Showing posts with label RAY C. Show all posts
Showing posts with label RAY C. Show all posts

Thursday, 19 September 2013

NANI KAKWAMBIA KWENYE MAISHA HAKUNA MAGEPU?RAY C ATOKA KWENYE UTEJA HADI KUNUNUA MKOKO WA MAANA



                  STAA wa Bongo Fleva Rehema Chalamila‘Ray C’  ameamua kuianika  gari  yake  ambayo anatembelea kwa sasa ...

Gari  hilo  ni aina ya Jaguar ambalo namba zake za usajili hazionekani vizuri ila mwishoni zinasomeka T…CHL,huku akiandika kwenye instragram kuwa… Jaguar don't care...CHL means Chalamila Family..... 

Pongezi  za  kutosha  zikufikie  Ray C  popote  ulipo. Huo  ni  mwanzo  mzuri  baada  ya  mateso  ya  madawa  ya  kulevya  yaliyokufanya  uwe  teja

Friday, 13 September 2013

RAY C NA ZAMARADI MKETEMA WAINGIA NDANI BIFU KALI KISA MWANAUME

 
                So Rehema Chalamila aka Ray C na mtangazaji wa kipindi cha Take One cha Clouds TV, Zamaradi Mketema haziivi? Katika kile kilichoacha wazi midomo ya watu wengi, warembo hao leo wameingia kwenye vita vya maneno kwenye mtandao wa Instagram. Alianza Zamaradi aliyepost picha yenye maneno ya mafumbo: 
aae8fb521c4a11e3842d22000a1f9ada_7 Picha hiyo aliiandikia maneno haya:
Huwezi amini sikuchukii ila nimezidi kukudharau!!!! Katika watu wa mwisho kabisa ambao siwezi kupanic nao hata siku moja ni WEWE.. Dont waste your energy.. you have so much to accomplish ndugu.. mi hunipi tabu kabsa, kabsaa, kabisaaaaaaaaa yani sanasana unanichekesha tu na vituko visivyoisha.. lol!! Ila sikulaumu sana sio kosa lako maskini… 
 
ungekuwa una akili usingefanya hayo ya kitoto tena hasa KWA KIPINDI HIKI.. na huenda hiyo sio akili yako mwaya.. NIMEKUSAMEHE BURE maana hapo ulipo hujielewi bado.. 

Dramas Dramas Dramas… sizipendagi ila huwa zinanifata zenyewe.. lol!!! Mbona naandamwaga hivi jamani kwani kosa langu nini mimi mtoto wa watu… hahahahahaaaa majanga haya @wemasepetu anyways sorry to my good people jamani kwa mapost ya aina hii.. 
 
sometimes inabidi coz mwisho wa siku mi ni binaadamu tu wa kawaida.”
 
Wema naye aliongeza kwa kuchangia: Mbona majanga….. dont waste ur tym to fools maamy…. nawe utaonekana a fool… fanya yako… wanaokufatilia wanatamani wawe kama wewe… na si kingine its called ENVY.”
 
“Sina hata time nae mammy bado ana vichembechembe kwenye ubongo.. maana ghafla tu anaanza kuniparamia jamani.. lol!!! Kishafulia anatafuta kick kwa kugombana na watu.. mtu wa zamani,” aliongeza Zamaradi.
 
Japokuwa Zamaradi hakutaja wazi nani mlengwa wa ujumbe huo, ni Ray C mwenyewe ndiye aliyejibu kwenye maelezo ndani ya post yake kwenye mtandao huo akisema:
 
“Hihihi kazi kwelikweli mi naweza posts zangu watu wanajihisi au wanaumia. Tatizo skuliiiii shauri yako #uki skuli kdg wala matatizo hakuna ila km huja skuliii mweeeh unakua mbulula mama we hujui fanya yako achana na watu weusi,” aliandika Ray C.
 
Aliongeza tena, “Haswa anajiona kichwa kumbe mbulula haswaa Hana lolote,Watu wameanza shughuli hizo anazofanya wenzie tulishazifanya kitambooooooooo,tushauza sura sanaaaaaaaaaa zaid ya miaka. 12 namuangalia simmalizi maana haeleweki.”

Haukuishia hapo, Zamaradi aliongeza tena kwa kuweka post mpya.

886c292a1c5c11e383d722000a1f99fc_7
“Nashusha sana hadhi yangu kwakweli dealing with watu wenye hasira na maisha ya watu wengine… this is not ME kabisa. Una mengi ya kutukaniwa lkn mi ni binaadamu ninaejua baya na zuri.. maisha yashakushinda wewe sasa USIPANIC.. jipange. Ushafanywa yote ya dunia ntakuweza wapi mie mtu wa zamani,” aliandika Zamaradi kwenye picha hiyo.
 
Ray C alijibu kwa kupost video hii:

Wednesday, 11 September 2013

RAY C NA OMMY DIMPOZ KUNANI ?

               Staa wa Ngoma ya Tupogo,Omary Nyembo,‘Ommy Dimpoz’na nguli wa muziki wa Bongo Fleva,Rehema Chalamila‘Ray C’wanatarajia kuachia ngoma yao? baada ya kupiga picha pamoja.
Ommy Dimpoz alipost picha hicha hiyo kupitia mtandao wa instagram huku akiandika Studio Flowwww wit the Legendary her self ...Kiuno bila Mfupa...Huku mashabiki wao wakisema kuwa… haya madimpoziii poz na kiuno bila kidari..

RAY C ALIANIKA "SHAIRI LA PENZI LAKE"INSTAGRAM ALBUM YAKE MPYA IPO MBIONI KUTOKA



Haya wale wenye kiu na ujio mpya wa Ray C mnaweza kuanza kuandaa makoo yenu sababu chakula kimeshawekwa jikoni na muda si mrefu mnaweza kukaribishwa mezani.

Ray C ameshea picha kadhaa akiwa studio na wadau mbalimbali akiwemo Bab Tale na Said Fella, na kama haitoshi ameweka mashairi ya wimbo wake ambao unaonekana ndio aliokuwa akiurekodi wakati anapiga picha hiyo na kuandika “Mashairi ya my new song…,its a very beautiful song…am sooooooo happy..Thank you Lord”.
Ray C lyrics
Unaweza kuyapitia na kuanza kutengeneza taswira ya kile kinachokuja kutoka kwa Rehema Chalamila amabaye anasubiriwa kama nguo ya Christmas au Idd kwa watoto.

Pia Ray C amesema album yake inakuja hivi karibuni

Tuesday, 10 September 2013

"NAJUTA KUMJUA LORD EYEZ MAISHANI MWANGU"....RAY C

INAWEZEKANA umekuwa ukisikia vitu vingi kuhusu lejendari wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ lakini hukupata chansi ya kumsikia mwenyewe akifunguka mwanzo mwisho juu ya kisanga kilichompata alipojikuta kwenye janga la matumizi ya dawa za kulevya.

Ijumaa Wikienda limefanya naye mahojiano (exclusive interview) ambapo amekidhi kiu yako ya kujua chochote kinachomhusu. UNGANA NAYE…
KWA MTU ASIYEKUJUA, UMETOKEA WAPI?
“Nimezaliwa Mei 15, 1982 mkoani Iringa. Kabla ya kuingia kwenye muziki nilifanya kazi ya utangazaji. Watu wengi walinijua wakati nikiwa Radio Clouds FM. Albamu yangu ya kwanza ni Mapenzi Yangu niliyoitoa mwaka 2003. Kilichofuata ni kujipatia mashabiki wengi sana ndani na nje ya nchi. Baadaye niliachia Albamu ya pili ya Na Wewe Milele ya mwaka 2004. Nilipata mialiko mingi nje ya nchi zote Afrika Mashariki, China, Uingereza na kwingineko. Kilichofuata ni singo kibao na tuzo hadi nilipopata matatizo mwaka jana. Unazikumbuka Mama Ntilie, Mahaba ya Dhati, Touch Me, Na Wewe Milele, Wanifuatia Nini na Nihurumie? Huyo ndiye Ray C mwenyewe.



MARA YA MWISHO KUONEKANA STEJINI NI LINI?
“Mara ya mwisho kufanya shoo au kuonekana stejini ni Julai, mwaka jana. (anawaza kidogo) Nakumbuka ilikuwa Nairobi Carnival nchini Kenya. Ilikuwa shoo ya kampuni moja ya simu. Nilifanya vizuri sana aisee. It was wonderful.

UTARUDI LINI STEJINI?
(Akiwa Studio za THT na Prodyuza Tudd Thomas na Imma The Boy anarekodi wimbo) Nipo chini ya management (usimamizi) wangu wa mwanzo kabisa wa Ruge Mutahaba. Ruge ni mtu ambaye anajua kumsimamia mtu. Siwezi kumwangusha amefanya kazi kubwa ya kunisimamia. Ni kama baba kwangu. Nina singo mpya kama 4 au 5. Naandaa albamu itayokuwa na ngoma zote kali nilizofanya kwa takriban miaka 10 sasa itaitwa The Best of Ray C. Itakuwa na greatest hits zangu zote nilizofanya kwa kipindi chote hicho. Tumuombe Mungu. Akinijali na kama mipango itaenda vizuri, Desemba mwaka huu nitarudi rasmi stejini. Nitafanya shoo maalum  kwa mashabiki wangu. Nitakuwa na nyimbo mpya kali na zile za zamani. Sipati picha kwa watu watakaohudhuria kwani watapata burudani adimu kutoka kwangu.

