Showing posts with label Ajali. Show all posts
Showing posts with label Ajali. Show all posts

Wednesday, 11 September 2013

PICHA ZA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA JIJINI ARUSHA HAPO JANA...


                       Hii ndio coaster iliyopata ajali ambayo baada ya ajali ilihama barabarani na kuelekea vichakani.

Huu ni upande wa mbele wa garri aina ya Suzuki Escudo ambao unaonekana kuumia sana, na baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wakishangaa jinsi ambavyo gari hiyo imeharibika.
 Huu ndio upande wa mbele wa coaster iliyopata ajali na abiria wote kutoka wakiwa wazima wa afya.
        ARUSHA jana usiku majira ya saa moja ilitokea ajali mbaya iliyohusisha gari  aina ya Escudo yenye nambari za usajili T600 AUC na Coaster yenye nambari za usajili T598 BNS. Ajali hiyo iliyotokea eneo la Makumira, wilayani Arumeru, jijini Arusha. Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wanasema chanzo cha ajali hiyo wamesema kuwa ni gari aina ya coaster iliyokua ikitokea jijini Arusha na ilipofika eneo la makumira ilitaka kupita gari iliyokuwa mbele lakini kabla gari hiyo haijamaliza kuipita gari hiyo, kumbe mbele kulikua kuna gari aina ya Escudo iliyokua ikitokea Moshi kuelekea Arusha ndipo zilipokutana uso kwa uso na kusababisha ajali mbaya.   
Katika ajali hiyo hakuna hata mtu mmoja aliyefariki ila dereva wa gari aina ya Escudo aliyefahamika kwa jina moja la Hussein maarufu kama Baunsa ndie aliyeumia sehemu za miguuni na kichwani lakini wasamaria wema waliweza kumtoa katika eneo la ajali na kumuwahisha hospitali

Friday, 30 August 2013

TASWIRA ZA AJALI ILIYOUWA WATU 41 NA KUJERUHI 33 NCHINI KENYA

Pichani juu ni taswira za ajali ya basi iliyouwa watu 41 na kujeruhi 33 katika eneo la Ntulele lililo kwenye mkoa wa bonde la ufa nchini Kenya. Basi hilo lilikuwa likiwasafirisha zaidi ya abiria 60 kutoka mji mkuu wa Kenya, Nairobi kuelekea mji wa Homabay uliopo magharibi mwa Kenya lilikosa mwelekeo na kupinduka mara kadhaa usiku wa kuamkia Alhamisi. Watu 33 walifariki papo hapo huku wengine 8 wakifariki baadaye walipokuwa wakipata matibabu hospitalini. Watu wengine 33 waliopata majeraha mabaya wanaendela kupata matibabu kwenye hospitali tofauti nchini Kenya. Akituma rambirambi zake kwa familia za marehemu, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amewataka madereva kuwa waangalifu na kuongeza kuwa hatua zitachukuliwa kuhakikisha maisha ya Wakenya hayapotei kwa ajali za barabarani. (Picha na Nation)

Thursday, 29 August 2013

ZAIDI YA WATU 40 WAMEFARIKI DUNIA KWENYE AJALI ILYOTOKEA KENYA



Takriban watu 41 wanadaiwa kuuawa baada ya basi moja la abiria lililokuwa likitoka Nairobi kuelekea Homabay Magharibi mwa Kenya kuanguka na kubingirikia mara kadhaa katika eneo la Narok.Polisi wamethibitisha kuwa miongoni mwa waliouawa ni watoto wanne.Mkuu wa polisi wilayani Narok Patterson Maelo amesema kuwa dereva wa basi hilo alishindwa kulithibiti katika eneo la kona na hivyo basi hilo kupoteza mwelekeo na kuanguka.Maafisa wa shirika la msalaba mwekundi ambao tayari wamefika katika eneo la tukio hilo wamesema kuwa watu wengine 33 waliojeruhiwa wamesafirishwa hadi hospitali ya wilaya ya Narok kwa matibabu.Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni miongoni wa viongozi waliotuma risala zao za rambi rambi kwa jamaa na marafiki wa abiria waliouawa.Katika ripoti iliyochapishwa katika mtandao wake wa twitter, rais Kenyatta ametoa amri kwa idara ya polisi kuchukua hatua dhidi ya wamiliki wa magari ya umma wanaokiuka sheria za barabarani. 
Source:BBC NEWS

