Showing posts with label DIAMOND. Show all posts

Saturday, 21 September 2013
PENNY: "DIAMOND AKISAFIRI HUWA NAPATA HOMA KABISA"
![]() |
| Penny au sukari ya Diamond |
Yule mwanadada anayewapandisha presha wadada wa mujini Penny mungilwa ama ukipenda muite sukari ya Diamond amechonga na thesuperstarstz nakueleza mengi kuhusu sukari wake huyo ambaye kwa sasa yupo nchini malaysia katika bonge la show.
Penny ambaye pia ni mtangazaji wa Tv hapa nchini tanzania amesema kwake hakuna wakati mgumu anaoupata kama Diamond akisafiri penny aliielezea thesupestarstz kuwa anaumia sana kumkosa sukari wake huyo na mara nyingi hujikuta akiugua kabisa kama diamond akimtajia safari.
Penny ameyasema hayo wakati diamond akiwa nchini malaysia kikazi alikokwenda kupiga bonge la show nchini humo na kumuacha penny ndani ya bongo....Kiukweli hakuna wakati mgumu na huwa naumwa kama diamond akisafiri yaani huwez amini nimemzoea sana bby wangu jamani alisema penny

Muandishi wetu alimdadisi kutaka kujua kwanini aumwe au hamtakii mwenzie mafanikio maana mtu kama diamond anaposafiri kikazi ujue ndio anaingiza mkwanja na pia anajitangaza yeye na nchi yetu kiujumla ambapo panny alianza kwa kuna kuwa hamtakii mafanikio nakuongeza kuwa..No nafurahi d anaposafiri na ninamtakia mafanikio mema ila nataka ujue hii nikutokana na jinsi tulivyoshibana na kuzoeana na sio mimi pekee yangu hata yeye nikisafiri hapati usingizi kucha ni simu hadi kunakucha alisema mwanadada huyo
![]() |
| Penny mapozi |
Hapo ni kama alimchokoza mwandishi wetu nakujikuta akitaka kujua kama huwa kuna wakati wanasafiri wote au lah!!,,Mbona mara nyingi tu alijibu kifupi na ndipo nilipomuuliza kwanini hali hiyo inamtokea akasema.... Unajua mimi na Nassebu tumekuwa kama mapacha sasa mmoja akienda mbali na mwenzie basi aliyebaki huwa kama mgonjwa na ndio maana diamond akiwa mbali na mimi utakuta tunaongea na simu hadi mimi na mzuia maana hatulali sasa na hii ni ili kunifanya nione tupo wote kiukweli tumezoeana sana aliendelea kusema penny
Hilo bango hapo juu ndio kazi liyompeleka Diamond huko Malaysia ambapoa kwa mujibu wake ni kwamba atahakikisha anaacha jina huko kama kawaida yake.
HII NDO HOTEL ALIYOFIKIA DIAMOND KWAAJILI YA SHOW YAKE HUKO MALAYSIA
I hope mashabiki wangu tayari mnafahamu kuwanimo nchini Malaysia kwa Tour ya kimziki,nashukuru Mungu nilifikia
salama kabisa mimi na team yangu yaWCB WASAFI,nimepata
mapokezi mazuri kiukweli kiasi cha kujiskia niko nyumbani.
Pichani ni chumba cha hotel ninamopumzishia mbavu zangu Tayari
kabisa kwa kwa kuwapa watu wangu wa Malaysia burudani inayowastahili pamoja na kuiwakilisha nchi yangu Tanzani..is gonn down babay!!!! ''Amesema diamond kupitia blog yake

