Muargentina huyo pamoja na kufunga mabao matatu peke yake usiku, pia alitengeneza bao la nne lililofungwa na Gerard Pique.
Haikuwa bahati yao, Ajax kwani walikosa hadi penalti baada ya kipa Victor Valdes kuokoa mkwaju wa Kolbeinn Sigthorsson.Messi alifunga mabao yake katika dakika za 22, 55 na 75, wakati Pique alifunga dakika ya 69.Kikosi cha Barcelona kilikuwa: Valdes, Alves, Pique/Bartra dk80, Mascherano, Adriano, Busquets, Fabregas/Xavi dk72, Iniesta, Sanchez, Messi, Neymar /Pedro dk72.Ajax: Vermeer, van Rhijn, Denswil, Moisander/van der Hoorn dk73, Blind/Schone dk78, Poulsen, de Jong/Serero dk59, Duarte, Bojan, Sigthorsson na Boilesen.
Mkwaju: Messi alifunga bao la kwanza kwa shuti la mbali la mpira wa adhabu
La pili: Messi akifunga bao lake la pili
Kiulaini: Messi akimtoka beki Stefano Denswil
Tabasamu: Messi akishangilia na beki wake, Dani Alves
Sergio Busquets akidhibiti mpira katikati ya wachezaji wa Ajax, Siem de Jong (kushoto) na Lerin Duarte
Anakosa: Kolbeinn Sigthorsson alikosa penalti iliyochezwa na kipa Victor Valdes
Alexis Sanchez akimvaa Daley Blind wa Ajax Uwanja wa the Camp Nou
Beki wa Barcelona, Adriano akimdhibiti Ricardo van Rhijn wa Ajax
Pique akienda hewani kuifungia Barcelona bao la tatu
Hasira: Neymar aking'aka baada ya kupoteza nafasi ya kufunga
Marafiki wa zamani: Javier Mascherano akichuana na Bojan Krkic anayecheza kwa mkopo
Wako vizuri: Barca wakishangilia ushindi wao Camp Nou
Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, AC Milan iliichapa Celtic 2-0 Uwanja wa San Siro, mabao ya Zapata dakika ya 82 na Muntari dakika ya 85.
Kikosi cha AC Milan kilikuwa: Abbiati, Zaccardo, Zapata, Mexes, Constant/Robinho dk76, Nocerino, De Jong, Muntari, Birsa/Emanuelson dk64, Matri/Poli dk87 na Balotelli.
Celtic: Forster, Lustig, Van Dijk, Ambrose, Izaguirre, Matthews/Boerrigter dk75, Brown, Mulgrew/Biton dk89, Samaras, Commons/Pukki dk77 na Stokes.
Christian Zapata akitimka kushangilia baada ya kuifungia bao la kwanza AC Milan dhidi ya Celtic
Mwafrika hatari: Sulley Muntari wa Milan akishangilia baada ya kufunga bao la pili zikiwa zimebaki dakika tano
Phillipe Mexes akimrukia Cristian Zapata baada ya Mcolombia kufunga
Ukuta mgumu: Wachezaji wa AC Milan wakiwa wameweka ukuta wakati beki wa kati wa Celtic, Charlie Mulgrew akipiga mpira wa adhabu
PANDE ZA DARAJANI
MECHI nne bila ushindi. Kama Rafa Benitez angekuwa bado yupo kazini, anerushiwa mayai viza.
Jose Mourinho amepata kipigo katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa baada ya Chelsea kuchapwa mabao 2-1 nyumbani na FC Basle.
Oscar alitangulia kuwafungia The Blues dakika ya 45, lakini Salah akasawazisha dakika ya 71, kabla ya Streller kufunga la ushindi dakika ya 82 Uwanja wa Stamford Bridge.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Cech, Ivanovic, Cahill, Luiz, Cole, Oscar, van Ginkel/Mikel dk75, Lampard/Ba dk76, Willian/Mata dk67, Eto'o na Hazard.
Basle: Sommer, Voser, Schar, Ivanov, Safari, Salah/Xhaka dk88, Diaz, Frei, Stocker/Ajetidk 83, Sio/Delgado dk65 na Streller.
Mkono kichwani: Frank Lampard (kushoto) akionekana mnyonge wakati Basle wanashangilia ushindi wao Stamford Bridge
Wanyonge: Gary Cahill, Oscar na John Obi Mikel wakisikitikia kipigo
Mshii wa mechi: Marco Streller (wa pili kushoto) akiifungia bao la ushindi Basle
Mkali wa vichwa: Streller (katikati kushoto) akishangilia na mfngaji mwenzake Mohamed Salah
Bao: Mohamed Salah (katikati) akishangilia na wachezaji wenzake wa Basle baada ya kusawazisha
La kusawazisha: Mohamed Salah (katikati) alifunga bao zuri
Huzuni tu: Jose Mourinho amefungwa mechi ya pili tangu arejee Stamford Bridge
Ujumbe kwa kocha: Shabiki la Chelsea akipeleka ujumbe kwa kocha Mourinho kwamba Juan Mata anastahili kucheza na si kukaa benchi
Benchi: Nahodha wa klabu, John Terry alisugua benchi
Anapeperusha bendera : Oscar akishangilia baada ya kuifungia Chelsea mwishoni mwa kipindi cha kwanza
Mikogo kwa mashabiki: Kiungo Mbrazil akishangilia bao lake
Oscar anakwenda kufunga
Ashley Cole akipambana na Salah
WATOTO WA WENGER
ARSENAL imeanza vyema Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kushinda ugenini mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Marseille Uwanja wa Velodrome, Ufaransa.
Mabao ya Gunners yalifungwa na Theo Walcott dakika ya 65 na Aaron Ramsey dakika ya 83, wakati la wenyeji lilifungwa na Jordan Ayew kwa penalti dakika ya 90.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Gibbs, Koscienly, Mertesacker, Sagna, Flamini/Myaichi dk90, Wilshere, Ramsey, Ozil, Walcott/Monreal dk77 na Giroud.
Marseille: Mandanda, Fanni, N'Koulou, Mendes, Morel, Romao, Imbula/Thauvin dk79, Payet/J.Ayew dk72, Valbuena/Khalifa dk89, A. Ayew na Gignac.
Kitu hicho: Theo Walcott ameifungia Arsenal
Kitu kingine: Aaron Ramsey amefunga bao la sita msimu huu
Si mchezo wangu: Mesut Ozil alicheza kiungwana katika ukabaji wake
Kipaji: Theo Walcott akipambana na kiungo wa Marseille, Mathieu Valbuena
Yuko juu: Jack Wilshere alicheza vizuri katika nafasi ya kiungo
Sito rafu? Buti la juu likimuelekea Mathieu Flamini
Rekodi ya klabu: Arsenal imetweet mechi zake 10 ilizoshinda ugenini
Hafunguki kwa urahisi: Steve Mandanda aliibania Arsenal hadi dakika ya 65
Yalaaa: Arsenal walifikiri walistahili kupewa penalti baada ya buti hili alilopigwa Per Mertesacker
Yuko juu: The Gunners ina sababu za kujivunia Ozil
La kufuta machozi: Jordan Ayew akifunga kwa penalti
Mchapakazi: Flamini alionyesha yeye ni mchezaji hodari
Mgumu: Arsene Wenger (kulia) atafurahia Mertesacker na Wojciech Szczesny (kushoto) wasiporuhusu mabao
Nambari moja: Walcott akiupungua umati wa mashabiki baada ya mechi
Alipigana: Olivier Giroud alishindwa, kufunga licha ya kupambana
No comments:
Post a Comment