Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akionesha bunduki iliyokamatwa mbele ya waandishi wa habari(hawako pichani)inayodaiwa kutumika katika mauaji ya bilionea wa madini Erasto Msuya.

 Bunduki inayodaiwa kutumika katika mauaji hayo.

Pikipiki mbili zinazodaiwa kutumika katika mauaji ya bilionea wa madini Erasto Msuya.
*******************
JESHI  la polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kunasa bunduki aina ya SMG  yenye namba za usajili  KJ10520  inayoaminika kutumika katika mauaji ya  mfanyabiashara bilonea wa madini ya Tanzanaiti , Erasto Msuya (43)  aliyeuawa kwa kupigwa risasi 13 kifuani Augosti 7 mwaka huu Mijohoroni  wilayani Hai.
Mbali  na bunduki hiyo jeshi hilo pia limefanikiwa kuwatia mbaroni watuhumiwa  wengine wanne wanaodaiwa kuwa ni watuhumiwa muhimu katika mipango ya  mauaji ya mfanyabiashara huyo anaye aminika kuwa na vitega uchumi vya  kutosha katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro.
Akizungumza  na waandishi wa habari jana ofisini kwake,kamanda wa polisi mkoa wa  Kilimanjaro,Robert Boaz,aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni ,Sadick Mohamed  Jabir(32) mkazi wa jijini Dar es salaam na Lang’ata
wilaya ya Hai na Karim Issa Kihundwa(33) mkazi wa Lawate wilayani Siha ambao wanatajwa kuwa ni muhimu katika mauaji hayo.
Alisema watuhumiwa hao wawili walikamatwa  eneo  la Kaliua wilaya ya Sikonge  mkoani Tabora wakiwa kwa mganga wa kieneyeji wakifanyiwa zindiko ili  wasitiwe mbaroni  na baada ya kuhojiwa na polisi walieleza jinsi  walivyoshiriki mauaji hayo na mahali walipoficha silaha na pikipiki  zilizotumika katika tukio hilo.
Boaz  aliwataja watuhumiwa wengine kuwa ni Jalila Zuberi  Said(28) mkazi wa  Babati mkoani Manyara pia anaishi wilaya ya kondoa mkoani Dodoma na  Joseph Damas Mwakipesile maarufu kwa jina la ‘Chusa’(35) ambaye pia ni  mfanayabiashara wa madini ya Tanzanite anayeishi Jijini Arusha ambaye  anashikiliwa na jeshi hilo kwa zaidi ya wiki mbili sasa.
Alisema  jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata pikipiki nyingine inayodaiwa  kutumika katika tukio hilo yenye namba za usajili T751 CKB aina ya  KINGLION rangi nyeusi  ambayo wakati wa tukio ilikuwa ikitumia namba za  bandia.
Kamanda  Boaz alisema Bunduki iliyokamatwa ilikutwa ikiwa imefichwa kwneye  tindiga katika eneo la Boroi kwenye mpaka  wa wilaya za Hai na Siha huku  akiendelea kutoa  wito kwa wananchi wapenda  amani  mkoani Kilimanjaro,kuendelea kutoa ushirkiano kwa jeshi hilo katika  kukomesha uharifu.
No comments:
Post a Comment