Showing posts with label Ommy Dimpoz. Show all posts
Showing posts with label Ommy Dimpoz. Show all posts

Thursday, 19 September 2013

OMMY DIMPOZ AMTAJA MCHUMBA WAKE NA NAMNA ANAVYOPENDA KUWA NA WATOTO WA KIKE

Kwenye mahojiano zaidi ya ‘Sema Yote’ aka Tell it All exclusive kwa Bongo5, Ommy Dimpoz amemzungumzia mchumba wake na jinsi ambavyo anapenda kuwa na watoto wa kike kuliko wa kiume.
0bd2f5c0206b11e389a722000a9e28d6_7
“Nina mchumba, watu wengi hawajui kuhusu mahusiano yangu lakini nina mchumba na natarajia Mungu akijalia ntakuja kumuoa. Yupo nje bado anasoma. Akimaliza shule ntamuoa,” alifunguka Ommy ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani kwenye ziara ya wiki tatu.
Swali ni Je! Mchumba huyo ni nani? Leo kupitia Instagram, ameshare picha ya msichana mrembo aitwaye Emmy na kusababisha maswali mengi kama ndiye yeye au lah.
c51d2bb2207611e39a2a22000a1fb02b_7
Emmy

“My Biggest fan in Swiss Emmy Mwarabu,” aliandika.
Katika hatua nyingine Ommy Dimpoz alisema anapenda kuja kuwa na familia ya watoto wasiozidi watatu na anapenda watoto wa kike zaidi.
“Lakini mimi napenda watoto wa kike zaidi. Basi tu automatically nimekuwa hivyo. Pengine ni kwasababu nimelelewa sana na mama yangu.”
Hata hivyo alisema hatopenda kuona wanae wanakuwa wanamuziki kama yeye.
“Kwa maisha ya muziki ninavyoyaona na jinsi ilivyo hii kazi nisingependa mwanangu afanye,” alisema.
Msikilize zaidi hapa.
-bongo5

Wednesday, 18 September 2013

PICHA ZA OMMY DIMPOZ ALIVYOWASILI MAREKANI..

 
             Hizi ni picha za Faraji Nyembo aka Ommy Dimpoz baada ya kuwasili Marekani jana na kupokelewa na wenyeji wake.Ommy Dimpoz anatarajiwa kufanya show ya kwanza Jumamosi ya wiki hii Washington DC, itakayofuatiwa na show ya pili Houston September 28 na show ya tatu Los Angeles October 5 kisha atarejea Tanzania kwaajili ya
fainali ya Serengeti Fiesta.

Thursday, 12 September 2013

OMMY DIMPOZ AELEZEA UTAJIRI WAKE

 
Ommy Dimpoz
Kwa maneno yao wenyewe, sauti zao wenyewe bila kulazimishwa na mtu, wasanii wataeleza siri zao, siri nzuri lakini ambazo hujawahi kuziskia sehemu yoyote, kuanzia mafanikio yao na mali zao, namna walivyofall in love, siri zao za utotoni, ndoto zao na siri zingine kibao.
Angalizo lakini, Sema Yote si kitu cha kila siku, ni kitu cha msimu na hakina muda maalum.
Leo tumemkamata Omar Nyembo aka Ommy Dimpoz ambaye kwa mara ya kwanza anatoa siri nzito, usishtuke sana, siri nzito kuhusu sehemu ya mali alizojikusanyia hadi sasa.
Msikilize hapa chini part 1

Wednesday, 11 September 2013

RAY C NA OMMY DIMPOZ KUNANI ?

               Staa wa Ngoma ya Tupogo,Omary Nyembo,‘Ommy Dimpoz’na nguli wa muziki wa Bongo Fleva,Rehema Chalamila‘Ray C’wanatarajia kuachia ngoma yao? baada ya kupiga picha pamoja.
Ommy Dimpoz alipost picha hicha hiyo kupitia mtandao wa instagram huku akiandika Studio Flowwww wit the Legendary her self ...Kiuno bila Mfupa...Huku mashabiki wao wakisema kuwa… haya madimpoziii poz na kiuno bila kidari..

Thursday, 29 August 2013

SHILOLE: MADEE AU OMMY DIMPOZ?... KILA MMOJA ANASWA NAE CHOBINGO

STAA wa Muziki wa Mduara, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, amewashangaza wasanii wenzake baada ya kunaswa chobingo kwa nyakati tofauti akiwa na wasanii wenzake, Hamad Ally ‘Madee’ na Omari Faraj ‘Ommy Dimpoz’. 
 Shilole akiwa na Madee.

Mpango mzima ‘uli-happen’ Agosti 25, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Singida Montel wakati wasanii hao walipokuwa katika shoo ya Serengeti Fiesta 2013 ‘Noma Sana’
Kwanza paparazi wetu alimfotoa Shilole picha kadhaa akiwa anafungwa zipu na Madee.



                                   ...Akiwa na Ommy Dimpoz.
 
Muda mchache baadaye, paparazi wetu alimfuma tena Shilole akiwa amekumbatiana na Ommy Dimpoz kwenye gari huku wakiwa wameangusha usingizi mzito hali iliyozua minong’ono ingawaje wawili hao walidai ni shangwe tu za Fiesta na hakuna uhusiano wa kimalovee kati yao.
                                     Katika pozi na Madee.