Chuo kilichopo mji wa Nsuka kimeshuhudia tena mauaji ya kikatili ya dereva wa tipa ambae amewapa mimba mjane na mtoto wake. Ripoti inasema dereva huyo amechomwa moto na mtoto wa kiume wa mjane huyo,Sunday Ugwoke.
Kutokana na habari zilizokusanywa Sylvester Ezema alikuwa amejishikiza kwenye kampuni ya Ferguso Nig. Limited huko Akpa Edem na alikokuwa anaishi alikuwa anashea fensi ya kawaida tu na mpenzi wake mjane. Taarifa zinasema kuwa alikuwa pia na mahusiano ya kimapenzi na mtoto wa kike wa mjane huyo ambaye alikuwa hajui mpaka alipofariki siku chache zilizopita ndipo alipokuja kujua.
Sylvester alichomwa moto mpaka akafa na Sunday ambaye alishamwonya aachane na mama yake na aache kufanya nae mapenzi kwenye chumba cha marehemu baba yake,ambacho kimepakana na chumba chake,Onyo ambalo marehemu Sylvester hakulizingatia na kuendelea na tendo hilo baya.Sylvester aliyapa kisogo maonyo ya Sunday akisema kuwa huyo mjane ni 'family friend' so hakuna atakayewashitukia. Kwa kutofuata maonyo,siku moja Sunday,alijikoki na pilipili ya kusagwa na petrol akamvamia yule 'lover boy'. Sylvester alipotoka tu mlangoni kwake, Sunday alimmwagia pilipili na petrol kisha akamuwasha moto.
Tuesday, 13 August 2013
"VIONGOZI WANAOMTETEA SHEIKH PONDA NI WANAFIKI WAKUBWA.....WAKATI ANAHUBIRI UCHOCHEZI MLIKUWA WAPI?"..WILLIAM MALECELA
Hii ni kauli ya mtoto wa kigogo hapa nchini maarufu kwa jina la William Malecela ambayo ameitoa kupitia blog yake akiuelezea mtazamo wake kuhusu Sakata la Ponda kupigwa risasi na polisi....
Malecela ameanza kwa kuuchambua wadhifa wa Sheikh Ponda, huku akikumbushia vurugu za mwembechai na mahubiri ya kichochezi ya Ponda dhidi ya serikali na wananchi wengine wa kawaida......
Kwa mujibu wa kauli yake, Malecela anadai kuumizwa na unafiki wa viongozi ambao wameanza kujitokeza na kumtetea kana kwamba kauli zake huwa hawazisikii...
-------------------------------------------------------------------HII NDO KAULI YAKE--------------------------------------------------------------------"Nimekuwa nikimfuatilia Sheikh Ponda kwa karibu sana toka wakati wa vurugu za MwembeChai, since then amegeuka kuwa a very mysterious creature almost becoming like John Gotti the once feared New York City's Mafian Don.
"Baada ya kusoma kwa makini comments nyingi sana between the media na Social Media za Tanzania, za kutoka kwa wananchi mpaka Viongozi wengi wa Siasa wa Taifa toka ashambuliwe majuzi, ninauona unafiki mkubwa sana na wa hali ya juu sana, kweli kama hili Taifa we are not Taifa la Wanafiki, basi we are almost there to become one!. I mean who is Ponda? What does he stand for? Who pays for his bills and WHY?
"I will never support violence, lakini here we have a Muslim Leader preaching violence, every where he talks the man preaches violence sijasikia Kiongozi yoyote wa Taifa akijitokeza kumlaani Ponda na message zake!,...
"Leo the very Violence he preaches comes to haunt him, eti tuna Viongozi wa Taifa wanaodai Uchunguzi na maneno mengi ya Siasa ambayo wala hayahusu kabisa.
"Wanatuambia nini sisi wananchi wengine wa kawaida kwamba ku-preach violence is ok but when that violence comes to haunt you then where is the government? Really? What government? Halafu eti kuna Viongozi wa Taifa hili wanaojaribu kujikomba komba na kuongea maneno ya kinafiki waonekane wapo sawa na hawa wanaomlilia? Please!!