UMENENEPA SANA NA ULISIFIKA KWA MAUNO STEJINI HADI UKAPEWA JINA LA KIUNO BILA MFUPA. JE, BADO YAPO?
(huku akijinafasi studio) “Hapa hapatoshi ningetoa shoo ya kufa ya mtu. Mauno yapo ya kutosha. Kiuno lainiii…)

SAUTI VIPI?
“(anapandisha sauti nyororo na kuimba moja ya ngoma zake kali zijazo) Umesikia kitu hicho? Sauti bado ipo vizuri mno.”

WATOTO WADOGO WANAKUJA KWA KASI KWENYE GEMU, INAKUPA PICHA GANI?
Chalenji ni kubwa lakini lejendi atabaki kuwa lejendi. Tumelitoa hili gemu mbali. Nafurahi kuona wadogo zetu wanafuata nyayo zetu na wanafanikiwa. Nafarijika nikimuona Recho wa THT (Winfrida Josephat) anafanikiwa kupitia aina ya muziki niliyoianzisha mimi. Hainipi shida zaidi ya kufurahia kuwa nimemkomboa mwanamke mwenzangu naye anapata shavu na kuweza kuendesha maisha.

WEWE NI KATI YA WASANII WALIOPATA USIMAMIZI MZURI TANGU MWANZO, NINI KIMETOKEA?
Ni kweli mwanzoni nilikuwa chini ya menejimenti ya Smooth Vibes. Ilipofungwa au ilipobadilika, niliamua kujitegemea. Nimekaa kwa zaidi ya miaka 6 au 7 bila kusimamiwa na mtu. Kama ulisikia nipo chini ya usimamizi fulani haikuwa rasmi. Sasa nimerudi kwa Ruge. Naamini nitafanya mapinduzi tena katika muziki huu ili ufike mbali zaidi.”

UMEFANYA KOLABO NA MSANII YEYOTE KWA HAWA WALIOIBUKA MIAKA YA HIVI KARIBUNI?
Nawakubali sana na tayari nimefanya mazungumzo nao. Nashukuru wakikutana na mimi wananiita lejendi. Wananipenda (anaingia Ben Pol, Ray anatabasamu). Nimepanga kufanya kolabo na Ben Pol (kicheko, wanakumbatiana). Pia nitafanya na Diamond (Nasibu Abdul), anafanya vizuri sana, namkubali. Nitafanya na Recho THT na Ommy Dimpoz (Faraji Nyambo) pia.

WIMBO WAKO WA MWISHO KABLA YA MATATIZO NI UPI?
“Ni Moto Moto niliofanya na akina Red San na Nonini wa Kenya. Sikuupeleka redioni nchini Tanzani lakini ukiingia mtandaoni kwenye You Tube utaona imesikilizwa na kutazamwa na mashabiki zaidi ya  348,142 hadi sasa

- ijumaa wikienda

Saturday, 7 September 2013

RAY C: SIJAPATA UKIMWI, SIJAOKOKA

MWANADASHOSTI anayejipanga kurejea kwenye gemu la Bongo Fleva kwa kishindo, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amefunguka ya moyoni akisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kupona madhara ya madawa ya kulevya bila kupata matatizo mengine ya kiafya huku akifafanua suala la kuokoka.

Mwanamuziki huyo alisema kuwa katika kipindi chote cha kupigana na madawa ya kulevya zaidi ya miaka mitatu iliyopita, alipitia mengi magumu lakini kikubwa ni kwamba hivi karibuni alipima na kujikuta yupo salama na hana Ukimwi.

Kuhusu suala la kuokoka, Ray C alisema ukweli ni kwamba mwanzoni alikuwa Mkatoliki lakini hivi karibuni alibatizwa na maji mengi katika Kanisa la Sloam lililopo Mbezi-Beach na kuungana na mama yake anayesali kwenye kanisa hilo.

“Namshukuru Mungu nimepona, sina tatizo la kiafya kama Ukimwi. Kuhusu kuokoka, mimi sijaokoka. Nilibatizwa na maji mengi. Napenda mahubiri ya Sloam. Nimeungana na mama yangu anayesali kanisani hapo ndiyo maana watu wanatafsiri kuwa nimeokoka.“Watu wakisikia mtu anasema ameokoka wanatafuta vitu ili kukujaribu. Kweli mimi sijaokoka lakini mahubiri yananiweka huru na nakuwa na amani zaidi,” alisema Ray C.

Thursday, 29 August 2013

RAY C SASA AAMUA KUOKOKA ABATIZWA RASMI LEO....!!

Yule dada yetu msanii maarufu wa nyimbo za ubongo wa fuleva leo hii amewaka bayana ya kuwa yeye na shetani sasa ni paka na panya. Amethibitisha hayo katika post zake za instagram. Wambea hatuna maneno mengi zaidi ya kusema angalia picha hizo na wote tuseme AMEN umechagua njia njema.
  •