Showing posts with label Fumanizi. Show all posts
Showing posts with label Fumanizi. Show all posts

Friday, 20 September 2013

WAKE WENZA WASHIKANA UCHAWI HUKO KIMARA...!!


 
WANAWAKE wawili walioolewa katika familia moja ‘wake wenza’, mama Hashimu na mama Fadhila, wakazi wa Kimara King’ong’o jijini Dar, hivi karibuni walifikishwa serikali za mtaa kwa kosa la kutukanana matusi ya nguoni pamoja na kushikana uchawi.
Inadaiwa kuwa wanawake hao ‘walimwagiana’ matusi hayo usiku wa manane na kusababisha watu wengine kukosa usingizi na kukusanyika kuwasikiliza.
Mara baada ya kufikishwa serikali ya mtaa, wake wenza hao walitakiwa kueleza ugomvi wao na kila mmoja kuanza kushusha tuhuma kwa mwenzake.
Mapaparazi wetu waliwashuhudia wakati wake wenza hao walipokuwa wakijieleza mbele ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa King’ong’o, Demetrius Mapesi na Mtendaji wake Amina Rashid.
Mama Hashimu alianza kuelezea kisa kizima na kufuatiwa na mama Fadhila ambaye wakati akijieleza alipandisha mori kiasi cha kumfanya atake kumrukia mwenzake.
Unajua nasikia hasira sana kwa sababu mama Fadhila ameniita mchawi huko mtaani unadhani mimi nitaelewekaje? Ukweli kauli hiyo inaniuma sana,” alisema mama Hashim na kuangua kilio.
Hata hivyo, baada ya kila mmoja kueleza ya moyoni, mwenyekiti wa serikali za mtaa pamoja na mtendaji wake, waliwaamuru wake wenza hao kupeana mkono na kuombana msamaha. 

“Sasa hapa hakuna kesi, kwani wote mna makosa, hebu niambieni mnawafundisha nini watoto wetu kwa matusi
mliyotukanana hadharani?” alihoji mwenyekiti na kuwataka wayamalize mambo hayo.
Aidha, mwenyekiti huyo aliahidi kuwafuatilia ili kuona kama watakuwa wamebadili tabia zao.
Kama vile haitoshi aliwaahidi kama watarudia atawahamisha mtaa pamoja na waume zao kwani mtaani kwao hawahitaji watu wanaotukanana ovyo na kuzushiana mambo ya kichawi.
Baada ya tamko la mwenyekiti, mtendaji wake aliwaamuru wake wenza hao kuandika matusi waliyotukanana kisha akawapiga faini ya shilingi 20,000 kila mmoja.
“Kutokana na matusi yenu nalazimika kuwapiga faini ya shilingi elfu ishirini kila mmoja, ingawaje kwa mujibu wa sheria ya Tanzania mtu akikutwa na hatia ya kutukana anatakiwa kutozwa faini ya shilingi elfu hamsini au kufungwa jela miezi sita,” alisema mtendaji huyo.
Kila mmoja alilipa nusu ya faini na kuahidi kumalizia huku wakisema kuwa hawatarudia kufanya kosa hilo tena

Thursday, 19 September 2013

MLOKOLE AFUMANIWA NA MKE WA MTU

            “Jamaa alikuwa akimuonya sana, lakini aliambulia matusi na kejeli, mwisho wa siku imekuwa hivyo na jamaa akawa hana la kujitetea”...
Stori: MWANDISHI WETU
MATUKIO na vitendo viovu vinaendelea kushamiri juu ya uso wa nchi! Kijana anayedaiwa kuwa muumini wa kanisa la kilokole (jina tunalo) la jijini Dar,  Faraji Oti amekutwa na mazito akidaiwa kufumaniwa na mke wa mtu aliyetajwa kwa jina moja la Jesca..

MANZESE, DAR
Tukio hilo lililoongeza furaha ya Shetani, lilichukua nafasi mwanzoni mwa wiki hii majira ya 11:00 jioni huko Manzese, jijini Dar.
Kwa mujibu wa watu wa karibu na wahusika hao, kisa kilianzia kwenye simu ambapo mwenye mke alidai kunasa mawasiliano ya jamaa huyo na mkewe.
Ilidaiwa kuwa ukaribu wa wawili hao ulianzia kwenye kwaya waliyokuwa wakiitumikia kisha kuzua mawasiliano tata.

