Showing posts with label Vituko. Show all posts
Showing posts with label Vituko. Show all posts

Saturday, 21 September 2013

"NINA WAKE FEKI WENGI SANA HAPA MJINI".....MZEE MAJUTO


             Majuto anasema kuwa ana watoto tisa ingawa hakuwa tayari kuwazungumzia mama wa watoto hao zaidi ya kumwongelea mkewe wa sasa, Aisha Mbwana kwa kuwa wake zake aliozaa nao baadhi ya watoto kwa bahati mbaya walishafariki dunia.
Alisema kuwa yanapokuja masuala ya familia huwa anapenda azungumze mkewe na kwa ridhaa yake. Kwa mujibu wa Majuto anapenda aitwe mke halali kwa kuwa wake feki anao wengi kupitia michezo ya kuigiza na wengine wenye fikira potofu hutumia picha hizo kutengeneza habari za uongo.
Aisha anaizungumziaje familia yake
Kama kawaida ya wanawake wa Tanga ana lafudhi ya huko ambayo huvutia kuzungumza nao, anaanza kwa kunieleza kuwa alianza kuitwa mke halali wa nguli huyo wa sanaa za maigizo mwaka 1997, walipofunga ndoa .
Anasema kuwa alikutana na nguli huyo maeneo ya Buguruni, Dar es Salaam, ambako alikuwa akiishi na dada yake aliyekuwa kaolewa na rafiki yake mzee Majuto, ‘Mwanachia’ (kwa sasa ni marehemu), ambaye walikuwa wakiigiza pamoja.
Anasema hakuwa na hili wala lile hadi alipoamua kuondoka na kurudi kwao maeneo ya Vingunguti, ambako ndiko walikokuwa wanaishi wazazi wake na kupewa taarifa kuwa posa imepelekwa kwa ajili yake.
Nilipoambiwa kuhusu hiyo posa sikufikiria kama atakuwa ni mzee Majuto kwa kuwa alikuwa ni kama shemeji yangu kutokana na kuwa karibu na shemeji yangu,” anasema Aisha ambaye ni mama wa watoto watatu.
Anaendelea kueleza kuwa siku ambayo wanafamilia walikutana na kumuuliza kama anamfahamu mchumba na kutajiwa jina kuwa ni Amri Athumani, aliuliza mara mbili kwa kuwa alikuwa hamfahamu huyo mtu hadi alipoambiwa kuwa ni King Majuto.
“Kwa mila za Wabondei mchumba wa kwanza anakubaliana na wazazi, halafu binti anapewa taarifa na kwa kuwa wazazi ni wakubwa inabidi binti akubali, na ndivyo ilivyokuwa kwangu nikakubali na kuolewa na Majuto,” anasema mama huyo.
Anaingia kwenye uigizaji kufuata nyayo za mumewe
Aisha anafafanuwa kuwa kabla ya kuolewa na Majuto hakuwa mwigizaji lakini baada ya kuolewa, mumewe huyo alimwingiza kwenye uigizaji na filamu ya kwanza kuigiza na mumewe huyo ni ‘Fukara hatabiriki’.
Mkewe huyo anasema kipindi hicho Majuto alikuwa anafanya kazi bila kuwa na kikundi zaidi ya wanafamilia, hivyo na yeye alikuwa mmoja wao akicheza kama mama na Majuto kama baba.

