 15 September 2013

HATIMAYE NCHI YA INDIA IMEFANIKIWA KUFYATUA KOMBORA LA NYUKLIA



                    Nchi ya India imefanikisha jaribio lake la kufyatua kombora la nyuklia la masafa marefu kwa mara ya pili, safari hii likiwa na uwezo wa kufika katika mji wa Beijing, China na maeneo kadha wa kadha ya barani Ulaya.

Jaribio hilo linaiweka India katika nafasi imara zaidi ya kuzalisha silaha zenye tishio la nyuklia.

Msemaji wa kituo cha utafiti cha nchini humo (Defence Research and Development Organisation - DRDO), Ravi K. Gupta akikaririwa na vyombo vya habari siku ya Jumapili, alithibitisha kwa kusema, "Jaribio lilifanikiwa. Lililenga na kufanikiwa kufikia shabaha katika uelekeo uliopangwa. Imekidhi malengo yote."

Majaribio ya kombora kama hilo katika siku zilizopita, yalifanikiwa kuyafikia maeneo ya Pakistani na magharibi ya China. Inasimuliwa kuwa India inajitahidi kuimarika kisilaha kwa nia ya kuwa sawa na nchi ya China na pia kujihami dhidi ya majirani zake ambao wanasadikiwa kuwa na silaha za nguvu na hatari za vita.

Nchi hizo mbili zina ushirikiano mwema ila zina historia ya mgogoro wa mpaka wa kuigombea Himalaya uliosababisha zikatwangana kidogo mnamo mwaka 1962.

India pia inajidhatiti kutokana na tetesi kuwa mahasimu majirani zao, Pakistani, wamejilimbikizia silaha za kivita zenye uwezo wa nyuklia ambazo zina uwezo wa kufyatuka kwa masafa mafupi ambayo yakilengwa vizuri yanaweza kusababisha madhara katika maeneo ya nchi za kusini mwa bara la Asia.

Hadi sasa, mataifa yanayotambuliwa rasmi na shirika la Umoja wa Mataifa kuwa na hifadhi ya silaha za nyuklia ni nchi 5 wanachama wa kudumu wa Baraza la umoja huo yaani - Uchina, Ufaransa, Urusi, Marekani na Uingereza (na Israeli).

VIDEO: HII NDIO SHULE YA SEKONDARI YENYE MAPACHA WATUPU

Tazama video hapo chini......

CHEKI WAFUASI WA RAIS ASSAD WA SYRIA WANAVYOUAWA MBELE YA WANANCHI

Askari wa kundi la ISIS akimwekea jambia shingoni mmoja wa wafuasi wa Bashir al-Assad kabla ya kumkata kichwa.
Baadhi ya mateka wanaomuunga mkono Rais wa Syria, Bashir al-Assad, wakiwekwa eneo la machinjioni.
Mmoja wa askari akiinua juu jambia kumkata mfuasi wa Bashir al-Assad.
Mtoto mdogo raia wa Syria akiangalia mwili wa mfuasi wa Bashir aliyekatwa shingo.
Watoto wakishuhudia mwili wa mfuasi wa Bashir aliyekatwa shingo.
Baadhi ya mateka wakisubiri kuuawa.
WATU wanaomuunga mkono Rais wa Syria, Bashir al-Assad, wamekuwa wakikamatwa na kuuawa mbele ya wananchi.  Mauaji yamekuwa yakifanywa kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukatwa shingo au viungo vya mwili kwa kutumia majambia na silaha zingine.
Haya yote hufanyika  mbele ya watu wanaoshangilia na wengi wao wakiwa na silaha. Miongoi mwao ni pamoja na watoto.  Mauaji ya mwisho ambayo yalinaswa hivi karibuni ni yale yaliyotokea katika mji wa Keferghan kaskazini mwa nchi hiyo.
Inasemekana mauaji hayo hufanywa na kundi la ISIS ambalo ni tawi la Al-Qaeda linalompinga Assad na wanaofanyiwa mauaji hayo ni kundi linalojulikana kama Shabiha (Mizimu) ambalo linamuunga mkono rais huyo.

Saturday, 14 September 2013

WALIOMBAKA MWANAFUNZI NDANI YA BASI WAHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA...


Wanaume wanne jana wamehukumiwa kifo kwa kuhusika na shambulio la ubakaji na mauaji ya msichana kwenye basi mjini Delhi.