OTI AONYWA
Habari zilidai, kuna wakati mume wa Jesca alimuonya Oti kukaa mbali na mkewe lakini jamaa alipuuza huku akidaiwa kutoa maneno makali na ya dharau kwa mwenye mali.
“Jamaa alikuwa akimuonya sana, lakini aliambulia matusi na kejeli, mwisho wa siku imekuwa hivyo na jamaa akawa hana la kujitetea,” alidai mmoja wa watu wa karibu na mwenye mke.

SIMU NI TATIZO?
Habari zilizidi kudai kuwa siku ya tukio mwanamke huyo alianza kutuma meseji kwa jamaa ya kumjulia hali na kuiacha simu mbele ya mumewe aliyejulikana kwa jina moja la Mustapha.
Ilisemekana kuwa mwenye mke aliamua kuendeleza mawasiliano hayo akijifanya Jesca na ndipo jamaa akaingia ‘kingi’, akapanga wakutane bila kujua aliyekuwa akibadilishana naye sentensi kwa njia ya meseji ni ‘mume mwenzie’.
Ilidaiwa kuwa ili kumshikisha adabu Oti, alimbana mkewe na kumwambia, pona yake afanikishe kupatikana kwake.
Kulinda ndoa yake, mke aliamua kuendelea kuchati na Oti na wakapanga wakutane na baada ya hapo mume akafuatilia  kwa nyuma hadi wawili hao walipokutana maeneo ya Manzese.
Ilidaiwa kuwa, baada ya Oti na Jesca kuingia kwenye gesti iliyopo maeneo hayo, jamaa huyo aliwajulisha marafiki na watu wake wa karibu ambao walifika eneo la tukio na kuwakuta wakijiandaa ‘kufanya yao’.
Habari ziliendelea kutapakaa kuwa Oti hakuwa na cha kusema zaidi ya kujitetea huku akiomba msamaha kwa madai ya kupitiwa na shetani.
Ilisemekana kuwa jamaa mwenye mke alimuamuru Oti aondoke zake huku washikaji wakimnyang’anya simu.
Baada ya kuzinyaka taarifa hizo, mwanahabari wa gazeti hili alitumia njia ya ‘kiitelejensia’ kuipata namba ya simu ya mtuhumiwa ambapo alipopigiwa alikiri kukutwa na masaibu hayo huku akijitetea kuwa hakuwa na uhusiano mbaya zaidi ya mazungumzo ya kawaida na kuomba msamaha kwa yote yaliyotokea.
“Ni kweli nilikutana na yule mwanamke lakini sikuwa na nia ya kufanya chochote naye, japo tuliwahi kuwa wapenzi siku za nyuma, pamoja na hayo sina jinsi zaidi ya kukiri na kuomba msamaha, nilishatubu kwa Mungu wangu,” alisema Oti na kuongeza:
“Narudia tena ndugu mwandishi, sina uhusiano mbaya na Jesca kwani hata siku hiyo nilikuwa na lengo la kusalimiana naye tu na si kufanya chochote kibaya.”

MASWALI TATA
Kama Oti alimwita mwanamke huyo kwa ajili ya salamu na mazungumzo ya kawaida mbona walikutwa chumbani?
Kama kweli Mustapha alikuwa na nia ya kumpata mbaya wake na kumchukulia hatua za kisheria kwanini hakuvihusisha vyombo vya usalama?
Ikiwa Jesca ana mume aliwezaje kumtumia meseji mpenzi wake wa zamani na baadaye kushiriki katika mtego?

Mezani kwa mhariri
Ijumaa linaendelea kuifanyia kazi habari hii na chochote kipya kitakachopatika tutawaletea.

-IJUMAA VIA GPL

Saturday, 24 August 2013

MUME AMFUMANIA MKEWE AKIBANJUKA NA RAFIKI YAKE

                                                      Nimesha aibika Jamani
KWELI duniani uaminifu kwa sasa ni sifuri! Hii ni aibu ya uzinzi! Jumatano iliyopita kwenye nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Kurasini jijini Dar, Kennedy Shayo, mkazi wa eneo hilo, alimfumania ‘laivu’ swahiba wake, Sebastian Masangula akiwa kwenye harakati za ‘kubanjuka’ na mkewe, Fatuma Shayo. Kwa mujibu wa chanzo makini, kwa muda mrefu Masangula alikuwa akimtokea mke wa rafiki yake kwa meseji tam’tamu za simu huku akisisitiza kutaka kuvunja naye amri ya sita ya Mungu.
                          Huyu Mwanaume kila kitu nampatia,sijui amefuata kitu gani huku
Inadaiwa kuwa, mwanamke huyo alimuonya Masangula aache kumfutafuata lakini jamaa huyo akawa ‘sikio la kufa’ na kuendelea kumsumbua shemeji yake huyo akitaka apewe penzi japo kiduchu.
                                                                   Ninaumbuka!
MTEGO WA KUMNASA MASANGULA WAANDALIWA
Baada ya Masangula kumsumbua shemeji yake kwa muda mrefu, mwanamke huyo alimuweka wazi mumewe ambaye alishtuka kupita maelezo ndipo wakaandaa mtego wa fumanizi kwa kuwashirikisha mapaparazi wetu wa kikosi cha Oparesheni Fichua Maovu ‘OFM’.