Thursday, 19 September 2013
VIDEO:MZUNGU WA KIMAREKANI AKIIMBA NYIMBO YA'MBAGALA' YA DIAMOND MWANZO MPAKA MWISHO

CHEKI HAPA
Tuesday, 17 September 2013
HII NDIO AUDIO IKIELEZEA MAJIBU YA DIAMOND KUHUSU KUIBA NYIMBO YA BABA LEVO NA DYNA PAMOJA NAKUMPA MIMBA DEMU WA KIDATO CHA NNE
Hatimaye Diamond Platnumz leo amejibu tuhuma kadhaa zilizokuwa zikimkabali ikiwemo ile ya Dayna Nyange kudai kuwa alitumia beat ya wimbo wake kurekodi wimbo wake unaotamba sasa, Number 1 na pia kuhusu Baba Levo kudai Diamond alimuibia chorus ya wimbo wake. Katika mahojiano na kipindi cha XXL cha Clouds FM, Diamond pia amejibu scandal kuhusu kumzalisha binti wa kidato cha nne skendo ya magazeti wiki iliyopita sikia majibu yake hapa chini
Monday, 16 September 2013
Saturday, 14 September 2013
MDADA WA KENYA ANAYEDAIWA KUWA MPENZI WA DIAMOND AJICHORA TATTOO YA DIAMOND.
![]() |
| Angel |
hao walikuwa bega kwa bega Nairobi na Mombasa wakati Diamond alipokuwa na show nchini humo na kwa mujibu wa mitandao ya huko iliripotiwa Angel kupata nafasi ya kulala na Diamond. Angalia tattoo hiyo hapo chini...
tattoo aliyojichora na hapo chini akiwa na Diamond

Thursday, 12 September 2013
DIAMOND AJIBU TUHUMA ZA KUMTUNDIKA MIMBA MWANAFUNZI NA ZILE ZA DYNA
Hatimaye Diamond Platnumz leo amejibu tuhuma kadhaa zilizokuwa zikimkabali ikiwemo ile ya Dayna Nyange kudai kuwa alitumia beat ya wimbo wake kurekodi wimbo wake unaotamba sasa, Number 1 na pia kuhusu Baba Levo kudai Diamond alimuibia chorus ya wimbo wake.
Katika mahojiano na kipindi cha XXL cha Clouds FM, Diamond pia amejibu scandal kuhusu kumzalisha mwanafunzi iliyoandikwa na magazeti ya leo.
Msikilize hapa akijibu.
Wednesday, 11 September 2013
MAMILIONI YAZIDI KUONGEZEKA KWA MSANII DIAMOND, HILI NDO DILI JIPYA ALILOPEWA NA VODACOM

Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa offer ya miito ya simu jijini Dar es Salaam. Kupitio ofa hio, wateja wanaweza kuchukua wimbo wa Diamond Platinumz kama Ring Back Tone (RBT) na wajishindie Tsh50,000 kwa siku. Kushoto ni msanii wa muziki ya kizazi kipya, Diamond Platinumz na kulia ni Meneja wa Mahusiano ya Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim.

Msanii wa muziki ya kizazi kipya Diamond Platinumz (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa offer ya miito ya simu jijini Dar es Salaam. Kupitia ofa hio, wateja wanaweza kuchukua wimbo wa Diamond Platinumz kama Ring Back Tone (RBT) na wajishindie Tsh50,000 kwa siku. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa (katikati) na kulia ni Salum Mwalim, Mejena wa Mahusiano ya Nje, Vodacom Tanzania.

Msanii wa muziki ya kizazi kipya Diamond Platinumz (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, punde baada ya kusaini mkataba utakaowezesha wateja kuchukua wimbo wa Diamond Platinumz kama Ring Back Tone (RBT) na wajishindie Tsh50,000 kwa siku. Anayeshuhudia ni Salum Mwalim , Mejena wa Mahusiano ya Nje, Vodacom Tanzania.