MPOKI APIGWA CHINI NA MZUNGU,NI BAADA YA KUJIPENDEKEZA CHEKI VIDEO UJIONEE


MTUHUMIWA AJISAIDIA HAJA KUBWA MAHAKAMANI..MATUKIO KATIKA PICHA

               KIOJA cha mwaka kilitokea Jumatano wiki hii katika Mahakama ya Jiji ya Sokoine Drive jijini Dar es Salaam, baada ya mkazi mmoja wa Buguruni, Hassan Omary kujisaidia haja kubwa kizimbani wakati akisomewa shtaka lake la uzururaji.
Mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Richard Magodi alikuwa akimsomea shtaka hilo, mbele ya Hakimu Mfawidhi, William Mutaki na alipotakiwa kukiri au kukanusha kosa lake, mtuhumiwa huyo alibaki kimya akiwa amemtumbulia macho hakimu.
Katika hali isiyotarajiwa, mtuhumiwa huyo alionekana akijikamua kama anayejisaidia na ghafla, harufu kali ya kinyesi ikatanda mahakamani hapo.
Hakimu alitahayari kufuatia tukio hilo, kwani aliziba pua yake kwa kutumia koti lake na kuuliza chanzo cha mtuhumiwa kufanya kitendo hicho kortini, lakini katika hali iliyoashiria kama ni kiburi, kijana huyo hakujibu chochote zaidi ya kutazama chini, licha ya swali hilo kurudiwa zaidi ya mara tatu.
Kutokana na kosa hilo ambalo liliharibu na kusimamisha karibu shughuli zote za mahakama kwa muda, Hakimu Mutaki alimhukumu kijana huyo kwenda jela kwa muda wa miezi sita ili kuwa fundisho kwa wengine wenye tabia hiyo.
Kana kwamba haitoshi, askari waliokuwepo mahakamani hapo walilazimika kumchapa bakora kijana huyo ili kumlazimisha kupiga deki baada ya eneo hilo kuchafuka vibaya kwa kinyesi kilichochanganyika na mkojo.

Thursday, 19 September 2013

HUYU NDIYE MWANAMITINDO KIKONGWE KULIKO WOTE DUNIANI.TAZAMA PICHA SABA ZA HUYU KIKONGWE MWANAMITINDO.



 
            Imezoeleka zaidi Dunia ya mitindo huwa ni ya vijana lakini hii tofauti kwa Kikongwe Jean Woods mwenye umri wa miaka 75 ndiye anayeelezwa kuwa ni mwanamitindo mzee kuliko wote duniani.

KALI YA MWAKA...!!! MWANAMKE ARUDISHIWA POCHI YAKE ILIYOIBWA ZAIDI YA MIAKA 20 ILIYOPITA..

                    jeri Cox Chastain akikagua baadhi ya vitu vilivyokuwamo ndani ya pochi hiyo.
  

Vitu visivyouzika ambavyo mwanamke mmoja alipoteza kwa zaidi ya kipindi cha miaka 20 hatimaye vimerejeshwa kwake.


Pochi ya rangi ya bluu bahari iliyoibwa Desemba, 1990 kutoka kwa Jeri Cox Chastain, mama aliyekuwa akifanya kazi mbili wakati huo, imerejeshwa katika himaya yake.
Msamaria mwema aliiona pochi hiyo katika paa la vigae vya jengo moja huko Spartanburg, South Carolina, majengo kadhaa kutoka sehemu ambako Chastain alikuwa akifanya kazi wakati huo, na kumpa kumbukumbu ya miaka kadhaa iliyopita katika mchakato huo.
Chastain anakumbukia siku hiyo, 'siku ya malipo,' kwa uwazi. Alikuwa akifanya kazi Hospitali ya Doctor's Memorial, ambayo ilifungwa mnamo mwaka 1994.
Pochi hiyo ilikuwa imeibwa wakati alipotoka ofisini kwake, kabati la chuma, kwenda kununua vitafunwa.
Wakati huo aliamini kuna mtu katika jengo la ofisi yake amemuibia fedha hizo na kisha kuitupa pochi hiyo.
"Nilihisi tu ilikuwa imetupwa kwenye pipa la taka mahali fulani."
Badala yake, Chastain alipigiwa simu kutoka polisi mapema wiki hii ikimweleza kwamba pochi hiyo aliyodhani imetoweka kabisa, imepatikana.
Shastain alikwenda kituo hicho cha polisi siku iliyofuata kuitambua pochi hiyo, ambayo ilikuwa katika 'hali safi.'
Ingawa pesa hizo zilizokuwamo, hakika, zilikwenda Shastain alifurahi kupita kiasi kuona mlolongo wa picha na kitabu cha kumbukumbu.
Picha mojawapo kwa namna ya kushangaza ilikuwa muhimu kabisa kwa Chastain.
Ilikuwa ni picha ya kijana wake, sasa ana miaka 28, alipokuwa na miaka mitano akiwa kavalia nguo ambazo wakati fulani zilikuwa zikimilikiwa na baba yake.
Pia katika pochi hiyo kulikuwa na kadi za manunuzi na hata kadi za huduma ya matibabu kwa ajili yake na mwanae, pia cheti cha kuzaliwa cha mwanae huyo.
"Kuna mtu anawezekana kuwa alichukua [vyote hivi] na kufanya maisha mapya kwa [wao wenyewe]."
Kwa sasa Chastain ana furaha kufanya safari hii ya kumbukumbu, lakini anataka kumshukuru mtu aliyerejesha pochi yake.
Hii hakika si mara ya kwanza mtu mwaminifu kurejesha pochi iliyopotea kipindi kirefu sana.