                               Yani huyu baba amenisumbua muda mrefu sana akinitaka 
Mtego huo ulianza kutegwa mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya Masangula kumuomba shemeji yake huyo wakutane kwenye gesti hiyo.
Siku ya tukio wawili hao walifika eneo hilo lakini Masangula kama machale yalimcheza na kuchoropoka kwenye fumanizi kwa kuomba udhuru huku akimwambia shemejiye kwamba waivunje amri ya saba siku nyingine


Mungu wangu aibu gani hii mimi? Nisameheni Jamani
LA KUVUNDA HALINA UBANI
Kama methali ya wahenga isemavyo ‘la kuvunda halina ubani’, ndivyo ilivyokuwa kwa Masangula kwani licha ya machale kumcheza siku ya kwanza na kuchoropoka, wiki iliyopita aliendelea kuomba penzi kwa shemejiye ndipo mtego ukapangwa tena na mzee mzima safari hii alinaswa laivu kitandani akimtolea udenda shemeji yake huku akiwa na kufuli tu. Shemeji mtu naye alifanya ‘magilini’ kama anataka kuvua nguo zake.

Mwanamke huyo kabla ya kuvua alimtonya mumewe aliyekuwa nje na mapaparazi kwamba, jamaa yuko kama alivyozaliwa, ndipo kikosi kazi kikavamia kwenye chumba namba nne ndani ya gesti hiyo na kumnasa Masangula.

MASANGULA ASHIKWA UGONI
Ndani ya chumba, mwenye mke aligongana uso kwa uso na Masangula aliyekuwa tayari kwa mechi.  Tukio hilo lilimfanya mgoni huyo achanganyikiwe na kushika tama kwa aibu huku akiomba msamaha kwa maneno mbalimbali ya huruma.

UMATI WAFURIKA
Dakika moja mbele, umati mtaani ulifurika kwenye gesti hiyo kila mmoja akitaka kuwaona waliofumaniwa.

MKE WA MASANGULA AITWA AONE AIBU YA MUMEWE
Baadhi ya wapambe walimpigia simu mke wa Masangula (mama Gire) afike eneo la tukio kushuhudia aibu ya mumewe lakini simu ya mama Gire ikawa haipatikani.
Wapambe hao waliamua kukodi Bajaj kumfuata kisha kumpeleka eneo la tukio.
Baada ya kufika, mama Gire alipigwa butwaa kumwona mumewe alivyonaswa.
“Masikini ya Mungu baba Gire, hivi umekosa nini nyumbani mume wangu? Hii aibu gani mume wangu, umenidhalilisha sana mtaani, huyo Shayo si unasemaga ni rafiki yako siku zote? Sasa leo iweje utake kumsaliti?”
Licha ya kuulizwa maswali na mkewe lakini mgoni huyo hakujibu chochote zaidi ya kujikunyata na kuwapigia magoti mkewe na rafiki aliyetaka kumsaliti kwa mkewe.

MAMA SHAYO ALONGA
Wakati mke wa Masangula akijutia aibu ya mumewe, Fatuma alianza kumwelezea  Masangula jinsi alivyoanza kumfukuzia kwa muda mrefu.
“Mumeo kwa muda mrefu alikuwa akinitongoza, najua lengo lake alikuwa akitaka anidhalilishe lakini kakuta mimi siyo mtu wa kihivyo,” alisema.
Naye mume wa Fatuma, akizungumza na mapaparazi wetu alisema amesikitishwa na kitendo kilichofanywa na swahiba wake huyo ambaye walikuwa kama ndugu.
“Mke wangu alivyonieleza mara ya kwanza sikumuamini, nikajua ni mambo ya wanawake, anataka kunigombanisha na rafiki yangu, lakini baada ya kunionesha ujumbe aliokuwa akitumiwa na ni namba ya rafiki yangu nilipigwa butwaa,” alisema Shayo huku akionekana mwenye jazba.
Hadi mapaparazi wetu wanaondoka eneo la tukio, Shayo alikuwa katika harakati za kumfikisha mgoni wake kwenye vyombo vya dola. 

Source:GPL