Muigizaji wa filamu za kibongo maarufu kwa jina Jackline Wolper amewaasa waigizaji wenzake wa kike kuacha kuvaa nguo za nusu uchi kwani ni kinyume na mila na tamaduni za kitanzania .
Wolper aliyasema hayo kufuatia kupigiwa kura na kushinda kama muigizaji wa kike mwenye muonekano wa kistaa...Akizungumza katika kipindi cha filamu cha Take One kinachorushwa Clouds Tv , Wolper alisemakuwa yeye hawezi kuvaa mavazi ya nusu uchi ila anavaa mavazi yanayomsitiri mwili wake na bado anapendeza kuliko hao wanaovaa nusu uchi halafu hawapendezi."Nawashukuru sana mashabiki wangu kwa kunipigia kura hadi kuibuka mshindi, na ni kweli najiamini kwa kuwa mimi hata siku moja huwezi kuniona nimevaa nguo za nusu uchi kama wengine" Wolper

STAA wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper juzikati alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuvunja glasi ya Rais wa Wasafi, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Tukio hilo lilijiri Agosti 28, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Serena, Posta jijini Dar ambapo staa huyo alikuwa kwenye uzinduzi wa video ya Diamond.
Ilikuwa wakati Diamond akisalimiana na mastaa mbalimbali, alipofika kwa Wolper aliigusa kidogo, ikaanguka.
Paparazi wetu alipomuuliza Wolper sababu ya glasi hiyo kuvunjika, alijibu: “Hata mimi sijui nini kimetokea, tulikuwa tunasalimiana ghafla tu glasi yake ikadondoka na kupasuka, sijui ni miujiza au nini loh!”
Diamond naye akatia neno: “Nimeshtukia glasi ipo chini tu, daah! Sina hata cha kueleza juu ya hili.”-GPL
LULU BATULI WOLPER KAJALA WEMA SEPETU
GAUNI alilolivaa mwigizaji wa filamu za Kibongo, Jacquline Wolper limeonekana kutibua hali ya hewa kutokana na ukubwa wa mpasuo kiasi cha midume kumtolea macho ya matamanio staa huyo.Tukio hilo lilichukua nafasi nje ya hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar wakati wa utambulisho wa video ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ inayokwenda kwa jina la My number One.
Wolper akiwa ameweka mapozi kwa ajili ya kupiga picha, aliwashtua wanaume waliokuwa wakielekea katika magari yao sehemu ya maegesho na kuanza kumtolea macho. “Father cheki mpasuo huo kushoto kwako hapo ulipokaa ni mahali pake?” alisikika mwanaume mmoja aliyepita karibu na alipokuwa amesimama Wolper.
Baada ya kusikika kauli hiyo, mwigizaji huyo alibaki akicheka na kusema kuwa hashawishiki na maneno yao.
“ Kwani ni peke yangu niliyevaa gauni lenye mpasuo mkubwa?” alihoji Wolper.