Monday, 12 August 2013

WADADA WA KITANZANIA WAZIDI KUPIGA PICHA ZA UTUPU NA KUZIWEKA MITANDAONI !!!






MAJANGA: WANAUME NAO WAAMUA KUTOKEA NA PEREUVIAN WEAVE NA NYUSI WANATINDA...!!


                                        DUNIA INAELEKEA UKINGONI DAH

MWANAFUNZI ALAZIMISHWA NGONO BILA KONDOMU NA MAJANGA MENGINE WILAYANI MAKETE...



Kata ya Iwawa ilipo shule hiyo.
 
Na Edwin Moshi wa Globu ya Jamii, Makete
Wafunzi wa shule ya sekondari Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe wamekiri uwepo wa wanafunzi wenzao ambao wanajihusisha na vitendo vya ngono na wengine wanaishi na virusi vya UKIMWI, licha ya jamii kudhani kuwa wanafunzi hawawezi kuwa na virusi hivyo kwa minajili kwamba bado ni wadogo.
 
Hayo yamebainika baada ya mtandao huu kufanya mahojiano ya kina na baadhi ya wanafunzi wanaosoma shuleni hivi karibuni kwa ruhusa ya mkuu wa shule hiyo Bw. Christopher Haule hapo kufuatia wananchi wengi wilayani hapo kudhani kuwa wanafunzi hao hawana maambukizi ya vvu kwa kuwa ni wadogo na huwenda hawajaanza kujihusisha na vitendo vya ngono.Mwanafunzi mmoja (jina linahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) amesema ana marafiki zake zaidi ya watano ambao wanaishi na virusi vya UKIMWI na hajui walivipataje, hivyo anaamini wapo wanafunzi wengi ambao wana maambukizi.
Amesema jamii inapaswa kuondokana na dhana potofu kuwa mabinti ama vijana wadogo hawana vvu waache mara moja kwa kuwa virusi vinampata mtu yeyote bila kujali umri.
“Mtu anayedhani kuwa wanafunzi huwa hawana vvu ni uongo, na pia waanatakiwa kuacha kujihusisha kimapenzi na wanafunzi kwa madai kuwa hawana vvu, lakini wakumbuke sheria za nchi haziruhusu kujihusisha kimapenzi na wanafunzi, jamani Ukimwi upo kwa kila mtu” alisema mwanafunzi huyo.Mwanafunzi mwingine amesema yeye hafahamu kama wanafunzi hao wenye vvu wanajihusisha kimapenzi na watu kwa kuwa wapo ambao wanaishi na wazazi wao na wengine wamepanga kwenye nyumba maarufu kama mageto ambao kwa kiasi kikubwa wako huru kufanya mambo yao kwa kuwa hawana muangalizi.“Ni kweli kabisa wapo wanafunzi wenye vvu wanaoishi wenyewe kwenye mageto, lakini mimi sijui kama wana wapenzi ama lah, maana ni ngumu kujua na mimi sipo hapa kwa ajili ya kufuatilia maisha ya mtu, na hao ninao kwambia kwa kuwa ni marafiki zangu na waliwahi kuniambia kuwa wanaishi na vvu” alisema mwanafunzi huyo(jina tunalo)
             Mmoja wa mwanafunzi aliyezungumza na mtandao huu
 
Mwanafunzi upande wa kushoto wa picha hii amemweleza mwandishi wetu kuwa mpenzi wake anamlazimisha kufanya mapenzi bila kondomu

