GAUNI alilolivaa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Jacquline Wolper limeonekana kutibua hali ya hewa kutokana na ukubwa wa mpasuo kiasi cha midume kumtolea macho ya matamanio staa huyo.Tukio hilo lilichukua nafasi nje ya hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar wakati wa utambulisho wa video ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ inayokwenda kwa jina la My number One.
Wolper akiwa ameweka mapozi kwa ajili ya kupiga picha, aliwashtua wanaume waliokuwa wakielekea katika magari yao sehemu ya maegesho na kuanza kumtolea macho.
“Father cheki mpasuo huo kushoto kwako hapo ulipokaa ni mahali pake?” alisikika mwanaume mmoja aliyepita karibu na alipokuwa amesimama Wolper.
Baada ya kusikika kauli hiyo, mwigizaji huyo alibaki akicheka na kusema kuwa hashawishiki na maneno yao.
“ Kwani ni peke yangu niliyevaa gauni lenye mpasuo mkubwa?” alihoji Wolper.
No comments:
Post a Comment