Msanii wa muziki ya kizazi kipya Diamond Platinumz (mwenye fulana nyekundu) akiucheza wimbo wake mpya ujuikanao kama My Number One, wakati wa uzinduzi wa mkataba utakaowezesha wateja kuchukua wimbo huo kama Ring Back Tone (RBT) na wajishindie Tsh50,000 kwa siku. Mkataba huo ni baina ya Diamond Platinumz na Vodacom Tanzania. SOURCE : ISSA MICHUZI
Tuesday, 10 September 2013
VIDEO YA BINTI WA KIDATO CHA NNE AKISIMULIA JINSI ALIVYOTONGOZWA NA DIAMOND(SIMULIZI YA UONGO)
MREMBO Sasha Juma, 20, kwa sasa anapitia kipindi cha majuto, analipia gharama ya kujivalisha ubandidu na kujisingizia kupewa mimba na supastaa, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’.
Sasha, akiwa na macho makavu, alitamka mbele ya waandishi wetu kuwa mimba hiyo aliyopewa na Diamond, ilimgharimu kufukuzwa shule akiwa kidato cha nne mwaka jana.
Unadhani Sasha analo tena? Ameshaumbuka na baada ya simulizi yake ya kutunga kushtukiwa, hivi sasa mrembo huyo anatishia kujiua.
Mr. Juma ambaye ni baba mzazi wa Sasha, aliliambia Risasi Mchanganyiko: “Huyu mtoto ametishia kujiua, anajua makosa aliyoyafanya. Anataka kutuvuruga vichwa, ukweli ni kwamba kila alichokisema kuhusu Diamond ni uongo mtupu.
“Nahisi kuna mtu yupo nyuma yake, sasa anataka kumtumia ili kumchafua Diamond, upande mwingine akili yangu inaniambia yule mtoto anataka umaarufu, maana najua yule ni mwigizaji, sasa pengine anataka kutoka.”
UONGO WA SASHA
Risasi, lilipata taarifa kuhusu malalamiko ya Sasha ambaye alikuwa akidai kupotezewa dira ya maisha na Diamond kwa sababu alimpa mimba na kumtelekeza na mtoto mwenye umri wa miezi minne.
Baada ya kupata ‘tipu’ hiyo, mwandishi wetu alimsaka kwa udi na uvumba mpaka Septemba 4, mwaka huu (Jumatano ya wiki iliyopita) ambapo mrembo huyo alitia maguu kwenye mjengo mkubwa wa magazeti pendwa nchini Tanzania.
Baada ya kuwasili makao makuu ya Global Publishers, Bamaga, Mwenge, Dar es Salaam, Sasha aliingizwa kwenye chumba maalum chenye mitambo ya kurekodi sauti na picha kisha akaanza kumwaga simulizi yake.
Alidai kuwa alikutana na Diamond, Mlimani City, mwaka jana, wakapeana namba za simu kabla ya kuanzisha uhusiano wa kimapenzi ambao uliwafikisha kwenye ‘kategori’ ya kuparamia kitandani na kutenda mchezo wa baba na mama pasipo kutumia na kinga.
“Nilipopata mimba Diamond alinishawishi nisitoe, akaniahidi atanisomesha hata kama nitafukuzwa shule. Baadaye nilifukuzwa shule, akazidi kunipa moyo kwamba atanilinda. Mimba ilipokuwa kubwa akapotea, nilipozaa hakujitokeza.
“Diamond akawa siyo yule ambaye alikuwa ananipa moyo. Alibadilika, hali hiyo ikanifanya nione mwanangu hana baba, hata cheti za kuzaliwa, sijamwandika Diamond, mtoto wangu nimempa ubini wa baba yangu, yaani ya Juma.”
NI UONGO MTAKATIFU
Ili kukamilisha habari hiyo ambayo ilitoka kwenye gazeti hili, toleo la Jumamosi iliyopita, mwandishi wetu aliwasiliana na baba mzazi wa Sasha (Mr. Juma) ambaye alipoambiwa kuhusu mwanaye kuzaa na Diamond, alishtuka kisha akasema:
“Unajua yule mtoto sikai naye, anaishi na mama yake. Mimi sijui chochote ila nashangaa, inawezekanaje apate mimba mpaka azae mimi baba yake sijui? Ngoja niongee na mama yake.”
Mr. Juma alipiga simu kuzungumza na mama yake Sasha mbele ya mwandishi wetu. Mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo;
MR. JUMA: Habari yako.
MAMA SASHA: Salama tu, za kwako?
MR. JUMA: Namshukuru Mungu, ebwana mbona Sasha kaongea na mwandishi wa habari anasema kapewa mimba na Diamond na amezaa?
MAMA SASHA: Wewe si unajua haya mambo ya vijana?
MR. JUMA: Mambo ya vijana kivipi? Ina maana mtoto anapata ujauzito mpaka anazaa wewe na baba yake hamjui?
