Wednesday, 4 September 2013

PENNY: DIAMOND SUKARI YA WAREMBO

                                      Penny Mwingila ‘Penny’ akipozi na Diamond
Mpenzi wa mkali katika tasnia ya Bongofleva, Penny Mwingila ‘Penny’ amekiri kuwa mpenzi wake huyo ni sukari ya warembo, hivyo hana wasiwasi naye.
Akiongea  katika ukumbi wa Kivukoni uliopo ndani ya Hoteli ya Serena muda mara baada ya kumalizika kuoneshwa kwa video mpya ya Diamond inayokwenda kwa jina la My number One, Penny alisema:
“Sishtuki na chochote katika video ile ya Baby wangu kwani natambua kuwa mpenzi wangu ni sukari ya warembo, ila namshauri atafute madansa wa kike wa hapa nchini afanye nao kazi kama wale Wasouth wanavyoonekana katika video yake mpya,” alisema Penny.
Video hiyo ya Diamond imerekodiwa Afrika Kusini ambapo kwa mujibu wake  wa Diamond ametumia shilingi milioni 48  kuandaa kazi hiyo.

No comments:

Post a Comment