Jaji Yogesh Khanna, ambaye aliwatia hatiani wanaume hao kwa shambulio la ubakaji na 'kusababisha' mauaji mapema wiki hii, alikataa ombi la mwanasheria wao la kuwapunguzia adhabu wateja wake hao.

Shangwe zililipuka kutoka kwenye umati wa watu nje ya mahakama hiyo ya Delhi pale wanasheria walipotoka nje kwa kasi na kutangaza hukumu hiyo iliyotolewa kutokana na shambulio hilo la Desemba mwaka jana, ambalo liliibua maandamano makubwa kote nchini India na midahalo kadhaa kuhusu uhalifu dhidi ya wanawake.


"Hii imeshitua jamii nzima ya wapenda amani," Jaji Yogesh Khanna alisema, akiwahukumu wanaume hao adhabu ya kunyongwa hadi kufa.
"Katika nyakati hizi huku uhalifu dhidi ya wanawake ukiongezeka, mahakama haziwezi kugeuka vipofu mbele ya makosa hayo ya kutisha."
Hukumu hiyo ilikuwa moja ya vipimo vikubwa kabisa kwa miaka kadhaa ya mtazamo wa kweli kinzani ya India kuelekea hukumu ya kifo.
Majaji wa nchini humo wanatoa, kwa wastani, hukumu 130 za kifo kila mwaka lakini India imeshaua watu watatu tu katika miaka 17 iliyopita.

Pichani ni nyuso za watu wanne walio hukumiwa adhabu ya kifo kwa ubakaji na mauaji ya kikatili ya  mwanamke kijana yaliya fanyika kwenye basi mjini New Delhi , Desemba mwaka jana.
Licha ya kusita kwake kutekeleza hukumu hizo, mwaka jana India ilipiga kura dhidi ya upitishwaji muswada wa Umoja wa Mataifa uliotaka ruhusa ya kusitishwa kwa muda adhabu za kifo.

Wanasheria wa watuhumiwa wote wanne walisema watakata rufani, kitu kinachomaanisha utekelezwaji hukumu zao unaweza kuwa miaka kadhaa ijayo. Kesi hii itakwenda katika Mahakama za Juu na kisha Mahakama Kuu.

Endapo zitathibitisha hukumu hizo, uamuzi wa mwisho utamtegemea Rais, ambaye ana mamlaka ya kufanya huruma.

Mmoja kati ya wanne hao, mwalimu wa gym Vinay Sharma, alimwaga machozi wakati akitolewa nje ya mahakama hiyo, ambako polisi wakiwa na vifaa vya kukabiliana na ghasia walijipanga kuzuia umati mkubwa wa wananchi.

Mwathirika huyo, ambaye alibakwa kwa saa moja na kujeruhiwa kwa nondo ndani ya basi lililokuwa kwenye mwendo, amekuwa alama ya hatari wanazokabiliwa nazo wanawake katika nchi ambayo ubakaji unaripotiwa kwa wastani wa kila dakika 21 na mashambulio ya tindikali na kesi za kukera yameshika kasi.

Mwanamke huyo, ambaye ametokea katika familia ya maisha ya kati na kufanya kazi kwenye kituo cha mawasiliano wakati akiwa anaendelea na masomo, hajatajwa kutokana na sababu za kisheria, lakini vyombo vya habari vya India vimempachika jina la Nirbhaya, neno la Kihindi linalomaanisha asiye na hofu.

"Leo tunaweza kupumua kidogo kirahisi," alisema mama wa mwathirika huyo, ambaye alimkumbatia ofisa mmoja wa polisi nje ya mahakama hiyo baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo. "Natumaini hukumu hiyo itawatisha watu kufanya makosa kama haya kwa siku za usoni."

Mawakili wa utetezi wameiasa mahakama hiyo kupuuza walichosema kimezagaa na shinikizo la kisiasa kutoa adhabu hiyo kali zaidi.

"Huu sio ushindi wa ukweli. Ila ni pigo kwa haki," wakili wa utetezi A.P. Singh aling'aka kwa jaji wakati hukumu hiyo ikisomwa.

"Jaji amechukua uamuzi huo chini ya shinikizo la kisiasa bila kujali uhalisia," aliwaeleza waandishi baadaye.

Waziri wa Mambo ya Ndani nchini humo, Sushilkumar Shinde, alikanusha kwamba kulikuwa na muingilio wa kisiasa, akisema: "Hakuna mamlaka yoyote ya sheria inayoathiriwa na serikali."