"Amepigwa risasi 20 Biliionea Arusha majuzi mbona hajatokeza Kiongozi hata mmoja wa Siasa kumlilia na kutaka waliompiga wakamatwe haraka sana?
"Amememwagiwa tindikali Mfanya biashara maarufu hapa mjini mbona hatujasikia hawa wanasiasa uchwara wakilia lia wakamatwe waliommwagia?
"Wananchi wangapi wanapigwa Risasi kila siku nchini mbona hatujasikia hawa Viongozi wakilalamika kwamba wahusika wakamatwe? Stop this madness please....
"Viongozi wote wanaolilia na ishu ya Ponda ni wanafiki wakubwa na ni hatari sana kwa hili Taifa. And yes I said it, ni wanafiki wakubwa they all need to go!
" I mean what is so special about Ponda kwamba Serikali iache kazi zake za kawaida ianze kuwatafuta waliompiga Risasi? Vipi wananchi wengi walioumizwa na kupoteza maisha yao kutokana na mafundisho ya sumu za Ponda?
"I mean it is about time now wale Viongozi wote wanaolialia kuhusu waliomrushia risasi Ponda kujiuzulu kwa sababu wote ni infit kuongoza hili Taifa, na Viongozi wa juu wa Serikali acheni kujipendekeza na maneno maneno ya kujifanya kuwatuliza hawa wanao lia lia, na maneno ya tume!
"Tume my left foot, Ponda ni mwananchi kama wengine wote so tatizo lake lichukuliwe kama mengine na Serikali should get tough na wajinga wajinga kama Ponda, nothing but a ******** in the cover of religion!,
"I mean wananchi Millioni 44 tunakaa tunasumbuliwa na mwanachi mmoja kila siku? how could that be? Enough! and yes I said it he is nothing but a coackroach in the cover of religion!!"
- MUNGU AIBARIKI TANZANIA!
Le Mutuz( William Malecela )

BILIONEA KUZIKWA LEO,JENEZA LAFUNGULIWA KWA RIMOTI....
Mazishi ya kifahari yanaandaliwa na familia ya marehemu Erasto Msuya, huku ikielezwa kuwa jeneza litakalotumika kubeba mwili wake linafunguka kwa kutumia ‘rimoti’.
Msuya aliyeuawa wiki iliyopita, anazikwa leo huku familia ikitangaza kutokulipiza kisasi kwa waliohusika, badala yake wamemwachia Mungu.
Kinachovutia katika msiba huo ni jeneza lililobeba mwili wa mfanyabiashara huyo lililoagizwa Nairobi, la aina yake huku likifunguliwa kwa kutumia ‘rimoti’.
Jeneza hilo lililoagizwa kutoka Kampuni ya Montezuma & Monalisa Funeral Home, linafunguliwa kwa kubonyeza kifaa maalumu hata mhusika anapokuwa mbali.
Hali hiyo ilionekana kuwaacha na mshangao maelfu ya waombolezaji waliofika kuaga mwili wakati wa ibada iliyofanyika nyumbani kwake, Kwa Iddi, wilayani Arumeru.
Mfanyabiashara huyo aliyeuawa kwa kumiminiwa risasi zaidi ya 20 na watu wasiojulikana, anazikwa leo nyumbani kwao eneo la Kairo Mirerani, Wilaya ya Simanjiro, mkoani Manyara.
Kaka wa marehemu, Israel Msuya, alisema jana kuwa mazishi hayo yatafanyika makaburi ya familia ya mzee Elisaria Msuya ‘Kikaango’, baba wa marehemu Erasto.
Kwa mujibu wa Kamati ya Maandalizi ya mazishi hayo inayoongozwa na kaka mkubwa wa familia ya Msuya, Gady, zaidi ya Sh100 milioni zimepangwa kugharimia shughuli za maombolezo na mazishi.
