Sunday, 25 August 2013

DR SLAA ATIKISA KIGAMBONI NA KUACHA MACHOZI YA FURAHA

Mkutano wa Maoni ya Katiba mpya ulianzaa mida ya Saa nne asubuhi katika uwanja wa mpira mjimwema stendi,
Watu wamepata fursa ya kuchangia maoni ya Katiba na kuuliza maswali ama ufafanuzi,

Vile vile Dr amewaeleza makutano kile chadema tunachotaka kiwemo kwenye katiba,

Maoni ya wananchi:

1) Wamependekeza suala la Ardhi litolewe mikononi mwa rais na liundiwe chombo maalumu kitakachoundwa na bunge,

2) Matibabu liwe ni haki ya kila mtanzania,

3) Madaraka ya Rais yapunguzwe,

4) Suala la elimu liwe ni haki ya kira raia na iwe elimu bora na ya BURE kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu,

Mkutano umemalizika salama saa sita mchana, na Helkopta ya Mh Dr Slaa ndio imepaa mida hii kuelekea Segerea,

Watu walihudhuria wengi sana,

Kivutio cha huzuni ya furaha nipale alipomaliza kuhutubia nakuanza kutoka ambapo kila mmoja alitaka angalau tu kumgusa mkono, lakini wakashindwa kumfikia na kuanza kububujikwa na machozi ya furaha,

Wanakigamboni tunawashukuru sana kwakuhuduria kwenu,

Pipoooooooooz Pawaaaaaaaaa!

No comments:

Post a Comment