MAMA SASHA: Baba nani, si wewe?
MR. JUMA: Mimi baba yake sijui, ndiyo maana nakuuliza wewe, maana nimesikia umekuwa unawasiliana na Diamond kuhusu hili.
MAMA SASHA: Nani kakwambia? Nimeshasema hayo ni mambo ya watoto, naomba umuulize mwanao vizuri, kama hauna namba yake nikutumie.
Katika mazungumzo hayo, Mama Sasha, hakumpa majibu ya moja kwa moja mzazi mwenzake, kuhusu binti huyo kupata mimba, kuzaa na Diamond kuwa mhusika.
RIPOTI YA WIKI HII
Mr. Juma alifika ofisi za Global Publishers na kueleza: “Jana (Jumapili iliyopita), nilimchukua Sasha na kuzungumza naye kwa kirefu, kwa kifupi alikiri kuwa hajawahi kupata mimba na yule mtoto si wa kwake.
“Mtoto imebainika ni wa dada yake, yaani mtoto mkubwa wa Mama Sasha ambaye anaitwa Khadija. Kuna kitu cha kujifunza hapa kuwa Sasha aliwadanganya mpaka watu ambao niliwakabidhi ili wamsaidie kisanii.
“Kabla sijaongea kwa kirefu na Sasha, nilizungumza na Thabit Abdul (mwanamuziki wa Five Stars) ambaye nilimkabidhi kwake kumsimamia kisanii, nikamuuliza inakuwaje mtoto anapata mimba? Akanijibu hata yeye anashangaa. Kwani hata yeye alishangaa kumuona Sasha akiwa na picha nyingi amebeba mtoto kwenye simu yake.
“Akamuuliza umezaa akajibu ndiyo. Hisia zangu zinazunguka katika mambo mawili, ama aliamua kutunga ili kupata umaarufu kupitia jina la Diamond au alitumwa na mtu. Jana wakati nazungumza na Sasha, nilikasirika sana, nikaona hatutafika pazuri.
“Ikabidi nimpigie simu rafiki yangu mmoja ili amwite azungumze naye. Kweli alimwita wakazungumza, baadaye yule rafiki yangu akaniambia Sasha kasema anaona mambo yanazidi kuwa makubwa, kwa hiyo anataka kunywa sumu afe. Namshangaa sana huyu mtoto, sijui ana kichaa gani?”
UKWELI NI HUU
Kwa mujibu uchunguzi wetu usio na shaka, mtoto aliyepigwa picha akiwa amebebwa na Sasha, mama yake halisi ni dada wa mrembo huyo ambaye ni Khadija.
Sasha na Khadija wanaunganishwa na mama yao lakini kila mmoja ana baba yake.
Uchunguzi zaidi ulibaini kuwa kwa sasa Khadija anaishi na mwanaye mkoani Tanga, huku Sasha akiendelea kupuyanga ndani ya Jiji la Dar, akiwa hajui tamu wala chungu ya kunyonyesha, vilevile hajawahi kusikia uchungu wa uzazi wala hatambui sura ya ‘leba’ ilivyo.
Khadija akizungumza kupitia simu ya Mr. Juma, huku mwandishi wetu akifuatilia mazungumzo, alisema: “Nikija Dar nitafika Global, mimi ndiyo mama wa yule mtoto na zile picha Sasha alipiga na mtoto siku ya arobaini yake.
“Sasha anataka kunisababishia matatizo na baba mzazi wa mtoto. Mimi kama mama mzazi wa mtoto, simjui Diamond, kwa hiyo hahusiki chochote na mtoto wangu.”
Aidha, Mr. Juma alisema kuwa alimpigia simu Diamond na kumuweka sawa kuhusiana na tuhuma ambazo binti yake alimsakizia.
“Diamond anajua kila kitu, nimeshaongea naye na nimejaribu kumtaka atulize munkari, maana ni wazi zile taarifa zimemchukiza sana. Kweli zimemchukiza.”
DIAMOND ANASEMAJE?
Gazeti hili lilipozungumza na Diamond, alisema: “Nilishasema simjui huyo Sasha, ahadi yangu ipo palepale, nitampeleka mahakamani. Amenichafua sana.
“Masharti yangu ni haya, kama anataka nimsamehe aende kweye redio na televisheni akatangaze kwamba sijampa mimba.”
ONYO
Aibu ambayo Sasha anakutana nayo sasa na tishio la kuburuzwa mahakamani ambalo analikabili kutoka kwa Diamond ni onyo kwa watu wengine ambao wamekuwa na tabia za kuwasingizia wenzao ili kujipatia umaarufu.
Risasi linazo taarifa kwamba tangu alipoumbuka, Sasha amekuwa mtu wa kujificha, akikwepa kukutana na watu ambao wanajua mkanda mzima wa simulizi yake ya kutunga.
Tazama video hapo chini
-GPL