Jeneza na gari maalumu la kubebea mwili wa marehemu yameagizwa kutoka Kampuni ya Montezuma & Monalisa Funeral Home ya Nairobi, Kenya kwa gharama ya Sh8 milioni.
Chakula, vinywaji, mapambo na magari ya kukodishwa kutoka Arusha kwenda Mirerani na kurudi yanatarajiwa kugharimu zaidi ya Sh80 milioni.
Katika hatua nyingine, polisi mkoani Arusha imeendelea kuwahoji wafanyabiashara maarufu wa madini ya Tanzanite wa Mji mdogo wa Mirerani, wilayani Simanjiro, wakidaiwa kuhusika na kifo hicho.
Habari zilizopatikana jana zinadai mfanyabiashara mmoja kijana ambaye aliibuka ghafla kuwa tajiri mkubwa kutokana na biashara ya madini ya Tanzanite, anashikiliwa Arusha kwa mahojiano.
Jana, kwenye viunga vya Mji wa Mirerani watu walitangaziwa kuwa mfanyabiashara huyo, alikuwa anashikiliwa kwa mahojiano kuhusiana na kifo hicho.
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, hakupatikana mara moja kuelezea suala hilo kwani simu yake ilipopigwa ilikuwa haipatikani.
Marehemu ameacha mke na watoto wanne, huku akiacha rasilimali nyingi ikiwamo jumba la kifahari lililopo Sakina kwa Idd, hoteli maarufu za SG Resort na Mezza Luna zilizopo Arusha.
Mwanananchi
NILIMPENDA SANA ELIKEM LAKINI MAMBO YAKABADILIKA!
MWAKILISHI pekee katika mashindano ya Big Brother The Chase kutoka Afrika Mashariki, Feza Kessy, amesema aliingiwa na fikra kwamba Elikem angekuwa mtu wa karibu yake, kwani waliingia ndani ya nyumba pamoja lakini mambo yalibadilika ndani ya siku 77 alizoishi humo.
Akizungumza na IK baada ya kutolewa ndani ya jumba hilo usiku wa juzi Jumapili, Feza alisema haikuwa rahisi kwake kutambua tabia halisi za Elikem mpaka alipokaa naye kwa muda mrefu ndani ya jumba hilo.
“Siku naingia ndani ya jumba niliongozana naye, nilimpenda kwa kumwona tu, lakini yeye bado sana kimapenzi,” alisema kabla ya IK kumrushia swali ‘Unampenda kweli Oneal?’, “ Ndio” alijibu Feza kwa sura ya aibu.
Feza alimweleza IK kuwa amekuwa akizozana mara kwa mara na Oneal kwa kuwa alihisi kwamba Feza alikuwa akimtumia jambo ambalo halikuwa sahihi.
Baada ya IK kumuuliza iwapo anadhani kuwa Oneal alikuwa na mwanamke mwingine akimsubiri nje ya jumba hilo, Feza alijibu; “Sina hakika na hilo.”
IK alipomuonyesha ni nani alimpendekeza kupigiwa kura za kutolewa, alishtuka baada ya kuona sura ya Dillish ikitokeza, hata hivyo Feza alisema ameshangazwa na kitendo cha Melvin kumpendekeza lakini alizungumza naye kabla kwamba alifanya hivyo.
Alipoulizwa anadhani nani atashinda, Feza alisema: “Siwezi kutabiri, lakini Angelo ni mtu ninayemhusudu zaidi.”
Wakati mpenzi wa Feza, Oneal, akitoka wiki iliyopita alisema: “Kazi niliyowahi kuipenda ndani ya BBA ni ndoa niliyofunga na Feza, niliifanya kama ndio kweli kwani nampenda sana yule binti” aliiambia Afrika.
