DHAMIRA ya watu wengi ni kutunza mimba hadi kufikia hatua ya kujifungua lakini wakati mwingine ujauzito unaweza kuchoropoka kutokana na sababu tofauti, iwe kwa kukusudia au bahati mbaya.Kwenye maisha ya mastaa wetu wa Bongo, wapo waliowahi kupata mimba lakini kutokana na sababu tofauti, zilichoropoka.
Amani linakumegea baadhi ya mastaa hao ambao wengine walianika sababu za mimba hizo kuchoropoka huku wengine wakifanya siri:
 |
| AUNT EZEKIEL |
Februari, 2011 aliripotiwa kuwa na ujuzito wa mwanaume ambaye mwenyewe hakumtaja lakini haikupita muda mrefu, mimba hiyo ilichoropoka pasipo kuweka wazi sababu.
 |
| JINI KABULA |
Mwaka jana alijinadi kuwa na ujauzito wa Mbongo Fleva, Maximiliam Bushoke. Mimba hiyo ikadumu kwa miezi kadhaa, ghafla ikachoropoka yenyewe kwa bahati mbaya.
 |
| WEMA SEPETU |
Kwa upande wake alitundikwa kibendi na aliyekuwa mpenzi wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’ lakini miezi kadhaa mbele ikatoka yenyewe kutokana na sababu za kitaalam.
 |
| LULU |
Mwaka jana aliripoti kwenye vyombo vya habari kuwa na mimba ya muigizaji mwenzake, marehemu Steven Kanumba. Wakati mapaparazi wakiendelea kufanya uchunguzi, ghafla ikadaiwa ‘kuyeyuka’ pasipo kujulikana chanzo.
 |
| LADY JAYDEE |
Huyu ni mke halali wa Mtangazaji, Gardner Habash. Mwaka 2011 mitandao ya kijamii iliripoti kuwa ni mjamzito na kudaiwa kuwa habari hiyo ilimpa faraja mumewe lakini furaha hiyo iliyeyuka ghafla wakati Lady Jaydee akionekana na tumbo kubwa, ikadaiwa mimba imechoropoka bila sababu kutajwa.
 |
| Baby Madaha |
Mwaka 2010 mkali huyo wa filamu na muziki Bongo, alidaiwa kuwa na mimba ingawa mwenyewe hakutaka kuweka wazi lakini baadaye ilidaiwa kuwa alikwenda kuichoropoa nchini Kenya.
 |
| JACK WA CHUZ |
Mapema mwaka huu aliripotiwa kuwa ni mjamzito lakini mwenyewe hakupenda kuweka mambo yake hadharani. Hata hivyo, vyanzo makini vilidai kuwa mimba hiyo ilikuwa ya mfanyabiashara mmoja jijini Dar lakini baadaye aliichoropoa pasipo kufahamika sababu
-USWAZI
Huyu ndiye Super Star Aunt Ezekiel at Nyama Choma Posta Ground Kijitonyama, jana aliambiwa kidonda chake kimeoza na mkono utakatwa kumbe ulikuwa ni uongo wa mchana, she is just fine!! "Mie niko fine mkono unaendelea kupona...haujaoza wala nini ni uzushi tu "

Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Gwantwa’ yupo hatarini kukatwa mkono kutokana na jeraha la chupa alilolipata hivi karibuni.
Tukio la Aunt kupigwa chupa na mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Yvonne nje ya Club Bilicanas, Posta jijini Dar, lilitokea Agosti 26, mwaka huu wakati staa huyo alipokwenda kujiachia na mshosti zake.
Baada ya kupigwa chupa siku hiyo, Aunt alikimbizwa katika Hospitali ya Aga Khan lakini bahati mbaya alikosa daktari wa kumtibu hivyo akalazimika kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Dk. Mvungi, Kinondoni ambapo alishonwa nyuzi sita pamoja na dawa za kukausha kidonda.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Aunt ni muoga wa dawa na wakati kidonda kikiwa bado hakijapona vizuri aliacha kumeza dawa alizopewa.