Monday, 9 September 2013
PENNY ATOA ONYO "MSICHANA ATAKAE MGUSA DIAMOND ATAJUA MIMI MTOTO WA KITANGA"

Mtangazaji nyota nchini ambae ni mchumba wa kupika na kupakua wa mwanamuziki Diamond Penny amevunja ukimya na kutoa onyo kali kwa wasanii wa kike na wasio wasanii kumlaia mbali baby boy wake Diamond.
Habari za uhakika toka kwa mtu wa karibu na Penny anaeishi nae maeneo ya Mwananyamala ambae pia aliomba hifadhi ya jina lake alisema “ Jamani Penny amejipanga kuolewa na Diamond kwani sasa hivi amecharuka na kutoa onyo kali kwa mwanamke yeyote atakae msogelea mchumbaake huyo la sivyo ataroka mtu” Alisema dada huyo ambae anafanyakazi nyumba ya jirani na anapoishi Penny
Penny amepiga mkwara huo hasa akimlenga zaidi msanii Lulu na Linah nk huku akitahadharisha kuwa anawaomba wote wenye tabia ya kuchukua wanaume za watu kwani yeye katika maisha yake hajawahi kuchukua mume wa mtu hivyo kama akihisi kuna ajenda yoyote ya siri kati ya mchumbaake na wasanii hao hakika ataroga mtu kwani yeye ni mtoto Mdigo halisi.
Aidha chanzo hicho kiliongeza kusema kuwa penzi la Penny na Diamond limefikia pazuri kiasi cha familia zao kutembelea na kula pamoja kama wakwe. Hata hivyo ilielezwa kuwa Familia ya Diamond imeshampa Baraka zote mtoto wao ili amuoe kabisa Penny na huku nae Penny akihimizwa kudumisha upendo wa dhati kwa Diamond ambae tangu aanze kuishi na mtangazaji huyo Diamond amebadilika sana kitabia kiafya nk.
Sunday, 8 September 2013
VIDEO ZA MASHABIKI WA DIAMOND WAKICHEZA NYIMBO YAKE MPYA MY NUMBE ONE INAFURAHISHA SANA
Diamond Platinumz kupitia account yake ya Instagram amekuwa akipost video tofauti za mashabiki wake wakicheza style mpya ambayo ameitumia kwenye wimbo wake wa Number One. According to Diamond video nyingine zinatoka nje ya Tanzania na baadhi zinatoka hapahapa Tanzania. Cheki baadhi ya hizi video.
Saturday, 7 September 2013
DENT KIDATO CHA NNE: NIMEZAA NA DIAMOND
MREMBO aliyetimuliwa shule akiwa kidato cha nne baada ya kutundikwa mimba, Sasha Juma ameibuka na madai kuwa amezaa na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
MCHEZO MZIMA
Habari kutoka kwa chanzo chetu cha kuaminika zilidai kuwa Sasha na Diamond walikutana katika mgahawa mmoja uliopo kwenye maduka ya Mlimani City, Dar na ndipo walipoanzisha uhusiano.
Ilidaiwa kuwa Sasha akiwa na marafiki zake alitoka kwenye moja ya maduka hayo ambapo alimkuta Diamond na binamu yake, Romy Jones wakiwa wamekaa nje ya mgahawa huo.
Ilidaiwa kwamba kwa kuwa Sasha anajuana na Romy muda mrefu, aliwafuata kisha akawasalimia ndipo Diamond akaonekana kuvutiwa na mrembo huyo na kumwambia kuwa atachukua namba yake ya simu ya kutoka kwa Romy kwa vile alikuwa nayo.
Chanzo chetu hicho kilizidi kutiririka kuwa baada ya hapo Sasha aliondoka na marafiki zake, kipindi hicho akiwa anasoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Dar es Salaam International iliyopo Sinza-Kumekucha, Dar.
WAKUTANA
Ilidaiwa kuwa Diamond alianza kuchati na Sasha kabla ya kukutana na ‘kufanya yao’.
Shushushu huyo alitonya kuwa Sasha na Diamond walikutana Sinza-Palestina, Dar wakati huo mwanamuziki huyo alikuwa akimiliki gari aina ya Toyota Opa.
