WAKALA wa staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, Jorge Mendes  amedai kwamba mchezaji wake ni staa aliyekamilika zaidi kuliko nyota wa  Barcelona, Lionel Messi.
                               Ronaldo, 28, amesaini mkataba mpya wa miaka mitano  ambao unamfanya awe mwanasoka anayelipwa zaidi duniani huku Mendes  akiamini kuwa staa huyo anastahili kwa sababu amekamilika kuliko Messi  licha ya ukweli kwamba Barcelona ndiyo timu bora zaidi ulimwenguni kwa  sasa.
                               “Cristiano Ronaldo ni mchezaji aliyekamilika zaidi  kuliko Messi. Licha ya heshima kubwa niliyonayo kwa Neymar, lakini  hakuna ubishi kwamba hakaribii uzuri wa Ronaldo,” alisema wakala huyo  ambaye pia anawasimamia Jose Mourinho na Radmel Falcao pamoja na kundi  kubwa la wachezaji wa Kireno na Kibrazili


 
No comments:
Post a Comment