Feza anaondoka ndani ya jumba hilo akiwa zikiwa zimebaki siku 14 tu mashindano hayo kumalizika, huku akiwa amewaacha washiriki saba wanaoendelea kuwania kitita cha Dola 300,000 (Sh 480 milioni)
Feza alipata kura nne kutoka Tanzania, Kenya, Uganda na Botswana. Cleo naye alipata kura nne kutoka Malawi, Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe huku Dillish akiongoza kwa kupata kura saba kutoka Angola, Ghana, Ethiophia, Namibia, Nigeria, Sierra Leone na nchi nyingine za Afrika.
Cleo na Dillish wamefanikiwa kuendelea kubaki katika mashindano hayo baada ya kupata kura nyingi zaidi kuliko Feza. IK alifunga shoo kwa kuwataka washiriki waitumie siku ya Jumatatu (jana) kuwapendekeza wanaostahili kuondoka na wasiangalie urafiki wao.
MAISHA YA RAIS KIKWETE YAKO HATARINI....
JENGO la ghorofa 19 lililojengwa karibu na Ikulu ya Dar es Salaam linadaiwa kuhatarisha maisha ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, UWAZI limefuatilia kwa umakini.
Uchunguzi uliofanywa umebaini kuwa, jengo hilo ni refu sana na waandishi wetu waliingia humo mpaka ghorofa ya 19 kisha kuona ukaribu uliopo na kubaini kwamba ni hatari kwa usalama wa ikulu na rais mwenyewe.
Baadhi ya wananchi waliozungumza na gazeti hili walisema kutokana na ghorofa hilo kuwa karibu na ikulu maadui wanaweza kulitumia kwa kupanda hadi juu na kuona kinachofanyika ikulu hivyo kama ni wenye nia mbaya wanaweza kutekeleza uhalifu kirahisi.
MMILIKI WAKE ANA ASILI YA NJE
Jengo hilo linalodaiwa ni la kigogo Mbongo mwenye asili ya Asia (jina tunalo) limekuwa kero katika eneo hilo kiusalama jambo ambalo limesababisha serikali kuingilia kati na kuwasaka walioruhusu ujenzi wake na kuwaburuza kortini.
Baadhi ya wakazi wa jijini Dar waliwalaumu viongozi wa serikali kwa kuacha ujenzi wa ghorofa hilo hadi kumalizika na watu kuhamia ndipo wakachukua hatua.
“Lazima tukiri kwamba kuna matatizo ya utendaji katika serikali yetu. Haiwezekani jengo linafikia ghorofa kumi na tisa ndipo serikali inaona, tunaamini walikuwa wanaona lakini waliamua kukaa kimya mpaka waliposhtuka kwamba, kumbe mtu akiwa juu anaweza kuchungulia ikulu kwa JK,” alisema mwananchi mmoja kwa sharti la kutotajwa jina.
WALINZI WA OBAMA WADAIWA KUWA CHANZO
Kuna habari kwamba, ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama nchini Tanzania Julai Mosi, mwaka huu ndiyo ulioibua mambo mengi juu ya kuwepo kwa jengo hilo kwani maafisa wake wa usalama walikataza watu kupanda hadi ghorofa ya 19 kwa maelezo kuwa wamegundua ni hatari kwa maisha ya viongozi, hasa Rais Obama aliyekuwa ikulu na JK.
Kikosi cha Majasusi wa Marekani (FBI) waliotangulia nchini miezi minne kabla ya ujio wa Obama ndiyo walioishtua serikali kwa kuwaambia watu wa usalama kuwa urefu wa jengo hilo ni hatari kwa ikulu kwa vile maadui wanaweza kulitumia.
FBI WALITEGA MITAMBO YAO JUU YA JENGO
Uchunguzi unaonesha kwamba, kwa vile FBI waliamini usalama wa ikulu ni mdogo kutokana na jengo hilo hivyo walilazimika kuweka mitambo yao juu yake na kuendelea kuwepo hapo kwa saa ishirini na nne kipindi chote cha ziara ya Obama.
FBI WALIONDOA MAGARI CHINI YA JENGO
Vyanzo vyetu vya habari ndani ya ikulu vililitonya Uwazi kuwa, mbali na FBI kuweka mitambo yao ya kiusalama, pia walilazimika kuondoa magari yote yaliyokuwa yamepaki chini ya jengo hilo na kuitahadharisha serikali ya Tanzania kuwa makini na ghorofa hilo.
WAPENDEKEZA JENGO LIVUNJWE
Habari zaidi zinasema FBI hao walipendekeza jengo hilo livunjwe ama liwe la serikali na waishi wana usalama wanaolinda viongozi wa kitaifa.
“Baada ya FBI kutoa taarifa hizo ikulu ndipo ‘mchawi’ alipoanza kutafutwa hadi kufikia hatua ya kukamatwa walioruhusu ujenzi huo,” kilisema chanzo.
KILA KITU KINAENDELEA
Waandishi wetu wamegundua kuwa pamoja na tahadhari iliyotolewa na FBI juu ya jengo hilo, lakini bado shughuli za kila siku zinaendelea sambamba na watu kuishi.
WALIOTOLEWA ‘KAFARA’ NI HAWA
Hivi karibuni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na Msanifu Mwandamizi wa Majengo, Richard Maliyaga walipandishwa kizimbani wakikabiliwa na mashitaka ya kutumia madaraka vibaya kwa kuruhusu ujenzi wa ghorofa hilo karibu na ikulu.
Washitakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo.
Washitakiwa walikana mashitaka na kuachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini watatu wafanyakazi wa serikali waliosaini hati ya shilingi milioni 50.
Source: Uwazi

HATARI....BILIONEA MWINGINE APIGWA RISASI DAR...!!!
MAUAJI ya wafanyabiashara wakubwa ‘mabilionea’ yameshika kasi nchini ambapo baada ya tajiri mkubwa Arusha, Erasto Msuya kuuawa kwa risasi hivi karibuni, Agosti 3, 2013 bilionea Elia Daniel Endeni (49) naye aliuawa kwa kupigwa risasi nje kwa mwanamke anayedaiwa kuwa ni mke wake mdogo aitwaye Juliana Labson (28).
Tukio hilo lilijiri siku hiyo saa 2 usiku maeneo ya Temeke Mikoroshini jijini Dar es Salaam ambako ni nyumbani kwa Juliana.
Tukio hilo lilijiri siku hiyo saa 2 usiku maeneo ya Temeke Mikoroshini jijini Dar es Salaam ambako ni nyumbani kwa Juliana.
Elia alikuwa na kampuni iitwayo Elia Herdons Ltd ya kupakua na kupakia mizigo ya makontena bandarini, maduka na majumba ambapo polisi walikuta shilingi 151,000,000 taslimu ofisini kwake akiwa amezihifadhi.
Ilidaiwa kuwa muda huo, Elia alikuwa amefika nyumbani kwa mwanamke huyo lakini kabla hajashuka katika gari lake, Pick-up lenye namba za usajili T 319 AFJ alichomolewa kwenye gari na kupigwa risasi na watu wawili wasiojulikana.
Taarifa zilieleza kwamba waliotekeleza unyama huo walikuwa wakimfuata marehemu huyo kwa nyuma wakiwa kwenye pikipiki.
Baadhi ya watu waliozungumza na gazeti hili walisema marehemu alikuwa na kawaida ya kufika nyumbani kwa Juliana nyakati za usiku na kabla ya kushuka kwenye gari, alikuwa akimpigia simu mwanamke huyo ili afungue mlango.
“Ilikuwa wakati anapiga simu ndipo alivamiwa na watu hao ambao walivunja kioo cha gari kwa kutumia kitako cha bastola kisha kutoa ‘loki’ ya mlango na kumchomoa.
“Walimdhibiti bila kutoa sauti, wakati huo sisi tulikuwa tumekaa nje tukishuhudia lakini tuliamini kwamba huenda walikuwa wamegongana barabarani kwani hata marehemu hakusikika akiomba msaada,” alisema mwanamke mmoja jirani ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.