Wednesday, 28 August 2013

BASI LA HOOD LAUA MTU MMOJA NA KUJERUHI 15

Mtu mmoja amefariki dunia na 15  wamejeruhiwa baada ya basi  la Kampuni ya Hood  likitokea kilombero kwenda jijini  Dar es salaam kumgonga  mtembea kwa miguu na kisha kuacha njia na kupinduka katika eneo la Kiembeni  Mikese Mkoani  Morogoro .
  

Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro  Bonifasi Mbao  akizungumza kwenye  eneo la tukio amesema chanzo cha ajali  hiyo ni mwendo kasi ambapo dereva wa basi  gari  ilimshinda na kugonga mtembea kwa miguu na kisha kupinduka ambapo  dereva wa basi amekimbia mara baada ya tukio la ajali...
 
Taarifa za  madaktari  katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro  zimeeleza  majeruhi wanaendelea na matibabu na mwili wa marehemu umehifahiwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa morogoro .

Source:ITV

BREAKING NEWS: WATU 13 WAMEFARIKI KATIKA AJALI YA GARI HUKO SHINYANGA...

Habari zilizoufikia mtandao huu hivi punde zinasema kuwa watu 13, wamefariki dunia na 11 wamejeruhiwa katika ajali mbaya iliyotokea usiku wa kuamkia leo katika kijiji cha ngongwa mkoani shinyanga kwenye ajali iliyohusisha gari aina ya hice lenye namba za usajiri t 756 chx na gari lililokuwa limeharibika lenye namba za usajili t 696 ams.

Akizungumza kwa njia ya simu kaimu kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga, kihema kihema, alisema kuwa miongoni mwa watu waliofariki dunia ni pamoja na dereva wa hice, iliyokuwa na abiria hao ikitokea kahama kuelekea ushirombo ambaye alifariki papo hapo, huku majeruhi wakipelekwa kupatiwa huduma ya kwanza katika hospitali ya wilaya ya kahama.
  KILELE CHA HABARI tunatoa pole kwa wahanga wa ajali hiyo....

Sunday, 25 August 2013

ANUSURIKA KUFA BAADA YA GARI LAKE KUGEUKA KUWA BRAKE YA BASI LILILOACHA NJIA NA KUGONGA HAPO JANA TEMEKE SUDAN

 Umati wa watu uliojitokeza ghafla baada ya ajali hiyo kutokea hapo jana maeneo ya Temeke Sudani
  gari ndogo aina ya Nissani likiwa limesukumwa kabisa hadi nje ya barabara na basi lililofeli kushika brake
 Nissani ilipokuwa brake ya basi hilo hapo jana Maeneo ya Temeke Sudan
 Hilo ndio basi la Mrisho Investment lililofeli brake na kugonga gari ndogo aina ya Nissani
 Gari aina ya Pajero likiwa limesukumwa hadi nje ya barabara baada ya basi hilo kufeli brake na kugonga gari ndogo hadi nje ya barabara
                Wadau wakiangalia ajali hiyo iliyotokea temeke jana
 Mwenye gari ndogo aina ya Mistubishi Pajero (mwenye Tshirt Nyeusi) lililogongwa na Basi akielezea jinsi alivyoweza kusukumwa kutoka barabarani hadi nje ya Barabara na basi lililofeli brake na kupitiliza hadi kugonga gari ndogo aina ya Nissan
Wakazi wa Temeke Wakiangalia basi lililoacha njia na kugonga gari ndogo aina ya Nissani hapo jana Temeke Sudani.Hakuna Aliyejeruhiwa wala Kuumia