Showing posts with label Madee. Show all posts
Showing posts with label Madee. Show all posts

Tuesday, 17 September 2013

MADEE ATUMIA MILIONI 128 KUJENGA NYUMBA YAKE MSIKILIZE ANACHOSEMA NA CHEKI PICHA YA MJENGO WAKE

Msanii kutoka kundi la Tip Top Connection Madee amesema kuwa nyumba yake aliyojenga maeneo ya Mbezi ya Morogogo Road mpaka sasa imemgharimu karibia milioni 125 na bado nyumba hiyo haijakamilika kama anavyotaka yeye.
Madee alisema kuwa alianza kujenga nyumba hiyo kama miaka 4 iliyopita na amesema kuwa ni pesa anazopata kwenye muziki peke yake tangua aanze kama miaka 14 iliyopita. Mungu akipenda amepanga kuhamia siku ya b'day yake mwakani tarehe 23 April.
 MSIKILIZE hapo chini zaidi; 

Thursday, 29 August 2013

SHILOLE: MADEE AU OMMY DIMPOZ?... KILA MMOJA ANASWA NAE CHOBINGO

STAA wa Muziki wa Mduara, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, amewashangaza wasanii wenzake baada ya kunaswa chobingo kwa nyakati tofauti akiwa na wasanii wenzake, Hamad Ally ‘Madee’ na Omari Faraj ‘Ommy Dimpoz’. 
 Shilole akiwa na Madee.

Mpango mzima ‘uli-happen’ Agosti 25, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Singida Montel wakati wasanii hao walipokuwa katika shoo ya Serengeti Fiesta 2013 ‘Noma Sana’
Kwanza paparazi wetu alimfotoa Shilole picha kadhaa akiwa anafungwa zipu na Madee.



                                   ...Akiwa na Ommy Dimpoz.
 
Muda mchache baadaye, paparazi wetu alimfuma tena Shilole akiwa amekumbatiana na Ommy Dimpoz kwenye gari huku wakiwa wameangusha usingizi mzito hali iliyozua minong’ono ingawaje wawili hao walidai ni shangwe tu za Fiesta na hakuna uhusiano wa kimalovee kati yao.
                                     Katika pozi na Madee.

Sunday, 25 August 2013

"POMBE YANGU"YAMUINGIZIA MADEE ZAIDI YA MILIONI 130

Hit maker wa Sio Mimi aka Pombe yangu, Madee amesema hadi sasa ameshaingiza zaidi ya shilingi milioni 130 kutokana na show mbalimbali alizopata hivi karibuni tangu aachie wimbo wake  huo.

Madee amesema pamoja na show za kawaida, makampuni ya simu yameshamsainisha show zaidi ya 12 ambazo zimekuwa zikimpa mkwanja wa nguvu.

Akiongea na mwandishi wetu, Madee  amesema pia muziki wake umetoa fursa kwa vijana wa Tip Top Connection ambao amekuwa akifanya nao kazi katika show mbalimbali.

“Nimekua nikiingiza Milioni 2 hadi 3 kwa wiki kutokana na Pombe Yangu. Ni tofauti na awali wakati tunaanza muziki kwa sasa ukifanya wimbo ukawa mkali basi ujue pesa zipo zinakusubiri. Pamoja na hayo wimbo ya Pombe Yangu umetoa fursa kwa vijana ambao nakuwanao kwenye show zang. Filamu ya “Pombe Yangu” pia imeajiri vijana,watu wametengeneza T-Shirt ‘Nani kamwaga Pombe Yangu’. Hiyo ni fursa wameitumia kupitia Pombe Yangu, alisema Madee.