KWA MAISHA HAYA YA ANASA YA MASTAA KWANINI WASIUZE UNGA.. 
  Ukifuatilia ratiba za  maisha ya anasa ya kila siku ya mastaa wa Kibongo, lazima utajiuliza kwa  nini wasiuze au kusafirisha madawa ya kulevya ‘unga’? 
Uchunguzi uliopewa sapoti  na baadhi ya mastaa hao, ulibaini kwamba suala la kupenda kujirusha  kuliko kazi ndiyo chanzo cha kufanywa ‘punda’ wa kusafirisha unga na  matokeo yake kunaswa na kuingia kwenye matatizo makubwa.
Uchunguzi huo ulibaini kuwa kuna baadhi  ya mastaa hao, ratiba zao za kujirusha na kula bata ndefu zimewabana  kiasi cha kushindwa kuendeleza vipaji vyao katika sanaa.
Ratiba za baadhi ya mastaa hao za kujirusha ni kama ifuatavyo;
JUMATANO
Ilibainika kuwa Jumatano, baadhi ya  mastaa hao hupenda kwenda kujirusha kwenye kumbi za starehe hasa katika  Klabu ya Bilicanas, Posta ambako mara nyingi kunakuwa na bendi  inayomwaga burudani huku wakishushia na pombe.
Ilibainika kuwa mastaa hao huondoka  kwenye kumbi hizo za starehe karibia kunakucha (majogoo) huku wakiwa  ‘tilalila’ na kwenda kulala.
 
 
ALHAMISI
Data zilizopatika kwa kumsoma msanii  mmoja baada ya mwingine zilibaini kwamba, kwa kuwa huchelewa kulala  Jumatano huku wakiwa na uchovu, Alhamisi huamka saa 10:00 jioni kisha  kuchati kidogo na marafiki kabla ya usiku kwenda kujirusha hasa New  Maisha Club kunakokuwa na burudani ya bendi.
Ilibainika kwamba wakiwa humo hujiachia kwa ‘masebene’ na kugonga pombe kama ilivyokuwa jana yake hadi majogoo.
IJUMAA
Uchunguzi ulibaini kuwa siku ya Ijumaa,  baadhi ya mastaa hao huamka tena saa 10:00 jioni na kinachoonekana ni  kati ya siku ‘bize’ kwa mambo ya starehe hivyo wanakuwa na mialiko  mingi.
Ilibainika kuwa baadhi yao huhudhuria  mialiko ya sherehe za harusi, send-off, kitchen party, birthday na  nyinginezo kabla ya baadaye kumalizia kwa kwenda kwenye ‘live’ bendi.
Mara nyingi hupenda kuhudhuria kwenye  shoo kama hizo katika Kumbi za Thai Village, Masaki, Nyumbani Lounge,  Ada Estate, Kinondoni au Club 24, Mikocheni ambako huko nako hukesha  hadi majogoo.
JUMAMOSI
Uchunguzi wetu ulibaini kwamba Jumamosi,  baadhi ya mastaa hao huamka saa 10:00 jioni kama kawa kisha kunyoosha  miguu hadi baa ambapo giza likiingia huzama tena kwenye burudani ya  bendi.
Wengi hupatikana katika kumbi  zinazoungurumisha muziki wa bendi za dansi. Huko nako huwa wanakula bata  ndefu hadi majogoo kisha kurejea nyumbani kulala.
JUMAPILI
Kama kawaida, baadhi ya mastaa hao  huamka saa 10:00 jioni kisha kwenda kujipumzisha ufukweni hasa Coco na  kuendelea kujirusha. Usiku mnene ‘hujimuvuzisha’ kwenye klabu za starehe  ambapo ama msanii wa Bongo Fleva anazindua wimbo au kunakuwa na shoo ya  kawaida ya muziki.
Kumbi za starehe zinazokuwa ‘bize’ na  mastaa huku kukiwa na shoo usiku wa Jumapili ni pamoja na Bilicanas na  New Maisha Club ambako huko nako huondoka majogoo kwenda kulala.
JUMATATU
Ilifahamika kuwa siku ya Jumatatu baadhi  ya mastaa hao huamka saa 7:00 mchana kisha kwenda saluni na baadaye  kufanya ‘window shopping’ katika maduka ya nguo, supermarket na sehemu  nyingine.
Baada ya hapo muda wa jioni, baadhi ya  mastaa hao hupendelea kwenda kuogelea (swimming) kisha kuibuka Coco  Beach kupata mihogo ya kuchoma, mishikaki, ‘shisha’, pombe na starehe  nyingine za kiutu uzima.
JUMANNE
Mara nyingi uchunguzi wetu ulibaini kuwa  siku ya Jumanne hutumiwa na wasanii hao kupumzika kutokana na uchovu wa  wiki nzima kabla ya ratiba kujirudiana tena kuanzia Jumatano.
WENYEWE WANASEMAJE?
BABY MADAHA
“Mimi naweza kujiachia kila siku lakini  mara nyingi natoka siku tano na ratiba zinaendelea kama kawa maana huwa  nalala mchana na nikitoka narudi saa 9:00 usiku.”
MIRIAM JOLWA ‘JINI KABULA’
“Siku hizi natoka mara mojamoja siyo kama zamani lakini nikiwa na kampani huwa narudi kulala saa 10:00 usiku.”
TAMRINA POSHI ‘AMANDA’
“Mimi huwa natoka kwenye ishu maalum tu.”
JACQUELINE PATRIC
“Naweza nisitoke wiki nzima lakini nikijisikia pia naweza kutoka wiki nzima na mambo mengine yanaendelea.”
WATOTO WA MBWA (TIKO, MARY & THEKLA)
“Siku hizi huwa tunatoka siku maalum, siyo kama zamani.”
YOBNESH YUSUF ‘BATULI’
“Inategemea, kama nimealikwa sehemu narudi saa 10:00 usiku au asubuhi maana kazi zetu siyo za kila siku.”
LULU MATHIAS  ‘AUNTY LULU’
“Huwa natoka siku ya Ijumaa narudi saa 8:00 usiku naamka 4:00 asubuhi. Pia natoka Jumapili kwa sababu Jumatatu nakuwa off.” 
KWA NINI WASIUZE UNGA?
Uchambuzi wa kina ulibaini kuwa mbali na  starehe hizo, pia kuna masuala ya mapenzi ambayo nayo huwa ni gharama  na pia hutumia muda wao mwingi.
Ilibumburuka kuwa kwa staili hiyo ya  maisha ya anasa huku baadhi wakisahau kwenda studio kurekodi na mazoezi  ya shoo (kwa wanamuziki) na kutoonekana lokesheni wakishuti filamu.
Ilifahamika kwamba kwa ratiba hizo,  anapotokea kigogo (mfanyabiashara wa madawa ya kulevya) na ‘kumsomesha’  msanii kuwa kuna dili la unga lazima akubali kuwa punda ili apate fedha  za harakaharaka za kutanulia asiachwe na watoto wa mjini.
Listi inazidi kuongezeka kila kukicha ya  mastaa mbalimbali ambao wanadaiwa kunaswa na unga wakiwemo Agness  Gelard ‘Masogange’ na shosti yake, Mellisa Edward, Sandra Khan ‘Binti  Kiziwi’, Saadah Ally, Aisha Bui, Mkwanda na Mbwana Matumla, Joseph  Kaniki na wengineo.
 
 
 
          
      
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment