Wednesday, 18 September 2013

IRENE UWOYA AAHIDI KUFICHUA SKENDO KUBWA NA MBAYA ZA ERICK SHIGONGO....


               Lile bifu linalondelea kati ya mwigizaji Irene Uwoya na mmiliki wa kampuni maarufu ya magazeti nchini Erick Shigongo limeshika sura  mpya baada ya mwigizaji huyo kuapa  kuzianika  hadharani  SKENDO  chafu  za  Erick  Shigongo  huku  akitangaza  wazi  kuwa  haogopi  kufa  wala  kumwagiwa  tindikali...

Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii Irene alitundika  maneno  yafuatayo:

“…Ipo siku ntaongea ukweli kuhusu shigongo na ushaid pia ntatoa...usilo lijua nikama usiku wa giza, ndo maana atawadanganya wasio na akili na wasio mjua....

"Nitapigana nae mpaka tone la mwisho la damu yangu,  ntasema kila kitu kwanin ananichukia na ntaweka kila kitu wazi....Then, wenye akili watajua naongea nini...

"Simuogopi hatakama atanichafua kiasi gan.Hizo kwangu ni matone yamvua bado mvua yenyewe...I don care kwa atakae muamini, but mwisho wa siku ukweli utaonekana na atatamani  ardhi ipasuke......

 mimi Irene Uwoya sijashawishiwa na mtu wala kulazimishwa, naahidi ya kwamba ntaongea  maovu  yake  yote…”

-Kwa hisani yaa bongomovie.

No comments:

Post a Comment