Kutoka kwenye jengo hilo hilo, miaka michache iliyopita alirejesha pochi iliyopotea tangu mwaka 1996.

Wednesday, 18 September 2013

NGEDERE ATIMUKA NA BUKTA YA BEKI WA TIMU YA SIMBA.

 
 Ngedere mmoja kwa jina la Sharobaro amekuwa kivutio katika kambi ya Simba iliyopo kwenye Fukwe za Bamba nje kidogo ya Jiji la Dar, eneo la Kigamboni, ambapo gazeti la Championi Jumatano lilimshuhudia ngedere huyo akivinjari katika vyumba vya wachezaji wa timu hiyo na kucheza na beki wa kikosi hicho, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ lakini baadaye akakimbia na bukta ya mazoezi ya nyota huyo.

Mara baada ya ngedere huyo kuchukua bukta hiyo na kukimbia nayo kwa umbali mfupi, Baba Ubaya alimfukuza huku akimuita kwa jina la Sharobaro ambapo aliiachia chini, kisha kumrukia mguuni na kurudi katika varanda ya chumba chake.

Baba Ubaya aliliambia gazeti hilo kuwa, ngedere huyo ni rafiki yake mkubwa na aliichukua bukta hiyo katika michezo yao na hana tabia ya kung’ata watu kama ilivyo kwa wengine: “Huyu ni rafiki yangu mkubwa, anacheza na wengi lakini mimi ndiyo kanizoea zaidi,” alisema Baba Ubaya.

VIDEO:JE...!! UNAMJUA MTU ALIYEVUNJA RECORD YA DUNIA KWA KUVUNJA NAZI KWA KIDOLE

       Huyu ndiye Mzee aliyewekwa katika kumbukumbu za GUINNESS WORLD RECORDS kwa kitendo cha kuvunja nazi kwa kidole kimoja haya ni maajabu na ni kweli.



 
Tazama video yenyewe hapo chini....  


Monday, 16 September 2013

KALI YA MWAKA...!!! MWANAUME NA MWANAMKE WALIOBADILI JINSIA WAAMUA KUWA WAPENZI NA KUTAKA KUONA...

Picture


                            Arin Andrews (kulia) na mwandani wake Katie Hill
 
Nchini Marekani, yenye watu waliojibadili jinsia, 'transgender' wapatao laki tisa, vijana wawili kati yao wamependana kimapenzi na huenda wakaoana.

Kijana Arin Andrews alizaliwa katika jinsia ya kiume, wakati binti Katie Hill alizaliwa katika jinsia ya kike.

Hivi karibuni, Arin alifanyiwa upasuaji wa kuondoa matiti yake (mastectomy) na kuanza kutumia vichocheo
vya hormone za kiume (testosterone) ili kujenga umbo la kiume kama anavyoonekana kulia kwenye picha. Alipoulizwa ikiwa hakujali kuwa na makovu kifuani mwake kwa ajili ya kuondoa matiti, alisema alikuwa radhi aishi na makovu kuliko kubeba matiti.

Akizungumza na wanahabari wa INSIDE EDITION, Arin ambaye awali alitambulika kwa jina la Emerald, anasema asingeweza kufikia hapo ikiwa asingepata upendo na ushirikiano kutoka kwa mpenziwe, Katie ambaye anayeelewa fika yanayoendelea kwenye kichwa chake.

Katie ambaye awali alitambulika kwa jina la Lucas, sasa hunyoa miguu yake ili isiwe na vinyweleo vingi kama mwanaume, jambo ambalo anasema lilimkosesha raha kila mara alipojitizama kwenye kioo kwa kujiona mbaya na asiyevutia. Anasema siku moja alipochoshwa sana na mawazo, alisema leo ni leo, liwalo na liwe; Akamketisha kitako mama yake na kumwambia "Usiku wa leo nitajiua endapo hutanisaidia," na hapo ndiyo ukawa mwanzo wa kuanza taratibu za kufanyiwa upasuaji wa kujibadili jinsia.

Mwaka jana, wazazi wa watoto hao wawili waliwakutanisha, na hapo ndipo mapenzi baina yao yalipowaka
.