Chanzo hicho kilisema tatizo la staa huyo kukatisha dozi lilisababisha kidonda kishindwe kupona na badala yake kikaanza kutengeneza usaha na taratibu mkono ukaanza kuoza.
“Mkono ulifikia hatua ukaanza kuoza kwani licha ya kushonwa lakini kilibadilika rangi ndipo alirudi hospitali.
Imeelezwa kuwa mapema wiki hii, Aunt alirudi tena katika Hospitali ya Dk. Mvungi na kusafishwa upya kidonda baada ya madaktari kugundua tatizo lilizidi kuongezeka.
Kwa mujibu wa nesi wa hospitali hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, hali ya Aunt ilimshtua daktari, akamwambia aombe Mungu kwani kidonda kilichimbika sana na tatizo kama hilo huweza kusababisha mtu kukatwa mkono.
“Iligundulika mkono ulikuwa unaoza, daktari alimwambia amuombe Mungu kwani hatua iliyokuwa imefikia ni mbaya hivyo asipokuwa makini tatizo hilo litamfanya akatwe mkono,” alisema nesi huyo.
Aunt alipigwa chupa akigombania penzi la mwanaume na Yvone .
-Gpl & Aman
Siri ya Aunt Ezekiel kupigwa chupa club na kujeruhiwa mkono wake imefichuka.Habari za uhakika zinadai kwamba Aunt alipigwa chumba na mrembo wa kike katika harakati za kugombea penzi la mwanaume... Mwanaume aliyekuwa akigombaniwa ni Jeff ambaye anadaiwa kuwa ni boyfriend wa Yvonne ( aliyempiga aunt chupa )..Kutokana na aibu hiyo, mastaa kadhaa wameongea na mpekuzi kwa nyakati tofauti na kueleza masikitiko yao dhidi ya aunt Ezekiel ambaye ni mke wa mtu... Katika maongezi hayo, mastaa hao walidai kwamba mambo anayofanya aunt hayaendani na matendo ya mke wa mtu. Aunt amekuwa ni mtu wa baa, club na madanguro mengine ya usiku, hali inayotia shaka uhai wa ndoa yake. " Aunt kapata mume mwelewa sana ambaye kakiheshimu sana kipaji chake kwa kuto-mbana.
"Cha ajabu yeye ameanza kufanya mambo ya aibu kwa kuendekeza ngono nje ya ndoa yake" alisema star mmoja wa kike aliyekataa kuwekwa wazi jina lake ..
Muigizaji mwingine wa kike ambaye hakuwa tayari kuchorwa mtandaoni alisema: "Aunt ajiangalie sana.Yeye ni mke wa mtu kwa sasa. Kitendo alichokifanya kimemchafua mpaka ukweni na asipokuwa makini atampoteza mume wake...
"Yvonne alikuwa anamlinda bwanake, mi siwezi kumlaumu sana ila nyie wanaume ni watu wabaya sana pia"
Mtuhumiwa aliyempiga chupa mwigizaji Aunt Ezekiel Jumapili iliyopita nje ya Ukumbi wa Bilicanas ndiye aliyewahi kumchana viwembe mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ mwaka 2011.Kumbukumbu zinaonesha kuwa, mwaka 2011 Lulu alivamiwa na wadada wa mjini baada ya kunaswa katika pozi tata na mwanaume wa watu maeneo ya Kariakoo, jijini Dar. Alipoulizwa juu ya sakata hilo, Lulu alitiririka hivi:
“Naweza kumkumbuka mwanamke mmoja, namfahamu kwa jina la Yvonne, alinivamia na kuanza kunishambulia huku mkononi akiwa ameshika wembe...” Mwishoni mwa wiki iliyopita, Yvonne huyohuyo ndiye aliyedaiwa kumpiga chupa mkononi Aunt ambapo haikubainika mara moja sababu za kufanya tukio hilo.
Aunt alipelekwa katika Hospitali ya Dokta Mvungi, Kinondoni na kushonwa nyuzi sita huku mtuhumiwa akishikiliwa na polisi.
MWIGIZAJI wa sinema za kibongo, Aunt Ezekiel Grayson ‘Gwantwa’ amenusurika kupasuliwa paji la uso kwa chupa baada ya kupigwa mkononi...
Usiku wa kuamkia Jumatatu, nje ya Ukumbi wa Billicanas, mwanamke aliyejulikana kwa jina moja la Yvonne alimpiga Aunt kwa chupa tupu ya bia na kumpasua mkono wa kushoto.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamedai kuwa, wakati Yvonne anatekeleza ukatili huo, Aunt alikuwa amesimama na marafiki zake waliotajwa kwa jina moja moja, Sajenti na Rehema.
“Ndani ya ukumbi shoo ilikuwa ikiendelea, Aunt, Rehema na Sajenti walisimama nje, ghafla alitokea Yvonne akiwa na chupa mkononi, akailenga kwenye paji la uso la mwenzake, bahati nzuri Aunt aliiona na kukinga mkono,” kilisema chanzo.
Kikaendelea: Vurugu kubwa ilizuka, ilibidi shoo ndani isimame ili kushughulia suala hilo. Aunt alikimbizwa Aga Khan, Yvonne akapelekwa msobemsobe Kituo cha Polisi cha Oysterbay, Dar ambapo anashikiliwa.
Baada ya taarifa hizo, juzi mchana, mwandishi wetu alifika nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala na kumkuta ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Ishu ni kweli kama mlivyosikia, lakini kule Agha Khan sikutibiwa, niliambiwa daktari hayupo mpaka saa mbili asubuhi na muda huo ilikuwa saa kumi alfajiri.
“Ilibidi niende kutibiwa kwa Dokta Mvungi, Kinondoni Hospitali ambako nilishonwa nyuzi sita.”
mwandishi: Madai ya Yvonne ni nini hasa?
Aunt: Yaani hata mimi sijui, nilishangaa sana. Kwanza lengo lake lilikuwa kunijeruhi kwenye uso, lakini niliiona chupa nikaikinga na mkono ndiyo maana ikaniumiza. mwandishi: Siku za nyuma uliwahi kuingia kwenye mzozo na Yvonne kwamba unamchukulia mpenzi wake aitwaye Joff, siyo kwamba ndiyo kisasi?
Aunt: Yale mambo yalipita, yeye ana maisha yake na mimi nina yangu.
Source:Risasi
JINA la Aunt Ezekiel siyo geni kabisa kwa wadau mbalimbali wa burudani hapa nchini, ni staa ambaye hivi sasa ana jina kubwa kupitia sanaa yake ya uigizaji wa filamu aliyoianza miaka sita iliyopita.
Japokuwa kwa sasa ni staa, amepitia mambo mengi magumu katika safari yake ya maisha mpaka kufikia hapo alipo hivi sasa.
Aunt alizaliwa mwaka 1988 mkoani Dar es Salaam, baba yake akijulikana kama Ezekiel Grayson’ Jujuman’ ambaye alikuwa ni mchezaji hodari sana wa timu ya Simba. Alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Bunge mwaka 1993 hadi 1998. Alienda kumalizia darasa la saba katika Shule ya Msingi Chanzige iliyopo Kisarawe, mkoani Pwani.
Vipi maisha yalikuwaje baada ya kumaliza shule?
“Kwa kweli maisha yalikuwa ni magumu mno kwa maana nilipomaliza shule tu, alijitokeza mwanaume na kutaka kunioa kitu ambacho mimi sikukipenda kabisa lakini baba yangu alitaka hivyo kwa vile uwezo wa kunisomesha hakuwa nao tena na maisha yalikuwa ni magumu sana
Alitoroka nyumbani kwao alfajiri
“Baada ya kuona mambo ya mimi kuolewa yanapamba moto huku yule mwanaume akizidi kuihudumia familia yangu, nikaona nikichelewa nitabebwa mzobemzobe, hivyo niliamua kutoroka alfajiri na mpaka natoroka, sikuwa najua naelekea wapi.
Aenda kufanya ‘uhausigeli’
“Baada ya kutoroka, asubuhi ile nilienda mpaka Ukonga, sehemu moja inaitwa Mazizini, nikagonga nyumba moja ya mtu na kumwambia natafuta kazi za ndani, bila kuchelewa yule dada aliniambia hata yeye anatafuta msichana, hivyo nilianza kufanya kazi nikawa namlea mtoto na kufanya kazi zote za ndani huku nyumbani kwetu wakinitafuta bila mafanikio.
Arudi nyumbani kwao
“Baada ya kufanya kazi kwa muda wa miezi mitatu, niliamua kumpigia simu baba yangu ambapo aliposikia sauti yangu alifurahi sana na kuniambia kuwa nirudi nyumbani wala hawataweza kuniozesha tena, hivyo niliamua kumuaga tajiri wangu na kumwambia narudi nyumbani kwetu.Aendelea na shule
“Niliporudi nyumbani bado nilimkuta yule mchumba lakini nilimwambia kama anataka kunioa anisubiri nisome, hivyo nilienda Iringa katika Shule ya Sekondari Kawawa na kuanza kidato cha kwanza mpaka cha pili, nikarudi Dar na kumalizia katika Shule ya Sekondari Makongo mwaka 2004.
Aingia kwenye urembo
“Baada ya kumaliza sekondari, nilijiunga na mambo ya computer pale Amana, lakini baadaye niliamua kushiriki mambo ya urembo ambapo niliibuka kuwa Miss Mwanza 2006 na kuingia katika shindano la kumsaka mrembo wa Tanzania lakini sikufanya vizuri na hapo ndipo nilipoingia kwenye uigizaji wa filamu ambapo filamu yangu ya kwanza kabisa ilikuwa ni Miss Bongo, iliyokuwa ya William Mtitu.
Afunga ndoa, azawadiwa kilo moja ya dhahabu
“Ilipofika mwaka 2007 nilifunga ndoa ya bomani na mfanyabiashara maarufu Jack Pemba. Yule mchumba aliyekuwa akinisubiri mwanzo alikuwa ameshakata tamaa na kuendelea na maisha yake, hivyo nilianza kuishi na Jack kama mke na mume huku akinisaidia katika mambo yangu ya sanaa.
“Baadaye alinizuia kwani alikuwa hapendi nitoke nyumbani na baada ya muda nilipata ujauzito wake kitu ambacho kilimfurahisha sana na kunizawadia vito vya dhahabu vyenye uzito wa kilo moja, lakini kwa bahati mbaya ilipofika miezi saba nilijifungua mtoto akafariki.
Kipigo chamkimbiza kwenye ndoa
“Ndoa ilikuwa ni nzuri, nilikuwa napata kila kitu ambacho nataka na kutembelea gari za kifahari lakini kitu ambacho nilikishindwa ndani ya ndoa hiyo ni kipigo kikali nilichokuwa nakipata, kwani nakumbuka kuna siku alinipiga kiasi ambacho mashuka meupe yalikuwa kama yamepakwa rangi nyekundu, hivyo bibi yangu alikuja kunichukua na kuondoka moja kwa moja.
Aendelea na maisha yake
“Baada ya kuondoka kwa Jack, nilianza kupigana katika maisha na niliingia kwenye uhusiano na mtu mwingine na nikaanza kuingia kwenye kucheza filamu ambapo huko jina langu lilizidi kukua siku hadi siku, hivyo nikawa naweza kuyaendesha maisha yangu ya kila siku, mpaka nilipokutana na mume wangu wa sasa, Sunday Demonte ambaye alinioa mwishoni mwa mwaka jana.

Kwa nini Tanzania na si Dubai kwa mumewe?
“Unajua kazi yangu kubwa mimi ni uigizaji ambapo huku Tanzania ndiyo kila kitu, sasa nikisema nikae Dubai muda wote ni lazima kipaji changu kitapotea, hivyo nafanya kazi zangu kwa kutengeneza filamu kama tatu, kisha narudi Dubai kidogo kukaa na mume wangu.
Nini kilichomuumiza na kumfurahisha?
“Siku zote naumia sana kuwapoteza wazazi wangu wawili, yaani baba na mama, nilitamani sana mpaka leo wawepo na waione kazi yangu na nilifurahi sana siku ambayo nilifunga ndoa yangu ya pili na Sunday Demonte,” anaeleza Aunt.