Kifaa hicho kikionyeshwa kwa wananchi, waumini na wanahabari.
Kifaa cha TMA kikitolewa katika transfoma.
JUZI (Jumapili) hali ya taharuki ilizuka kwa waumini wa Kanisa la KKKT Usharika wa Kijitonyama wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam baada ya kuonekana kifaa cha Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kilichosadikiwa kuwa bomu.
Kifaa hicho ambacho kilifungwa katika boksi kilikutwa juu ya transfoma umbali wa takribani meta 20 kutoka nje ya kanisa hilo.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jana, Mtabiri Mwandamizi wa TMA, Agustine Kanemba alisema kifaa hicho huwa kinarushwa kila siku kwenda angani kwa urefu wa kilometa 55,000 kikiwa kimeambatana na puto.
Alisema kikifika huko puto hupasuka na kusababisha kifaa hicho kudondoka chini jambo ambalo linasababisha wao kupata taarifa za hali ya hewa ya anga baada ya hatua hiyo.
Source:GPL
No comments:
Post a Comment