Friday, 13 September 2013

HUYU NDIYE JIMAMA ANAYE WAFANYIA MASSAGE WANAUME KWA KUTUMIA MAZIWA YAKE

                 Baada ya kukosa kazi katika sehemu za mambo ya massage kutokana umbile kubwa alilonalo hatimaye mwanamama huyu aja na mbinu kabambe yenye mafanikio ya kuwa-massage wanaume kwa kutumia maziwa yake yenye ukubwa wa kutosha!

 Kristy love ambaye anatokea Atlanta Georgia ametumia mwaka mzima kujifunza kazi hiyo  ila sasa anavuna mapesa mengi kwa siku baada ya kuwafanyia massage wateja wake kwa maziwa yake makubwa.

"Nilipomaliza shule ya massage hakuna  aliyetaka kuniajiri..nilikuwa naulizwa kama naweza kusimama siku nzima wakifikiria uzito wangu utakuwa kikwazo,hamna mtu aliyeenita'' alisema Kristy "Nikaamua kuanza kufanyia watu nyumbani na mteja mmoja aliwahi kuniambia nipandishe blauzi nikamwambia sifani mambo hayo,nilikuwa naona aibu kwa sababu ya mwili wangu mkubwa! lakini nikagundua huenda kuna kitu kwenye maziwa ukiamua kuyatumia kwa massage..nikaweka tangazo kwenye gazeti simu zikawa zinamiminika'' alisema "Mwanzo ilikuwa ngumu sana kutokana na umbile langu nikawa nazima taa wakati nikimfanyia mteja massagelakini siku zilivyoenda nikawa najiamini zaidi"


Kristy yupo singo na haoni aibu kwa mwili alionao japo madaktari wanamshauri kuwa unaweza kumletea matatizo kama ya moyo siku za usoni

Huwa anazingatia kuangalia mteja wake kama anapumua vizuri pindi anapokuwa kamlalia anam-massage.

Sunday, 8 September 2013

MWANAMKE AVUA NGUO HADHARANI ILI APIGANE NA BOYFRIEND WAKE ALIYESIKIA ANATEMBEA NA DADA YAKE

Msichana huyu pichani alishuka kwenye kimin bus na kuanza kupigana na boyfriend wake. Yani alifikia hadi hatua ya kuvua nguo ili apate attention ya boyfriend wake na watu waliokuwa wanashuhudia tukio hilo la aibu.     
Kutokana na taarifa zilizokusanywa na Reportghananews.com, msichana huyo alikasirika baada ya kujua kuwa boyfriend wake huyo anamahusiano ya kimapenzi na dada yake mwenye miaka 17.
Hivi ilikuwa kitu sahihi kweli kujidhalilisha yeye na boyfriend wake mbele za watu hivyo?Eti kisa kaibiwa....jamani these things happens everyday na maisha yanaendelea yanini sasa kuongezea uharibifu,kuibiwa uibiwe wewe,kuvua nguo uvue wewe,si ndo majanga yenyewe haya?! 

Friday, 6 September 2013

MAZISHI YA AJABU YA RASTA YAFANYIKA WILAYANI IFAKARA, JENEZA LA PAKWA RANGI YA BENDERA YA JAMAICA...