WEMA ATAJWA
Ilidaiwa kuwa Sasha alipotimba eneo la tukio aliingia ndani ya gari la Diamond na kuongea naye kuhusu mapenzi ambapo msanii huyo alimwambia kitu ambacho alichovutiwa kwake ni jinsi mrembo huo alivyofanana na Wema Isaac Sepetu ambaye aliwahi kuwa mwandani wa jamaa huyo.
Madai yalizidi kushushwa kuwa baada ya mwanamuziki huyo na Sasha kukubaliana walipanga kuonana kesho yake katika hoteli moja maarufu iliyopo Sinza-Madukani, Dar ambapo msanii huyo alimwambia mrembo huyo atangulie atapewa ufunguo na kuoneshwa chumba na wahudumu.
Ikasemekana kwamba baadaye Diamond alifika na kuungana na wenzake chumbani.
Ilidaiwa kuwa jamaa alipotimba chumbani alimbebea ‘mtoto’ kinywaji laini aina ya Saint Anna.
‘Niuzi’ za chumbani zilidadavuliwa kuwa wakati wakiendelea kupiga kinywaji mdogomdogo ndipo staa huyo akaomba ‘mchezo’.
Ilisemekana kuwa Sasha alileta zile za ‘nataka sitaki’ lakini baadaye alimsihi kwa nguvu zote watumie kinga ambapo mwanamuziki huyo alimwambia asijali hawezi kumpa mimba kuna mbinu ataitumia.
Chanzo hicho kiliendelea kushusha madai kuwa baada ya kumaliza mambo yao, Diamond alimchukulia Sasha usafiri wa Bajaj na kumpa shilingi elfu 80 na kumwambia kuwa wataendelea kuwasiliana.
Ilidaiwa kuwa mawasiliano yaliendelea ambapo mwezi mmoja na nusu baadaye, Sasha alianza kujisikia vibaya na walipopanga kukutana mara ya pili, mrembo huyo alimweleza jinsi anavyojisikia ambapo Diamond alinunua kipimo cha kupimia mimba na kukuta tayari Sasha alishanasa.
Ilielezwa kuwa baada ya kuona hivyo Diamond alimsihi Sasha asitoe ujauzito huo na kumwambia kuwa akifanya hivyo anaweza kufa na kama atajifungua yeye (Diamond) atamsomesha mrembo huyo na kumlea mtoto wao.
Mpashaji wetu aliendelea kusema kuwa baada ya kuachana hapo, waliendelea kuwasiliana japo siyo kama mwanzo na baadaye mawasiliano yalikatika kabisa huku Sasha akiwa tayari amefukuzwa shule. Mama yake Sasha alijaribu kumpigia simu Diamond lakini msanii huyo akawa anajibu kuwa atawasiliana naye baadaye, jambo ambalo hakuwa akilitimiza hadi alipojifungua mtoto wa kike katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar na kumpa jina la Rujeina.
SASHA AKIRI
Baada ya kupata madai hayo, mwandishi alimsaka Sasha ili kuthibitisha ambapo mwanzo alisita kuzungumza lakini baadaye akakiri kuzalishwa na mwanamuziki huyo na kudai kuwa kwa kuwa hamjali tena, naye aliacha kumfuatilia.
“Ni kweli nimezaa na Diamond. Mtoto ana miezi mitatu sasa. Unajua yeye ndiye alinikatisha masomo na kusema kuwa ataniendeleza na atamlea mtoto hivyo alivyokaa kimya sikuona tena sababu ya kumfuatilia kwa vile kwetu napata kila kitu,” alisema Sasha.
HUYU HAPA DIAMOND
Alipotafutwa Diamond kupitia simu ya kiganjani akiwa Nairobi, Kenya na kupewa nafasi ya kusema ukweli juu ya ishu hiyo, alieleza:
“Hahahaaa…mbona hiyo ishu ni kubwa sana kwangu! Ukweli huyo mwanamke simjui kabisa. Lete stori nyingine achana na hiyo.”
Katika kuonesha ‘usiriazi’, mwandishi aliendelea kumbana Diamond lakini bado alizidi kumkana Sasha.