Mwanamke huyo aliendelea kusema kwamba hakukusikika mlio wa risasi, bali marehemu alianza kulia ghafla akiomba msaada.
Aliongeza kuwa watu walipokaribia eneo la tukio, wauaji hao walipiga risasi mfululizo hewani, kitendo kilichowafanya watawanyike kuokoa maisha yao na majambazi hayo yakatoweka.
Inadaiwa majirani walipofika, walimkuta tajiri huyo akiwa amelala katika dimbwi la damu huku ameishiwa nguvu kiasi kwamba alishindwa kuongea chochote.
Habari zinasema mke huyo mdogo aliyezaa naye watoto wawili, alipotoka ndani alizimia baada ya kuona Elia akiwa katika dimbwi la damu.
Muda mfupi baadaye, polisi walifika eneo la tukio na kumchukua majeruhi kumpeleka Hospitali ya Temeke ambapo alifariki dunia akiwa njiani.
Taarifa zinadai kwamba Julai 28, mwaka huu marehemu Elia alikoswa na risasi akiwa njiani kwenye gari akitokea msibani Same, Kilimanjaro.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, ACP Engelbert Kiondo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba walifika katika eneo hilo wakiwa na wasiwasi kwamba huenda watu hao walimnyang’anya bastola.
“Ilitubidi twende ofisini kwake Kurasini na kupekua, tukaikuta bastola. Hili suala linaonekana ni kisasi kwa sababu wamemuua bila kuchukua kitu chochote, tunaendelea na upelelezi,” alisema Kamanda Kiondo.
Mazishi ya Elia yalifanyika Jumatano iliyopita, Same ambapo Juliana alikuwa miongoni mwa waombolezaji. Mke mkubwa wa marehemu aishiye Kimara King’ong’o jijini Dar ndiye aliyekuwa ameongoza msiba huo.
Monday, 12 August 2013
MAZOEZI MATATU YA KUZUIA MATITI YA MWANAMKE YASILALE NA KUWA MALAPA
Ikiwa wewe umechelewa(ulikuwa hujui hili wakati matiti yako yanaota) basi msaidie mdogo wako au binti yako anaekuwa hivi sasa, ili asije kujisikia vibaya pale wanaume watakapokuwa wakiponda matiti kwa kuyaita "malapa"....
Kwanza kabisa hakikisha mtindo wa kulala ni kifudifudi (kulalia tumbo), kwa kufanya hivyo kunasaidia kwa kiasi kikuwa kufanya matiti yako pumzike, kwamba hakutakuwa na kuning'inia kama utakuwa umelala chali(lalia mgongo) au kiubavu.
Zoezi...1
Asimame wima dhidi ya mlango au ukuta kisha aegeshe matiti yake mahali hapo kwa nguvu kisha aachie (ajitoe ukutani), zoezi hili hufanya matiti yaume sana lakini wewe kama dada mpe moyo kuwa avumilie. Afanye hivyo mara 20 kila asubuhi.
Zoezi....2
Simama wima huku mikono yako ikiwa imenyooshwa huku na kule kisha ipeleke mbele nakukutanisha viganja vyako alafu irudishe nyumba kadiri uwezavyo (sio lazima ikutane) ila utahisi maumivu fulani sehemu ya matiti (misuli yafanya kazi hapo)....fanya hivyo mara 10 na ongeza hesabu njinsi unavyokua.
Zoezi...3
Ukiwa umesimama wima na mikono yako imenyooshwa huku na hule inanyue taratibu kuelekea juu na kutanisha vidole vyako huko juu kisha rudisha mikono ilipokuwa (imenyooka huku na kule).
KWA USHAURI ZAIDI NA STORI ZA MAPENZI, INGIA JUKWAA LA WAKUBWA
<<BOFYA HAPA>>

Subscribe to:
Posts (Atom)