“Mimi kwa upande wangu Kusema kweli nina mpenzi na nilishawahi kupima vvu mwaka jana (2012) na kujikuta sina maambukizi namshukuru Mungu kwa hilo, na pia nimekuwa nikifanya mapenzi kwa kutumia kondomu lakini kuna wakati mwingine hatutumii mimi na mpenzi wangu na mara nyingi yeye ndiyo ananishawishi tusitumie, na huyo mpenzi wangu si mwanafunzi ni jamaa tu wa pale mtaani kwetu, na mimi huwa nakwenda home kwake(Nyumbani kwake) na wakati mwingine anakuja geto kwangu, ili atumie kondom huwa namwambia leo ni siku zangu za hatari, hapo ndipo atavaa kondomu” alisema mwanafunzi huyo wa kike ambaye anaishi kwenye nyumba ya kupanga.Akizungumzia suala hilo, diwani wa kata ya Iwawa Benjamin Mahenge alikiri kuwepo kwa tatizo la ukimwi kwa kila mtu, na kuongeza kuwa hata wanafunzi wapo wenye vvu ingawa ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na miaka iliyopita na pia wapo wanafunzi wanaojihusisha na vitendo vya ngono, na ambao wameshabainika wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria

Diwani wa kata ya Iwawa Benjamin Mahenge (kushoto) akizungumza na mwandishi wa habari hizi
"Unajua ni ngumu mwanafunzi kuniambia mimi ama kiongozi mwingine kuwa anajihusisha kimapenzi na mtu lakini kwako mwandishi kasema, mimi ninaomba wawe wawazi ili tuweze kuwasaidia hasa pale linapojitokeza tatizo hasa mimba kwa kuwa hawawataji wahusika" alisema Mahenge
Mahenge amesema huu ni muda wa jamii kubadilika na kuondokana na dhana potofu kuwa wanafunzi hawawezi kuwa na vvu, na pia wawaache wanafunzi hao wasome na si kuwarubuni na kujikuta wakifanya nao mapenziPia amesema wapo wanafunzi katika kata yake ambao wamepanga na uangalizi wao si mzuri kwa kuwa wanajiamulia mambo yao wenyewe hata kama si mazuri kutokana na kukosa uangalizi wa watu wazima.
 “Unakuta mwanafunzi kajipangia kwenye chumba chake, yeye ndio kila kitu, akitaka kusoma haya, akitaka kwenda disco hakuna wa kumuuliza, hii ni hatari pia” alisema Mahenge
Moja ya nyumba iliyoko Makete mjini amayo wanafunzi wamepanga

KWA WANAWAKE, FAHAMU DALILI 10 ZA MWANAUME ANAYEKUPENDA KWA DHATI......

Kwa wanawake leo tuangalie dalili kumi za mwanaume anayakupenada kama ifuatavyo hapa chini.......

ANAVYOTAZAMA
Mwanasaikolojia Zick Rubin kutoka Chuo cha Havard nchini Marekani aliwahi kusema kwamba watu wanaopendana hutumia asilimia 75 kutazamana kuliko wasiopendana, ambao kiwango chao ni asilimia 30-50. 

Hii ina maana kwamba mwanaume anapotumia muda wake mwingi kumtazama msichana na kugeuka taratibu kuangalia vitu vingine kama mtu asiyependa kuacha kumwangalia, ujue anampenda.

MIPANGO 
Mwanaume anayekupenda atakushirikisha kwenye mipango yake hasa ya muda mrefu. Mfano akitaka kununua kiwanja, kujenga nyumba atakuambia na pengine kutaka mchango wako wa hali na mali katika kulifanikisha hilo. Ukiona mwanaume anakuficha mambo yake, tambua kuwa huyo ana walakini kwenye penzi la dhati na la muda mrefu.

ATAONESHA HUZUNI
Katika maisha ya mapenzi kuna wakati wa kuhuzunika. Mwanaume mwenye upendo wa dhati atashirikiana nawe wakati wa huzuni na kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa unapata furaha. 


ATAKUAMINI
Dalili nyingine ya kupendwa na mwanaume ni kuaminiwa kwenye maisha kwa ujumla. Yaani mwanaume anayekupenda hatakuficha kitu, mfano pesa zake, atakupa uhuru kwenye simu yake na kukuamini katika usimamizi wa miradi yake.

ATAKUPA NAFASI
Ninapozungumzia nafasi nina maana atakukaribisha kwake bila hofu na kukupa nafasi ya kuingia na kutoka bila mipaka, atakupa nafasi ya kuweka vitu vyako kwenye kabati na kuruhusu nguo, picha na vitu vyako kuonekana wakati wote chumbani kwake.

UTAKUWA MWANAFAMILIA

Mwanaume aliyefikia chaguo la mwisho kwa mwanamke humshirikisha mpenzi wake kwenye masuala yake ya kifamilia, mfano atamwalika kwenye vikao vya harusi, kipaimara, atatoa nafasi ya kuambatana naye kuona wagonjwa, kusalimia ndugu na atakuwa huru kukutambulisha kwao.

ATAZUNGUMZA NAWE KUHUSU WATOTO
Kwa kuwa wanaume wengi hufikiria kuwa na familia, mwanaume anayekupenda atazungumza nawe mipango ya kupata watoto kwa kuwa atakuwa amekuchagua wewe kuwa mama wa wanaye na atapenda mazungumzo hayo.

ATAKUSAIDIA
Kwa kuwa kukwama ni sehemu ya maisha yetu, mwanaume anayekupenda atakuwa tayari kukusaidia unapokwama. Kila mara atahakikisha kuwa unakuwa na mafanikio na yeye atakuwa tayari kukupunguzia usumbufu wa maisha, kwa kukufuata kazini, kukusaidia baadhi ya mambo na hata ya nyumbani.

ATAJITOLEA
Ninaposema kujitolea ninamaanisha atakuwa tayari kufanya mambo yako na kuyaweka yake nyuma. Kwa mfano akiwa anapenda mpira na siku hiyo kuna mechi, lakini muda huo ukamwambia akufuate kwa mjomba wako atakuwa tayari kuacha furaha yake na kukujali wewe. Huyu ni mwanaume anayekupenda kwa dhati.

ATAAMBATANA NAWE
Wapenzi wengi wasiokuwa na mapenzi ya dhati huona aibu kuambatana na wapenzi wao kwenye mikusanyiko ya watu, lakini mwanaume anayekupenda atafurahia kutoka moyoni kuongozana nawe kwenye halaiki ya watu na kufurahia uwepo wako bila kuona aibu.

Mada hii inaishia hapa, hebu jiulize mwanadada, huyo uliyenaye anakufanyia haya, kama sivyo kwa kiwango kikubwa utakuwa na kazi ya kuhakiki penzi lako na pengine kujenga misingi mipya ya uhusiano wenu kabla haujavunjika.

PICHA 2 ZA JUSTIN BIEBER AKIWA MTUPU ZA ZAGAA MTANDAONI

 
msanii Justine Bieber zawagumzo mtandaoni huku picha hizo zikimuonesha msanii huyo wa muziki akiwa hana nguo hata moja isipokuwa ni Kifaa cha muziki tu alichokishika kikiwa kimezuia sehemu nyeti za mwili 
 
 Hivi sasa imekuwa ni kawaida kwa wasanii wengi kupiga picha hizi na kuweka katika mitandao Dhamira ikiwa ni kutafuta kuzungumziwa sana na mashabiki au wananchi kwa ujumla na pia kuongeza umaarufu wa mtu huyo.

TCRA YAJIPANGA KUZIFUNGA SIMU ZOTE ZA KICHINA ( SIMU FEKI )

Mamlaka ya mawasiliano nchini, TCRA inaandaa utaratibu wa kufunga simu zote ambazo hazina viwango vya ubora stahiki kwa lengo la kuzuia uingizwaji wa bidhaa hizo nchini ambazo zimekuwa zikiuzwa kiholela.
 

Meneja mawasiliano wa TCRA ‘Innocent Mungy’ amesema mamlaka hiyo kwa sasa inazunguka nchini kutoa elimu kwa wananchi ili wazitambue simu mbovu na madhara yake katika mawasiliano kabla ya kufikia zoezi hilo.

Zoezi litaanza kwa   kutoa tahadhari kwa wananchi kabla ya  zoezi la kuzima simu kuanza  ili  kuhakikisha kuwa   wananchi  hawaathiriwi  na  zoezi  hilo.
 
Ameongeza kuwa mwongozo wa kuzima simu wenye lengo la kukabiliana na uingizwaji wa simu bandia nchini, unatekelezwa kwa mujibu wa sheria ya mwaka 2010 ya mawasiliano ya elektroniki na posta (EPOCA) pamoja na kanuni zake za mwaka 2011.
 

HIVI NDIVYO FANGASI INAVYOSHAMBULIA SEHEMU ZA SIRI..!! **ZINGATIA

LEO tuangalie fangasi wanaoshambulia sehemu za siri, yaani Tinea cruris. Aina hii ya fangasi ndiyo inayofahamika na  Watanzania wengi zaidi ya aina nyinginezo na waathirika huwashwa sana sehemu za siri. Dalili zake
Kuna dalili nyingi sana za ugonjwa huu lakini kubwa kuliko zote ni kuwa fangasi hawa huambatana na muwasho mkali wa eneo lenye maambukizi hasa sehemu za siri, rangi ya ngozi ya eneo lenye maambukizi hubadilika na kuwa na muundo wa duara, mfano wa sarafu.

Dalili nyingine ni ngozi kukauka kisha kubanduka, na kama mgonjwa asipopata tiba mapema basi atatokwa na majimaji kwenye eneo la ngozi lililoathirika pamoja na kutoka kwa harufu mbaya kwenye eneo hilo.

UNAVYOAMBUKIZWA
Kuna njia nyingi zinazoweza kusababisha uambukizi wa maradhi haya, lakini ili uambukizaji huu uwezekane lazima kuwe na mazingira rafiki ya kuwezesha fangasi kuishi na kuhama kwa urahisi.

Mazingira haya rafiki kwa kuruhusu fangasi hawa kuweza kutoka kwa mtu mmoja au sehemu moja ya mwili kwenda kwa mwingine huhitaji uwepo wa hali ya joto pamoja na majimaji sehemu iliyoathirika na maambukizi hutokea kwa kugusana na mtu aliye na maambukizi tayari.

Mtu anaweza kupata maambukizi ya fangasi hawa kwa kushirikiana kimapenzi na mwenzake aliye na ugonjwa au kwa kushirikiana mavazi na mtu aliyekwisha pata maambukizi au kushirikiana taulo au hata sabuni na  vifaa vya usafi wa mwili kwa mtu zaidi ya mmoja.

Watu ambao huweza kupata maambukizi ya fangasi wa sehemu za siri ni wale wanaofanya kazi zinazohusisha ukaaji kwenye maji yaliyotuama kwa muda mrefu, wanaoshiriki mapenzi na wenza wenye maambukizi ya fangasi hao na wote ambao wana fangasi za kwenye vidole kwani fangasi wale wanaweza kuhamishwa kupitia kwenye kucha na kuhamia kwenye eneo hilo la siri;

-Wengine wanaoweza kupata maradhi haya ni wale wanaofanya usafi wa mwili kwa kutumia maji yaliyobeba vimelea vya fangasi hao, wasiojikausha vizuri maungo ya sehemu za siri, watu wenye maradhi yanayosababisha kushuka kwa kinga, hususan kisukari, wanaovaa nguo zaidi ya moja hali inayosababisha mwili kushindwa kupunguza joto lake hivyo kutoa jasho, wanaovaa nguo za kubana sana hasa zile zinazobana sana kwenye maeneo ya maungo ya siri na  wenye unene wa kupindukia;

Lakini watu wanaokunywa dawa za kuua vimelea (antibiotics) kwa muda mrefu au wenye ujauzito ambao huchangia kushuka kwa kinga ya mwili nao wanaweza kupata ugonjwa huu.