MAHARAMIA 1O WANAWAKE HATARI KWA MADAWA YA KULEVYA DUNIANI 
             IPO   dhana kwamba wanawake ni daraja hatari sana. Machoni huonekana laini  lakini wanaweza kutenda mambo ambayo ni vigumu kwa mtu wa jinsia ya  kiume. Biashara ya madawa ya kulevya inahitaji watu hatari, katili,  wenye roho isiyotishika. 
 
Mireya Moreno Carreon.
 Nancy Botwin katika ‘siriz’ yake ya Weeds kwenye TV, anajaribu  kuonesha jinsi mwanamke anaweza kuwa hatari katika biashara ya bangi na  madawa ya kulevya kwa jumla, hata hivyo katika uhalisia, hajawafikia  hata chembe wanawake hawa hatari ambao wameitikisa dunia.Hawa ni  maharamia 10 wauza unga, wametengeneza fedha nyingi na kila mmoja  ameshahusika kwa namna moja au nyingine na mauji. Kwa muuza madawa ya  kulevya, kitendo cha kutoa roho ya mtu kipo jirani yake sana.
  
1. GRISELDA BLANCO 
 Inawezekana huyu ndiye akawa muuza unga mwanamke katili, mwenye uwezo  mkubwa kuliko wote kuwahi kutokea katika historia ya dunia. Ameshahusika  na mauaji ya watu zaidi ya 200. Ni raia wa Colombia, akiwa na miaka 11,  tayari alishahusika na tukio la utekaji wa mtoto. 
 
Baadaye alihamia  Marekani, kwenye Jimbo la Florida ambako alitengeneza mtandao wa madawa  ya kulevya ambao ulimpa utajiri mkubwa.
2.  SANDRA AVILA BELTRAN  
 Ni raia wa Mexico, alizaliwa mwaka 1960. Aliwahi kupewa jina la Mungu  wa Kike wa Madawa ya Kulevya. Vyombo vya habari nchini mwake vikamwita  Malkia wa Pacific. Serikali za Marekani na Mexico zinamtaja kuwa kiungo  wa magenge ya unga ya Sinaloa Cartel la Mexico na Norte del Valle Cartel  la Colombia. 
 
Anadaiwa kujipatia mabilioni ya dola kwa usafirishaji wa  unga kati ya Colombia, Mexico na Marekani. Kwa sasa yupo gerezani nchini  Mexico kwa kosa la utakatishaji wa fedha haramu.
3. ANGIE SANCLEMENTE VALENCIA  
 Ni raia wa Colombia, aliwahi kushika taji la urembo la taifa katika  nchi hiyo lakini alinyang’anywa baada ya kubaini ameshaolewa. Mume wake  alikuwa mmoja wa vinara wa unga na walipoachana, alitumia njia zilezile  kujipatia utajiri haramu. 
 
Alikuwa na genge kubwa la wasafirishaji wa  cocaine na kila mtu alimlipa dola 5,000 kwa safari moja. Alisafirisha  zaidi Argentina, Uingereza na Mexico. Ana umri wa miaka 35, yupo  gerezani Argentina tangu Oktoba 27, 2010.
4. KATH PETTINGILL  
 Alizaliwa mwaka 1935. Jina lake la utani ni Bibi Kizee Shetani (Granny  Evil). Ni mwenyeji wa Jiji la Melbourne, Australia. Alianza kama kahaba  kabla ya kugeukia madawa ya kulevya. 
 
Alipoteza jicho moja baada ya  kupigwa risasi katika moja ya matukio ya uharamia, akimtetea binti yake,  Vicky, aliyekuwa anadaiwa dola 300 na maharamia wenzake. Nguvu ya  mtandao wa unga aliyoitengeneza, ni hatari na imehusika na mauaji mengi  nchini Australia.
5. ENEDINA ARELLANO FELIX  
 Katika genge ambalo lilikuwa linaongozwa na kaka zake, Ramon na  Eduardo, mwanzoni yeye alishika nafasi ya umeneja wa fedha. Baada ya  Ramon kuuawa na Eduardo kukamatwa, alishika uongozi. 
 
Maofisa usalama wa  Mexico waliwahi kukiri kwamba Enedina ndiye alikuwa dira ya kaka zake.  Ana umri wa miaka 
 
 Amebadili mfumo na sasa  anaendesha kazi zake kisayansi, 
 hakuna fujo za magenge ya wahuni kiasi kwamba inakuwa ngumu kumtia hatiani. 
6.  BLANCA CAZARES SALAZAR  
 Ni raia wa Mexico, alianza kujihusisha na utakatishaji wa fedha haramu,  aliponogewa akajikita kwenye unga. Ana umri wa miaka 37.
 
 Biashara yake  ameitanua na yupo makini sana. Anaongoza mtandao mkubwa wenye makundi  42. Ni ngumu kumkamata kwa sababu hahusiki moja kwa moja. Marekani  imempiga marufuku kuingia nchini humo.
 
7. MARIA JIMENEZ
 Ana umri wa miaka 27. Alikuwa  kiongozi wa genge lililokufa la La Tosca. Baada ya kufanya biashara kwa  muda mrefu, alikamatwa mwaka jana nchini kwake Mexico kwa tuhuma za  usafirishaji wa unga na mauaji. Baadaye alikiri kuua watu 20 na mpaka  sasa yupo jela.
8.  EDITH LOPEZ LOPEZ  
  Anajulikana kama Malkia wa Kusini. Amekuwa kinara wa madawa ya kulevya  tangu alipoolewa na haramia wa unga, Raul Nunez Morales, maarufu kama 
 
The Cowboy. Tangu mwaka 2000, Edith amebaki kuwa mmoja kati ya wanawake  tisho kwa biashara hiyo haramu duniani.
 
9. THELMA WRIGHT 
 Alishirikiana na marehemu  mumewe, Jackie Wright katika biashara ya unga kati ya miaka ya 1980 na  1990. Mwaka 1986, mumewe aliuawa, kwa hiyo akashika usukani kwa kulisuka  genge lao la Black Mafia ambalo lilifanya matukio mengi. 
 
Hata hivyo,  kwa kuhofia maisha ya mtoto wake, Jackiem,  kuharibika, aliachana na  kazi hiyo na kufanya shughuli nyingine halali. Ni mara chache sana  kutokea.
10. MIREYA MORENO CARREON  
 Ndiye  mwanamke pekee kushika nafasi ya juu kwenye Genge la Zetas. Ndani ya  kipindi kifupi alifanya matukio mengi ya utakatishaji wa fedha haramu na  usafirishaji wa unga. 
 
Akiwa nchini kwake, Mexico, mwaka 2010, maofisa  usalama wa siri walimkamata akiwa akiwa na gari lenye cocaine na bangi  na mpaka leo yupo korokoroni.
  
 
 
 
          
      
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment