Saturday, 31 August 2013

IGP SAID MWEMA AWABADILI MAKAMANDA MTWARA NA VIWANJA VYA NDEGE

                            


                         Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Mikoa na Vikosi.

Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara  Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Linus Sinzumwa ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Idara ya Upelelezi  na nafasi yake inachukuliwa na Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Zelothe Stephen  kutoka Makao Makuu ya Polisi.

Aidha, aliyekuwa Kamanda wa Polisi  Viwanda vya ndege Kamishina Msaidizi (ACP) Deusdedit  Kato amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi  na nafasi hiyo inachukuliwa na Kamishina  Msaidizi wa Polisi (ACP) Selemani Hamisi kutoka Makao Makuu Idara ya Upelelezi.

Wengine ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Hamad Hamad anayeenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Viwanja vya ndege ambapo hapo awali nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na David Mwafwimbo aliyehamishiwa mkoani Lindi kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Lindi (OCD).

Uhamisho huo ni wa kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.

Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

SUMU YA NYUKI INAANGAMIZA VIRUSI VYA UKIMWI KABISA




 Wanasayansi kutoka chuo kikuu cha tiba Washington, Marekani  wamegundua katika utafiti wao kuwa sumu iliyopo katika mwili wa nyuki iitwayo toxin melittin inaweza kuvivunjavunja na kuviharibu virusi vya Ukimwi pasipo kuacha madhara katika chembehai za mwili.
Habari hii imeelezwa katika taarifa ya tiba za dawa za kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi iliyotolewa mapema mwaka huu.
Watafiti hawa wanaeleza kuwa matokeo ya utafiti huu kufika katika hatua kubwa inayoleta matumaini ya kupamba na VVU  kwa kuweza kupata dawa ya kupaka ya majimaji ndani ya uke itakayotumika kupambana na maambukizi ya VVU.
Dk Joshua Hood anasema: “Matumaini yetu ni kwa maeneo ambayo hali ya maambukizi yapo juu na vigumu kuzuilika, dawa ya majimaji mazito inaweza kutumika kupaka ndani ya uke katika kuzuia maambukizi ya mwanzoni kabisa.”
Sumu ya nyuki, melittin, imeonyesha uwezo wa kupambana na VVU kwa kuvunja ganda linalomzunguka kirusi na virusi wengine kwa kulitoboa na kuacha matundu.
Mwandishi mwandamizi wa makala za biokemia,  Dk Samuel Wicline, Profesa wa Biochemia wa Taasisi ya Russel Hornsby anafafanua kuwa kuwa vijipande vidogo vilivyoshindiliwa vya sumu ya nyuki vimeonyesha kuwa na tabia ya kuweza kuua chembe hai zenye saratani.
Anaeleza mtaalamu huyo kuwa hii si mara ya kwanza katika ugunduzi wa tiba ya namna hii, kwani mwaka 2004 wanasayansi wa Croatia walitoa taarifa yao katika jarida la sayansi ya chakula na kilimo kuwa mazao ya nyuki, ikiwamo asali na sumu ya nyuki  vina uwezo wa kutumika kutibu na kuzuia saratani.
Chembehai za mwilini zenye afya huendelea kubaki salama pasipo kupata madhara wakati wa tiba kwani sumu hiyo ya nyuki imetengenezewa na kitu kama ngao ambayo ikikutana na seli za mwili hudunda na kwenda mbali bila kujishikiza.
Hii ni kwa sababu ya seli za mwili ni kubwa kimaumbille kuliko sumu ya melittin, wakati kwa  virusi vya Ukimwi ni vidogo kuliko melittin, hivyo ikikutana navyo ngao hiyo haiwezi kuzuia kirusi kidunde kwani ni kidogo, hivyo  kirusi hudakwa na melittin na kushikamana, hivyo kirusi huweza kuharibiwa.
Dk Hood anaeleza kuwa vijipande vilivyoshibishwa na sumu ya melittin huweza kushikamana na kirusi na kutoboa tundu katika ganda la kirusi na kuchana ganda lote, hivyo kirusi huweza kuvunjwa.
Wakati tiba kwa kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU, yaani ARVs zinafanya kazi kwa kuzuia uwezo wa virusi kujidurufisha, kwa tiba ya melittin hushambulia sehemu muhimu ya kimaumbile ya  virusi ambayo ndiyo nguzo imara kwa virusi.
Source:Mwananchi.

CHEKA AMTWANGA MMAREKANI NA KUCHUKUA UBIGWA WA DUNIA


Bondia Francis Cheka wa Tanzania (kulia) akimuadhibu mpinzani wake Mmarekani, Phill Williams, wakaati wa pambano lao la raundi 12 la kuwania Ubingwa wa Dunia uzito wa Super Middle (WBF) lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu. Katika pambano hilo Bondi Mtanzania Francis Cheka ameweza kumgalagaza kwa Pointi mpinzani wake na kutwaa ubingwa huo.

MSICHANA AKUTWA AMEJINYONGA NJE YA UKUMBI WA DISCO

KULWA Shaban (18) mkazi wa Gongo la Mboto, jijini Dar amedaiwa kujinyonga na mwili wake kukutwa  ukinin’ginia kwenye mti pembezoni mwa ukumbi wa disko maarufu kwa jina la Majita.
Akizungumza kwa machungu, mama wa kijana huyo, Rehema Omar alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo siku nne kabla ya kukutwa akiwa amejinyonga, Kulwa aligombana na baadhi ya marafiki zake ambao walichukua tofali na kumpiga nalo mdomoni na kusababisha meno mawili  kung’oka.
Tulimpa fedha kwa ajili ya kwenda kujitibia kisha alirejea nyumbani na kuendelea kujiuguza majeraha kwani yalikuwa ni makubwa,” alisema Rehema.
Mama huyo aliendelea kusema wakati mwanaye akiendelea kuuguza kidonda ndipo alipopatwa na maswahibu hayo baada ya kwenda disko na wenzake.
Siku hiyo niliingia kulala na ilipofika saa tisa usiku niligongewa mlango na watu wawili na kuambiwa hali ya mtoto wangu ni mbaya  pasipo kubainisha amefanya nini,” alisema mama huyo.
Chanzo kingine kilipenyeza madai kuwa, siku ya tukio Kulwa alikutwa amejinyonga mwenyewe baada ya kutoka disko lakini mama yake mzazi hakukubaliana na madai hayo.
Nimeumia sana kwani mwanangu hawezi kujinyonga kwa sababu hakuwa na tatizo lolote ukizingatia nguo aliyokuwa ameivaa tuliikuta imechanwachanwa, mwanangu amekufa kifo kibaya sana,” alisema mama huyo huku akidondosha machozi.
Marehemu Kulwa alizaliwa na pacha wake, Doto ambaye walikuwa wakitembea naye mara kwa mara isipokuwa siku hiyo ambayo mwenzake alikutwa na umauti.


CHALZ BABA AIFUNGUKIA NDOA YAKE!

         SIKU chache baada ya kuvuta jiko, Prezidaa wa Mashuja Band, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ amesema anafurahia maisha ya ndoa na kamwe kazi haiwezi kumtenganisha na mkewe.
 Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Chaz Baba alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa mkewe, Rehema Sospeter ni muelewa hivyo atakapokuwa mzigoni usiku, hawezi kuwa na hofu.
“Mimi na mke wangu tumedumu kwenye uchumba kwa takriban miaka minne hivyo ananijua kiundani na mimi namjua pia, hatuwezi kutofautiana,” alisema Chaz. Mkali huyo alitarajiwa kurudi jukwaani Ijumaa hii (jana) baada ya kumalizika kwa fungate lake

LIVERPOOL IMEFIKIA MAKUBALIANO YA KUMSAJILI BEKI WA PSG MAMADOU SAKHO


Liverpool have reached an agreement with Paris Saint-Germain to sign centre-back Mamadou Sakho.

The Reds will pay the Ligue 1 champions a €17 million fee for the 23-year-old defender as Brendan Rodgers looks to improve his defensive options for the 2013-14 campaign.Sakho has played over 150 league games for PSG, with the Frenchman having been capped 14 times by his country, and he will compete with Daniel Agger and Kolo Toure for a place in Rodgers's starting XI.Liverpool are also close to agreeing a deal for Sporting Lisbon youngster Tiago Ilori, with the Reds having tabled a €7m offer plus performance related bonuses to sign the 20-year-old.


Rodgers has felt the need to dip into the market for defensive reinforcements with the future of Martin Skrtel remaining up in the air, with Napoli strongly linked with a move for the Slovakia international.

The Anfield manager's options have been further limited with Sebastian Coates sidelined with a long-term knee injury, while Andre Wisdom's patchy pre-season performances have done little to convince Rodgers that he is ready for a regular first-team berth.

There is better news regarding Kolo Toure's fitness, however, with Rodgers revealing on Friday that the Ivorian could recover from a groin problem in time to face Manchester United on Sunday

SOURCE:GOAL.COM

PICHA: SAMAKI WA AJABU KAPATIKANA KAFA KANDO YA BAHARI NCHINI NIGERIA

whale alpha beach lagos nigeria