Tuesday, 17 September 2013

CHEGE NA TEMBA KUANZA ZIARA YA MIEZI 3 ULAYA WIKI IJAYO..

Wasanii wa Kundi la TMK Wanaume Family Chege na Temba wanatarajia kuanza ziara ya miezi 3 barani Ulaya kuanzia wiki ijayo.Akizungumza na mwandishi wetu, meneja wa kundi hilo Said Fella amesema leo ndio wanategemea kupata Visa na wiki ijayo (September 25) Chege na Temba wataondoka nchini wakielekea nchini Sweeden ambako watafanya show ya kwanza (October 5).

Temba na Chege watashiriki show za Serengeti Fiesta Musoma siku ya Ijumaa hii na kumalizia Shinyanga siku ya Jumapili zikiwa ndio show zao za mwisho za Fiesta kabla ya kuondoka nchini .

Msanii mwingine wa Bongo Ommy Dimpoz aliondoka nchini Jana kuelekea Marekani ambako atakuwa na show kadhaa kabla hajarejea nchini kushiriki fainali ya Serengeti Fiesta Dar es salaam, huku Diamond Platnumz naye anatajaria kwenda nchini Malaysia wiki ijayo ambako atafanya show (September 20


No comments:

Post a Comment