Friday, 6 September 2013
DULLY SYKES "NAMFANANISHA DIAMOND NA MAREHEMU KANUMBA KWA UWEZO WA KUTHUBUTU"

Dully Sykes alikuwa akiongea na Bongo5 kwenye uzinduzi wa video ya video mpya ya Diamond uliofanyika wiki iliyopita kwenye ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
“Diamond ni namba moja kwasababu yupo tayari kujitoka kwa kila kitu,” alisema Dully. “Naweza kumfananisha Diamond na mtu kama Kanumba. Kanumba alikuwa ana uwezo wa hata kuchukua nauli yake ya kwenda sehemu kama Ghana kwenye tamasha la movie lakini ilimradi kujitengenezea status yake. Kwahiyo Diamond ni mtu ambaye tayari ameshajitolea kwaajili ya kuutetea muziki wetu.”
Pia Dully amesema mwishoni mwa mwaka huu anatarajia kuiongezea vifaa vipya studio yake ‘4.12’ ili kujiimarisha zaidi kwenye utayarishaji wa muziki ambao anasema kwa sasa anaufurahia zaidi kuliko hata kuimba.
Thursday, 5 September 2013
PRODUCER AKATA MZIZI WA FITINA KATI YA DIAMOND NA DYNA

Baada ya sakata la kuibiana nyimbo lilichokua takribani siku mbili kati ya msanii Diamond Platnum na Dayna Nyange,producer Shedy ameamua kukata mzizi wa fitina kwa kuuanika ukweli wa mambo....
Akiongea na #Team tizniz,Shedy amefunguka kama ifuatavyo:
“Beat hii nilitengeneza mimi kwa idea zangu mwenyewe. Alikuja Dayna akaupenda ule mdundo na mimi sikumnyima , akafanya demo lakini hakulipia kitu.
"Sasa ikapita zaidi ya miezi sita kila nikimuliza vipi anasema bado atakuja kufanya.Kuna siku Diamond akaja studio ,akataka kusikia midumdo niliyonayo.
"Bila hiyana, nilimchezea midundo mbalimbali kama mteja, ila jamaa akavutiwa sana na ule mdundo ambao Dayna aliufanyia demo.
"Baada ya Diamond kuupenda mdundo huo, niliamua kumpigia simu Dayna na kumuelezea kwamba Diamond kapenda kufanya kazi katika ile beat,Dayna akakubali kabisa,
"Sasa nashangaa yeye kusema diamond kamuibia wakati alikubali yeye mwenyewe."
WOLPER AVUNJA GLASI YA DIAMOND
STAA wa Bongo Movie, Jacqueline Wolper juzikati alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuvunja glasi ya Rais wa Wasafi, Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Tukio hilo lilijiri Agosti 28, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Hoteli ya Serena, Posta jijini Dar ambapo staa huyo alikuwa kwenye uzinduzi wa video ya Diamond.
