HATIMAYE Halmashauri ya Manispaa ya Iringa imeivunja nyumba iliyokuwa ikijengwa katikati ya makaburi ya Mtwivila ambayo iliripotiwa na mtandao huu na vyombo mbali mbali vya habari likiwemo gazeti la Jamboleo , radio Ebony Fm na radio Cloud FM pamoja na nyumba nyingine mbili ambazo pia zilikuwa zikianzwa kujengwa eneo hilo .
Pamoja na kuendesha zoezi la kuzivunjwa nyumba hizo ambazo zilikuwa katika hatua ya mwanzo kabisa pia Halmashauri hiyo imetoa muda wa siku 30 kuanzia leo kwa mmiliki wa nyumba nyingine iliyokutwa imekamilika ambayo pia imejengwa karibu na makaburi ya Mtwivila eneo ambalo waziri Mkuu Mizengo Pinda alikaa wakati wa mazishi ya aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli marehemu Iddi Chonanga
Hatua ya kuvunjwa kwa makaburi hayo imekuja ikiwa ni siku mbili zimepita baada ya mtandao huu wa matukio daima kuibua suala hilo kuibua ujenzi huo holela na ni siku moja baada ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Manispaa Bi Terresia Mahongo kutoa agizo kwa maofisa mipango miji , afisa ardhi na mwanasheria wa Manispaa ya Iringa kufika eneo hilo ili kuchukua hatua sitahiki.
Zoezi la kuvunja nyumba hizo leo majira ya saa 3 asubuhi limeongozwa na maofisa mbali mbali wa Manispaa ya Iringa akiwemo mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bw Innocent Kihaga pamoja na mgambo zaidi ya watano wa Halmashauri hiyo.
Mgambo wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na viongozi mbali mbali wakielekea kuvunja nyumba zilizojengwa makaburi ya Mtwivila leo
Mgambo wa Manispaa ya Iringa na mwanasheria katikati Bw Innocent Kihaga wakielekea kuvunja nyumba zilizojengwa makaburini Mtwivila
Mgambo wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wakivunja nyumba iliyojengwa katikati ya makaburi ya Mtwivila
Kaburi hili la Rashid M. Lukuvi likiwa jirani kabisa na ukuta wa nyumba hiyo iliyovunjwa
Uvunjaji wa nyumba wa nyumba ukiendelea huku mmiliki wake amepewa siku 30 kuanzia leo kuivunja
Wananchi ambao wamezika ndugu zao katika makaburi hayo wakishuhudia zoezi hilo
Hii ndio nyumba ambayo ipo jirani na kaburi la marehemu Idd Chonanga aliyekuwa diwani wa kata ya Nduli kaburi lenye mashada kushoto ,na hapo waliposimama mgambo ndipo alipokaa waziri mkuu Mizengo Pinda wakati wa mazishi na viongozi mbali mbali wa mkoa wa Iringa
No comments:
Post a Comment