Wednesday, 18 September 2013

NGEDERE ATIMUKA NA BUKTA YA BEKI WA TIMU YA SIMBA.

 
 Ngedere mmoja kwa jina la Sharobaro amekuwa kivutio katika kambi ya Simba iliyopo kwenye Fukwe za Bamba nje kidogo ya Jiji la Dar, eneo la Kigamboni, ambapo gazeti la Championi Jumatano lilimshuhudia ngedere huyo akivinjari katika vyumba vya wachezaji wa timu hiyo na kucheza na beki wa kikosi hicho, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ lakini baadaye akakimbia na bukta ya mazoezi ya nyota huyo.

Mara baada ya ngedere huyo kuchukua bukta hiyo na kukimbia nayo kwa umbali mfupi, Baba Ubaya alimfukuza huku akimuita kwa jina la Sharobaro ambapo aliiachia chini, kisha kumrukia mguuni na kurudi katika varanda ya chumba chake.

Baba Ubaya aliliambia gazeti hilo kuwa, ngedere huyo ni rafiki yake mkubwa na aliichukua bukta hiyo katika michezo yao na hana tabia ya kung’ata watu kama ilivyo kwa wengine: “Huyu ni rafiki yangu mkubwa, anacheza na wengi lakini mimi ndiyo kanizoea zaidi,” alisema Baba Ubaya.

No comments:

Post a Comment