Ilikuwa wakati Diamond akisalimiana na mastaa mbalimbali, alipofika kwa Wolper aliigusa kidogo, ikaanguka.
Paparazi wetu alipomuuliza Wolper sababu ya glasi hiyo kuvunjika, alijibu: “Hata mimi sijui nini kimetokea, tulikuwa tunasalimiana ghafla tu glasi yake ikadondoka na kupasuka, sijui ni miujiza au nini loh!”
Diamond naye akatia neno: “Nimeshtukia glasi ipo chini tu, daah! Sina hata cha kueleza juu ya hili.”
-GPL
Wednesday, 4 September 2013
PENNY: DIAMOND SUKARI YA WAREMBO
Penny Mwingila ‘Penny’ akipozi na Diamond
Mpenzi wa mkali katika tasnia ya Bongofleva, Penny Mwingila ‘Penny’ amekiri kuwa mpenzi wake huyo ni sukari ya warembo, hivyo hana wasiwasi naye.
Akiongea katika ukumbi wa Kivukoni uliopo ndani ya Hoteli ya Serena muda mara baada ya kumalizika kuoneshwa kwa video mpya ya Diamond inayokwenda kwa jina la My number One, Penny alisema:
“Sishtuki na chochote katika video ile ya Baby wangu kwani natambua kuwa mpenzi wangu ni sukari ya warembo, ila namshauri atafute madansa wa kike wa hapa nchini afanye nao kazi kama wale Wasouth wanavyoonekana katika video yake mpya,” alisema Penny.
Video hiyo ya Diamond imerekodiwa Afrika Kusini ambapo kwa mujibu wake wa Diamond ametumia shilingi milioni 48 kuandaa kazi hiyo.

Tuesday, 3 September 2013
DIAMOND AMPIGA KIJEMBE WEMA KWENYE WIMBO WAKE MPYA WA MY NUMBER ONE!
Baada ya kuisikiliza kwa makini nyimbo hii yenye mahadhi flani ya kiafrika zaidi tulifika kwenye dakika ya 2 na sekunde 50 (2:50) ya nyimbo hii na ndipo ukatokea “ubishi” ambao tukaona sio mbaya tukiupeleka kwa wasomaji wetu ili kupata maoni Zaidi.
Katika sehemu hii ya mwisho ya nyimbo hii Diamond anatamka maneno ambayo baadhi ya watu tuliokuwepo katika mabishano hayo tunasema kuwa yanamlenga mwanadada wetu muigizaji, Wema sepetu kama “vijembe” kwake, diamond anamalizia wimbo wake kwa kusema “TUACHE TULALE” maneno ambayo kwa wale wanafuatilia habari za watu hawa wawili yalioongewa na mpenzi wa diamond wa sasa VJ penny kwenye tukio la wapenzi hao kumrekodi mwanadada Wema Sepetu kwenye simu alipokuwa akimbembeleza mpenzi wake wa zamani (Diamond Platnumz) warudiane, tukio liliotokea miezi kadhaa iliyopita.
Swali likawa, Je maneno haya yatakuwa yanamlenga Wema??? Kama siyo kwanini Diamond ayatamke sehemu ambayo hata haihusiani nayo kwenye wimbo???
Subscribe to:
Posts (Atom)