Zaidi ya watu 39 wameuawa na wengine 150 kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kuliteka jengo lenye maduka la Westgate, jijini Nairobi, Kenya.
Tukio hilo lilitokea jana mchana ambapo watu waliokuwa wakizungumza lugha ya kigeni, inayodhaniwa kati ya Kiarabu au Kisomali, kuvamia jengo la ghorofa na kushambulia watu kwa risasi.
“Hawakuwa wakizungumza Kiswahili. Walikuwa wakizungumza kwa lugha kama vile Kiarabu au Kisomali, lakini sina hakika sifahamu lugha hizo,” alisema mmoja wa mashuhuda aliyefanikiwa kutoka ndani ya jengo hilo na kujitambulisha kwa jina moja la Jay.
Shuhuda mwingine aliyejitambulisha ni mfanyakazi wa Ubalozi wa Uholanzi jijini Nairobi, Rob Vandijk, alisema tukio hilo lilitokea wakati akipata chakula cha mchana ndani ya jengo hilo.
Alisema watu hao waliingia ndani ya jengo la maduka hayo
na kuanza kushambulia watu kwa risasi.
Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu, Abbas Guled alisema: “Ninachoweza kusema tuna takriban maiti 20. Majeruhi ni wengi.”
Katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja baadaye, Rais Uhuru Kenyatta alithibitisha kuwa zaidi ya watu 39 walikufa katika shambulizi hilo la kinyama, na wengine 150 kujeruhiwa.
"Vyombo vya usalama vinafanya kila jitihada kuthibiti eneo hili na kuwakamata waliohusika," asema Mr Kenyatta, akiongeza kuwa naye pia amepoteza wanafamilia katika tukio hilo.
Polisi Waingia
Taarifa zingine zilisema kuwa polisi waliwasili eneo la tukio dakika 30 baada ya watu hao kuvamia jengo hilo.
Kamanda wa Polisi wa Kenya, Inspekta Jenerali David Kimaiyo alisema kwamba polisi walifika katika jengo hilo baada ya kupata taarifa, ambapo nao walianza kujibizana kwa risasi na magaidi hao waliokuwa hapo ndani.
Alisema watu hao wanaosadikiwa ni magaidi walikuwa wakijaribu kuiba pesa katika jengo hilo, kabla ya polisi hawajatokea na kuanza kurushiana risasi.
Helikopta za polisi zilionekana zikilizunguka jengo hilo kwa juu kuhakikisha hakuna mhalifu yeyote ambaye anaweza kutoroka.
Mashuhuda walisema kwamba walikuwa wakipata chakula cha mchana jirani na jengo hilo, ghafla wakashuhudia milio wa risasi kutoka katika eneo hilo.
Polisi walifanikiwa kuingia katika jengo hilo baada ya kukaa kwa muda mrefu kuangalia namna ya kuingia kwa sababu hawakujua watu hao walikuwa wamejificha eneo gani.
Baada ya polisi kuingia katika jengo hilo watu waliokuwa ndani walipata fursa ya kutolewa, huku polisi wengine wakiendelea kuwatafuta wahalifu hao.
Al-Shabab Yanena
Wakati shambulizi likiendelea jana jioni, wanamgambo wa kikundi cha Kiislamu cha Al-Shabab walivyambia vyombo vya habari kupitia Twitter kuwa wamehusika na tukio hilo.
“Tulishaionya serikali ya Kenya kuwa dhahama itaikumba kama isipoondoa vikosi vyake kutoka Somalia,” Al-Shabab waliandika kupitia akaunti yao ya Twitter inayoitwa @HSM_Press.
Wanamgambo hao waliongeza kuwa wamefanikiwa kuua watu wengi ( 100 ) kuliko idadi inayotajwa na serikali ya Kenya, huku wakibeza jitihada za uokoaji.
Kutokana na malalamiko kutoka kwa waathirika wa tukio na vyombo mbalimbali vya usalama, FastCompany inaripoti kuwa Twitter ililazimika kuifunga akaunti hiyo usiku wa kuamkia leo.
HIZI NI TWEET ZAO KATIKA ACCOUNT YAO NYINGINE MAANA WANAZO KAMA 3 ivi:
No comments:
Post a Comment