              MAZISHI ya rasta mmoja maarufu kwa jina la Rasta Gido aliyekuwa dereva wa bodaboda yameonekana kushika nafasi ya juu katika rekodi ya marehemu wote waliozikwa Ifakara, Morogoro miaka ya karibuni.
Rasta Gido alipata ajali mbaya ya kugongwa na gari aina ya Fuso, Julai 28, mwaka huu eneo la Ifakara Kibaoni.
Aliaga dunia akipatiwa matibabu katika Hospitali ya  Mtakatifu Francisca ya mjini Ifakara.
Akizungumza na waandishi wetu juzi, jijini Dar baada ya kurejea kutoka kwenye msiba huo, mjomba wa marehemu  aitwaye Avi Simba alisema msiba huo uliongozwa kwa imani ya kirasta bila kuhusisha mchungaji wala shehe huku waombolezaji wakivalia kofia za  kirasta zenye rangi za kijani, nyekundu, njano na nyeusi hali iliyozidisha kuyafanya mazishi hayo kuwa ya aina yake.
Mbali na kofia hizo, jeneza la marehemu lilipakwa rangi hizo za kirasta zilizotajwa hapo juu, hivyo kulifanya eneo lote la msiba kutawaliwa na taratibu za kirasta.
“Mimi na ndugu zangu wote tulikaa chini na kukubaliana kuwa marehemu azikwe kwa imani ya kirasta bila kufuata taratibu za dini yoyote ile,” alisema mjomba huyo wa marehemu.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, baadhi ya wananchi waliohudhuria msiba huo walijikuta kwenye wakati mgumu kutokana na utaratibu wa mazishi uliowekwa na ndugu na jamaa wa marehemu ambao ni jamii ya rasta tofauti na taratibu za dini yake aliyokulia Rasta Gido ya Romani Katoliki.
Hali iliyoongeza mazishi hayo kuwa ya aina yake ni Wazungu waliofika msibani hapo sanjari na mwongozaji wa mazishi hayo, Rasta Side ambaye ni mchumba wa mmoja wa Wazungu hao.
Mbali na hayo yote, kwenye mazishi, hakukutumika machepe na majembe kufukia kaburi la marehemu huyo badala yake ilitumika mikono kufanya kazi hiyo mwanzo hadi mwisho.
Kutokana na msiba huo, madereva wa bodaboda wa eneo la Kibaoni waliamua kusitisha shughuli zao ili kuungana na mwenzao katika safari yake ya mwisho.
Madereva hao walimlaani vikali dereva wa Fuso aliyemgonga Rasta Gido wakidai kuwa hakuwa makini barabarani na kusababisha ajali hiyo mbaya.
Nayo familia ya marehemu ilijikuta kwenye wakati mgumu kutokana na jukumu zito la malezi alilowaachia rasta huyo kwani ameacha watoto watatu, Rose, Neema na Stanislaus ambao wote bado wanahitaji msaada.
Marehemu Rasta Gido alizikwa kwenye makaburi ya familia ya Kibaoni, Ifakara mkoani Morogoro.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Ameni.

Wednesday, 4 September 2013

MGANGA FEKI (TAPELI) APATA KIPONDO KITAKATIFU

 

kijana aliyetambukwa jina la atupele bedoni  alijikuta akiambulia kipigo ch mwizi baada ya kutapeli vijana wa bodaboda chunya  mchezo mzima ulikuwa hivi  
Kijana Atupele alieleza kuwa yeye ni mganaga wa kienyeji  ila hakuweza kufanya mabo yake alimwambia kijana mmoja ampe simu ili aweze kuzizalisha ila akashindwabbsi ndipo ukawa mwanzo wa kipigo kwake kilisema  chanzo chetu kwamba kijana huyo alifanya mchezo huo kwa takribani wiki mbili

 
Baada ya mwandishi wetu kufika eneo la tukio ndiyo ikawa pona pona ya Atupele Bedoni

Wednesday, 28 August 2013

DUNIANI KUNA MAMBO:HII NDILO JENEZA LENYE KIYOYOZI NDANI

Hili ni sanduku ya aliyekua Mfalme wa Roma(self-appointed Roma king),Florin Cioaba aliyefariki wiki moja iliyopita kwa mshtuko wa moyo huko Uturuki. Sanduku lake lilikua na Kiyoyozi kama lionekanavyo pichani.

Hivi karibuni watanzania tulishangazwa pale tulipoona sanduku la Billionea wa Arusha ambalo lilikua likifunguliwa kwa 'Remote Control'. Nadhani sanduku hili pia litawashangaza wengi.



Sunday, 25 August 2013

MASANJA SASA NI MCHUNGAJI KONDOO WA BWANA NA ANAFANYA MIUJIZA KATIKA MIKUTANO YA INJILI....

NA HAYA NDO MANENO ALIYO ANDIKA

NIMEONA MUNGU WANGU AKIPONYA WAGONJWA NA KUFUNGUA WALIFUNGWA NA MAGONJWA SUGU....
NIMAOMBI YANGU JUMAPILI YA LEO, KILA JAMBO LILILOKUSUMBUA KWA MDA MREFU,IWE NI
UGONJWA,SHIDA YA NDOA,KAZ,BIASHARA,MASOMO,LAANA,NK,MUNGU WANGU AKUHURUMIE NA UPOKEE UPONYAJI. tamka maneno haya kwa imani rafiki Yangu .
ASANTE MUNGU KWA KUNIHURUMIA,NIMEPONYWA