Showing posts with label Shilole. Show all posts
Showing posts with label Shilole. Show all posts

Saturday, 21 September 2013

"KUTOVAA NGUO ZA NDANI HUSUSANI KWA WANAWAKE NI KUJIDHALILISHA"....SHILOLE


IMEBAINIKA kuwa baadhi ya wasanii wa kike nchini hawavai nguo za ndani kwa madai kwamba joto linawaumiza na kuwasababishia michubuko katika baadhi ya sehemu za mwili wao

Hali hiyo ya kutovaa nguo za ndani inasababishwa na wasanii hao kutaka kupata hewa na kuepuka kubanwa kwa madai kuwa wanahitaji kuwa huru zaidi na mavazi wanayovaa huku baadhi ya sehemu zao za mwili kuonekana vizuri

Hayo yalibainishwa jijini Dar es Salaam na  msanii wa filamu pamoja na muziki wa miondoko ya miduala Zuwena Mohamed 'Shilole' alipokuwa akizungumza na jarida hili ....Shilole alisema kuwa kutovaa nguo za ndani hususani kwa mtoto wa kike ni kujiaibisha na kujishushia heshima katika jamii

Alisema kuwa wapo wasanii ambao hawavai nguo za ndani kwa madai kuwa wanaogopa kuchubuka jambo ambalo yeye aliliona si sahihi hivyo na kudai kuwa tabia ya kujirahisisha katika maswala ya ngono ndiyo inayopelekea kuvaa bila nguo yoyote ndani

"Unajua kiukweli ni kujishusha thamani hauwezi kukaa bila ya kuvaa nguo ya ndani tena mtoto wa kike ni kujidharilisha hata kama ni kuiga tusifikie huko jamani" alisema Shilole

Pamoja na hayo aliongezea kuwa sababu nyingine inayosababisha wasanii hao kubaki utupu ni kuonyesha viungo vya mwili wao jinsi walivyoumbika jambo ambalo yeye aliliita ni njia moja wapo ya kujidharilisha na kuutangaza uhuni kwa jamiii

"Kama hauna makalio makubwa huna tuu hata usivae nini hayaonekani hivyo ni bora ujistili kama mtoto wa kike" alisema Shilole

Alipoulizwa kuwa na yeye ni miongoni mwa wasanii wanaokaa utupu Shilole alisema kuwa amelelewa katika mazingira ya kuvaa nguo mbili kabla haujavaa ile inayoonekana na jamii hivyo hawezi kutoka nyumbani bila ya kuvaa nguo ya ndani

Kwa upande wake mwanamitindo Joketi Mwegelo alisema kuwa wasanii hao wanaovaa nguo bila ya kuvaa za ndani wanatakiwa kujistiri na kwenda na mazingira ili waendelee kulinda heshima yao kwa jamii

Alisema kuwa kama mtoto wa kike ni vyema ukafuata maadili na mazingira ya nchi hivyo basi kukaa utupu ni moja ya kujidharilisha na kushusha soko lako katika sehemu yako ya kazi na kuchangia kupunguza mashabiki ambao kwa namna moja au nyingine unaweza kuwapoteza kutokana na tabia

Sunday, 15 September 2013

ANGALIA VIDEO YA SHILOLE ALIPOMKATIKIA MAUNO YA NGUVU MSHABIKI WAKE KWENYE FIESTA 2013 MJINI DODOMA

ANGALIA VIDEO HAPO CHINI....

SHILOLE ARUHUSU KUSHIKWA KILA SEHEMU YA MWILI WAKE NA MWANAUME ALIPOKUWA JUKWAANI.


Kulishika kama utakavyo umbo la kuvutia la mwanadada Shilole ni ndoto ya wanaume wengi. Lakini vipi kama ndoto hiyo ikikuijia katika wakati ambapo hujajiandaa kabisa? Utaona aibu kuitimiza? Huenda jibu hili anaweza kuwa nalo kijana wa Dodoma aliyepata bahati hiyo ya mtende kwenye jukwaa la Serengeti Fiesta
mjini Dodoma jana usiku.
Akiwa amevalia nguo iliyolichora vema umbo lake, Shilole alimpa nafasi kijana huyo kuiota ndoto hiyo walau mara moja katika maisha yake. Kijana huyo aliyekuwa amevalia t-shirt nyekundu hakufanya ajizi. Akionesha kufurahia ‘fursa’ hiyo ya aina yake, jamaa alionekana kunogewa kulishika na kulikumbatia umbo la Shilole ambaye alimruhusu afanye chochote.
Chochote lakini sio vyote!!!
Mbele ya umati mkubwa wa wakazi wa Dodoma, Shilole alimruhusu jamaa huyo alikamate kiume paja lake jeupe huku akikata kiuno na kumshika begani.
Tukio hilo lilivuta hisia za maelfu ya wakazi wa Dodoma waliokuwa wakishangalia mwanzo mwisho. Ama hakika, Shilole anajua kuwapa raha mashabiki wake.

Saturday, 7 September 2013

SHILOLE AANIKA TUMBO LAKE NDANI YA SERENGETI FIESTA MBEYA


IMG_0273

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,ambaye kwa sasa anafanya vyema kwenye anga za muziki huo,Neylee akiimba kwa hisi jukwaani huu wakati tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea kwa shangwe ndani ya uwanja wa Sokonine.

Wakazi wa jiji la Mbeya wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Sokoine,ndio kwanza shoo inaanza ambapo msanii aliyewahi kuiwakilisa shindano la BSS,Walter Chilambo ndiye aliyefungua pazia la onesho hilo usiku huu.


Tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea usiku huu kwenye uwanja wa Sokoine,Mkoani Mbeya

Mama wa miduara ya Kibongofleva,Shilole akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.


Sehemu ya umati wa watu.


Mkali mwingine wa hip hop (bongofleva),Ney wa Mitego akikamua jukwaani usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013,kwenye uwanja wa Sokoine,mjini Mbeya.

Wakazi wa jiji la Mbeya wakitoa heshima kwa baadhi ya wasanii waliotangulia mbele za haki, kwa kuwasha tochi za simu zao usiku huu.



Rich Mavoko na skwadi lake wakilishambulia jukwaa.




Wasanii mahiri katika miondoko ya hip hop,Stamina na Young Killer wakilishambulia jukwaa la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Sokoine usiku huu.

Ni shangwe tu kwa wakazi wa jiji la Mbeya usiku huu ndani ya uwanja wa Sokoine.

 
Mmoja wa sanii mahati wa kizazi kipya,Ommy Dimpo akiwaimbia mashabiki wake singo yake mpya iitwayo Tupogo usiku huu ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013.

MKali wa kukamua mangoma kutoka Clouds FM,Dj Zero akiwarusha maelfu ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wanaondelea kumiminika kwenye uwanja wa Sokoine usiku huu.


Msanii aliyewahi kulwakilisa shindano la BSS,Walter Chilambo ndiye aliyefungua pazia la onesho hilo usiku huu,pichani akitumbuiza mbele ya mashabiki wake.


Baadhi ya watu wakifuatilia yanayojiri usiku huu kwenye tamasha la Seremgeto Fiesta 2013 ndani ya uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya.


Mkali wa Mahaba,a.k.a tajiri wa Mahapa kutoka mwambao wa Pwani,Cassi Mganga akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu ndani ya tamasha la serengeti fiesta 2013,kwenye uwanja wa Sokoine mkoanni Mbeya.




Thursday, 29 August 2013

SHILOLE: MADEE AU OMMY DIMPOZ?... KILA MMOJA ANASWA NAE CHOBINGO

STAA wa Muziki wa Mduara, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, amewashangaza wasanii wenzake baada ya kunaswa chobingo kwa nyakati tofauti akiwa na wasanii wenzake, Hamad Ally ‘Madee’ na Omari Faraj ‘Ommy Dimpoz’. 
 Shilole akiwa na Madee.

Mpango mzima ‘uli-happen’ Agosti 25, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa Singida Montel wakati wasanii hao walipokuwa katika shoo ya Serengeti Fiesta 2013 ‘Noma Sana’
Kwanza paparazi wetu alimfotoa Shilole picha kadhaa akiwa anafungwa zipu na Madee.



                                   ...Akiwa na Ommy Dimpoz.
 
Muda mchache baadaye, paparazi wetu alimfuma tena Shilole akiwa amekumbatiana na Ommy Dimpoz kwenye gari huku wakiwa wameangusha usingizi mzito hali iliyozua minong’ono ingawaje wawili hao walidai ni shangwe tu za Fiesta na hakuna uhusiano wa kimalovee kati yao.
                                     Katika pozi na Madee.

Friday, 23 August 2013

SHILOLE AAMBULIA MATUSI BAADA YA KUANIKA TUMBO LAKE MBELE ZA WATU......!!



 Msanii wa filamu za Kibongo,na mwanamuziki wa Bongo Fleva Zuwena Mohamed‘Shilole’amenangwa kwenye mtandao wa instagram baada ya kupost picha akiwa na madansa wake huku wakiacha matumbo yao wazi.



Wednesday, 14 August 2013

SHILOLE ACHEZEA KIPIGO KISA MADENI

Msanii nyota kwenye tasinia ya muziki na filamu bongo Zuwena Mohamed “ Shilole” mwishoni mwa wiki iliyopita alionja joto ya jiwe baada ya kutiwa mtu kati na wakina dada waliokuwa wanamdai kiasi kikubwa cha pesa.


Habari za uhakika zilizothibitishwa na mmoja wa wakina dada hao waliokuwa wanamdai zilisema kuwa wanawake hao waliamua kuchukua hatua za kumtia adabu Shilole baada ya kupata taarifa kuwa siku hiyo alikuwa ana hama kwa kukimbia na teni lao “ Ishu ilikuwa hivi sisi tunamdai huyu dada lakini cha kushangaza amekuwa akitupiga chenga sana na ona alivyokuwa sio mstaarabu kumbe siku hiyo alikuwa anahama na deni letu ndio maana tuliamua kwenda kumzingua” Alisema dada huyo aliomba jina lake lihifadhiwe.

Dada huyo aliendelea kufunguka mengi kuhusu sakata hilo “ Unajua sisi tunafanya biashara zetu hivyo kuna siku Shillole alikuja na kusema amekwama kipesa hivyo tumuazime pesa na tukafanya hivyo lakini cha kushangaza mwezi wa sita huu hataki kurudisha na amekuwa akitukwepa mara kwa mara hivyo majirani ndio wakatushtua kuwa anataka kuhama kwa staili ya kutoroka na deni letu ndipo tulipoenda wanawake wanne na kumshushia kipigo” Alisema dada huyo

Baada ya taarifa hizo Shilole alitafutwa kupita simu yake ya mkononi pamoja na kupita kwenye makoloni yake hakuweza kupatikani isipokuwa majirani mbalimbali walikili kutokea kwa tukio hilo la kufedhehesha kwa msanii huyo.